Bwana Yesu asifiwe, kuanzia tarehe 1/1/2017 tutakuwa tukihamia katika website yetu iitwayo www.egospeltz.org

TESTIMONIES


NGUVU YA SADAKA KATIKA KUJIBU MAOMBI YA MTU
Mfungwa mmoja alisikia Mwakasege anafundisha habari za sadaka Diamond Jubilee kupitia redio. Naye akapata msukumo wa kutoa sadaka na kwa kuwa alikuwa gerezani alimwomba mke wake aende Diamond Jubilee lakini alipofika, alikuta semina imekwisha kwa kuwa ni ya siku moja. Basi alirudi kumwambia mumewe kuwa semina ni ya siku moja nayo ilishaisha. Yule mfungwa akamwambia nenda tafuta hata ofisi yake. Basi mkewe akazunguka hatimaye akapata ofisi za waandaaji wa semina basi akijieleza kisha akatoa sadaka yake. Haikupita majuma mawili yule kaka kesi yake ilifutwa. Kwa hiyo unaweza kuona nguvu ya sadaka inavyoweza kukutoa mahali fulani na kukuweka mahali pengine

MAAJABU YA KUOTA KWA MSALABA
Msalaba mmoja waota sehemu moja karibu na kanisa liitwalo Francis wa Asis huko Hale Tanga. Msalaba huo unakua kila wakati. Kama ulikwenda asubuhi kuuangalia ukirudi jioni unaukuta umeongezeka upana na urefu.Yesu anajidhihirisha kwa ishara wake up..

ATHARI ZA KUTAFUTA UTAJIRI WA HARAKA
Mama mmoja alimtoa mwanae kafara bila kujua kwa nia ya kutaka duka lake lifanikiwe (Huyu mama na mumewe hawakuwa wakristo). Akaambiwa lete kitovu na nywele za mwanao wakati huo akiwa ametoka kujifungua basi akapeleka yule mtoto akawa zezeta kwa miaka saba. Walikwenda kwa waganga watafute ufumbuzi juu ya mtoto wao maana waliamini kutoa kitovu na nywele zake hamna mahusiano. Lakini hawakufanikiwa kisha ikawa siku moja mama yake mkubwa yule mtoto pamoja na mwenzie walikuwa wamepanda basi kwenda kwa Mzee wa Upako basi kijana mmoja akaiona ile hali ya mtoto ikamsumbua. Akawauliza mama yake mkubwa mnaelekea wapi wakasema twaelekea kwa Mzee wa Upako yule kijana akawaambia Mzee wa Upako ndio mimi. Basi Mungu akampa ufunuo wa ile hali. Kisha akaomba kumpigia mama yake mzazi simu akamueleza yote aliyoyafanya asiue ndio yalimsabababisha mtoto wao matatizo. Akamuambia ngoja nikuongoze sala ya toba. Aliposema amen mtoto akaanza kutembea basi zima watu wakashanga wakaanza kusema Yesu Yesu Yesu …!

HACKING IS A SPIRIT DID YOU KNOW?
Je wajua kuna "spirits of hacking" inawezekana unashangaa. Mtu mmoja kutoka Nigeria alipatwa na hizi roho akasababisha wizi wa pesa kwa watu wengi sana ikiwepo watu wa ulaya na marekani. Hizi roho humpa uwezo wa akili usio wa kawaida kuiba kupitia mtandao.Roho hizo zilikuwa tano ambapo zilimfanya kuiba kwa mtandao katika maisha yake lakini zilikuwa zikihakikisha fedha anazopata kwa wizi huo zinaisha vibaya ili aendelee na tabia hiyo. Kwa maelezo zaidi bonyeza link hii uone ushuhuda huu https://www.youtube.com/watch?v=aeSNc1RJkLs

SIO KILA RAFIKI NI MZURI
Marafiki wanaweza kuwa watu wema vilevile kuwa watu wabaya. Dada mmoja alipata roho ya nyoka "spirit of snake" kupitia marafiki zake. Roho hii ilimrudisha nyuma sana katika mambo yake mpaka masomo.Roho hii ilifanya agano naye kwa njia ya tatoo. Kwa njia hiyo hii roho imekuwa ikimtumia huyu dada kuwapeleka watu kuzimu. Watu wote watakaomtamani au watakaomkasirisha huwapeleka kuzimu. Tuwe makini sana hususani wakina kaka wanaopenda sana wanawake na pia wakina dada wanaopenda sana wanaume. Kwa maelezo zaidi bofya link hii uone kwa undani ushuhuda huu https://www.youtube.com/watch?v=QiJtio9n4Lc&spfreload=10

 USITEST VISIVYOONJWA
Usionje pombe au kilevi chochote maana ukijaribu hutaweza kuacha kirahisi. Mtu mmoja kutoka Cameroon alipokuwa mdogo alikuwa akiumwa na jino. Kisha jirani yake akamshauri aweke tumbaku kwenye jino. Kweli yule kijana akafanya hivyo. Siku ya pili hakuambiwa tena bali alifanya vilevile kwa kuwa alidai ilimsisimua baada ya muda ikawa tabia yake. Aliishi hivyo mpaka alipokuwa chuo ambapo alipatwa na kifua kikuu. Bahati nzuri neema ya Mungu ilimponya. Sina hakika kama neema hii inaweza kukujilia wewe unayevuta sigara, bangi au kunywa pombe au kutumia kilevi chochote. Kwa maelezo zaidi bonyeza link iliyo hapa kuona kwa zaidi https://www.youtube.com/watch?v=rEgCUSWowzMeople

UMUHIMU WA KUOMBA
Wakati mwingine unapoambiwa omba unakata na pengine huoni umuhimu wake kabisa maana umekua ukiona mambo yanaenda hata kama huombi hebu ona hili. Kijana mmoja alipatwa na roho ya ushoga "spirit of gay" wakati akiwa anaogelea. Utaona watu wengi wanaingia kwenye maangamizi kwa sababu tu hawaombi. Kama u mdau wa kuto kuomba hebu badili leo hayo mazoea. Roho hi iliyo mwingia ni mfano tu yamkini ziko roho nyingi zinazoweza kukuvaa kama huna kinga ya damu ya Yesu. Kwa maelezo zaidi bonyeza hii link ujionee kwa macho https://www.youtube.com/watch?v=J5WxzcYfKiI

INTENET SIO MBALI LAKINI INATUMIKA VIBAYA
 Kuwa makini na facebook. Kumbe shetani hutumia wasichana na wanaume wazuri mitandaoni ili kuwakamata vijana wengi na kuwaonganisha katika ulimwengu wa giza. Usipende kujiunga urafiki na watu usiowajua maana inawezekana ni maagent wa shetani. Hebu tazama kijana huyu ambaye ameteswa na shetani sababu ya facebook. Bonyeza hii link ujionee kwa macho https://www.youtube.com/watch?v=IS5pWiaiyh0

MIZIKI YA DUNIA SI MIZURI
Kuwa makini na miziki kwani mapepo na roho za shetani zimetumika sana kuwateka watu. Kijana mmoja alitekwa maisha yake na roho za kuzimu kisa muziki. Leo hii yakupasa uwe macho kama unapenda miziki ya dunia achana nayo kuanzia sasa ili uwe salama. Chaguo ni lako. Kwa macho jionee jinsi miziki ya dunia ilivyomtesa kijana huyu na kumpa maangamizi bonyeza hii link https://www.youtube.com/watch?v=TjbllQA3lfo

NIMEPATA UKIMWI KWA SABABU SIKUTII SAUTI YA MUNGU
ASOMAYE NA AFAHAMU!!
Naitwa Anna naishi Tabata, nimezaliwa mwaka 1987 hapahapa Dar, nina Elimu ya Chuo Kikuu.Ninatoa ushuhuda huu uwe onyo na fundisho kwa wadogo zangu na dada zangu. Hapa nilipo ni mwathirika wa Ukimwi. Niliokoka mwaka 2003 na kwa kweli nalimuona Bwana katika maisha yangu ya wokovu,  nilifurahia maisha niliyokuwa nayo kwakweli, washirika na Mchungaji walinipenda sana na pia nilikuwa kiongozi wa sifa pale kanisani. Baada ya kumaliza Chuo na kupata shahada yangu nilifanikiwa kupata kazi katika Benki moja hapa hapa Jijini Dar.

Miaka ikaenda na umri wa kuolewa ulipofika pale kanisani kulikuwa na kijana mmoja alikuwa akimpenda sana Mungu na kujitoa kwa huduma pale kanisani, huyo kijana alitaka kunioa...., nikakubali! Tatizo yule kijana alikuwa na Elimu ya kidato cha nne na alikuwa akifanya biashara ndogo ndogo ambazo zilikuwa zikimwingizia kipato na kuweza kuyamudu maisha yake ya kila siku. Kuna wakati nilikuwa najaribiwa nimwache kwani niliona hanifai kwani mimi nilitaka mtu mwenye elimu kama yangu au angalau anizidi na pia niliwaza kuwa itakuwa shida kwangu kumtii na kunyenyekea akizungumza kama Kiongozi wa famila na wakati nimesoma kuliko yeye, kweli hilo lilinitesa saaana. Alipotaka kumwambia Mchungaji juu ya mahusiano yetu nilimwambia tusubiri kidogo tusomane tabia ingawa kiukweli sikuwa na nia hiyo,,, nilikuwa nataka kubuy time ili ikitokea kijana handsome na msomi kuliko huyo atokee ili nibadiri maamuzi. 
Kweli siku ikaja nikiwa natoka kanisani siku moja kijana mmoja tulikuwa tunasali naye alinibeba kwa gari yake njiani kila mmoja alikuwa kimyaaaa!!! Nikawa nawaza moyoni kuwa huyu ndiye mwanaume mwenye sifa za kuitwa mume wangu lakini kamwe nisingeweza kumwambia kitu. Safari ikaendelea tukafika nyumbani akanishusha. Niliumiaaaa sana kwanini hakusema neno lolote?????

Ikawa jioni kisha asubuhi siku nyingine, siku hiyo nikiwa kazini simu yangu ya mkononi iliita moyoni nikawa natamani awe yule kijana. Kuangalia simu ilikuwa ni ya yule kijana kweli, niliruka kwa furaha bila hata kujua anaenda kusema nini.., alinisalimu kisha akaomba anitoe out siku hiyo.., nikwambie ndugu yangu toka niokoke ndio mara ya kwanza nilimsikia mtu akiniambia kutoka out, na hapo nilijibu bila kufikiri mara mbili.., YEEEEES!!! Alicheka akakata simu nami nikabaki nimeishika ile simu mpaka rafiki yangu pale ofisini aliponishtua akinitania kuwa mapenzi yataniua kwani yeye alijua naongea na yule mchumba wangu kwani walimfahamu baadhi ya rafiki zangu na hapo wapo walionitia moyo kuolewa naye na wengine waliniona zuzu kuwa nataka kuolewa na mtu nisiyeendana naye kwani hakuwa na cash ya kutosha.

Baada ya simu ile kiukweli nilishaanza kumdharau yule mchumba wa mwanzo hata sikutaka hata kuona simu yake wala meseji, nikawa najibu nionavyo ingawa yeye alikuwa mnyenyekevu na siku zote alinitia moyo kuwa ipo siku maisha yatabadirika na kuwa vile nataka.., hapo tena sikutaka kusikia kitu ila huyu kijana mpya. Siku hiyo tumetoka out tulienda Serena na hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kwenda hapo kufurahi.., tukiwa hapo tuliongea mengi ila sikusikia lolote juu ya mahusiano, nilianza kumchukia kidogo kidogo. Baada ya masaa kama mawili alisimama akaenda msalani, siku hiyo ndo niligundua kuwa alikuwa ni Mhasibu kwenye Kampuni moja hapa
jijini na alikuwa na Masters so hapo niliona niko na mwenye sifa haaaasa!! Ambaye nilijua ndugu, rafiki na hata kanisani wakijua ndo mtarajiwa nitaheshimiwa zaidi. Aliporudi yule kijana alikaa kimyaa kama mtu aliyekuwa akitafakari jambo.., akaniuliza swali.., Anna will you marry me?? Kweli nilingoja wakati kama huo ufikeeee.., nilitabasamu.., nikajibu.., Yes baby!!


Alisimama akanikumbatia nami bila kufikiria niliitikia. Alinirudisha home siku hiyo nilikuwa na furaha sana. Yule kijana alizidisha upendo kwangu kweli nikajisahau kuwa nimeokoka.., akawa ananichukua kwenda kwake Mbezi Beach tukawa tunashinda wote mpaka usiku, na wakati mwingine nalipotoka kazini nilikwenda kwake bila hata kusema, penzi lilipozidi tukawa tunashiriki tendo la ndoa na kwa jinsi nilivyompenda sikujali kwenda bila kinga sembuse kuwa tutendalo ni dhambi mbele za Mungu. Yule kijana wa mwanzo alipoona vituko vimezidi aliniacha akaoa binti mwingine.

Mchumba wangu mpya nikamwambia tumwambie Mchungaji tuoane akaniambia twende taratibu kwani mimi ndio wake.., nilikubali japo kwa shingo upande. Haukupita muda niliumwa sana, nikalazwa hospitali VIPIMO NILIVYOFANYIWA VILIONYESHA MBALI NA MARALIA KALI NILIYOKUWA NAYO....., NILIKUWA NIMEATHIRIKAAAAA!! Nililia kwa uchungu saaana, nikajichukia na kumchukia sana yule kijana. Ajabu ni kuwa yule kijana sikumuona tena kuja kuniangalia wala baada ya kutoka sikumuona kanisani tena.
Mdogo wangu na dada yangu, NIPO KITANDANI sasa nikisubiria siku nitaondoka. Nimeandika ushuhuda huu kukuonya...., WEWE MSICHANA MWENZANGU..., SIMAMA NA MUNGU....., MTANGULIZE MUNGU KWA KILA JAMBO...., MACHO YASIKUPOTEZE, ELIMU YAKO, PESA YAKO, UZURI WAKO USIACHE VIKUPOTEZE. MUHESHIMU MUNGU OKOKA KWELI KWELI, KAMA WATEMBEA KWA IMANI BASI AMINI JUU YA MUMEO MUNGU ATAKUPA AFANANAE NAWE KWA VIGEZO VYAKE NA SIO VYAKO WEWE. USIMCHANGANYE MUNGU HUKU UKIISHI MAISHA MACHAFU MTAANI, USIUFANYE MWILI WAKO KITUO CHA UTALII KWANI HILO NI HEKALU LA ROHO MTAKATIFUUU!! USIMDHARAU MTU KWA NAMNA YOYOTE LEO WEWE HUJUI KESHO YA HUYO MTU...., YULE KIJANA NILIMKATAA SASA NI TAJIRI ANA VITU
VYOTE NILIVYOKUWA NATAKA BUT NOW IT'S TOO LATE KWANI NALITAMANI VITU NISIVYOVITOLEA JASHO. KUBALI MTU SI KWA VILE ALIVYO TU BALI PIA ATAKAVYOKUWA BAADAE, KUBALI KUANZA SIFURI NAYE MUINUKE PAMOJA, LIENI NA KUCHEKA PAMOJA.., MTABARIKIWA. NAPIGANA VITA NAMI HAPA NIKIAMINI MUNGU AMENISAMEHE NA SIKU MOJA TUONANE MBINGUNI.
Nakupenda sana. Mimi Anna K

KUNA WAKINA DADA/MAMA WANATUMIA NGUVU ZA GIZA KUVUTA WANAUME
Tunamwitaji Mungu aingilie kati wakati vijana wanapofanya uamuzi wa kuchagua wenzi wao maana kuna watu wanatumia nguvu za giza kupata wanaume au wanawake. Mama mmoja amekuwa akitumia shanga kiunoni ama mkononi kuvuta wanaume. Ewe dada, kaka kuwa makini mweke Mungu wa kwanza kama ndio uko kwenye hatua hii kuliko akili zako au hisia ili usiingie gharama usioweza kuilipia. Bonyeza hii link ili ujionee kwa macho https://www.youtube.com/watch?v=-7AAfVqEbTQ

UMUHIMU WA KUTEMBEA NA YESU  
Mama mmoja aliingiliwa na jini akiwa anafua mtoni saa 7 za mchana. Jini hilo lilimfanya kuwa mwanamke dume kwa kusimamisha mzunguko wake hivyo kumpelekea akose mahusiano ya ndani na mumewe hata akawa mgumba. Kuomba ni swala muhimu zingatia. Bonyeza link hii ili uone ushuhuda huu https://www.youtube.com/watch?v=ml4C4bfSiWo

USIPOKUWA NA YESU UKO MASHAKANI
Kuwa na Yesu ni jambo la muhimu. Dada mmoja aliingiliwa na roho ya ukahaba akiwa darasa la nne tu huko Botswana. Akiwa darasa la saba alikuja mkaka akamwambia kuwa anapenda macho yake kuanzia hapo alitumia macho yake kuvunja ndoa za watu kwa kuchukua waume za watu. Roho hiyo pia ilimfanya mlevi wa kupindukia kwa kunywa bia 24 kwa siku pamoja na whiskey. Mpendwa unayenifuatilia ni muhimu ukakaa na Yesu sawasawa ili uwe salama. Bonyeza link hii ujionee zaidi. https://www.youtube.com/watch?v=Sfdcx7TZabg

ATHARI ZA KUCHANGIA VITU NA WATU
Kuchangia vitu na watu kwaweza kugarimu maisha yako. Dada mmoja alichangia apple na mtu na hapo ikawa mwanzo wa roho ya ukahaba. Kuwa makini usichangie vitu ambavyo si lazima vichangiwe kwa kuwa unaweza kugharimika haijalishi huyo mtu ni wa karibu yako kwa kiasi gani. Hebu bonyeza hii link ujifunze zaidi https://www.youtube.com/watch?v=iZUm4TN5dvA

ATHARI ZA MISINGI MIBOVU KATIKA FAMILIA
Shughulikia misingi ya familia au ukoo wako maana ukiiacha itaharibu maisha yako. Dada mmoja anajikuta akiwa kahaba kwa sababu tu ukoo wao ulikuwa na roho ya ukahaba. Kuanzia mama yake hata ndugu zake. Hii ilimfanya aishi kwa ukahaba siku zote. Tena yeye hakuchagua mvulana awe na pesa asiwe nazo alichojali kwake ni ukahaba tu. Angalia namna watu wanavyoishi kwa mateso bila wao kupenda. Bonyeza link hii uone simulizi yote https://www.youtube.com/watch?v=gLT4z1mEOuc

NAMNA MITANDAO INAVYOWEZA KUWAUNGANISHA WATU NA KUZIMU
Dada mmoja avamiwa na nguvu za giza kupitia skype akizungumza na mhindi mmoja aliyedai kuwa anasaidia waafika wakue kwenye umodo matokeo yake alipata nguvu za kikahaba. Ndugu mpendwa usipende maisha mepesi mepesi kaa na Yesu atakufanikisha muda ukifika kuwa mvumilivu. Shetani ameanzia system ya kutajirisha watu mapema bila kuhangaika hii imefanya wengi wamkatae Yesu na kumwangukia. Bonyeza link hii ujionee https://www.youtube.com/watch?v=A0VSBSpCnQY

NAMNA SHETANI ANAVYOFANYA KAZI MASHULENI
Niliwahi kusoma ushuhuda mmoja ulionishangaza sana. Kilikuwa na shule moja ambayo ilikuwa imezungushiwa uzio. Kwenye mlango mkubwa wa kuingilia shuleni hapo, palikuwa na mti mkubwa sana ambao umekuwapo hapo kwa zaidi ya miaka 50. Kumbe ule mti ulikuwa ni makao ya wachawi. Kila mwanafunzi aliyefika shuleni hapo alianza kuwa anapoteza fahamu shule hiyo ilipoanza haikuwahi kufaulisha wanafunzi wowote, iwe wa kidato cha 2, 4 au 6.

Siku moja katika kipindi cha dini walimwalika mwinjilisti mmoja kuja kufundisha. Wakati anafundisha na kuombea wale wanafunzi. Binti mmoja alilipuka sana na kuanza kukimbia kuelekea kwenye ule mti mkubwa na kuanza kusema "Sisi ni wachawi tunakaa kwenye huu mti, huu mti ni ngome yetu,tumechukuwa fahamu za wanafunzi hawa hakuna hata mmoja atakayefanikiwa." Yakadai kuwa yamegeuza matokeo ya mtihani wa taifa, kwamba huwa wanachanganya fahamu za wasahishaji wanaosahihisha mitihani ya hiyo shule. Kwamba kama wanafunzi akipata 90% msahishaji anaandika 09%. Hebu fikiri ndugu msomaji wanafunzi wangapi maisha yao yameharibika kwa sababu yao. Njia ya kupona mshike Yesu kwa bidii.

VIJANA WALIOPEWA JUKUMU KUWAPELEKA WANAWAKE KUZIMU
Niliwahi kusoma ushuhuda wa mtumishi mmoja wa Mungu. Alisema, siku moja akiwa anahudumia watu ofisini kwake, waliingia vijana wawili ofisini, wakijifanya wahitaji. Lengo lilikuwa kwamba yule mtumishi angetoa pesa kuwasaidia, wangeipeleka kuzimu na kumfunga ili huduma yake isipate upenyo wa fedha. Alipokataa kuwapa fedha na kuwaambia fedha iliokuwepo ni kwa ajili ya kazi ya Mungu na si vinginevyo wale vijana walimkejeli na kumwambia awaombee. Wakati ananyoosha mkono kuwaombea vijana, ghafla kijana mmoja akaanguka chini na kuanza kutembea kama nyoka huku akivua nguo.

Alikuwa akidai kuwa moto ulikuwa ni mkali sana. Alijua nguo zote ikiwemo za ndani, jambo lilomshangaza yule mtumishi ni kwamba katika maumbo ya juu ya sehemu za siri za yule kaka yalikuwa ni kichwa cha nyoka na kwenye tundu ambalo mbegu za kiume hutokea vilitoka vitu kama ulimi wa nyoka. Kwa haraka yule mtumishi alichukua mafuta ya upako na kumwagia katika sehemu za siri za yule kijana, ghafla zile sehemu za siri zikarejea kawaida.

Alipotulia yule mtumishi wa Mungu akamuuliza, Kwa nini sehemu zako za siri zilikuwa kichwa cha nyoka? Akakiri, "Ndio ni kichwa cha nyoka kwa sababu mimi ni mchawi na nimeunganishwa na kuzimu. Na nimetumwa kuwaunganisha wanawake na kuzimu kwa kuzini nao. Ninapozini nao nawaingizia sumu kwenye sehemu zao za siri. Pia alisema kuwa alipewa jukumu la kupanda sumu katika matumbo yao ili kusababisha uvimbe, ugumba na magonjwa mbalimbali". Alipoulizwa ni wanawake wangapi umezini nao ndani ya wiki hizi 2? Akajibu, "Nimezini na wanachuo 8, wamama wafanya biashara 4 na mabinti wasio na kazi kama 6. Fikiria kama wanawake wote hawa wameweza kuingiziwa sumu ya kichawi na kuunganishwa na ufalme wa giza. Je mwisho wa maisha yao utakuwaje?????????????????????????????

APUMBAZWA AKILI SHULENI KWA KUIBIWA NYWELE ZAKE
Mtoto mmoja ambao wazazi wake walikuwa ni maprofesa wa chuo kikuu. Chakushangaza yule mtoto alikuwa wa mwisho darasani. Walijaribu kumletea waalimu mbalimbali wa kumfundisha masomo ya jioni lakini ilishindikana. Mama yake alikuwa ameokoka. Siku moja akiwa anahudhuria maombi mtumishi alipewa ufunuo juu ya yule mama na kusema, "Kuna mama mtoto wake anafeli darasani, umejaribu kila namna ya kumsaidia imeshindikana lakini hivi ninavyoongea mtoto wako amefunguliwa. Nywele zake zilizokuwa zimeibiwa zimeaachiliwa "

Moja kwa moja yule mama akasema, "Asante Yesu kwa kumfungua" Aliporudi nyumbani akamwambia mume wake kuwa mtoto wao amefunguliwa. Pia akamwambia yule mtoto kuwa hatakaa afeli tena. Hazikupita siku nyingi yule mtoto akafanya mtihani. Matokeo yalipotoka alipa maksi za juu tangu alipoanza shule, waalimu walishangaa na kuhisi labda aliibia. Hivyo wakampa mtihani aufanye upya akiwa pekee yake kwenye chumba kingine, chakushangaza alifaulu kuliko hata ya ule mtihani wa awali. Je ni wangapi kama huyu wamekuwa wakionewa hivi? Inawezekana hata wewe umetumbukia katika hili.

2 comments:

  1. Ni neno la Mungu pekee ndilo linaloweza kutuweka huru. Tumwamini Mungu.

    ReplyDelete
  2. Asante Kwa shuhuda nimebalikiwa Sana hakika Mungu ni mkuu

    ReplyDelete