BARAKA AMA LAANA
Tangu mwanzo Mungu
alimuumba mwanadamu aishi kwenye baraka na sio laana Mw 1:27-28 inatueleza juu
ya jambo hilo.Kila mtu maadamu anapumua Mungu alimtamkia mambo matatu
alipoumbwa na yeye.Kama vile Mw 1:27-28 inavyotueleza na mambo hayo ni
"Ubarikiwe","Ukaongezeke" na "Ukatawale".Na siri
hii sio wengi wanaoijua kwa maana kanisa la leo halitaki mafundisho bali
wanataka mahubiri ili wawahi kutoka maana mahubiri mara nyingi hayatumii muda
mrefu na badala yake watu wengi kukaa kwenye giza kwa kipindi kirefu.Swali
ambalo mimi na wewe twapaswa kujiuliza ni kwamba kati ya mambo haya matatu
ambayo Mungu ametutamkia tulipokuwa tunakuja duniani Je yametimia
kwetu?Utagundua kuwa hakuna ambacho kimetia kwetu ngoja nikupe mifano michache
ili uweze kuelewa kile ambacho Mungu anakutazamisha,kama mwanafunzi kwanini
hufaulu vizuri darasani na wewe ni mtu alieokoka au aliemkabidhi Mungu
maisha?Kama wewe ni mfanyakazi mahali popote kwa nini hupandishi cheo au
mshahara wako hauongezwi?Nadhani mpaka hapo tupo pamoja kama hujapata kitu bado
usiwe na wasiwasi Mungu atakufunulia kitu maana amekuchagua hata kukusukuma
kusoma waraka huu.
Laana ni kinyume na
baraka.Sio wote walio na fedha nyingi wamebarikiwa na sio wote wasio na fedha
nyingi wamelaaniwa.Fedha iliyo ya baraka ni ile isiyokutesa fedha inayotesa sio
baraka bali ni laana kama nilivyotangulia kukueleza kuwa laana ni kinyume cha
baraka.Baraka ni mafanikio yenye amani na furaha Kumb 11:26-28.Mungu
anakukumbusha kuwa ameweka vitu viwili kwenye maisha yako ambavyo ni laana na
baraka.Nae amekupa nafasi hivi leo ya kuchagua kimoja wapo katika ya baraka na
laana.Lakini laana itaambatana na wewe pale ambapo utakaposhindwa kusikia kile
ambacho Mungu anakueleza.Pia utabarikiwa tu pale ambapo utasikia sauti ya Bwana
lakini kusikia huja kwa neno la Mungu.Laana inatokana na dhambi ngoja
nikufikirishe kidogo je umewahi kufikiri kuwa unapotenda dhambi umekuwa
umelaaniwa?Unaweza ukafikiri kuwa ninakudanganya lakini biblia inasemaje juu ya
laana?Mtu anapata laana pale tu anaposhindwa kusikia sauti ya Mungu.Na dhambi
ni nini?Je si kushindwa kusikia sauti ya Mungu hivyo kushindwa kutimiza haki
yote kunakupelekea kupata laana Kut 20:5
Lakini unapopata
laana si kwamba laana hiyo haiwezi kuondoka lakini biblia inasema kuwa Yesu
alifanyika laana kwa ajili yako ukisoma Gal 3:13 utaona kuwa Yesu achukua laana
yako ili wewe uwe mzima. Omb 5:7,Mt
23:30-31,Lk 11:50-51 usihofu juu ya hali uliokuwa nayo hivi leo amini tu Yesu
yu kwa ajili yako .Hivyo toba yako itakupatanisha na yeye na kujenga tena upya
maisha yako na kufuta laana yako.Uwe na uhakika kuwa laana haitokani tu makosa
yako tu lakini pia waweza kupata laana kwa makosa ya wazazi wako au ndugu zako
ikiwapo mababu ,mabibi,mashangazi na watu wengine wa kale.
MUNGU ANAVYOTUMIA
SADAKA KUGUSA MAISHA YAKO YA BAADAE
Yer 29:11 Ninayajua
mawazo ninayowawazia ni mawazo ya amani.Mara chache tunatazama kwa jicho la
Mungu lakini mara nyingi tunatazama kama mtumishi atazamavyo na makanisa
yatazamavyo.Nayajua mawazo ya amani (mafanikio) na kukupa tumaini.Mungu
anapanga maisha kwa ajili yako hata kabla hujazaliwa lakini si ukizaliwa ndio
anapanga mustakabali wako wa baadae ukisoma maandiko anasema ni ndie nitangazae
mwisho kabla ya mwanzo.Mpango anaokupa imekupasa kuufuata.Lakini wakati
mwingine hawezi kukupa isipokuwa
umeachia sadaka.
Mw 15:17-19 Ibrahimu
alikuwa akihojiana na Mungu juu ya maisha yake ya baadae.Mungu alimwambia
Ibrahim kuwa yeye na uzao wake watamiliki nchi lakini alipotaka kujua atamiliki
vipi Mungu akamwambia achilia sadaka.Na Ibrahim alipoachilia sadaka Mungu alimueliza
habari ya miaka 400 baadae hii ni sababu sadaka ya Ibrahim ilikwenda na
kunyakua habari ya vizazi vinne kwa Ibrahim hapo baadae.Hivyo kuna nguvu ya
ajabu ilio katika sadaka isiyo ya kawaida.Kuna wakati Mungu hubadilisha maisha
yako mabaya bila wewe kuachilia sadaka.Ebr 11:31,Jos 2:3 Kitendo cha Rahabu
kuwapokea wale watumishi kilimgusa Mungu na kubadili maisha ya Rahabu.
Mw 7-8,Mw 8:21 Nuhu
alipata wazo la kuachilia sadaka ili Mungu aseme juu ya maisha yake ya
baadae.Baada ya gharika maisha duniani yalikuwa ukiwa kila mahali
pakaharibika.Baada ya kuharibu maisha ya duniani akamwambia Nuhu aanze maisha
mapya ambayo hapo mwanzo hayakuwepo Nuhu akaamua aachilie sadaka maana
mazingira alioyakuta baada ya gharika sio yale alioyazoea ndipo Mungu akaweka
agano naye.Baraka ambazo zipo kwenye agano ni kubwa kuliko baraka ambazo hazipo
kwenye agano.Kuna wakati utoaji wako wa
sadaka unaweza ukagusa mabadiliko katika maisha yako ya sasa.Lakini si utoaji
wa Kaini.Mungu akikubali sadaka yako utajua tu .
Umuhimu wa kuwa
mwangalifu utoapo sadaka kwenye uwepo wa Mungu.
Matokeo ya sadaka
yako yanatokana na mahali ambapo unatoa sadaka yako na pia uaminifu juu ya
utoaji wa sadaka.Kumb 12:10-13.Onyo la Mungu ni hatari si kila mahali utatoa
sadaka bali pale ambapo tu yeye yaani Mungu amelikalisha jina lake.Kumb
12:11,Mt 18:20 wawili watatu
wakutanikapo kwa jina langu mimi nipo katikati yao.Palipo na jina la Kristo
pana uwepo wake ,palipo na uwepo wake pana jina lake.Katika kitabu cha Matendo
ya Mitume wana wa Skewa ambao walikuwa watoto wa kuhani walikuwa wanatengeneza
mapepo.Hawa walimwombea kichaa kwa jina la Yesu,lakini pepo lililokuwepo ndani
ya kichaa likawauliza wao ni wakina nani?Maana si kila anayelitaja jina la Yesu
yeye anashuka.Sio tu kutaja jina la Yesu ila lazima uwepo wake uwepo.Shetani
haogopi jina la Yesu likitajwa mahali ambapo
hakuna uwepo wake bali huogopa jina la Yesu mahali ambapo kuna uwepo
wake.
Si kila mahali
mtumishi wake anapokuwepo basi yeye yupo lakini alipokuwapo Mungu na mtumishi
wake atakuwepo.Mungu alimuumba mwanadamu aishi kwenye uwepo wake kama vile
samaki aishivyo kwenye uwepo wa maji ndio maana antusihi tutoe sadaka kwenye
uwepo wake.Kut 23:15 wala hapana atakae ingia mikono mitupu.Mungu alisema hivyo
si kwamba hana fedha za kuwatunza watumishi ila anakujengea mazingira ya
kunyakua kilichopo kwake maana mbingu na nchi na vyote viijazavyo nchi ni mali
yake ,ukitazama Ebr 11:17-39 utagundua kuwa asilimia 45 ya maisha ya mwanadamu
yamejengwa kwenye sadaka.Hii ilitokana na dhambi kuingia duniani maana pale
mwanzo Adamu alikuwa akizungumza na kuhojiana na Bwana bustanini lakini dhambi
ikatenanisha mawasiliano ya Mungu na Adamu hivyo kupelekea matumizi ya sadaka
kwa sehemu kupokea vilivyo vya Mungu.Maana kanuni ya sadaka ni kunyakua vitu
unavyohitaji kwa Mungu.
Kut 23:15 maandiko
yanasema wala hapana mtu atakayekuja mbele zangu mikono mitupu.Kut 34:20,Kumb
16:16.Ngoja nikufikirishe jambo jipya ambalo Mungu anatamani wewe ulijue ili
usiwe mtu wa mazoea au desturi.Saa ya kutoa sadaka ni saa ya kukutana na Bwana
alipo.Pia ni saa ya kutokea mbele za Mungu au kuuonana na uwepo wa Bwana.Mk
12:41-44 Unapokwenda kutoa sadaka usienende kutoa sadaka kwa sababu ya wazee wa
kanisa au mchungaji bali kukutana na Bwana.Unapotoa sadaka kwenye uwepo wa
Bwana Mungu anapima kutokana na kipato chako na maisha yako kwa ujumla.Na
inawezekana usipate riziki kutokana na hiyo sadaka.Unaweza ukachezea vyote na
si sadaka katika uwepo wa Bwana.
Hakuna huruma kwenye
utoji wa sadaka.Mfano ni Mama wa Selepta alipelewa Elia amlishe .Kupokea sadaka
ya mjane ni ngumu lakini Mungu anataka ichukulliwe ili apate kuachilia ili
kuachilia kile ambacho Mungu anataka kuachilia kwake.Mungu anapoagiza utoaji wa
sadaka usifikirie au kutafsiri kwa hali ya ubinadamu.Mt 6:21 Hazina ya mtu
ilipo ndipo na moyo wake utakapokuwepo.Unapotoa sadaka uwe na uhakika unaanika
moyo wako.Mhu 5:1 Nyumbani kwa Mungu ni mahali ambapo Mungu anatawala mahali
ambapo uwepo wa Bwana unatawala.Wengi wanaenda kanisani kusikiliza
mahubiri na kuabudu.Kusikilza mahubiri
haina maana upo kwenye uwepo wa Bwana.Watu wengi tukienenda kanisani hatufikiri
kukutana na uso wa Bwana bali mchungaji/mtumishi au kwenda kutangaza mavazi
Mwimbaji anatakiwa akamwimbie Mungu na si kuwa pambo la ibada.Sadaka haitolewi
bila kufuata utaratibu.Unapotaka kutoa sadaka signal inakwenda mbinguni kuwa
sadaka inakuja kunyakua hitaji .
Bora kutii kuliko
sadaka maana si kila sadaka ni sadaka.Mungu alimwambia Samueli amwambie Saui
kuwa Mungu hahitaji sadaka yako kwa sababu Sauli alitaka kumtolea vitu ambavyo
Mungu alimwambia aziangamize lakini Sauli alikiri kufanya kosa hivyo kumpelekea
kupoteza ufalme wake Mdo 5:3-9.Lakini sababu hiyo ilimfanya apoteze ufalme wake
mbele za Bwana.
Mdo 5 Inatuambia
habari za Anania na Safira ambao walikwenda kutoa sadaka miguuni pa Mtume
Petro.Hakuwa na mawazo kuwa Mungu ndiye aliyekuwa akipokea sadaka yake bali
Mtume Petro hatakama ni Mtume Petro hakuwa na uhakika wa madhabahu iliyokuwa
ndani ya Petro.Maana Anania na Mkewe Safira waliazimia kuwa wauze kiwanja kisha
wapeleke sadaka yao kanisani lakini kwa sababu waliona kuwa fedha walizopata
kutokana na uuzaji wa kiwanja hicho ni nyingi walipatana kuzipunguza kisha
wazipeleke kwa mtume wasijue madhabahu ilio kwa mtume ndio hiyo ya Mungu
isitoshe hawakuwa wanakwenda kutoa kwenye madhabahu ya Mtume Petro ambayo ndio
alipo Mungu alie hai kilichowatokea ni kifo.Sadaka iliyo mbele za Bwana
isipozaa hairudi kama huamini muulize Kaini kama yeye alirudishiwa sadaka yake
na Bwana.Lakini sadaka ya Sauli ilikataliwa kabla ya kutolewa.
Wasaa wa kutoa
sadaka ni wakati wa appointment wewe na Mungu wako hivyo ni wakati nyeti mno na
wamakini sana wa kuzungumza na Mungu kupitia sadaka na kuweza kunyakua mahitaji
yako kwa Mungu.Apandae mbegu si kitu wala amwagiliae bali akuzae.Huwezi kununua
jibu la Mungu kwa sadaka bali jibu hupatikana kutokana na itifaki alioiweka
yeye.Usitoe sadaka kwa sababu mtumishi anashida bali mpe kwa sababu umepata
kibali hivyo Mungu atakujaza kila unachohitaji.Unapotoa sadaka usitoe kwa sababu unamsaidia Mungu maana
vyote viijazavyo ni mali yake.
FAHAMU UMUHIMU WA KUJUA UHALISI WA KUWEPO KWA ULIMWENGU WA ROHO
Ulimwengu wa roho upo tena ni halisi kama vile ambavyo ulimwengu wa kimwili upo na tena nao ni halisi!Mara tano mtume Paulo ansisitiza katika waraka wake kwa Waefeso juu ya ulimwengu wa roho ,kwa uzito ambao kila msomaji wa waraka huu atawekewa ndani ya moyo wake hamu zaidi ya yake kutaka kuujua ulimwengu wa roho.
Msisitizo huu unaupata unaposoma Waefeso 1:3,20 Waefeso 2:6 Waefeso 3:10 na Waefeso 6:12.Ukisoma mistari hii kwa kuunganisha utaisoma kama ifuatavyo:"Atukutuzwe Mungu ,Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni,katika ulimwenguwa roho ndani Kristo…..
….aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho akatufufua pamoja naye akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho katika Kristo Yesu ili sasa,kwa njia ya kanisa,hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho."
Je unauna msisitizo huu wa mtume Paulo juu ya ulimwengu wa roho ulivyo mkubwa?Unaweza kuona tu ya kuwa kiu aliyonayo katika kutufahamisha ,ni ili tuyajue sasa tukiwa katika mwiili mambo ya ulimwengu wa roho kwa lengo la kuutumia ufahamu huu kwa ajili ya ufalme wa mbinguni wakati huu!
Hebu tuiangalie na kuitafakari zaidi mistari hii inayohusu ulimwengu wa roho iliyomo katika kitabu cha Waefeso.Unaposoma Waefeso 1:3 unaona wazi kabisa ya kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya ulimwengu wa roho na baraka zote ambazo mtu anatakiwa azipate katika Kristo Yesu.Unaposoma maneno ya mistari ya Waefeso 2:5-10,utaona ya kua kuna uhusiano ulio dhahiri kati ya ulimwengu wa roho na:
- Mamlaka ambayo mtu aliyeokoka anakuwa nayo ndani ya Kristo Yesu-katika ulimwengu wa roho yanayodhihirika katika mazingira yake ya ulimwengu wa kimwili;
- Kutembea au kuenenda kwa mtu katika kusudi la Mungu alilokuwa ameumbiwa ingawa kusudi hilo lilikuwa limehaririwa na uasi(dhambi)
Unapoendelea kutafaakari mafundisho ya Mtume Paulo unakutana na Waefeso 3:10.Maneno ya mstari huu yanatuhimiza kujua juu ya huduma au jukumu la kanisa katika kutoa/kuijulisha hekima ya Mungu kwa falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho.
Hii ni dhahiri ya kuwa kanisa au mtu akiwa ndani ya Kristo au mtu alieokoka ana majukumu yaliowazi anayotakiwa ayaelekeze katika ulimwengu wa roho wakati bado yupo kwenye alimwengu wa mwili?Unanielewa mpaka hapo ?Huu ni ukweli usiofichika mtu ni roho,anayo nafsi,na anaishi katika mwili.Soma 1The 5:23
Kwa mantiki na uelewa huu tunajua ya kuwa mtu ameumbwa na anaouwezo wa kuishi katika ulimwengu wa roho na ulimwengu wa mwili kwa wakati mmoja hasa akiwa duniani kabla hajafa?Unaelewa nini mpaka hapo?Unaona nini katika misisitizo hii ya Mtume Paulo?
La Kwanza:Unaelewa na anaona ya kuwa ulimwengu wa roho ni halisi ambao tunaweza kuujua na pia tunatakiwa tuujue.
La Pili:Unaelewa na unaona ya kuwa ulimwengu wa roho una sehemu kubwa katika maisha ya kila siku ya mtu awe ameokoka au awe hajaokoka!
La Tatu:Unaelewa na unaona ya kuwa kuokoka kunampa mtu aliyeokoka hadhi kubwa,na thamani kubwa katika ulimwengu wa roho ambayo imefichwa kwa mtu isipokuwa macho yake ya ndani, au macho yake ya kiroho yawe yamefunguliwa apate kuona !
Kwa mfano:Si kila ushindani unaokutana nao kwenye maisha au vita unavyokumbana navyo mara kwa mara chanzo chake ni ulimwengu wa nuru.Biblia inasema kwenye Waefeso 6:11-13
"Vaeni silaha zote za Mungu mpate kuweza kuzipinga hila za shetani ,kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama bali juu ya falme na mamlaka,juu ya wakuu wa giza hili,juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu,mpate kuweza kushindana siku za uovu…"
Ni dhahiri kuwa ulimwengu wa roho ndio unaotengeneza maisha ya ushindani na upinzani,na vita ambayo unakumbana navyo katika maisha yako na kusababisha mafanikio yako yasiwe katika kiwango kinachotakiwa .Ukiunganisha maneno ya Waefeso 6:11-13 na yale ya Waefeso 6:18 utaona ya kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya maombi na ulimwengu wa roho na ile hali ya madhara ya upinzani na ushindani ambao mtu anasongwa nao kila siku katika maisha yake.
MGAWANYO WA ULIMWENGU WA ROHO
Ulimwengu wa roho una mgawanyo au umegawanyika katika maeneo mawili makubwa: Ulimwengu wa giza na Ulimwengu wa nuru.Ulimwengu wa nuru unajulikana zaidi kama ufalme wa mbinguni au mfalme wa Mungu.Ufalme wa giza unajulikana kama Ufalme wa Shetani.
Mungu alipomuumba mtu alimuumba ili awe sehemu ya ufalme wa nuru au ufalme wa mbinguni.Tena alihakikisha ya kuwa mtu akiwa kwenye ufalme wake au ufalme wa mbinguni awe pia na nafasi ya kiutawala na kiumiliki katika ulimwengu wa roho ili imwezeshe pia kimwili kumiliki na kiutawala katika nafasi atakayopewa katika ulimwengu wa kimwili!
Tunalifahamu hili kwa kuangalia na kusoma katika sura ya kwanza ya kitabu cha Mwanzo.Mtu alivyoumbwa kama tunavyosoma katika Mwanzo 1:26-27 aliumba roho yake tu.Maana yake ndio uliokuwa uumbaji wake wa awali wa mtu.Kwa tafsiri nyingine tulikuwa roho hapo tulipoumbwa kama naye Mungu alivyo Roho.Ili tuweze kuweza kuishi katika mazingira ambayo Mungu alishayaweka tayari aliamua kutufanya nafsi hai angali tukiwa roho tukiangalia Mwanzo 2:7 inatueleza vizuri habari hizi.
Kwa hiyo maagizo ya kiumiliki na kiutawala aliyopewa mwanadamu katika Mwanzo 1:26-27 yanaonyesha na kudhihirisha ya kuwa mtu alipewa awe na nafasi ya kiumiliki na ya kiutawala katika ulimwengu wa roho hata kabla hajapewa mwili na nafsi.Tunaposoma katika Mwanzo 1:26 Mungu akimwambia mtu yaani mwanaume na mwanamke ya kuwa wakatawale Na katika Mwanzo 1:27 anawaambia Zaeni mkaongezeke mkaijaze nchi na kuitiisha mkatawale
Mungu alipokuwa anazungumza nao juu ya kuitiisha nchi alikuwa anazungumzia juu ya mtu kumiliki nchi. Kumiliki ni neno lililotafsiriwa kutoka kwenye neno hili la kiingereza la dominion.Dominion lina maana ya utawala wa kifalme katika eneo husika ambao unampa mmiliki mamlaka ya kifalme yanayotolewa kwa kutumia usemi au neno la kifalme la mmiliki.
Tuko pamoja mpaka hapo?Ninalotaka ulione ni kwamba mtu alipoumbwa alipewa pia nafasi ya kifalme katika ulimwengu wa roho ili amiliki na kutawala akiwa katika ufalme wa Mungu.
NI MUHIMU KUJUA MKAO ULIOKUWA NAO ILI UWEZE KUTEMBEA NA MUNGU MAISHANI
Maendeleo ni magumu sana kwa watu hususani wakristo kwa maana wengi bado hawajatambua ni mkao wa aina gani waliokuwa nao,hivyo kushindwa kutambua mazingira na hususani nyakati wanazo[ita katika maisha yao.Nehemia 2:17 inasema Kisha nikamwambia mnaona hali hii dhaifu tulionoyo jinsi Yerusalemu ulivyo hali ya ukiwa na malango yake yalivyoteketezwa kwa moto haya na tuujenge tena ukuta wa Yerusalemu ili tusiwe shutumu tena.Nehemia alipojua kuwa walifanya makosa kwa kuoa wanawake wa Misri ndipo alllipowaeleza wenzie la kufanya (Ukisoma kuanzia ile sura ya pili)
Matatizo kutoisha miongoni mwa familia mbalimbali ni kutokana na kutokua na ujuzi maandiko yanasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.Kumbe ukosefu wa maarifa ni sababu kubwa ya watu wengi kushindwa maisha ikiwemo watanzania wengi pasipo kujali dini zao.Katika Waamuzi 6:13-14 tunaona Gideoni atambua kama Mungu yu pamoja nao mbona bado wako utumwani hivyo katika maisha yapo maswali ambayo unapaswa kujiuliza na mtu huweza kujiuliza tu kama ametambua mkao aliokuwa nao.Gideoni alitambua mkao waliokuwa ndio maana alifikia uwamuzi wa kujiuliza swali kama hili.
Mfano ni kwanini watu wanachoma makanisa,vijana wanaona kanisa ni uzushi, watu wanakesha kwenye mabaa lakini hawataki kukesha kanisani na pia watu wanachangia harusi lakini hawachangii michango ya kanisa kama ujenzi na kadhalika.Mathayo 19:16-22 Mtu mmoja anataka kujua jinsi ya kupata uzima wa milele.Unaposoma vizuri utagundua kuwa hapo awali walikuwepo watu ambao walikuwa na shauku sana kumfahamu Mungu na kutambua jinsi ya kufika mbinguni lakini watu wa leo hana bidii katika kumjua Mungu aliye hai.
katika maisha yako tamani kujua nafasi na kusudi la Mungu ambalo ameweka juu yako.Hivi sasa wewe ni mwanafunzi tamani kujua kwanini unasoma sio kukaa nyumbani bado swala hili ni changamoto kwa watu wengi maana wengi wanakwenda shule kwa sababu wazazi wao ni wakali hivyo kulazimika kwenda shule au wengine walipozaliwa waliukuta utaratibu watu wanaenda shule hivyo naye akaingia kwenye system.Sababu ya wanafunzi wengi wa vyuo kukosa kazi baada ya masomo yao ni kutotambua nafasi zao maishani.
Mtu yeyote ambaye ni mwombaji na anaomba kwa jinsi ya kibiblia anajua ya kuwa si maombi yote mtu ayaombayo yanajibiwa katika muda ule ambao alitaka yajibiwe!Pamoja na kwamba ungetaka yajibiwe haraka lakini yanapochelewa kujibiwa usikate tamaa na ukaacha kuombea jambo hilo!Yesu Kristo alisema juu ya mazingira kama haya ya kuwa "imewapasa kumwomba Mungu siku zote wala wasikate tamaa" Luka 18:1
Fikiria ingekuwaje kwa wana wa Israeli ikiwa Musa angekata tamaa kuendelea kuomba kwa sababu ya kutojibiwa haraka maombi yake kuhusu kubadili maamuzi ya farao juu ya utumwa wa wana wa Israeli! Lakini hakukata tamaa aliendelea kuomba na pia aliendelea kwenda kwa Farao kuangalia kama maombi yake yamejibiwa!Tunaposoma habari hii katika kitabu cha Kutoka 5:12 tunaona ya kuwa mazingira yaliyokuwepo wakati huo yalitosha kumkatisha tamaa Musa lakini tunaona hakukata tamaa!
Hatimaye maombi yake yalizaa matunda.Mungu aliingilia kati na Farao akaamua kuwaachia wana wa Israeli wasiondoke!Na mimi nataka nikutie moyo ya kuwa ikiwa bado ndani yako unasikia kuliombea jambo unalosubiri jibu lake maana yake hiyo ni ishara ya Roho Mtakatifu kukuambia endelea kuliombea jambo hilo.Ombea jambo hilo hadi usikie mzigo au msukumo huo wa kuliombea uliokuwa nao moyoni mwako umeondoka na unasikia furaha au uasikia uhuru fulani au unasikia raha nafsini.
Ukisikia hivyo hivyo ni ishara ya maombi yako kujibiwa hata kama kwa jinsi ya macho ya kimwili bado jibu halionekani.Kwa hiyo badala ya kuomba wewe shukuru juu ya kujibiwa maombi yako na endelea kushukuru hadi jibu litakapotokea kwa jinsi ya mwili.Usikubali hali ya kukata tamaa iingie ndani yako wakati Mungu wako anatawala katika kiti cha enzi kama Mungu wa mbingu na nchi!
SIJUI KAMA UNAFAHAMU UMEITWA NA BWANA ILI UWE MWOMBAJI
Maadamu una nguvu sijui kama unatambua Mungu amekuita ili uwe mwombaji na si tu wa matatizo yako bali wa wote . Kwa maana gani Mungu amekupa nguvu wewe ili ukawe msaada kwa wengine ndio maana wewe hauko ICU wa hodini bali upo mitaani kusudi lako kuwepo mitaani sio kutimiza idadi ya watu waliopo mtaani bali upo ili kuwa msaada kwa wengine nillikupa mfano wa wagonjwa lakini tambua ipo serikali,taasisi na kanisa linahitaji maombi yako bila wewe kuambiwa kama wanataka maombi yako . Yak 4:16a Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi na kuombeana mpate kuponywa.Kumbe tumewekwa katika utegemezi katika mambo yote ikiwemo maombi ndio maana Paulo anasema sisi tu viungo.
Hivi uliwahi kufikiri kwa nini ukipata shida unataka maombi ya watu lakini wewe usijapokuwa na shida huna sababu ya kuombea wengine?1Kor 4:1-2 Inasema Mtu na atuhesabu hivi kuwa tu watumishi wa Kristo na mawakili wa siri za Mungu.Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili ndio mtu aonekane kuwa mwaminifu. Uwe na uhakika kama umehitajika kuwa mtumishi huna budi kukaa kwenye maombi kama neno linavyokusukuma ili upate kuwa wakili mara nyingi watu wengi huhesabu habari za uwakili kwa matazamio ya sadaka kama kanisa la leo lizamavyo lakini uwakili ni maisha yako yote.
Unaposema kuwa wewe u Mkristo maana yake u mtumishi wa Kristo na mtumishi wa Kristo kama maadiko yanavyotuambia kwenye 1Kor 4:1 na hutumika kwa jinsi ambavyo Yesu alivyoagiza ikiwemo uwajibikaji kwenye maombi.Hivi uliwahi kufikiri kuwa kuna mambo ambayo hayaendi vizuri ya nchi ukamnyoshea kidole rais,mambo haendi vizuri shuleni ukamnyoshea kidole kiranja au mambo yaliwahi kuharika mahali ukamtuhumu mwenzako naami haya yote uliwahi kuyapitia bali hukupata kufahamu kuwa mambo yakiharibika chanzo ni wewe maana hukusimama kwenye zamu yako?Maana uliitwa utumike kwa ajili ya wenzako.
Leo hii wapo waliovitandani,wasafiri,waliokata tamaa,waliofiwa,waliokataliwa na wengineo wengi wote hawa wanahitaji maombi yako.Ndio maana wewe ni mzima hivi leo.Ndio maana wewe nilikuambia kuwa ukipata matatizo wewe unakimbilia kuombewa mbona wewe hukutakusaidia wengine kama hao wao ambao wanauhitaji kama wako wakati ulipokuwa mhitaji?Hivyo natamani ujijengee dhana ya kuombea wengine ikiwemo na Israeli.
Mt 24:42 maandiko yanasema kesheni basi kwa maana hamfahamu siku ipi atakayokuja Bwana wenu.Najua swali la haraka ambalo utajiuliza ni kwamba tukeshee nini lakini jibu tunapata kupitia Mt 26:41 maandiko yanasema, Kesheni, muombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.Miili yetu ni dhaifu ndio maana twahitajika kuomba ili kila wasaa tukae kwenye kusudi la Mungu .Kama andiko linavyosema tunagundua kuwa tunaanguka kwa sababu miili yetu ni dhaifu hivyo basi Mungu anahitaji uombe kwa ajili ya wengine ambao ni wazuri lakini wameanguka kwa udhaifu wa mwili,mfano mtu mdhinifu.
Ngoja nikuulize je shetani anakula?analala?anavaa?Bila shaka jibu lako ni hapana basi kama ni hapana maana yake kazi yake ni moja tu kukuwinda wewe si usiku si mchana,ndio maana sasa Mungu anakuhimiza umuhimu wa kukaa kwenye maombi ili uweze kumshinda kweli maana yeye hutumia muda mwingi kwenye agenda moja angali wewe unazo agenda nyingi kushughulikia kwa wakati mmoja.Lakini kupitia maombi waweza kusimama.
Mt 24:20 inatuambia Ombeni ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi au wakati ya sabato.Maana yake usijijengee dhana ya maombi ya zima moto bali uwe na maombi ya mfululizo katika maisha yako hata kufa jitahidi.Maombi ya zimamoto yalimgharimu Petro.Aliambiwa na Yesu utanikana mara tatu Yesu akifahamu kuwa Petro ataomba maana anayofursa ya kubadili hali hiyo bali Petro aliishia kulala hata Yesu alipomchukua kuomba pale kwenye Milima ya Mizeituni na matokeo yake ya kuanguka yakaanza mara tu baada ya Yesu kujiliwa na Jeshi la Mafarisayo ambapo alimkata sikio mtumwa wa Kuhani Mkuu yaani Kayafa na hapo baadae kumkana mara tatu kama Yesu alivyosema.
MAMBO YANAYOMFANYA MTU AWE NA YESU ALIYENYAMAZA NDANI YAKE
SIJUI KAMA UNAFAHAMU UMEITWA NA BWANA ILI UWE MWOMBAJI
Maadamu una nguvu sijui kama unatambua Mungu amekuita ili uwe mwombaji na si tu wa matatizo yako bali wa wote . Kwa maana gani Mungu amekupa nguvu wewe ili ukawe msaada kwa wengine ndio maana wewe hauko ICU wa hodini bali upo mitaani kusudi lako kuwepo mitaani sio kutimiza idadi ya watu waliopo mtaani bali upo ili kuwa msaada kwa wengine nillikupa mfano wa wagonjwa lakini tambua ipo serikali,taasisi na kanisa linahitaji maombi yako bila wewe kuambiwa kama wanataka maombi yako . Yak 4:16a Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi na kuombeana mpate kuponywa.Kumbe tumewekwa katika utegemezi katika mambo yote ikiwemo maombi ndio maana Paulo anasema sisi tu viungo.
IMANI KATIKA KANISA LA BWANA
Katika kanisa Imani imegawanyika katika makundi mawili.
- Imani ya Hamasa au Kuhamasishwa
- Imani ya Kujengwa
Imani ya Hamasa au Kuhamasishwa
Mtu anapookoka moja kwa moja anapokea Imani ya kuhamasishwa au hamasa Mdo 2:38-39.Hii ni kwa sababu alipokwenda yamkini kwenye mkutano wa Injili,semina au fellowship hakuwa amepanga kuwa anakwenda kuokoka bali kile kinachotokea ni kwamba wakati yupo kwenye semina au mkutano wa Injili anajikuta neno linamchoma na kuamua kumkabidhi Yesu maisha yake.Na tendo hili hufanyika katika roho ya mtu kwa maana gani?Maswala mengi ya kiroho yanayofanyika kwa haraka pasipo kufikiria huwa hayahusishi akili.Ndio maana mtu anapookoka anapata msukumo ambao sio wa kawaida ndani yake.
Imani ya hamasa ni imani ya dharura huwa haidumu Roho Mtakatifu anamgajawia kwa wakati huo maana kuna uhitaji wa haraka ili usipotee.Na mara nyingi sio lazima huyu ambaye amepata imani ya hamasa aelewe anachoamua kukiamini bali kile kinachotokea ndani yake huwa anapata msukumo ambao hakuwa wahi kuwa nao kwa kawaida na kumpelekea kuamini kwa sababu hiyo roho ina ugonjwa wa kufisha ambao mtu hawezi kuujua maana hu mdanganyifu.
Imani hii ya hamasa huwa haidumu kwani hukaa kwa kitambo tu baadae hutoweka.Tambua kuwa wakati mtumishi anahubiri nguvu za Mungu zinapita kupitia neno la Mungu na maombi yanayofanyika hivyo kupelekea upako kushuka mahali hapo na kugusa watu nakupelekea mioyo wa watu kulainika maana Mungu naye ni Roho kwa hiyo roho ya mtu huwasiliana moja kwa moja na Mungu kwa itifaki ya mawasiliano yaliopo na kumfanya mtu amini kuwa yeye ndiye.Kutokudumu kwa imani hiyo pia hupelekewa na mabadiliko ya mazingira.Wakati unaipokea hiyo imani ulikuwa kwenye uwepo wa Mungu unapoelekea nyumbani unakutana na uwepo wa nyumbani ambao haufanani na uwe wa kwenye semina au mkutano wa Injili na si tu nyumbani yamkini kazini au shuleni.
Lengo la kuwepo kwa Imani ya hamasa.Imani ya hamasa ipo kwa sababu ya matukio ya haraka Mdo 2:41.
Imani ya Kujengwa
Ni imani inayokuja kwa mtu kupitia mtu kulielewa jambo na kubadilika fikra zake.Imani hii huanzia akilini kwani mtu hupambanua anachoelezwa na kuamua kufanya maamuzi.Mazingira ya nje hayahusishwi .Katika Imani ya kujengwa kitu kikubwa ni uelewa ni si hamasa kwa maana gani huyu mtu alikwisha kupata hamasa pale alipookoka na anachohitaji ni darasa la kile kilichomfanya aokoke Mdo 2:42.
Imani ya kujengwa ina majibu ya muda mrefu maana yake sio tomato ya mchina iliyokuwa na expire date.Imani ya hamasa inaweza kumgharimu mtu afanye safari mpaka kwa mtumishi kwa ajili ya maombi.Kwa sababu huyu mtu hajajua bado kuwa anaweza yeye mwenyewe akafanya maombi na kupokea.Hivyo mtu wa jinsi hii akikaa kwenye mafundisho ni rahisi kuelewa na kuondokana na wokovu wa utumwa.
Vichochezi vya Imani ya hamasa
- Maombi hasa ya vita
- Upako
- Kufunga
Si vibaya kufanya maombi ya vita ,kuwa na upako na kufunga sana lakini ukikosa neno ukawa unafanya hivi hata uaminifu bado utakuwa na imani ya hamasa.Rum 10:17 inatuambia imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la Mungu.Kwa maana hiyo haijalishi ni mfungaji kiasi gani kama huna neno ndani yako bado imani yako ni ya hamasa.Mtu anapokuwa na upako anakuwa na imani ya kuchochea na kitu kinachochochewa maana yake kitu hicho kina wakati wa kuzimika.Hivyo kubaki na imani ya hamasa humfanya mtu awe Mkristo wa kuchovya na si original maana waweza kuyumbishwa usipokuwa na Imani yakujengwa.
Vichochezi vya Imani ya kujengwa
- Kusukuma neno kwa wingi
- Mafundisho
- Kusoma vitabu vya kiroho
Mt 8:5-13 utagundua kuwa yule Akida alitambua kuwa Yesu kumjia mgonjwa wake haina maana sana lakini imani ya kujenga iliokuwa ndani yake ilimsukuma yule Akida kumwambia Yesu aseme neno tu naye mgonjwa wake atapona.Neno ni Yesu mwenyewe akiisha tambua hayo akaona vema kupata neno na si Yesu kwenda kwake maana hatahivyo yeye hastahili kuingia kwake.Neno ni mchujo wa andiko.Wengi wanasoma andiko na si neno.Kwa mfano Gal 3:1-5 wengi hutafakari vibaya neno hili kwa sababu bado wana imani ya hamasa na kupelekea kukosa ufahamu juu ya ukweli wa neno hilo.
Wajenzi wa Imani ya hamasa
Mara nyingi ni wainjilisti au wahubiri.Mfano mwinjilisti aweza kutumia neno moja kuinjilisha kwa muda mefu akisisitiza neno hilo hilo.Na mara nyingi hutumia mikutano ya Injili au ibada kufanya hivyo
Wajenzi wa Imani ya kujengwa
Mara nyingi mjenzi ni mwalimu.Yeye hutumia semina kupeleka ujumbe.Huwezi kutumia mikutano ya Injili kupeleka neno.
Angalizo wajenzi wa hamasa wana umuhimu usije ukawachukia.Hao Mungu amewaweka ili kukusaidia wewe ndugu yangu ukue kwenye Injili.Ili uweze kufika kwenye imani ya kujengwa lazima upitie imani ya hamasa ndio maana hao wapo kukusaidia wewe.
MAMBO YANAYOMFANYA MTU AWE NA YESU ALIYENYAMAZA NDANI YAKE
Yamkini umeokoka lakini udhirihisho wa Yesu ndani yako hauonekani.Hivyo kupelekea mtu kuteswa na kunyanyasika unaweza ukakuta hata mapepo wanamtesa huyo mtu lakini ameokoka.Kuna mapepo ambayo Yesu ni ngumu kwake kuyatoa lakini si kwamba hawezi kuyatoa,hii ni lugha ngumu kidogo.Katika moyo kuna kiti ambacho hukaliwa na watu wawili ambao ni Mungu ama shetani lakini mamlaka ya kukaa ya Mungu ama shetani yapo kwa Mungu mwenyewe.Hivyo kukaa kwa shetani ndani mtu humfanya Yesu ashindwe kumtoa pepo ndani ya mtu huyo.Isipokuwa mmiliki wa kiti kuwa na ridhaa ya kutoa huyo pepo kwa maana hii kama mtu angemruhusu Mungu akalie hicho kiti maana yake angempa fursa ya kutoa huyo pepo.Ukisoma Ufu 3:20 anasema tazama nasimama mlangoni nabisha mtu akisikia sauti yangu na kufungua mlango nitaingia kwake na kufanya makao mimi na Baba.
Kuna mambo ambayo humfanya mtu kuwa na Yesu asiyesema
- Kumfahamu shetani zaidi kuliko Mungu Gal 4:7
Sisi akili yetu inamwona shetani kuliko Mungu hatukupewa wokovu wa utumwa bali wa uhuru.Mtu akisikia mtu anakanyaga bati la nyumba usiku anahisi uwepo wa shetani na kisha unaanza kukemea lakini neno la Bwana linasema malaika wa Bwana hufanya kituo akiwazungukia wote wamchao na kuwaokoa.Yamkini ni malaika ndio anatembea juu ya bati lako.Wakati mwingine unaweza ukatishwa na mikataba ya kuzimu lakini fahamu kuwa uweza wa Mungu nani yako una nguvu. Watu wanajengwa kwenye misngi ya kumuogopa shetani na sio MUNGU. Biblia inatuambia tuvae silaha za mwili ili tuweze kuzishinda hila za shetani, lakini wakristo wanashika silaha badala ya kuvaa silaha. Penda kumjua MUNGU kuliko kumfahamu shetani.
- Ukosefu wa Imani Ebr 11:1
Imani ni kuwa hakika ya mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasiyoonekana. Imani katika kanisa sehemu tatu(3) Mt. 8:23-27, Imani haba,waliopoteza imani na ambao hawana imani. Imani inahusisha mambo yafuatayo; Kuhama,hisia na mawazo. Kuhama ni kupelekwa kwenye ulimwengu wa roho japo upo kwenye ulimwengu wa mwili yamkini unatamani uhame kwenye ulimwengu wa mwili lakini unashindwa kuingia kwenye ulimwengu wa roho kwasababu umekwingwa au miunombinu ya kiroho imeharibika, miundombinu hiyo ni akili,roho,hisia N.K. Hivyo kupelekea kumkwamisha roho mtakatifu kupita ipasavyo lakini unaweza kutengeneza hiyo miundombinu kupitia kidonge cha Lk 3:4-6, Mt.4:5-6, shetani anamwambia YESU ajitupe chini akiwa na maana imani ya YESU itakua kama yake kwani alijua imani ya YESU ni kubwa hivyo kwa kijitupa kwake kungemfanya imani yake ipungue kama yake.
- Kufanya huduma ya mazoea, haiwezekani mguu wako uwe mbovu halafu ukacheza rafu huduma ni kujipanga lazima uwe na nidhamu ya hali yako kwa maana ya imani ya kiwango ilchonacho isizoee kutumika kwako leo kuwe hivyo hivyo kila siku kwani MUNGU hubadilika kutokana na mazingira, yamkini leo akakupa ufunuo wa maji na kesho akakupa wa mafuta. Mara nyingi hii imeleta shida sana hususani kwa watumishi ambayo wameinuka kwa fikra zao batili wasiweze kufundishwa na kuhekimishwa yote.
- Kutokufanya toba halisi
Toba ni maungamo ya dhambi zako mbele za Mungu. Zab 51:1-19 tunaona toba ya Daudi mbele za Mungu.Toba hutakiwa kuwa na mwelekeo yaani direction. Mwelekeo huo ni ule uendao mbele .Toba inahusika na vitu vitatu navyo ni nafsi,mwili na roho pia. Lakini roho ndio huwa ya kwanza kuokoka.Ndio maana mhubiri akisema nani anataka kwenda Mbinguni kila mmoja atasema kuwa anataka kwenda.Lakini chachu ambayo huweza kuwafikisha huko ni ngumu kwao kuenenda nayo ili kufika huko.Hii ni sababu roho zao zinautayari lakini miili yao haiko tayari Mt 26:41.Ili mtu huyo akae vizuri Mungu anafanya pairing yaani uahinisho wa roho ya mtu huyo na mwili wake ili mwili afanane na roho kwa kupitia hamasa ambayo humpa mtu kukaa katika maombi,kufunga na neno lake lakini hutumia gharama kubwa wakati mwingine kukuletea watumishi toka mbali kukuinjilisha.
- Maisha ya desturi
Ili Yesu afanye kazi ndani ya maisha yako na aonekane lazima uondoe dhana nzima ya mazoea.Kwa mfano unakuta mwanafunzi anafeli kila wakati na wenzake kufaulu anaona ni sawa.Hii inajitokeza katika mashule mpaka kuwajengea wengine kuona kuna watu walizaliwa wafaulu na wengine kufeli ili kuwapa vichwa na baraka zote wanaofaulu wazidi kufaulu na wasipite katu wanawaita ' T.O ' wasijue kuwa Mungu hata wao aliwapa u 'T.O' hivyo hiki ni kitu kibaya lakini mzizi wa fitina ni mazoea yaliojengeka.Lakini kumbe angetambua kuwa hata wao wanauweza kama wao lakini walichokifanya ni kumzimisha Yesu ndani yao afiwafanyie kama wengine kutokana na imani iliyojengeka kwao.Au wanafunzi wa shule za kata wanawaona wanafunzi wa shule za private kuwa wanaakili atakama huko shuleni kwao ni wa mwisho.
Ili Yesu aliye ndani yako azungumze yaliopo hapo juu ni muhimu uyazingatie.Wakati mwingine unaomba huoni matokeo.Utagundua kabisa kuna uhusiano mkubwa wa tafakari hii na imani.Rum 10:17 Inatueleza imani huja kwa kusikia na kusikia huja kwa neno la Mungu.
KUOKOKA SI KIGEZO TOSHELEVU KUKUFANYA UFIKE MBINGUNI
Mara nyingi tumekuwa tukitumia neno nimeokoka kama kigezo cha kuonyesha kuwa sisi ni tu watu wakwenda mbinguni bila kuwa na uhakika kama mbinguni tutafika.Ngoja tumtazame Musa nawe utagundua Mungu anachojaribu kukufikirisha
Musa alikuwa nabii wa kwanza na mtu mpole na binadamu pekee aliyekuwa akiongea na Mungu ana kwa ana lakini tukisoma Hes 20:7-13 Tunaona Mungu akizungumza na Musa na kumpa maelekezo kama maandiko yanavyoeleza kuanzia aya ile ya nane. Kulikuwa na maelekezo matano kama yanavyoelezwa katika aya ya nane.Lakini Musa katika maelezo hayo alifanikiwa kutekeleza baadhi kama Hes 20:9 inavyoeleza lakini mengine alishindwa kutekeleza.
Hes 20:10b Musa na Haruni wakasema "Sikieni enyi waasi ; je! tuwatokezee maji katika mwamba huu?Utagundua Musa alitumia kauli ambayo Mungu hakumwagiza atumie "Sikieni enyi waasi" kama Hes 6:22-27 ilivyoeleza. Pili akasema "Tuwatokezee maji katika mwamba huu?"Mungu ndiye aliyemwambia Musa akatoe maji na si yeye Musa aliyekuwa na kibali cha kuwatolea wana wa Israeli maji. Tatu Musa alipiga mwamba mara mbili badala ya mara moja kama Hes 20:11 hivyo alikosa imani na kupelekea kupiga mwamba huo mara mbili.
Katika maneno ambayo Musa aliwaita wana wa Israeli enyi waasi alikuwa akiwadharau wana wa Israeli. Asikumbuke hata yeye aliua mtu kule Misri.Hili lilikuwa kosa lake la kwanza.Maneno yale ya pili yalioandikwa katika Hes 20:10c yalionesha kujiinua kwa Musa ukikumbuka yeye aliamriwa na Bwana lakini akawaambia Wana wa Israeli atawafanyia yeye na Haruni.
Katika Hes 20:11 Musa aligonga mwamba mara mbili mara na ilimbidi agonge mwamba mara moja hii ili onyesha kukosa kwake imani kama Hes 20:12a inavyotueleza.Kwa hiyo utagundua alikiuka maeneo matatu.Mungu akamwambia kama maandiko yanavyosema katika Hes 20:12 kuwa yeye na Haruni hawataingia katika Kanani.
Lakini hebu jaribu kufikiri Mungu aliamua kumpa Musa uongozi wa kuwatoa Wana wa Israeli utumwani kuwapeleka Kaanani,lakini hivi baadae anabadilisha mtazamo alioweka kwa ajili ya Musa. Kumbuka Musa alikuwa mtakatifu lakini hakuweza kukamilisha kusudi la Mungu.
Tazama mambo madogo matatu tena yaliohusisha ulimi na tendo ambayo sio rahisi ukafikiri kuwa Mungu angebatilisha mtazamo wake, yalitosha kumzuia Musa kuendelea kuwaongoza Wana wa Israeli mpaka Kanani. Na hatimaye Musa kuishi kuiona Kanani kwa picha ambazo Mungu alimletea maana Mungu bado alikuwa akimpenda kwa utumishi wake ulio tukuka.
Sasa tazama wewe unayesema umeokoka halafu uongo kukujaa, masengenyo kwa wingi, unafiki tele na anasa kukumbatia je! waweza kupona katika siku hiyo?Ngoja nikueleze safari ya mbinguni si lelemama kama unavyofikiri Musa alikuwa mteule wa Bwana lakini hakufanikiwa kukamilisha kusudi la Bwana.
Ngoja nikukumbushe Musa ni kati ya watu ambao walifunga siku 40 bila kula kama biblia inavyoeleza. Hivyo Mungu anatamani ufahamu jinsi gani Musa alivyojitoa kwake lakini alishindwa kumaliza kusudi lake.
Sasa sisi tunaosema kuwa tumeokoka lazima uhakikishe uwe unamaanisha mwili na roho. Siku hizi tumeokoka roho angali mwili bado na kama mwili bado kuingia mbinguni bado hakupo. Kwa sababu mtu yuasema ameokoka halafu ni mlevi,mzinzi,fisadi na msengenyaji. Furaha iweze kutimia lazima mwili nao uokoke
Najua mtu atajiuliza sasa mwili unaokoka vipi?Majibu ndio haya kwa kufunga , kusoma neno la Mungu na kuomba Fil 4:2.Kombination hii huufanya mwili kuokoka na kwa haraka sana.Mungu akutie nguvu sana
KUFUNGULIWA UFAHAMU
Maarifa hayaji pasipo kukaa darasani. Ili uweze kuwa na maarifa penda mafundisho maana huwezi kupata maarifa kama hujapata mafndisho Mit 12:1-2. Mtu yeyote ambaye ufahamu wake haujafunguliwa atatumia nguvu zaidi.Ndio maana biblia inasema enenda na wenye hekima nawe utakuwa na hekima .Umaskini uliopo Tanzania unasababishwa na kukosa maarifa.Kanisa la leo lina Yesu lakini limeshindwa kumtumia kwa sababu ya kukosa maarifa.Ujinga hauondoki kwa kufunga na kuomba. Hakuna kitu kibaya kama kufanya vita bila maarifa. Kwa kadiri ufahamu wako ulivyofunguka ndivyo Mungu atakavyokutumia.Ni kweli tunampenda Yesu lakini tatizo ni kukosa ufahamu juu ya Yesu tulienae ndio maana hakuna matunda katika maisha yetu.
Chochote usichokuwa na ufahamu nacho hata utumie nguvu hutafanikiwa nacho. Unaanzisha biashara inakufa unamkemea shetani kumbe tatizo si shetani bali huna ufahamu.Biblia inaahadi 3000 sasa mbona sisi tu maskini?tunateswa na mapepo?watu wanafeli?ndoa zinavunjika?Kumbe utakubaliana nami ukosefu wa ufahamu ndio tatizo.Maarifa ya roho ni nguvu ,hatumiliki kwa sababu ya nguvu bali kwa sababu ya maarifa.Kuwa na maarifa ni jambo muhimu wakristo wengi hawataki maarifa bali wanataka maombi tu.Sisi hatupendi kusoma biblia ndio maana hatuwezi kupata uelewa.
Wenye maarifa ndio wanaofanya vitu vipya mfano Mwafrika wa kwanza ndio aliweza kutengeneza simu mara baada ya kuanza tangu 2006.Isa 5:13-14 Watu wanakuwa mateka kwa sababu hawana ufahamu.Watu wanateswa wanaangaika na mateso mpaka kufika eneo la kuyazoea kwa sababu wamekosa ufahamu.Kinachobadilisha maisha yako sio andiko bali ni ufunuo wa andiko kwa maana gani biblia inasomwa na wengi hata wasiomwamini lakini hawana uzima kwa sababu hawapati ufunuo wa wanachokisoma.
Kuwa mateka wa kiroho au wakimwili humfanya mtu kukosa maarifa.Tanzania kuna wahubiri wengi lakini hakuna waalimu wengi.Na hii sawa hata katika nyanja ya elimu ya nchi wanafunzi ni wengi lakini wakufunzi ni wachache hivyo kuwafanya wengi kukosa maarifa kwa watu wengi.Mdo 2:42 Kanisa la kwanza walidumu katika mafundisho lakini kanisa la leo ukizidisha muda wa neno la Mungu wanakukasirikia.Halafu wanapenda mahubiri kuliko mafundisho.Unajua kazi ya mahubiri ni kutoa hamasa.Hii hufanyika sana kwa ajili ya watu wanaotaka kuokoka hususani kwenye mikutano ya Injili.
Watu weni wanashirika na kanisa lakini hawana shirika na Yesu matokeo yake ni nini anaumia huku anafurahi kumbe anateseka.Zab 119:11 Daudi anasema moyoni mwako nimeliweka neno lako nisije nikakutenda dhambi.Daudi alijua kuwa namna pekee ya kuendelea kuhifadhi uwepo wa Mungu ndani yake ni kuliweka neno la Mungu ndani yake huu ni ufahamu aliokuwa nao Daudi juu ya mahusiano yake na Mungu.
Watu hufunguliwa kwa kusikia Yn 8:31 na kinachowafanya wafunguliwe ni nini hata wafunguliwe?Unaweza kujijibu wewe mwenyewe kuwa ni ufahamu.Sikiliza ukijua kuwa kwa kupigwa kwake umepona huwezi kungoja kumtafuta mtumishi kama ukiwa mgonjwa maana unaifahamu kanuni ya utoaji.Neno ni roho tena lina uzima Yn 6:23 maana Mungu hulituma neno lake ili upate kupona. Rum10:17 Imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la Mungu.
Hakuna uponyaji wa kweli usio ambatana na neno la Mungu.Matatizo ulionayo yataisha kwa kusikia neno la Mungu maana huliangalia neno lake ili kupata kulitimiliza kama u mgonjwa na amesema hakuna mwenyeji atakaye kuwa mgonjwa kama asemavyo Isa 33:24 hutangoja uhubiriwe maana umekwisha jua namna ya kusuluhisha tatizo.Uponyaji namba moja ni ule wa ndani,maana mambo yakikaa vizuri ndani na nje atomatically kutatengenezeka .
Yn 8:31-32 Utaifahamu kweli na hiyo kweli utakuweka huru.Kweli ya Mungu unayoifahamu ndio itakayo itakayokuweka huru.Ufahamu wako kwa jinsi unavyofunguka ndivyo unavyosogea mbele.Paulo anasema hawazi tena kama zamani.Namna ya kufikiria kwako ulopokuwa darasa la saba hakufanani na utakavyofikiri kama kidato cha nne.Ni kweli wewe ni mkristo tena una biashara lakini huna ufahamu wa kuendeleza unaelea kwenye mawazo ya wengine na si ya kwako.
Kuna kweli za duniani na shetani pia maana watu wanaambiwa duniani hakuna watakatifu duniani wao wako mbinguni lakiniZab 16:3 inasema Watakatifu waliokuwepo duniani hao ndio bora ninao pendezwa nao.Sasa kama anasema anafurahishwa na watakatifu inakuwaje watuambie duniani hakuna watakatifu.Hii inasababishwa na ukosefu wa ufahamu wengi hawasomi biblia na kwa sababu kasikia mtu akisema anakuambia imeandikwa.
Shetani ndo baba wa uongo na Yesu ndio baba wa kweli.Kuna kweli nyingine zinakufanya wewe uwe mtumwa mfano kweli ya mganga una matatizo halafu anakuambia jirani yako hakupendi ndio chanzo ni kweli mligombana kwa kitu kidogo bali yeye anatumia hicho kigezo kulinganisha na matatizo ulikuwa nayo.Huku nawe ukiona ni kweli kupenda yeye atafuta kula nyama hajala yapata miezi kadhaa.Halafu unaambiwa kalete mbuzi mwekundu na kuku wa bluu.
Madaktari nao wana kweli yao inafika wakati wanakuambia huna ugonjwa hii ni kweli vifaa vyao na maarifa yao ya kidaktari yanaishia hapo lakini ipo kweli ambayo huendelea pale wengine wanaposhindwa kuendelea.Na hii ndio moja wapo ya kanuni ya maarifa ya Mungu.Wanasayansi wafikia mwisho wa mawazo yao wananeno wanapenda kutumia linalosema "nature".Rahisisha maisha yako kwa kuondoa ushamba.
Hos 4:4-6 inasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.Hata sadaka inahitaji elimu ili uweze kuitoa kwa ukamilifu wote .Situ sadaka hata neno lake linataka elimu ili uweze kulitumia maana watu wengi husoma andiko lakini hawapokei mabadiliko ndani ya nafsi zao.
Sikiliza haiwezekani gari limeharibika ukalipeleka kwa seremala.Hivyo basi maisha yako yameharibika mpelekee Yesu ayatengeneze.Huwezi huru kiroho na kimwili kama huna maarifa ya Mungu Mith 11:9. Huponi kwa sababu ya maombi bali kwa sababu ya neno la Mungu,unaposikia neno la Mungu unafunguka.3Yoh 1:2 Maandiko yanasema mafanikio yako yapo katika roho yako.Ufahamu wako ukifungwa ni ngumu kufanikiwa katika eneo lolote katika maisha yako.Ayu 17:4.Ufahamu hukufanya uafanikiwe. Maeneo ya ufahamu ni uchumi,fedha,mambo ya kiroho,mambo ya ndoa na utumishi.
Vifungo moja wapo vya kiuchumi ni matumizi mabaya ya pesa.Hii ni roho ya kutapanya.Na hii ni roho ambayo haina utaratibu wa kukusanya.Ukipata pesa inakuletea mahitaji ambayo wakati haukuwa na pesa haukuwa nayo.Mfano unapata msukumo wa kula kitimoto.Kuwa tajiri lengo la kuwa na mipango na sio swalala kuwa na mali.Mtu asiye na malengo huongozwa na pesa na mara nyingi huwa hawana utulivu.Pesa inakwenda kwa mtu mwenye utaratibu nazo na wenye nidhamu nazo.Tatizo sio kuwa na mali bali hata hiko kidogo namna gani unaweza kukitumia kukutoa mahali ulipo.
Ndugu yangu huna nafasi nyingi za kufanya maamuzi bali leo fanya hiyo hatua sasa ili usiwe mtumwa tena bali mshindi daima.
TAFUTA KIBALI KWA BWANA KWANZA MENGINE UTAZIDISHIWA
Kama isemavyo Mw 37-42 Yusufu aliyekuwa mtoto wa mwisho katika familia ya Yakobo naye alionyeshwa kukubaliwa na Bwana alipokuwa angali mdogo lakini nduguze yaani waliomtangulia kama kaka zake walimchukia kama isemavyo Mw 37:1-9. Sababu ni kuoteshwa ndoto juu ya maisha yake ya baadae na jinsi Mungu atakavyomwinua lakini yeye hakuwachukia akizidi kutafuta kibali kwa Bwana juu ya ndoto hizo alizooteshwa.
Siku moja Yusufu aliagizwa akawaangalie nduguze lakini kwa sababu kaka zake walikuwa na kinyongo juu yake wakaazimia wamuue maana walijua atakuwa juu yao. Lakini kwa sababu alikuwa amepata kibali kwa Bwana Mungu akasema na kaka yao Yuda wasimuue bali wamuuze kwa Wamidiani Mw 37:21-28.Hivyo utaona mkono wa Mungu ulikuwa juu yake. Unapopata kibali mengine si tatizo kama Yusufu alivyookolewa katika kuuwawa.Huu ni mfano tu lakini ni zaidi ya mengi.
Wengi tunataka uponyaji lakini hatutaki kibali, ndio maana wengi twapenda kuombewa na si kuomba. Ngoja nikueleze ukitafuta kibali Mungu anashuka kwako. Wamediani walimuuza Yusufu kwa Potifa naye alipata kibali nyumbani pale hata Potifa akamwamini kiasi cha kumwachia nyumba yake na mali zake zote Mw 39:1-6. Unajua unapopata kibali kwa Bwana haijalishi uko wapi ,kwa wakati gani na kwa mazingira gani.
Watu wengine twatafuta mvuto kwa watu anasa na mali nyingi pasipo kutafuta kibali kwa Mungu. Naye Mungu alitaka kutufundisha kuwa tunapokuwa upande wake hatuna la kupungukiwa.Ngoja kupe mfano ukisoma Lk 5:1-11 utakutana na mtu anayeitwa Petro huyu alikuwa akitafuta samaki usiku kucha asipate kitu lakini Yesu alipokuja alikuwa akitafuta mahali pa kusimamia kama jukwaa kwa ajili ya kufundisha naye alipanda chomboni mwa Petro kumbuka hili Petro alikuwa na kila sababu ya kukataa lakini aliacha uwepo wa Bwana ufanye kazi na hii ilimfanya Yesu asiondoke bure akamwambia Petro shusha nyavu.
Hivi leo kama utamruhusu Yesu hatakuacha bure kama alivyo mwambia Petro ashushe nyavu.Usiku kucha Petro hakupata samaki lakini aliposema Bwana Yesu samaki walijileta wenyewe.Swali utakalojiuliza hawa samaki walikuwa wapi muda wote.Ngoja nikupe jibu mgomo kwa wanafunzi haukuanza leo bali ulianza toka zamani.Samaki waligoma kuingia kwenye nyavu kwa sababu kabla ya Yesu kuja Petro hakupata kibali bali alipomruhusu Mungu samaki walisikia sauti ya Yesu na kuelekea kwenye nyavu
Hivyo tunajifunza kuwa kusoma sana na kuacha kumpa Yesu maisha hakusaidii na ndiyo maana wanafunzi wengi wanapata shida wakifeli wakati wanasoma sana. Ngoja nikueleze hata maksi pia zimekugomea kwa sababu Yesu hajaruhusu kukujia maana hukumpa kibali. Lakini hata Petro baada ya kupata samaki wengi aliwaalika wengine maana yake hakuwa mchoyo na uwepo wa Mungu ndani yake.
Hatimaye akamwambia Yesu ondoka kwangu maana mimi ni mwenye dhambi uliwahi kujiuliza kwa nini anafikia hapo hii ni sababu anajua kuwa Mungu hakuwa upande wake kwa kipindi kirefu na sasa amegundua ukisoma Lk 5:1-11 hata wale samaki aliopata hakungoja kuwauza aliamua kuungana na Yesu maana alijua samaki ilikuwa kidogo bali kulikuwa na zaidi kwa Bwana.
Ngoja turudi kwa Yusufu baada ya mafanikio makubwa aliopewa na Mungu katika nyumba ya Potifa Yusufu alikuwa mzuri pia ,watu wanajichubua kwa vipodozi vya gharama na bado hawawi wazuri lakini biblia hainielezi kama Yusufu alikuwa na vipodozi lakini biblia inasema alikuwa mzuri wa uso hata hata kutamanika 39:6-12 mke wa Potifa akaanza kubabaika akitaka kufanya mapenzi naye lakini Yusufu alijali kutunza kibali cha Bwana hakutaka kumkosa Mungu kama ingekuwa leo vijana wangeona ndio nafasi kumbe Yusufu yeye aikuwa anaona tofauti maana alijua kilichokuwepo kwa Mungu ni kikubwa kuliko kilichopo kwa huyu mwanamke.
Lakini baada ya huyo mwanamke kuona kuwa ameshindwa ili asiaibike alimzushia kuwa amembaka. Ninachotamani uelewe ni kwamba hata kubakwa hakukuanza leo au kwa wanaume bali wanawake ndio walioanza hivyo.Yusufu apelekwa gerezani lakini hakujali namna watu watamtazama bali kutunza kibali kwa Mungu. Biblia inaeleza hata gerezani alipata kibali machoni pa mkuu wa gereza kila mahali anakuwa na mvuto hivi hujagundua bado hii si kawaida. Akawekwa kuwa msimamizi wa wenzake Mw 39:21-23.
Haijalishi uko kwenye mazingira gani bali Mungu anapoamua kushuka na kukubariki hata waweke vipingamizi watashindwa kama Mke wa Potifa alivyoshindwa. Hata kama ni wazazi wako wamekukataa kwa ajili ya Yesu ndugu huna cha kupoteza bali wanaopoteza ni wao maana laiti wangejua unachoona na kukutumia vizuri wangenufaika na utukufu wa Yesu wetu.
Kumbe unapokataliwa na watu wa karibu Mungu anakuinua kupitia watu wa mbali.Nduguze Yusufu kuoteshwa ndoto kwa Yusufu ndio msaada kwao wasingemuuza bali wangemtunza.Haya Mungu anampa ndoto Farao asiyoielewa kama isemavyo Mw 41:1-7 .Swali moja nikuulize unadhani ndoto ile ilikuja kwa ajili ya nini?Kusudi halisi ya ndoto ile ni kumwinua Yusufu maana wasaa ulikuwa umefika.
Wenye hekima wote wa Misri pamoja na waganga na wazee wote lakini hawana majibu.Mungu anamtoa Yusufu gerezani ili akatoe majibu .Sikiliza shida ni mlango wa kupita usiache kibali cha Mungu huondoka ndani yako kwa sababu ya shida hili ndio kubwa twajifunza kutoka kwa Yusufu.
Mw 41:25-27 Farao anashangaa jinsi hekima zake zilivyo za ajabu .Sikiza Mungu akikuinua hata wabaya wako watajua tu sikia maneno ya Farao Mw 41:38b Tupate wapi mtu kama huyu mwenye roho wa Mungu ndani yake?
Hata Farao ambaye huamini miungu mingine anasadiki kuwa Mungu aliyenae Yusufu si wa kawaida.
Mtukuze Mungu kwa nafasi aliokupa ili wakati ukifika akutukuze duniani na mbinguni pia.
USIJIJENGEE HOFU JUU YA MWANADAMU AU KITU CHOCHOTE NDANI YAKO BALI HOFU YA MUNGU ALIYE HAI NDANI YAKO
Ikiwa mwanadamu ni kazi ya mikono ya Mungu haitupasi kumwogopa mwanadamu bali yeye Mungu ambaye ndiye mfinyanzi wetu kama isemavyo Hes 13:17-33 Musa alichagua watu kumi na mbili kwa utaratibu wa kabila za Israeli kama alivyoagizwa na Bwana ili wakaipeleleze nchi.Walitumia siku zipatazo arobaini kufanya upelelezi huo hatimae kurudi kuleta taarifa Hes 13:25-27
Lakini taarifa yao ilitawaliwa na hofu ya watu waliokuwa huko Kanani wakisema ni hodari tena huishi kwenye maboma ijapokuwa nchi hiyo imejaa maziwa na asali kama isemavyo Hes 13:28. Lakini Kalebu na Yoshua kati ya wale kumi na wawili peke yao waliona tofauti kuwa Israeli inaweza kuwapiga wale watu.Wale wengine walisahau ukuu wa Mungu wao kutokana na Kut 7-12 alipokuwa akiwapiga watu wa misri na kupelekea waondoke utumwani Je si huyo awezae kuwaepusha na mkono wa hao watu.
Lakini tatizo hili halikuwa kwa wale walioagizwa kule kupeleleza hata sisi leo hii licha ya Ukubwa wa Mungu bado tuna kuwa na mashaka katika maisha yetu hususani kwa wale wenye nguvu ya pesa juu yetu.Unajua hofu hutoka kwa shetani katika maisha yetu ili kujenga dhana ya kushindwa katika maisha yetu.Na sio kweli Mungu hakutuwekea kushindwa bali kushinda.
Yn 11:7-8 Utagundua wanafunzi wa Yesu walipata hofu juu ya maisha yao maana walitaka kupigwa kwa mawe katika Uyahudi lakini Yesu anawaambia warudi hawakufahamu kuwa hofu haiwezi kuzuia kazi ya Mungu kutendeka hivyo basi Yesu alijua nguvu ya Mungu ilivyo kubwa kuliko hata wale wanaotaka kumpiga kwani Mungu aweza kuwanusuru na mkono wa watu wa Uyahudi na sivyo wanafunzi wake walivyofikiri ijapokuwa walikuwapo naye kwa muda mrefu wasielewe anachowaambia.
Hata leo hii tujijengee dhana ya kuwa mawakili wema kwa kusema ukweli katika maeneo yetu ya kazi tusihofu juu ya waajiri maana Mungu ni mwajiri mkuu.Hata hivyo nasi kama wanafunzi tulio mashuleni hatupasi kuacha kusema mambo ya yakini.Maana twajipatia swawabu na hazina zetu huifadhiwa.Ukiendelea kusoma Yn 11:9-10 utaona Yesu anawauliza wanafunzi wake kuwa saa za mchana si kumi ,halafu akawaeleza kuwa mtu akienda mchana hajikwai kwa sababu anayo nuru lakini nyakati ya usiku hujikwaa.Hivyo Yesu alikuwa anaawatazamisha wanafunzi wake kwa habari ya mkono mkubwa wa Mungu uliojuu yao.
Lakini yupo mtu mmoja ambaye hakuwa mkristo aliagizwa na wenzake akachukue chakula cha Bwana kanisani yaani mkate aje nao ili nao wauone.Naye alipopata kufanikiwa kuupata ule mkate hata aondoke nao aliona tundu limetengenezeka katika mkono wake maana alikuwa ameuficha mkononi.Baada ya kuona hayo alirudi kanisani na kuomba kubatizwa na kisha kuombewa ili mahali palipotoboka pazibike.Hivyo ndugu kupitia mtu huyu utagundua hapo awali huyu mtu hakuwa na hofu ya Mungu lakini Mungu alivyojidhihirisha aliogopa hata kutaka kubatizwa
Ndugu unayaona mambo mengi kuhusu Mungu usitamani ghadhabu ikupate kisha umwogope haitasaidia lakini hebu tengeneza mazingira sasa ya kuwa na hofu ya Mungu.Maana siku ile atatubagua kama kondoo na mbuzi.Hivyo ndugu natamani ubadilishe mtazamo wako sasa ili Yesu akusaidie.
Ukisoma Mt 25:31-45 Utaona tu kwamba Yesu anasema siku ile atawabagua watu kama kondoo na mbuzi chakupendeza Yesu hakuficha kwamba ubaguzi huo utakuwa kwenye misingi ipi ukisoma utaona ipo kwenye habari ya uwakili yaani alivyokupa Mungu na matumizi sahihi yake.Ni ngumu kuwa wakili mzuri kama huna hofu ya Mungu.Jijengee hofu ili uishi maisha ya starehe.
DHAMBI ISIYO SAMEHEWA...! ! !
Bwana Yesu amesema kwamba: "...Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho Mtakatifuhawatasamehewa." - (Mathayo 12:31)
Je! Nini maana ya KUMKUFURU Roho Mtakatifu?
Tukianza na neno KUFURU, maana yake ni: Kusema maneno yakumtukana Mungu au kufanya matendo yanayomtukana Mungu. Tukiendelea kusoma Mathayo 12:32 tunaona Bwana Yesu anasema kwamba:
"Naye mtu ye yote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifuhatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao." (Mathayo 12:32)
Ni kweli kuwa Yesu ni Mungu; lakini, Je! Yesu anamaanisha nini kuhusu dhambi isiyosamehewa ya KUMKUFURU Roho Mtakatifu?
Kumkufuru Roho Mtakatifu maana yake ni hii; Biblia Takatifu inasema kwamba:
"Kwa maana HAO WALIOKWISHA KUPEWA NURU, na KUKIONJA KIPAWA CHA MBINGUNI, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, wakaanguka baada ya hayo, HAIWEZEKANI KUWAFANYA UPYA TENA HATA WAKITUBU; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na KUFEDHEHESHA kwa DHAHIRI." (Waebrania 6:4-6)
Kumkufuru Roho Mtakatifu ni kuzitukana kazi za Mungu ambazo hakika kazi hizo ziliwahi kuyagusa maisha yako. Hapa namaanisha ya kwamba: mf. Yawezekana mtu alikuwa ni Mkristo na analijua neno la Kristo vizuri; mtu huyo baadae akaja akakengeuka na kuanza kuutukana Ukristo pamoja na matendo ya Mungu ambayo yanatendeka kwa uwezo wa Roho Mtakatifu; mtu huyo atakuwa ANAMKUFURU Roho Mtakatifu na KAMWE HATASAMEHEWA.
Tumeona hapo Biblia Takatifu imesema kuwa: "...wakaanguka baada ya hayo, HAIWEZEKANI KUWAFANYA UPYA TENA HATA WAKITUBU..." (Ebr 6:6) ni kwa sababu wamefanya "...KUFEDHEHESHA kwa DHAHIRI." Wamezitukana kazi za Mungu kwa makusudi; dhambi hiyo ndiyo Yesu anasema kamwe haitasamehewa. Biblia Takatifu inazidi kusema kwamba:
"Maana, kama TUKIFANYA DHAMBI KUSUDI baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, HAITABAKI TENA DHABIHU KWA AJILI YA DHAMBI; bali kunakuitazama hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao. Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma... Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkana Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano ALIYOTAKASWA KWAYO kuwa ni kitu ovyo, na KUMFANYIA JEHURI Roho wa neema?" (Waebrania 10:26-29)
Kuzitukana kazi za Mungu ni dhambi ambayo kamwe haiwezi kusamehewa. Tunapaswa tuwe makini sana juu ya hili. Leo hii tumepewa neema ya wokovu; na pia tumeziona kazi za Mungu maishani mwetu; isije ikatokea siku mmoja mtu akakengeuka na kuutukana Ukristo. Hilo ni jambo la kutisha na KAMWE HALITASAMEHEWA.
Wapendwa; Tusonge mbele katika wokovu. Tuishi maisha ya toba kila wakati; na pia, tuzidi kuihubiri kweli ya neno la Mungu bila ya kujitakia maslahi binafsi.
"Ee Bwana Yesu, nakuomba uwe nasi daima; kamwe asije akatokea mmoja miongoni mwetu akazikufuru kazi Zako. Naomba Roho Mtakatifu uwe nasi daima; utuongoze na kutulinda katika jina la Yesu Kristo. Amina."
Pumzi ya mwanadamu ni taa ya BWANA. - (MITHALI 20:27)
PUMZI YA MWANADAMU NI TAA YA MUNGU.
Je! Ni wapi uwezapo kutenda dhambi na Mungu asikuone? Je! Waweza kuishi pasipo kuvuta pumzi?
Biblia Takatifu inasema kwamba;
"Pumzi ya mwanadamu ni taa ya BWANA; Hupeleleza yote yaliyomo ndani yake." (Mithali 20:27)
Mpendwa; kila unapopumua Mungu anakuona, hata ujifiche gizani bado tu Mungu anakuona; Je, ni nani awezaye kuishi bila kupumua? Kila uvutapo pumzi, Mungu anakuona; na kupitia hiyo pumzi yako Mungu anapeleleza mambo yote ufanyayo.
Jitahidi kila wakati unatenda mambo yampendezayo Mungu.
UWEZA WA JINA LA YESU
Mtume Paulo anasema katika Waraka wake kwa Wakolosai sura ya tatu na mstari wa kumi na saba kuwa; “Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika JINA LA BWANA YESU, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.”
Hii ina maana ya kuwa, tukila tule katika Jina la Yesu Kristo. Tukilala tulale katika Jina la Yesu Kristo. Tukizungumza tuzungumze katika jina la Yesu Kristo. Tukiimba tuimbe katika jina la Yesu Kristo. Tukitembea tutembee katika jina la Yesu Kristo. Tukisafiri tusafiri katika jina la Yesu Kristo. Tukilima shambani tulime katika jina la Yesu Kristo; na kadhalika.
Kwa nini tunatakiwa tufanye mambo yote katika jina la Yesu Kristo? Jina hili la Yesu Kristo lina sehemu gani katika maisha yetu ya kila siku?Kama tunatakiwa kufanya mambo yote katika jina la Yesu Kristo, kwa nini hatufanyi hivyo?Ukitafakari maagizo tuliyopewa katika biblia utaona ya kuwa, maisha yetu yote yanalitegemea jina hili la Yesu Kristo.
Kama mambo yetu yote yanatakiwa yafanyike kwa jina la Yesu, basi ni muhimu tujifunze zaidi na zaidi kila siku juu ya jina hili la ajabu.Ni maombi yangu kwa Mungu Baba, katika jina la Yesu Kristo ya kuwa maneno yaliyomo katika somo hili yatachochea kwa upya kiu iliyomo ndani yako ya kutaka kufahamu zaidi siri iliyomo ndani ya jina la Yesu Kristo.
JINA LA YESU KRISTO – MOJAWAPO YA FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI
“Nami nakuambia ….. na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni” (Mathayo 16:18 – 19).
Maneno haya ya Yesu Kristo yanatuonyesha kuwa, nia yake ni kulijenga kanisa lililo na mamlaka kuliko shetani. Kanisa ni mwili wake (Waefeso 1:22 – 23). Wakristo waliookolewa kwa damu ya Yesu Kristo ni viungo vya mwili wa Kristo – ni viungo vya kanisa (1 Wakorintho 12:12, 13, 27). Kwa hiyo Yesu Kristo anaposema atalijenga kanisa lake wala milango ya kuzimu haitalishinda – ana maana ya kuwa, kila mkristo aliye wake anajengwa kiroho awe na mamlaka ya kumshinda shetani.
Ni budi tufahamu ya kuwa, Yesu Kristo hawezi kutuambia tufungue kama hakuna kitu cha kukifungua. Hawezi kutuambia tufunge kama hakuna kitu cha kufunga. Kwa hiyo ni lazima kuna vitu vya kuvifunga na kuna vitu vya kuvifungua.
Pia, tufahamu ya kuwa, Yesu Kristo hawezi kutuambia tufunge na kufungua kabla hajatupa uwezo na mamlaka ya kufanya hivyo. Uwezo na mamlaka tunapata ndani ya Kristo aliyetukabidhi funguo za ufalme wa mbinguni.Itakuwa haina maana kwa Yesu Kristo kutukabidhi funguo bila ya kutufundisha namna ya kuzitumia. Hawezi kutukabidhi mamlaka bila kutufundisha namna ya kuyatumia.
Yesu Kristo anasema tukifunga au tukifungua, mbinguni nako kunatia mhuri kitendo hicho. Hatuwezi kufanya hivyo kama tulichokifanya hakifanani na mapenzi yake. Ndiyo maana tunaomba kuwa mapenzi yake yatimizwe hapa duniani, kama yanavyotimizwa huko mbinguni. Kwa maneno mengine tunaweza kusema ya kuwa ukifanya kitu chochote katika mapenzi ya Mungu, Ufalme wa mbinguni utakuwa upande wako.
Aina za Funguo:
Biblia inazungumza juu ya funguo za aina tano zifuatazo:
1. Funguo za Ufalme wa Mbinguni – Mathayo 16:19 – Yesu Kristo amekabidhi funguo hizi kwa wakristo (Kanisa).
2. Funguo za mauti na za kuzimu – Ufunuo 1:18 – Funguo hizi anazo Yesu Kristo – baadaye atampa Malaika mmoja funguo za kuzimu ili amfunge Ibilisi (Ufunuo 20:1-3).
3. Ufunguo wa nyumba ya Daudi – Isaya 22:22; Ufunuo 3:7. Ufunguo huu anao Yesu Kristo.
4. Ufunguo wa kawaida wa mlango – Waamuzi 3:25.
Neno ‘funguo’ lililoandikwa katika Mathayo 16:19; Ufunuo 1:18; Isaya 22:22 na Ufunuo 3 – 7 lina maana ya ‘mamlaka’. Kazi ya funguo ni kufunga na kufungua. Kwa hiyo ukipewa funguo maana yake umepewa mmalaka ya kufunga na kufungua.
Kwa mfano, mtu akikupa funguo za chumba – maana yake una mamlaka juu ya chumba hicho kukifunga na kukifungua. Mtu yeyote akitaka kuingia kwenye chumba hicho hawezi kufanya hivyo bila kupata ruhusa toka kwako ya kumfungulia. Ukipewa funguo za gari maana yake kwa muda huo ambao una funguo hizo za gari, una ‘mamlaka’ juu ya hilo gari kulifunga lisitumike au kulifungua litumike. Mtu akitaka kulitumia ni budi aje kwako kwa ajili ya kufuata funguo.
Kwa hiyo Yesu Kristo aliposema ametupa funguo za ufalme wa mbinguni alikuwa ana maana ya kuwa ametupa ‘mamlaka’ ya ufalme wa mbinguni. Ni vizuri ufahamu hapa ya kuwa ufalme wa mbinguni ni ufalme wa Mungu ulio na mamlaka juu ya falme nyingine zote – ufalme wa shetani, ufalme wa wanyama, ufalme wa wadudu, ufalme wa mimea, ufalme wa ndege, na kadhalika. Ikiwa wewe ni mkristo uliyeokoka basi fahamu ya kuwa, una mamlaka uliyopewa na Yesu Kristo juu ya falme hizi zote!
Yesu Kristo anaendelea kusema kuwa; lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.
Kwa mfano ukiamua kumfunga ibilisi asikusumbue katika maisha yako, mbinguni pia wanasimamia utekelezaje wa jambo hili. Hata kama ibilisi ataamua ‘kukata rufaa’ juu ya uamuzi wa kumzuia asikusumbue na akaenda kwa Mungu kuomba aachiliwe – Mungu atamwambia ‘rudi kwa aliyekufunga, akikufungua nami nitakufungua, lakini asipokufungua nami sikufungui’
Unaweza kusema mbona shetani alipewa ruhusa na Mungu kumjaribu Ayubu. Kumbuka kuwa Ayubu aliishi katika agano la kale na sisi tunaishi katika agano jipya ambalo ndani yake tuna mamlaka ya kumfunga shetani kwa jina la Yesu Kristo.Kuna wakristo wengi wameonewa na ibilisi kwa kuwa hawajui mamlaka waliyo nayo na namna ya kuyatumia.
Jambo jingine ninalotaka uone hapa ni kwamba Yesu Kristo alisema ametupa “funguo ZA ufalme wa mbinguni”; na hakusema ametupa ufunguo wa ufalme wa mbinguni.Neno hili ‘ZA’ lina maana ya kuwa kuna funguo za ufalme wa mbinguni zaidi ya mmoja. Kumbuka kuwa kuna tofauti ya funguo za ufalme wa mbinguni na zile funguo za mauti na za kuzimu
TAFAKARI JUU YA JINA LA YESU KRISTO
“Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali YATAFAKARI MANENO YAKE MCHANA NA USIKU, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapofanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.” (Yoshua 1:8)
Mtu mmoja aliwahi kuniuliza swali hili: “Je kutafakari maana yake nini?” Kila mara ninapofundisha somo hili nakutana na swali la jinsi hii . Naamini kuwa swali hili linawatatanisha wengi kwa sababu bado hawajatofautisha kati ya kusoma neno na kutafakari neno.
Kusoma neno ni tofauti na kutafakari neno. Kulitafakari neno ni zaidi ya kulisoma neno. Watu wengi huwa wanasoma neno zaidi kuliko kulitafakari.
Kutafakari maana yake nini?
Maana ya karibu sana ya neno kutafakari ni kuwaza. Ni kusoma neno huku unalicheua na kulitafuna rohoni mwako.
Kutafakari ni njia mojawapo kubwa ya kuweza kuilisha roho yako. Yesu Kristo alisema “Imeandikwa, mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.” (Mathayo 4:4)
Mkate ni chakula cha mwili wa nje ulio wa nyama na damu; neno la Mungu ni chakula cha mwili wa kiroho. Kinywa kinapokea chakula na meno yanatafunwa na kukivunjavunja huku kikilainishwa na mate, tayari kwa kumeza.
Kusoma neno ni kama kinywa, kazi yake ni kulipokea neno. Kutafakari ni kuvunjavunja hilo neno huku Roho wa Mungu akililainisha liwe tayari kumezwa na roho yako. Kutafakari neno kunamletea mtu siri ya ajabu ya uhakika na ushindi ndani ya Kristo. Sisi ni watenda kazi pamoja na neno la Mungu hapa ulimwenguni. Tunaliwakilisha Neno la Kristo mahali tulipo na ulimwenguni pote. Na kwa sababu hiyo, Imeandikwa, “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote.” (Wakolosai 3:16)
Huwezi ukawa na Neno la Kristo moyoni mwako bila ya kuitumia siri ya kutafakari. Kukariri neno la Kristo hakutoshi peke yake kukuletea uhakika na ushindi kiroho na kimwili kama vile kutafakari kunavyofanya ndani ya mtu. Kutafakari ni kuwaza. Kulitafakari jina la Yesu Kristo ni kuliwaza jina hili. Tatizo kubwa sana ambalo linawapata watu ni tatizo la mawazo. Na huu ni ugonjwa mkubwa sana ambao umewakwamisha wengi katika maisha yao ya kiroho.
Kutafakari na kuwaza ni jambo la rohoni, - ni jambo la rohoni! Si jambo la akili kama wengi wanavyodhani.
Mtu anapowaza, au kutafakari jambo huwa ni jambo linalofanyika rohoni mwake, ingawa utadhani linafanyika katika ubongo. Je! Wewe unayesoma somo hili sasa hivi unawaza nini rohoni mwako, unatafakari nini? Mara nyingi utaona mtu anaposoma Neno mawazo yake mara nyingi yanakuwa mbali sana, kwa hiyo hakuna anachoelewa katika hayo anayosoma.
Pia, hata wakati watu wanasikiliza neno la Mungu, mara nyingi mawazo yao yanakuwa mbali sana na neno linalofundishwa. Hii inajidhihirisha hasa ukimwuuliza mtu huyo muda mchache baadaye, juu ya neno lililofundishwa maana hatakumbuka.
Unapoumwa huwa unawaza nini? Wengi wanautafakari ugonjwa, na wengine hata kukata tamaa anapoona hauponi haraka. Wengine wanapoumwa wanawaza na kutafakari kufa kuliko kuishi.
Unapokuwa una matatizo huwa unawaza nin? Unapokosa maelewano na mwenzako, nyumbani, kazini au mahali popote, huwa mawazo yako yanawaza nini?
Unapokuwa huna fedha au vitu fulani vya kimwili huwa unawaza au kutafakari nini? Tunaweza kusema mengi lakini swali kubwa ni hili; “Kila wakati huwa unawaza nini na kutafakari nini?” Je! unafahamu ya kuwa matendo yako na maneno yako , ni matokeo ya mawazo uliyonayo? Mtu husema anachokitafakari au kukiwaza, na pia hutenda anachokitafakari au kukiwaza moyoni mwake.Ukitaka kumfahamu mtu alivyo rohoni mwake, sikiliza maneno anayosema na angalia matendo anayoyatenda.
Sijaona katika biblia ambapo mtu wa Mungu ameambiwa aitafakari shida yake, awaze juu ya ugonjwa wake au udhaifu wake.Kumbuka kuwa maneno ni chakula cha roho, hali ya roho yako inategemea sana ni maneno gani unayasikia kila wakati na kuyatafakari.Unapotafakari shida, magonjwa, hofu, unaifanya roho yako ijengeke katika hayo. Ukilitafakari jina la Yesu Kristo roho yako inajengeka katika jina hili.
Watu wengi sana wamejengeka katika kumwogopa shetani kuliko Mungu. Hii hali ipo hata kwa watu wa Mungu. Hayo ni matokeo ya kumtafakari shetani na majaribu anayowajaribu, kuliko kumtafakari Mungu na uweza wake.Neno la Kristo linakosa nafasi katika roho za watu, kwa sababu roho za watu zimejaa mawazo ya dunia hii na shida zake. Roho za watu zimejaa mawazo yanayopinga na kwenda kinyume kabisa na neno la Kristo.Roho za mtu ni uwanja wa vita. Ukishinda vita katika mawazo, utakuwa umeshinda vita katika mwili, katika roho na katika maneno.
Wakati mmoja nilianza kujiuliza kwa nini Nabii Ezekieli aliambiwa ale gombo la chuo, na mtume Yohana aliambiwa ale kitabu kilichofunguliwa.Sikuelewa kwa nini hawakusoma tu maneno ambayo yalikuwa yameandikwa bila kula gombo la chuo na kitabu kilichofunguliwa. Mungu alikuwa ana uwezo wa kuwaambia wayasome maneno aliyokuwa anawaonyesha – lakini badala yake aliwaambia wale – kwa nini?Nilikuwa siioni tofauti ya kusoma na kula. Kuna tofauti kubwa kati ya kusoma ujumbe wa Mungu na kula ujumbe wa Mungu. Soma Ezekieli 2:7 10; 3:1 – 3 na Ufunuo wa Yohana 10:1 – 2; 8 – 11.
Mtu anapokula chakula, huwa kinatafunwa na kulainishwa kabla ya kumezwa. Na kikimezwa na kuingia tumboni, kinanyonywa na kuingia katika mishipa ya damu inayozunguka mwili mzima na kukisambaza chakula hicho katika sehemu zinazohitajika.Mtu anapotembea, ukweli ni kwamba ni chakula kile alichokula ndicho kinachotembea. INGAWA yeye ndiye anayeonekana anatembea.
Kwa hiyo Ezekieli na Yohana walipokula ujumbe wa Bwana uliokuwa umeandikwa katika gombo la chuo na katika kitabu kilichofunguliwa, ujumbe huo uliingia ndani yao kama vile ambavyo wangekula nyama.Ujumbe huo uliingia kwenye damu yao na ukajenga misuli. Kila sehemu ilikuwa imejaa ujumbe wa Mungu. Ujumbe huo ndio uliowafanya wapate nguvu ya kutembea, na kuishi na kusema.
Kwa mtazamo mwingine tunaweza kusema, Ezekieli na Yohana walikuwa ni ujumbe wa Mungu uliokuwa unatembea.Na sisi tukilitafakari neno la Kristo; na likijaa ndani yetu kwa wingi, tunakuwa ni neno la Kristo linalotembea; tunakuwa ni neno la Kristo linalosema; tunakuwa ni neno la Kristo linaloponya.
Tunafika mahali ambapo kuishi kwetu kunakuwa ni neno (Kristo) – kama vile Paulo alivyosema “Kuishi ni Kristo” (Wafilipi 1:21). Tukilitafakari jina la Yesu Kristo, tunakuwa ni jina la Yesu Kristo linalotembea,,, Je! unauona umuhimu juu ya jambo ninalokuambia la kutafakari?Mtu anashindwa kuwa mtendaji wa Neno kwa kuwa moyoni mwake hakuna neno. Anabaki kuwa mtendaji wa maneno mengine aliyonayo mawazoni mwake tu.
“Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome); tukiangusha MAWAZO na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara KILA FIKRA ipate kumtii Kristo” (2 Wakorintho 10: 3 – 5).
Hii ina maana kuwa fikra zako ziwaze sambamba na Neno (Kristo).Katika kuishi kwetu na kuenenda kwetu tuwe tunatafakari nini mioyoni mwetu, ili roho zetu zipate chakula safi cha kiroho?
“Hatimaye, ndugu zangu, mambo yoyote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo ya staha, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema, ukiwapo wema wowote, ikiwapo sifa nzuri yoyote YATAFAKARINI HAYO” (Wafilipi 4:8).
NI SILAHA GANI ZA KUVAA KWENYE VITA
Ili uweza kupigana lazima uwe na silaha.Swali ambalo waweza kujiuliza kwa nini niwe na silaha.Jibu la haraka ni kukinga maangamizi na kupambana,haya ndio majibu unayoweza kujipa kwa haraka.Swali la pili ambalo pia utajiuliza kama silaha hutumika vitani basi hutumika yeyote? Nikienda na gongo nitafanikiwa?bunduki?bomu?
Ndipo tunapata majibu kutoka 1Sam 17:38-39.Ukisoma eneo hili utagundua kuwa Sauli alimvika Daudi mavazi ya vita kama chapeo ya shaba na dirii.Lakini Daudi alishindwa kustahimili mavazi yale.Ukisoma aya ya 39 anasema "Siwezi kwenda na vitu hivi maana sikuvijaribu.
Hivyo Daudi alishindwa kutumia mavazi ambayo hakuwahi kuyatumia.Mungu akaniambia kuwa sio kila silaha kwa jina la silaha yaweza kutumika vita bali zipo sihala maalum zinazoweza kutumika kwa ajili ya vita na hili somo kwa Daudi lianza kwake mapema maana Mungu alifahamu siku ataligusa jina la Daudi kwa vita hivyo akatengeneza mazingira ya Daudi kujua matumizi ya silaha kwa mahali sahihi na wakati sahihi.
Ndugu usichoke lakini twende pamoja ili tulifikie kusudi la Mungu katika ujumbe huu.Unajua mtu mwingine ni rahisi mtu kukubali mavazi ya mfalme lakini asijue kuwa hayatampeleka kwenye kusudi la moyo wake na matokeo yake kufa.Asijue mfalme alifundisha kuvaa silaha za aina hiyo na sio yeye.
Uchaguazi wa silaha ni muhimu sana katika vita ili ujihakikishie ushindi.Baada ya Daudi kuacha mavazi ya mfalme aliamua kuchukua fimbo, mawe na kombeo.Ujiuliza kwa nini yeye achague hivi hukumbuki ndivyo Mungu alivyomuandaa kama isemavyo 1Sam 17:34 "Mtumishi wako alikuwa akichunga kondoo za baba yake na alipokuwa akija simba au dubu akamkamata mwana kondoo wa lile kundi, mimi hutoka nakumfuata,nikampiga...
Uchaguzi wako wa silaha Je umetegemea mafunzo uliyoyapata?Hili ndio tatizo la wakristo wengi hatutumii maarifa tuliopata kwa ajili ya vita bali nguvu nyingi.Na matumizi ya nguvu nyingi siku zote hutuangusha kwa sababu wakati mwingine maadui wana nguvu nyingi.
1Sam 17:40f inasema Daudi akamkaribia Mfilisti.Ngoja nikueleze kitu hapa kwa sababu amechagua silaha sahihi,ndio maana alipata ujasiri wa kumkaribia Daudi.Nadhani angekuwa amevaa silaha za mfalme za vita yamkini angepata hofu maana hakuzizoea.Lakini yeye alikubali kutumia silaha ambayo ameizoea hata kumfanya apate uhuru wa kuingia vitani.
Ushindi vitani unaanza kwa hatua ikiwemo kuondoa hofu na ndilo alilofanya Daudi.Aliandaa mazingira ya kumkabili adui yake pasipo hofu.Kwa hali ya kawaida haikuwa rahisi kwa Daudi kupigana na Goliati.Lakini sihala alizozichagua zilimtengenezea mazingira ya kumfanya awe mshindi.Ndio maana ukisoma 1Sam 17:42 inatueleza kuwa Goliati alipomtazama Daudi alimdharau maana moja alikuwa mdogo na pili silaha alizokuja nazo.Labda Goliati alidhani Daudi angekuja na silaha mfano wa zake.Lakini hakuwa na ufahamu juu ya kile alichokitazama Daudi.
Mungu anachokueleza ndugu yangu ni kwamba tatizo si unayepigana naye yukoje ama amekujaje kwenye vita tatizo ni uchaguzi wa silaha.Daudi aliletewa jitu kubwa tena asiyetairiwa lakini alipambana naye.Unaweza ukaona kuwa Daudi alichukua mawe,fimbo na kombeo.Lakini hizi hazikuwa silaha zake bali zilikuwa mfano wa silaha zake.Kama isemavyo 1Sam 17:45b "Wewe unanijia mimi na upanga na fumo na mkuki bali mimi ninakujia kwa jina la Bwana wa maajeshi Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana .Ikiendelea aya ya 46 na 47 utaona maneno ya Daudi juu anayemtegemea.
Sasa Mungu anatufunulia siri hii kwamba silaha nzuri na ya uhakika katika maisha yako ni jina lake.Maana yeye ni Mungu wa majeshi.Hii kanuni Daudi aliijua hata ukisoma Efe 6:11 inasema Vaeni silaha zote za Mungu.Mpate kuweza kuzipinga hila za shetani.Hivyo kwa sababu Daudi alijua hii kanuni ilimfanya apate ushindi mbele ya Goliati ambapo hapo awali wana wa Israeli walidhani isingeli wezekana kupambana naye hata mfalme wao Sauli ambaye ndio Amiri jeshi wao.
Uchaguzi wa silaha ni muhimu sana Efe 6:10-19 ameeleza vyema juu ya jambo hili.Lakini msisitizo mkubwa na jambo la muhimu ni kwamba silaha za Mungu huvaliwa zote na moja na nyingine kuachwa.Zingatia mahali hapa maana wakristo wengi wanashindwa na shetani wakati mwingine si kwamba hajatumia silaha za Mungu ,ametumia silaha ya Mungu mfano maombi lakini hakutumia zote.Mungu ni umoja hivyo mfumo wa vitu vyake vipo katika umoja pia.Hivyo kushindwa kwa mtu kutumia silaha zote za Mungu humfanya ashindwe maana amekiuka kanuni ya vita ya Mungu.
Mtu ataniuliza mbona Daudi alitumia jina la Mungu tu? Lakini kumbuka wakati ule ni wa Agano la kale.Yesu aliwaambia watu sikuja kuitangua torati bali kuitimiliza.Hivyo basi kuna mambo hayakuwa na budi kutimilika ikiwepo hili.Nadhani tuko pamoja mpaka sasa.Ninachotamani usihisi kuchoka lakini natamani utumie Muda mrefu ili maisha yako yapige hatua nyingine yenye mwelekeo maana Kanani twaweza kufika kwa hatua zenye muelekeo.
Hivyo ndugu yangu zinatia umuhimu wa uchaguzi wa silaha ili ujihakikishie nafasi ya kushinda.
Hivyo ndugu yangu zinatia umuhimu wa uchaguzi wa silaha ili ujihakikishie nafasi ya kushinda.
NAMNA YA KUMILIKI NA KUTAWALA KATIKA MAOMBI
Nakusalimu kwa jina la Yesu Kristo!
Tunaamini ya kuwa – ile kwamba Mungu amekupa nafasi ya kuisoma barua hii, inatuonyesha ya kuwa, moyo wako unafuatilia kwa karibu sana chakula cha kiroho, ambacho Mungu ametupa kwa ajili ya watu wake.
Msukumo mkubwa tulionao mioyoni mwetu katika huduma hii ambayo Mungu ametupa ni: Kuujenga ufalme wa mbinguni (au ufalme wa Mungu) katika mioyo ya watu na katika jamii pia.
Ndiyo maana Mungu alipotuambia: “Lisha Kondoo zangu” (Yohana 21:17); tulijua ya kuwa ataweka ndani yetu chakula kwa ajili ya watu wake, kwa kusudi la kuujenga ufalme wake.
Eneo mojawapo ambalo tumekuwa tukiwahimiza watu wa Mungu, ni juu ya kutumia njia ya maombi katika kuujenga ufalme wa mbinguni, sawasawa na maneno ya Yesu katika Mathayo 6:9,10.
Yesu Kristo alisema hivi: Basi ninyi salini hivi; “Baba yetu uliye mbinguni; jina lako litukuzwe; ufalme wako uje;; mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama mbinguni”.
Kwa barua hii ya mwezi huu , tunataka tukukumbushe na tukuhimize ya kuwa, unaweza kumiliki na kutawala kwa njia ya maombi.
Hebu tafakari nasi mistari ya biblia ifuatayo:
“…..ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa, ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi” (Ufunuo wa Yohana 5:9,10)
“…..zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo” (Warumi 5:17)
Tafsiri nyingine ya maneno ya ufunuo wa Yohana 5:10 inasema; “…..ukawafanya kuwa ufalme wa makuhani kwa Mungu wetu; nao kama wafalme wanamiliki juu ya nchi”. Na tafsiri nyingine inasema, “…..ukawafanya kuwa wafalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.”
Lakini sii tu kwamba “wanamiliki juu ya nchi”, pia Warumi 5:17 inatuambia “watatawala katika maisha tuliyonayo kwa Yule mmoja, Yesu Kristo”.
Kila msomaji mzuri wa biblia anajua ya kuwa, makuhani kazi yao ni kuomba au kufanya maombi…..tena wanawekwa na Mungu wala hawawekwi na wanadamu katika kuifanya kazi hiyo. Lengo la Mungu kutufanya “wafalme na makuhani” katika Kristo Yesu ni ili tuweza kumiliki na kutawala juu ya nchi.
Kwa hiyo, ikiwa walio ndani ya Kristo – wamefanyika makuhani kwa Mungu, na ya kwamba wanatakiwa “kumiliki na kutawala” – ina maana wanatakiwa na Mungu kumiliki katika nchi na kutawala katika maisha haya kwa njia ya maombi.
“Kumiliki” maana yake nini? Na “kutawala” maana yake nini?
Kwa tafsiri iliyo nyepesi kuielewa ni kwamba “kumiliki” ni uwezo wa mwisho anaopewa mtu juu ya matumizi ya kitu. Kwa mfano: mmiliki wa eneo fulani la ardhi ni mtu Yule mwenye uwezo wa mwisho juu ya matumizi ya eneo hilo la ardhi. Tena, kwa mfano; mmiliki wa nyumba ni mtu Yule aliye na uwezo wa mwisho juu ya matumizi ya nyumba hiyo.
Kwa tafsiri iliyo nyepesi kuielewa ni kwamba; “kutawala” ni uwezo wa mwisho anaopewa mtu juu ya maamuzi ya jambo. Kwa mfano: mtawala ndiye mwenye uwezo wa mwisho katika eneo analotawala juu ya jambo gani lifanyike, na ni jambo gani lisifanyike. Kwa mfano, mtu anapotawala na kumiliki nyumba, ina maana ana uwezo wa mwisho juu ya nyumba yenyewe, na juu ya wote wakaao ndani yake.
Hii ina maana ya kuwa, kwa njia ya maombi tunaweza, au tunao uwezo wa mwisho juu ya matumizi ya vitu mahali tulipo; na tunao uwezo wa mwisho juu ya maamuzi ya mambo mbalimbali katika maisha kwenye maeneo tuliyopo!
Ukiangalia katika maisha ya makuhani, na wafalme waliotutangulia katika agano la kale; tunaona wakimiliki na kutawala kwa njia ya maombi.
Kwa hiyo ikiwa ,matumizi ya vitu mahali tulipo siyo mazuri au hayamtukuzi Mungu, ina maana waliopewa uwezo wa kumiliki matumizi ya vitu hivyo kwa njia ya maombi, hawajafanya sehemu yao. Hawajaombea juu ya matumizi ya vitu hivyo!
Je! Kuna jambo lolote unalolifahamu lililofanyiwa uamuzi ambao si uamuzi mzuri, au ni uamuzi unaokwenda kinyume na misingi ya ufalme wa Mungu? Ukiona hivyo ina maana maombi ya jinsi hii ninayokufundisha hayajafanyika juu ya jambo hilo!
Mungu anataka watu wake walio ndani ya Kristo wamiliki na kutawala kwa njia ya maombi. Au tuseme ya kuwa Mungu anataka watu wake walio ndani ya Kristo wawe sehemu ya wamiliki na watawala kwa kutumia maombi – kwenye maeneo waliyomo.
UMUHIMU WA UPAKO WA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUKUFANYA UWE KIONGOZI
Je, unajua umuhimu wa upako wa Roho mtakatifu katika kukuandaa uwe kiongozi? Inawezekana unajua, na inawezekana hujui; hata hivyo ujumbe huu utakupa kufikiri kwa upana zaidi, juu ya faida za upako wa Roho Mtakatifu katika maisha yako.
Je, unajua umuhimu wa upako wa Roho mtakatifu katika kukuandaa uwe kiongozi? Inawezekana unajua, na inawezekana hujui; hata hivyo ujumbe huu utakupa kufikiri kwa upana zaidi, juu ya faida za upako wa Roho Mtakatifu katika maisha yako.
Mfalme Daudi alipakwa mafuta ya Roho Mtakatifu mara tatu katika maisha yake. Daudi alipokuwa mjini Bethlehemu, alipakwa mafuta hayo kwa mara ya kwanza.
“Ndipo samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na Roho ya Bwana akamshukia Daudi kwa nguvu tangu siku ile” (1Samweli 16:13).
Tunajua pia kwa kusoma Biblia ya kuwa, Daudi alipakwa mafuta mara ya pili (2 Samweli 2:4), na mara ya tatu (2 Samweli 5:3), akiwa mjini Hebroni.
Mistari hiyo ya Biblia inatupa kujua ya kuwa, kazi ya upako wa pili, ilikuwa ni kumsimika Daudi na kumsaidia “awe mfalme juu ya nyumba ya Yuda” Na kazi ya upako wa tatu, ilikuwa ni kumsimika Daudi na kumsaidia “awe mfalme juu ya Israeli”
Ikiwa ni hivyo, ule upako wa kwanza alioupata akiwa Bethlehemu ulikuwa ni kwa ajili ya nini?
Swali hili ni muhimu kupata jibu lake kwa kuwa tunasoma ya kuwa Daudi “akatawala miaka arobaini, Huko Hebroni alitawala miaka saba na miezi sita; na katika Yerusalemu alitawala miaka thelathini na tatu juu ya Israeli wote na Yuda” (2Samweli 5:4,5).
Unaliona hili? Ufalme wa Daudi unahesabiwa toka upako wa pili hadi ule upako wa tatu tu! Ikiwa ni hivyo, ule upako wa kwanza alioupata akiwa Bethlehemu ulikuwa ni wa nini? Ikiwa ulikuwa ni wa kumsimika awe mfalme, mbona hatuoni ukitajwa kama sehemu ya kipindi cha kutawala cha Daudi?
Sisi tunaamini ya kuwa upako ule wa kwanza, ulikuwa ni wa kumpa maandalizi mazuri na anayostahili, ili aje awe mfalme sawa na matazamio aliyokuwa nayo Mungu juu yake!
Ni maeneo gani hayo ambayo upako ule wa kwanza ulimpa maandalizi ya kuwa kiongozi? Soma maeneo haya saba aliyoandaliwa na upako huu:
1. Aweze kuanza kufikiri kama kiongozi aliye mtumishi wa Mungu, ili aweze kuja kulitumikia kusudi la Mungu atakapokuwa kiongozi. Hii ni muhimu asije akajikuta ana ‘mindset’ ya mchunga kondoo akiwa kiongozi, badala ya kuwa na ‘mindset’ ya mtumishi wa Mungu aliye kiongozi pia. Soma Zaburi 89:20 na Matendo ya Mitume 13:36, na Zaburi 78: 70,71.
2. Afanyike mzaliwa wa kwanza kwa Mungu kama Lango lake. Hii inatupa kujua kuwa kwa upako huo wa kwanza, Mungu aliumba ndani ya Daudi, ‘attributes’ za uzaliwa wa kwanza ambazo alikuwa hana. Kumbuka Daudi alikuwa mtoto wa nane wa Yese, lakini Mungu aliumba ndani ya Daudi vitu vilivyomfanya awe mzaliwa wa kwanza kwake! Soma Zaburi 89:20,27. (Fikra: Iliyokuwa inajengwa ndani yake katika hili ni: Ajizoeze kufikiri kama lango au kwa kujua anawajibika kwa Mungu kwa jili ya watu wengi. Asitumikie cheo kibinafsi)
3. Aweze kuongozwa na Mungu ili aishi katika miji iliyokuwa sehemu ya mpango wa Mungu, juu ya maisha yake ya kiuongozi. Soma 2 Samweli 2: 1-4, Soma ilivyokuwa kwa Yesu katika Mathayo 2:5,6, 13 – 15, 19 – 23. Soma pia Yeremia 29:7, 11. (Fikra: Miji ni vituo muhimu katika hatua za Mungu kukutengenezea maisha yako ya baadae, kwa hivyo uombee na uwe raia mwema).
4. Aweze kuinuliwa na Mungu watu wa kumsaidia katika safari yake ya kuwa kiongozi. Soma 1Samweli 22:1,2 na 1Samweli 18:1 na 1 Mambo ya Nyakati 12:14 – 18,23. (Fikra: Mungu anaweza kukuinulia watu kusaidia mafanikio ya ndoto zako hata wale usiowategemea).
5. Kumpa uvumilivu wa kusubiri kipindi cha Mungu katika maisha yake, ili aweze kuwa kiongozi kwa ratiba ya Mungu, na sii katika ratiba ya mashabiki wake! Soma: 2 Samweli 5:4,5 (Fikra: usitumie muda wa kusubiri kulalamika bali utumie katika kujiandaa kwa ajili ya maisha yako ya baadae).
6. Kumtengenezea mazingira ya kukutana na Goliati, ili alichobebeshwa katika maisha yake na Mungu kwa siri, kijulikane na watu wote ambao Mungu alikusudia awe kiongozi wao baadaye. Soma 1Samweli 18:6,7 na Wagalatia 2:9. (Fikra: Vikwazo sii vizuizi kwako bali ni fursa kwako ili ufanikiwe na ujulikane).
7. Kumtengenezea fikra zilizojizoeza kujua ya kuwa upinzani wa kumpinga asiwe kiongozi utajitokeza katika maisha yake. Msimamo huo wa Kifikra ulimsaidia awe na utulivu na hekima katika kuushughulikia huo upinzani. Soma 1Samweli 18:9, 14, 15,20,21,29.
Hebu tafakari mambo hayo saba tena na tena; utajikuta na wewe unahitaji upako huo wa kwanza kama aliopewa Daudi. Au unaweza ukawa unajua ni nani anaweza kuwa anauhitaji ili awe kiongozi bora!
Ni maombi yetu kwa Mungu ya kuwa utaliona jambo hili katika umuhimu na uzito unaostahili.
tenda neno mtumishi. nimebarikiwa na huu ukurasa. natumaini nitazidi barikiwa na kurasa zijazo
ReplyDeleteNakushukuru mtu wa Mungu maana umekua mtu wa kwanza kutuma comment nashangaa kwa nini watu hawatumi comment naomba usome sana kurasa nyingine pia uwahasishe wengine wasome blog hii na kuweka comment
Delete