Bwana Yesu asifiwe, kuanzia tarehe 1/1/2017 tutakuwa tukihamia katika website yetu iitwayo www.egospeltz.org

ARCHIEVE 2

BILA MABADILIKO ITAKUGHARIMU


Unapoanza mwaka usidhani unaanza kwa bahati mbaya tu. Sikiliza naomba unielewe vizuri, wapo wangapi kama wewe hawakuweza kupita mwaka lakini wewe umepita si tu kwamba umestahili. Ngoja nikueleze unajua kukaa duniani pia ni majaribu maana kuna hesabu inatakiwa kutolewa mbele za Bwana wetu Yesu Kristo. Hivyo natamani uelewe kuwa kuna majukumu ambayo Mungu ameyataka kwako yatendeke yasiofanania na wengine.

Tunaposoma Mt 25:14-30 tunaona watumwa waliopewa talanta na Bwana wao alipokuwa akisafiri wakafanyie kazi. Ili kila mmoja alete ujira wake sawasawa na namna walivyotumika hata Bwana wao atakaporudi. Walipewa mmoja talanta tano, mwingine mbili na mwingine moja na biblia inasema kila mmoja sawa na kadiri ya uwezo wake.

Ina maana gani? Bwana wao ni Yesu Kristo, watumwa ni mimi na wewe na talanta ni vipawa, karama au makusudi ya Mungu. Utagundua talanta hizi walipewa kwa idadi isiyofanana hii ina maana makusudi ya Mungu kwa watu hayafanani hivyo usije ukaiga kusudi la mwenzio itakugharimu. Maana Bwana alitoa hiyo talanta anajua ya kuwa hakuna mwingine aliyepewa talanta kama yako. Ukiiga ya mwingine utashindwa kuzalisha ya kwako. Na ndio maana watu hawafanani kimajina ili kutofautisha makusudi ya Mungu katika maisha yetu.

Kama biblia inavyotueleza hivi leo umeingia mwaka mpya jiulize nafanya nini utagundua haukuingia kwa bahati mbaya. Fikiria gari alilopanda mwenzako ndio hilo unalopanda wewe lakini yeye alipata ajali mpaka kufa, chakula anachokula mwingine ndio hicho unachokula wewe lakini mwenzio kapelekwa kwa operation. Haya ni mambo ya ajabu yahasimuliki kwa kirahisi mno lakini ngoja nikueleze hukuja duniani kushangaa magari na magorofa wala kushabikia wengine.

Wewe ni sawasawa na mchezaji uwanjani. Una namba yako na hiyo namba yako haifanani na mwingine usipocheza vizuri katika namba yako maana yake utapelekea timu kushindwa na hata hivyo kocha kwa sababu anataka kuimarisha timu akigundua wewe ni mwenye makosa utakaa benchi tu. Kwa huruma kocha huweza kukupa muda wa kubadilika usipobadilika basi anakutoa maana sabu zipo nyingi.Hivi uliwahi kujiuliza kwa nini hatuna Yesu wengi duniani waokoe watu hii ni kwa sababu kila alie kuja duniani alikuja kwa mpango kamili.

Ngoja nikuambie kuna watu wanafanya mambo ambayo Mungu hakuwaagiza na hiyo itawagharimu wengi sana maana wanashulika sana na mavazi, kula, kunywa, kusoma, kazi, mume, mke au watoto na vingine vyenye mfano na hivi. Kumbe wanajiangamiza wenyewe maana sio talanta waliopewa.

Nataka ulewe kuwa katika mwaka Mungu ambao amekupa kuna kuongezeka na kupungua pia hebu tutatazame nini kilitokea Bwana wao aliporudi biblia inasema katika Mt 25:19-30 tunaona majibizano kati ya wale watumwa na Bwana wao aliporudi. Wale waliozalishwa walibarikiwa na kuongezewa lakini yule mmoja ambaye hakuzalisha alipokonywa na kupewa aliozalisha 5 ziada kisha akatupwa kwenye giza ambako ndiko kuliko na kilio na kusaga meno.

Ndugu yangu jifunze kunyenyekea acha kuishi kwa mkumbo itakugarimu. Utaratibu wa Mungu ni kwamba una gharimika kwanza kisha anakubariki lakini utaratibu wa shetani unabarikiwa kwanza kisha gharama baadae. Sikiliza kile Mungu anachokufundisha badilika anza kuzalisha.

Barikiwa sana


Na Henry Nicholaus  

MITEGO YA ADUI


Tukubali tukatae tunae adui naye ana mawakala wake. Kama Mungu naye alivyo na mawakala wake maana shetani amekopi na kupesti utaratibu wa Mungu na hata mfumo wa serikali yake. Naye kila siku hutega mitego. Kama huwezi kutegua mitego huwezi kuishi maisha ya ushindi. Katika mitego kuna umaskini, magonjwa, kufungwa ufahamu, uvunjifu wa ndoa, kufeli, uzinzi n.k  Mitego hiyo huweza kufanyika kwa maneno yako au maneno ya wengine Mith 6:2. Mitego inaweza ikategwa kutokana na vinywa vyetu. Wako wengine wako kwenye magonjwa, madeni, matatizo mengine hii ni kwa sababu shetani amewatega.

Licha Ayubu kuishi maisha yasiyo na dhambi bado shetani alimtega Ayu 22:10. Hiyo mitego ikiteguka unakuwa huru. Mitego haiondoki kwa sababu unaichukia bali huondoka kwa sababu unajua kuitegua. Unaweza ukategwa katika fedha zako, ukazila pasipo kutoa zaka. Hivyo basi hizo pesa zinakuwa mtego kwako. Katika Eze 21:21 Mfalme wa Babeli alikaa katika njia panda akaweka terafi (ni kipimo cha kichawi ambacho hutumika kukamata watu na kuangalia nyota zao au kuwafanya chochote. Kwa mfano kupitia terafi huweza kuangalia figo na kutia ugonjwa ndani kisha ukaanza kusumbuliwa na gonjwa hata madaktari wasiweze kukupatia tiba.

Laana ya mizimu hutokana na matendo ya shetani waliofanya baba zetu kwa kumtumikia. Kut 20:4-5 Kuna laana zinatutafuana lakini imejengeka kuwa ni mazoea kwetu. Laana utaiagundua kwa matokeo. Ukiwa unapenda sana kukuna sikio ni moja wapo ya ishara  ya kutafunwa na laana za mizimu. Isa 25:7 Ukatae uso wa stara maana kuna maisha ulionayo ambayo huwezi kushangilia au kufurahi. Uso wa stara ni uso wa nuksi usiobadilika au wenye mikosi.Ukiwa hata fedha haziwezi kuja kwako. Mal 2:3 Mungu akikemea mbegu kwa ajili yako unakufa, unafilisika, unakopa ovyo, ulivyoanzisha vinakufa kama biashara. Ukipakwa mavi katika uso wako hupatikibali. Katika ulimwengu wa roho kuna watu wamepakwa mavi.

Uso wa sitara ni uso mbaya sana. Laana ya mizimu ndio inayo vutia uso wa stara. Kama baba yako hakununua baiskeli wewe utapakizwa boda boda katika maisha yako. Uso wa stara hauondoki kwa kuomba, lazima ufundishwe na mtu mwenye ufahamu.

Ukiwa na utaji unakuwa kama mtu aliyefunikwa na kitu usoni asiyeweza kuona vitu vizuri. Unakuwa mtu wa kuiga huna mawazo au mtazamo wa kwako.Sisi hatuna kopi duniani. Ndio maana unaweza ukakuta mtu analalamika anasema nchi hii haina pesa. Kumbe yeye hana pesa ila nchi ina pesa. Ukiona mtu wa namna hii ujue ya kuwa uso wake una utaji.Utaji ukivunjika kwko utajua mpango wa Mungu kkatika maisha yako.2Kor 3 ishara ya kuwa na utaji ni uzito wa kufikiria.

Hivyo ndugu yangu kataa roho ya utaji kwa jina la Yesu na roho ya stara pia. Ili uweze kufanya mambo yako kwa ustadi na weledi katika kumwamini Mungu .

Ubarikiwe

Na Henry Nicholaus  


 MAOMBI


Maombi ni mtandao wa kiroho ambao moja kwa moja hutuunganisha na baba yetu aliye mbinguni.

Maombi kwa mkristo ni silaha pekee ambayo huitumia katika kupambana na kuyashinda majaribu mbalimbali unayokumbambana nayo.

Lakini wakristo tulio wengi hatujui jinsi ya kuomba hii ni sababu hatumruhusu Roho Mtakatifu aingie moyoni mwetu na atawale maisha yetu ya kiroho tunakua na nia mbili Yak 4:4-5

Na wengi wetu tunategemea vitu tuvipate kirahisi hali tukijua yupo mpangamizi wa ulimwengu.Lakini hatuvipa kwa sababu hatuombi Yak 4:2.Pia katika maombi yetu yatupasa kusemezana na Bwana Mungu wetu kwa unyenyekevu hali tukijua kuwa uwezo na mamlaka ni katika yeye peke yake

Katika maombi yatubidi tumsihi sana Mungu wetu ili atusaidie tuweze kuvaa vinywa vyenye mamlaka.Hii ni kwa sababu kwa uamuzi wa kuwa mwana maombi.Awali ya yote yakupasa kuwa na imani iambatanayo na matendo ili kutokana na imani iliyojitosheleza tuweze kufikia kiwango cha juu cha maombi ambapo ndipo tunapopokea mamlaka Efe 4:13 "Hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa amani na kufahamu sana mwana wa Mungu hata kwa mtu mkamilifu hata kufika kwenye cheo cha ukamilifu wa kristo".

Hivyo basi kama vile jinsi Yesu alivyowafundisha wanafunzi wake kuomba si zaidi sana na sisi pia tumwombe Bwana wetu Yesu Kristo azidi kutuonyesha jinsi ya kuomba .Amen

Barikiwa

Na Anotite Sanga



IKIMBIE ZINAA


Mw 6: 1 - 5 Mungu hukasirishwa sana na zinaa.Watu hawa katika kipindi cha Nuhu walipendezwa na zinaa mno.Hivyo Mungu akaazimu awaangamize kwa maji.Lakini utagundua hii ni hukumu ya pili.Lakini hukumu ya kwanza ilikuwa ni kupunguzwa kwa siku za kuishi.Swali ambalo tutajiuliza kwa nini siku zipunguzwe?Hii ni kwa sababu watu wanakumbatia dhambi na dhambi hiyo ni zinaa.Biblia inatufundisha kabla ya kizazi cha Nuhu dhambi ilikuwepo Mw 4:8 -10.Lakini biblia haikutufundisha kuwa Mungu alipunguza miaka.Hivyo tunajua dhambi ya zinaa ndio kigezo ambacho kilimfanya Mungu apunguze siku za kuishi.Bado tunaweza kujiuliza kwa nini siku zipunguzwe neno lake linatueleza kuwa zinaa ndio dhambi inayofanyika juu ya mtu.Hivyo huleta unajisi wa Mungu maana miili yetu ni hekalu lake 1Kor 3:16

Hivyo basi tumekuwa wanyany'anyi maana kusema nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala lakini nyinyi mmeifanya kuwa pango la wanyany'anyi Mt 21:13.Lakini wale wasomaji wa biblia wataelewa kuwa Sodoma na Gomora iliangamizwa kwa sababu ya zinaa Mw 18:20 - 21, 19:1 - 8, Yuda 1:7.Ikiwa Mungu aliwatenda hivi Sodoma na Gomora ni kitu gani kilichowafanya wanadamu wa leo amini kuwa Mungu amebadili mawazo yake juu ya watendao uasherati? Yer 30:23,Wimb 2:7,Mith 6:23 - 26

1Sam 2:22 - 34 Hofini na Fenehasi walipangiwa kufa siku moja kwa sababu walifanya zinaa nao bado walikuwa wakifurahia.Na hii ndio sababu Mungu anatuambia kuwa hawezi kuchukuliana na mwanadamu afanyae mambo ya jinsi hii.Lakini Mungu anatufundisha kwa habari ya siku za mwisho kuwa mambo yaliotokea kipindi cha Nuhu na wakati wa kipindi cha Sodoma na Gomora nao yatokea pia katika siku za usoni 2Tim 3:1 - 6, kwa sababu tu wanawake wengi wanapenda fedha na anasa wamejikuta wakiingia kwenye uzinifu.

Swali la kujiuliza hivi ni kwa nini watu wanaelezwa kuwa uzinifu au uasherati ni mbaya lakini wanaendelea.Hii ni kwa sababu kuwa wote hawana akili kabisa Mith 6:32.Tunaweza kujiuliza kuwa sababu ya ujinga inatoka wapi?Roho wa Mungu anatueleza inatoka Lk 8:9 - 14.Ni dhahiri kabisa palipo na zinaa kuna uharibifu kama Ukimwi,kutokuolewa/kuoa,kuvunjika kwa ndoa,kufungwa kwa mfuko wa uzazi au kutozalisha mbegu za uzazi na mwisho kabisa mauti na ndio maana shetani anawekeza sana mambo haya katika movie,internet na muziki.Nilikuwa namwambia mtu mmoja kilichobaki tu ni picha za ngono kuhalalishwa kuwa matangazo halali,ili kubandikwa ukutani na kuonyeshwa kwenye video.

Nataka kukueleza kuwa jambo hili halikuja kwako kwa bahati mbaya, na ndicho niwaambiacho watu kuwa neno haliji ili ulisikie tu bali huja kwa mpango maalum.Hivyo hata habari za kukimbia zinaa zimekuja kwako kwa mpango maalum1Kor 10:11.Kitu cha muhimu upate kujua kuwa zinaa inakimbiwa ukitaka kuishinda lakini ukishindana nayo utaanguka tuu na hii ndio sababu ya Yusufu kuchopoka wakati mke wa Potifa alipokuwa akimlamisha kufanya zinaa Mw 39:7 - 12.Hivyo usijifanye komandoo mbele ya zinaa 1Kor 10:12

Na Henry Nicholaus    


 ISHI KULINGANA NA NYAKATI NA MAJIRA YALIYOAMRIWA NA MUNGU KWAKO


Mhubiri 3:1-8
"Kila jambo kuna majira yake na wakati.Kwa kila kusudi chini ya mbingu".Mhu 3:1

Wakati kwa kusudi bali majira kwa jambo.

Kuna tofauti gani kati ya wakati na majira? Wakati ni kipindi alichokuwa nacho mtu kwa ujumla LAKINI Majira ni muda halisi uliopo ndani ya wakati.Wakati hubeba kusudi ambalo hutimilika kwa kuzaliwa kwa majira ya mambo tofautitofauti yanayoleta ukamilifu ya wakati huo.

Mfano wa kawaida
Vijana walio na umri kwanzia miaka 12-18 kwa mtazamo wa kawaida wanatazamiwa kuwa katika wakati wa kupata elimu ya sekondari LAKINI katika wakati huo hubeba majira mbalimbali kama majira ya mitihani ili kuweza kupimwa na kufikia kusudi ambalo ni kumaliza elimu hiyo,likizo kwa mapumziko na mengineyo

Kwa nini tuishi kulingana na majira na nyakati zilizoamriwa kwetu?

Inapaswa Ijulikane kuwa Mungu alitujua kabla hatujakuwapo kwenye ulimwengu huu,hivyo nyakati na majira yetu katika maisha yalishapangwa au kuwekwa fixed Yer 1:4a

Sababu

  i)  Sisi ni wawakilishi wa maisha haya tuliopewa na Mungu kwa ajili ya utukufu wake hapa duniani.Hivyo           imetupasa kuyatumia kama ilivyo wakati na majira alivyotuamuru sababu tutatoa hesabu siku ya mwisho ya habari ya uwakili wetu 1Pet 1:17


ii) Kulingana na nyakati na majira kunatuwezesha kupata mafanikio aliyokusudia Mungu kwetu Isa 48:17

Mungu awabariki

Na Salome .J. Senkoro


JE UNA HABARI KUHUSU TUKIO LA KUTISHA LINALOKUJA HIVI KARIBUNI?


DALILI ya mvua ni mawingu. Mtu mwenye busara aliyeanika nguo zake nje, anapoona mawingu yametanda kila mahali, anajua kwamba mvua wakati wowote inaweza kunyesha, hivyo anafanya haraka kwenda kuzianua nguo hizo. Vivyo hivyo, Yesu Kristo anatuonya kwa msingi huohuo, kuzitambua ishara za zamani hizi yaani dalili za nyakati hizi za mwisho, au za mwisho wa dunia, na kuyajua yale yanayokuja ili tujiandae vema kuyakabili. Biblia inasema katika MATHAYO 16:2-3, ”Akajibu akawaambia kukiwa jioni, mwasema, kutakuwa na kianga; kwa maana mbingu ni nyekundu. Na asubuhi, mwasema, leo kutakuwa na dhoruba; kwa maana mbingu ni nyekundu, tena kumetanda. Enyi wanafiki, mwajua kuutambua uso wa mbingu; lakini, je ishara za zamani hizi hamwezi kuzitambua?“ Sasa je, ni nini dalili za mwisho wa dunia?

Kilicho na mwanzo kina mwisho, na mwisho wa dunia uko karibu sana. Dalili mbalimbali za mwisho wa dunia, zinatajwa katika Biblia, kwa mfano katika MATHAYO 24:3-14; 1TIMOTHEO 4:1-5; 2 TIMOTHEO 3:1-5; na UFUNUO WA YOHANA 22:6-7,10-12. Dalili zote zimetimia, na zinazidi kuwa dhahiri mbele ya macho yetu. Moja kati ya dalili zinazotajwa ni wachafu kuwa wachafu na maasi kuongezeka (UFUNUO 22:11; MATHAYO 24:12). Kabla ya maangamizo wakati wa Nuhu na pia wakati wa Sodoma na Gomora, uchafu uliongezeka sana. Vivyo hivyo siku hizi, tukiona mambo haya ya uchafu yanaongezeka, tujue hiyo ni dalili ya mwisho wa dunia. Je, uchafu huu umeongezeka hivi leo? Jibu ni kwamba, ni kwa namna ya kutisha.

Pamoja na sheria kali ya kujamiiana, ambayo inawafanya watu wanaonajisi watoto wadogo, wabakaji na walawiti, kupewa adhabu ya kifungo; bado vitendo hivi vinaongezeka kwa kasi kama vile watu hawajali! Karibu kila siku tunasikia habari hizi katika vyombo vya habari. Wengine wanaripotiwa kulawiti watoto wadogo waliowazaa wenyewe! Wengine wanalawiti wazee wa miaka zaidi ya sabini! Wengine wanawabaka mama zao! Mtu mmoja anaripotiwa kuwalawiti watoto wadogo watano wa shule ya msingi, zamu kwa zamu! Sehemu mbalimbali duniani, wanaume wanaoripotiwa kuwaacha wake zao kwa sababu hawataki kulawitiwa, wameongezeka sana. Huko Marekani na Ulaya, ndoa za wanaume kwa wanaume (mashoga) na wanawake kwa wanawake(wasagaji) zimekuwa ni jambo la kawaida. Waziri Mkuu wa nchi moja kubwa Ulaya, anataka ushoga uhalalishwe na Bunge la nchi yake. Maaskofu wa dhehebu moja kubwa la Ukristo, hivi karibuni, walipiga kampeni ya kutaka ushoga uhalalishwe! Wachafu watazidi kuwa wachafu!

Dalili nyingine ya mwisho wa dunia, inatajwa katika Biblia, ingawa haiko wazi sana katika tafsiri ya Kiswahili. Katika Biblia ya Kiingereza ya tafsiri ya King James Version(KJV) katika MATHAYO 24:7, tunasoma, …. ”…and there shall be famines and pestilences…..“ "Pestilences,“ ni magonjwa mabaya ya kuambukiza yasiyokuwa na dawa au tiba. Leo tunaishi nyakati za kuwepo kwa Ukimwi, ugonjwa mbaya wa kuambukiza usio na tiba. Hii ni dalili ya mwisho wa dunia.

Vivyo hivyo, dalili nyingine inatajwa katika MATHAYO 24:14, ”Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.“Kwa kutumia teknolojia ya kisasa, Injili inahubiriwa kwa kasi ya kutisha. Kwa mfano kwa kutumia ”satellite“, Mwinjilisti mmoja anayeitwa Billy Graham, tarehe 14 April 1996, alihubiri Injili na nchi zote ulimwenguni walisikia Injili kwa wakati huohuo, wakati yeye akiwa Marekani. Hatusemi kwamba mwisho wa dunia utakuwa leo au kesho. Siku ile wala saa, hakuna aijuaye, lakini yote haya ni mawingu ambayo ni dalili ya mvua! Maana yake ni kwamba, tuko ukingoni kabisa na wakati wowote ule mwisho wa dunia unakuja!

Mwisho wa dunia utakuwaje? Mfululizo wa matukio ya mwisho wa dunia, utatanguliwa na tukio la kutisha litakalotokea ulimwenguni wakati wowote kuanzia sasa, maana dalili za mwisho huu tumekwisha kuona kwamba zinatimia machoni petu hivi sasa. Tukio hili , linaitwa ”Kunyakuliwa kwa watu waliookoka“, na linaelezwa katika 1 WATHESALONIKE 4:15-17, "Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele…“

 Kunyakuliwa, ni tendo la kuchukuliwa kwa kitu ghafla, kwa kasi kubwa na kuondolewa pale kilipokuwa; katika hali ya kuwaacha watu wamepigwa butwaa, kwa jinsi wasivyoweza kukipata kitu hicho tena. Watu waliookoka, muda si mrefu ujao, watanyakuliwa kwa jinsi hii na Yesu Kristo. Yesu anakuja kufanya kazi hii, haraka wala hatakawia (WAEBRANIA 10:37). Siku ya kunyakuliwa kwa watu waliookoka, sehemu nyingine dunia itakuwa usiku, sehemu nyingine mchana, maana majira duniani yanatofautiana. Jua likitua sehemu moja ya dunia, linachomoza sehemu nyingine ya dunia.

Wakati wa kunyakuliwa kwa watu waliookoka, ikiwa ni mchana, watu wote waliokufa tangu zamani za kale wakiwa wameokoka na wakawa wamekwenda mbinguni, watafufuliwa na kutokea duniani tena. Kila mmoja atawaona. Watakuwepo watu wengi kwa ghafla, mitaani kila mahali, waliokufa zamani wakiwa wameokoka. Hata kama kwenye makaburi ya zamani, siku hizi kuna Jengo la ofisi, watatokea humo humo ofisini. Dakika moja kufumba na kufumbua, watu waliookoka ambao wako hai duniani nao wataungana pamoja nao, na wote watabadilishwa miili yao na kupewa miili ya utukufu wa milele, isiyoharibika. Biblia inasema katika 1WAKORINTHO 15:52-53, ”Kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.“

 Katika wale watakaokuwako duniani, watatwaliwa wale waliookoka tu na kuishi katika utakatifu mpaka mwisho. Watakuwepo wawili wakilima kondeni au shambani, mmoja ameokoka na mwingine hajaokoka, ni mwenye dhambi. Aliyeokoka atatwaliwa, ambaye hajaokoka ataachwa. Ikiwa ni katika basi, treni au eropleni; dereva au rubani ameokoka, atatwaliwa, na wenye dhambi watabaki. Tunasoma katika MATHAYO 24:40-41, ”Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa; wanawake wawili watakuwa wakisaga, mmoja atwaliwa, mmoja aachwa.“

 Ikiwa itakuwa usiku, na katika familia fulani mume hajaokoka, mke ameokoka, watoto wakubwa hawajaokoka, na wako watoto wadogo wasiojua mema na mabaya; mume huyo mlevi anayempiga vita mkewe kwa sababu ameokoka, ataamka asubuhi na kushangaa kuona mkewe kitandani na watoto wadogo hawapo. Atawauliza watoto wakubwa, Mama yenu yuko wapi?“ watajibu, ”hatujui“. Atatoka nje kwenda kuuliza, na kila mahali itaripotiwa Polisi, kwamba wako watu waliotoweka usiku, pamoja na watoto wote wadogo. Katika kituo cha Polisi pia, kutakuwepo na polisi waliotwaliwa. Baada ya uchunguzi duniani kote, waandishi wa habari ambao hawajaokoka, walioachwa, watatoa ripoti katika magazeti, ”Mamilioni ya watu kote duniani wameripotiwa kutoweka usiku wa jana. Uchunguzi umeonyesha kwamba waliotoweka ni walokole ambao wamekuwa wakidhaniwa kuwa wamechanganyikiwa au ”kupotea.“ Taarifa zaidi zinaeleza kwamba watoto wadogo wote pia wametoweka. Taarifa za uchunguzi zinaonyesha kwamba waliotoweka wamenyakuliwa kwenda kumlaki Yesu mawinguni kama walokole walivyokuwa wakihubiri!“

 Hawa watakaotwaliwa, wataungana na wale waliofufuliwa, na kisha wote kwa pamoja; watavutwa kama kwa sumaku, kwa mvuto utakaotoka kwa Yesu atakayekuwa mawinguni. Yeye hataonekana kwa wale watakaokuwako duniani. Wenye dhambi nao watajaribu kupaa, haitawezekana. Itakuwa kama kuku na ndege wanaposhitushwa na kishindo. Ndege hupaa angani, lakini kuku akijaribu kupaa huishia kwenye kichanja cha kuanikia vyombo! Sumaku itawavuta waliookoka tu, kama jinsi sumaku inavyovuta vyuma tu na kuacha mchanga au udongo! Baada ya wenye dhambi kuachwa, ndipo kitakapokuwapo kilio na kusaga meno hapa duniani. Itafuata dhiki kubwa ya miaka saba, ambayo namna yake haijawahi kutokea. Biblia inasema katika MATHAYO 24:21, ”Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.“ Wenye dhambi watateswa kwa namna ya kutisha. Watu watatamani kufa kutokana na mateso na maumivu, lakini mauti itakuwa imeondolewa (UFUNUO 9:2-6). Wataiambia milima na miamba, tuangukieni, watamwomba Mungu awahurumie, huruma na uvumilivu wake utakuwa umekoma (UFUNUO 6:15-17; ISAYA 26:16-18). Wale walionyakuliwa huko juu watakuwa katika karamu ya Arusi ya Mwanakondoo baada ya kupewa kila mtu taji zake (UFUNUO 19:5-9; 2WAKORINTHO 5:8-10).


Mpendwa msomaji, parapanda inaweza kulia usiku wa leo. Je, utakuwa kundi lipi? Utanyakuliwa au utaachwa? Ikiwa wewe ni mwenye dhambi, hujaokoka, utaachwa kwa hakika. Hata hivyo, bado una nafasi ya kutubu dhambi zako. Ukifanya hivyo huku ukimaanisha moyoni kuziacha dhambi zote, utasamehewa sasa hivi, na hivyo kuokoka. Na sasa hivi utahesabiwa kuwa miongoni mwa wale watakaonyakuliwa (MITHALI 28:13; LUKA 1:77). Je uko tayari kutubu, na kuokoka? Najua uko tayari. Basi fuatisha sala hii fupi kwa dhati kutoka moyoni:
 
”Mungu wangu, asante kwa kunipa ujumbe huu kabla tukio hili halijatokea. Natubu dhambi zangu zote nikimaanisha kuziacha. Yesu Kristo naomba unisamehe dhambi zangu zote na kuniokoa. Naamini sasa kwamba umeniokoa, katika Jina la Yesu. Amen.“


 Tayari umeokoka. Ili uutunze wokovu wako mpaka wakati wa Kunyakuliwa, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu (ZABURI 119:11).
MUNGU AKUBARIKI!!!

Na Henry Nicholaus

SPEAK THE WORD OF GOD IN A LOUD VOICE SO THAT IT CAN CAUSE EFFECT IN YOUR LIFE


"Kitabu hiki cha Torati kisiondoke kinywa mwako bali yatafakari maneno yake usiku na mchana upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yalioandikwa humo maana ndipo utakapoifanikisha njia yako kisha ndipo utakapositawi sana" Yos 1:8

Tunapoutafakari kwa kina sana mstari huu tuna mengi ya kujiuliza.Kuna mahusiano gani ya neno la Mungu kuwa kinywani mwako na kufanikiwa au kustawi kwa mtu.Uwepo wa neno la Mungu kinywani husababisha kinywa kuwa na mamlaka ya uumbaji.Mamalaka hayo ya uumbaji ndio ambayo huzaa ustawi na mafanikio.Tunaposoma Mw 1:3 Mungu akasema na iwe nuru ikawa nuru.Tunaona nuru ilikuja kwa sababu ya lile neno liliotamkwa kutoka katika kinywa cha Mungu.Na ukizidi kufuatilia utagundua kuwa huu ndio utaratibu ambao Mungu aliutumia katika uumbaji isipokuwa wa mwanadamu.

Kinywa kina nguvu ya uumbaji unapotaka kufanikiwa tamka hilo neno ulilolisikia kwa sauti kupitia kinywa chako mwenyewe.Huweza kubadili hali uliokuwa nayo hata kama kwa hali ya kawaida unaona ya kuwa ni ngumu kubadilika.Mahali pengi maandiko yanatueleza kuwa neno la Mungu lina nguvu katika vinywa vyetu Zab 33:9 inatoa ufafanuzi juu ya jambo hili.

Yamkini u mgonjwa,kipofu,huelewi darasani,hamna amani katika familia yako au una matatizo mengi yaliokukumba.Hebu fanya uamuzi usio na majuto wa kutafuta neno la kukuvusha kisha liseme kwa kinywa chako kwa kurudia rudia mara kadhaa.Au kumbuka neno lolote ambalo uliwahi kulisikia hapo awali ambalo lahusu mazingira kama hayo.Kisha litamke kwa sauti ili upokee matokeo.

Na ndio maana shetani hulinyakua neno la Mungu ndani ya mtu asipolielewa.Hii ni kwa sababu anajua kuwa pindi atakapoliacha neno kwa mtu litazaa.Hivyo huliondoa mara moja ili lisizae matunda Mt 13:12-19.Maana tabia ya neno ni kuzaa pale linapoachiliwa.

Tazama Mt 13:35 inasema ili litimie neno lililonenwa na nabii akisema.Jiulize huyu nabii alinena hilo neno lini lakini mara baada ya miaka mingi neno litatimia na ndio maana nilikueleza kuwa tabia ya neno ni kutimilika linaposemwa bila kujali ni kwa kipindi gani litatokea.Lakini sharti litokee hata hivyo pasipo kujua sisi kama vijana tumekuwa tukijinenea maneno ya kushindwa,udhaifu,hofu na mengine mabaya yakiwemo.Kujipa a.k.a tusizozifahamu maana yake bila kujua maana ya maneno yale yana athari kubwa katika maisha yetu.

Wewe leo unawaza kujinenea nini?Kumbuka ardhi na mbingu huweka rikodi ya maneno yetu hivyo wakati uliokusudiwa unapofika ni lazima hilo neno litimie.Unaweza ukasikia mzazi anamwambia mwanae wewe ni kichaa na maneno mengine mengi lakini inawezekana wewe ni mmoja wapo ulieambia maneno hayo ama kama hayo lakini iko damu isafishayo Ebr 9:14.Maana unaposoma Isa53:5 mstari wa mwisho unasema na kwa kupigwa kwake sisi tumepona juu kuwa siku hii ya leo umepona lakini pale unapofanya maamuzi ya kuamini na kumkabithi maisha yako Yesu anafuta maneno yote mabaya maana kwake yeye ya kale yamepita tena yamefanywa kuwa mapya

Ubarikiwe

Na Henry Nicholaus

UTAWALA WA DHAMBI NDANI YA MTU HULETA UTUMWA


Kila binadamu atendaye dhambi mbele za Mungu ni chukizo mbele zake.Maana dhambi ni kinyume cha adili (jambo sahihi) naye Mungu hupendezwa na yaliyo mema.Lakini bado tunafanya maovu mbele za Mungu Yer 8:10 "Basi kwa hiyo nitawapa watu wengi wake zao na mashamba yao,nitawapa wale watakaowamiliki maana kila mmoja hutenda mambo ya udanganyifu".Tunanyany'anwa mamlaka tuliopewa na Mungu mwenyewe kwa sababu tunamchukiza Mungu inatupasa tujue kuwa hasira ya Mungu juu ya sisi tutendao maovu ni kubwa haistamiliki Yer 10:10

Wakristo wengi tunajua kuwa tunaenenda njia ya uovu wakati huo huo tunajua kusudi la Mungu juu ya binadamu ni kukaa katika mpango wa Mungu.Tunashindwa kuenenda katika hayo kwa sababu hatuna akili ndani yetu tumelikataa neno la Bwana kila mara tunapolipokea Rum 1:28,Mith 1:29,1Kor 5:34 tumwombe sana Roho atusaidie kutumia akili tunayoipata ipasavyo maana ni wengi wanaotamani kulisikia neno na kupata akili ya namna hiyo.Lakini sisi tunaoipata tunaidharau.

Tunaweza kukaa katika mpango wa Mungu maana yeye ni Mungu wa rehema na wala si mchoyo wa fadhili pia si mwepesi wa hasira Yona 4:2 .Utakapogeuka kuwa mwaminifu na kuendelea mbele na wala si nyuma yeye ni wa haki hata akuondolee udhalimu wote.Lakini tusiwe wa maneno tu.Maana tumekuwa tukitubu sana lakini hatupo tayari kuachana na mwenendo wetu wa dhambi na hapa ndipo hasira ya Bwana huonekana juu yetu Yer 8:6 Tunayaweza yote katika yeye atutiaye nguvu.

Amani ya Mungu iwe nawe


Na Maria Lodrick 


UMUHIMU WA KUOMBEA NDOA ZA WAZALIWA WA KWANZA


Mimi sijui unachoweza kufikiri juu ya somo hili lakini Mungu anataka kukufikirisha kwa namna nyingine nami sielewi kuwa uliwahi kuwaza kwamba utafundishwa kitu kama hiki, basi fuatana nami kwa karibu sana ili usikie kile Mungu anachotaka kukufikirisha.Natamani ujifunze kujiombea mwenyewe ili Mungu akupe kuona umuhimu na akupe nguvu za kuomba juu ya kuoa au kuolewa kwa mzaliwa wa kwanza au juu ya ndoa yake.

Mtu mmoja aliyekuwa na umri karibu miaka 60 alikuwa akishukuru Mungu kwa ajili ya sendoff na harusi iliyotangazwa katika ukoo wao.Maana toka utotoni hadi utu uzima hakuwahi kuona au kusikia sendoff na harusi halali katika ukoo wao.Hii ilitokana baada ya kuamua kushughulikia tatizo lao kwa mtazamo wa mzaliwa wa kwanza.Ndipo Mungu akawajibu mpaka mwaka 2010

Je unajua ya kuwa hali ya ndoa na pia hali yakuoa na kuolewa kwa sehemu kubwa inapatikana kwenye lango ambalo ni mzaliwa wa kwanza katika ukoo au familia husika.Na ndio maana kuoa au kuolewa kwa mzaliwa wa kwanza kunakuwa shida na kupigwa vita kwelikweli kwa kuwa wao ni lango na mkondo wa Mungu.

Je unajua baraka moja wapo ya mtu kuwa mzaliwa wa kwanza kwa haki ni kupata msaada wa uongozi wa Mungu katika kuoa na kuolewa kwake na hii ndio sababu Isaka alivyokuwa anaachilia baraka za mzaliwa wa kwanza kwa Yakobo Mw 28:6 tunasoma ya kuwa katika kumbariki alimwagiza akasema usitwae mke kwa binti za kanani

Unadhani kwa nini iwe hivyo.Hii ni sababu si kila mwanaume/mwanamke ameandaliwa kwa ajili ya mwenzi wa mzaliwa wa kwanza.Bali mwenzi wa mzaliwa wa kwanza ameandaliwa kupitisha mtoto atakayebeba lango la haki la mzaliwa wa kwanza.

Naamini unakumbuka jinsi kuoa kwa Yakobo kulivyokuwa kwa matatizo na katika mazingira ya kukatisha tamaa.Shetani alikuwa anatafuta Yakobo asimwoe Raheli ili kukwamisha kuzaliwa kwa Yusufu Mw 29:19 - 21,25 - 28,31,30:22 - 24

Sasa unaweza kuelewa kwa nini hali ya kukosa mtoto katika ndoa ya Ibrahimu kulileta maamuzi mabaya ya kuzaa na msichana wa kazi.Hii ni sababu shetani alitaka Ishmaili achukue nafasi ya uzaliwa wa kwanza wa haki ambayo ni ya Isaka.Ni kweli Mungu alimwambia Ibrahimu kuwa atakayetoka katika viuno vyake ndiye atakayekurithi Mw 15:4.Lakini si kwa kuzaa na mwanamke yeyote aliyemtaka yeye au kushauriwa na mke wake.

Ishimaili alitoka katika viuno vya Ibrahimu ni kwa nini basi Mungu alimkataa.Tofauti ya Isaka na Ishimaili ni nini wakati wote wametoka katika viuno vya Ibrahim?Tofauti zao zilikuwa ni tofauti ya matumbo ya mama zao waliowazaa.Ubora wa tumbo la Sara ulikuwa kutoka kwa Mungu.

Sii kila tumbo la kila mwanamke limeandaliwa kwa jinsi hii.Na kwa sababu hii ni rahisi mwanamke anayeolewa na kijana aliye mzaliwa wa kwanza atakuwa na uwezo wa kumzaa Isaka kwa ajili ya Mungu na kwa ajili yako.Tena ni muhimu kujua kuwa si kila msichana atapata nafasi ya kuolewa kirahisi na Ibrahimu.Uwe na hakika kuwa shetani atajaribu kuwasumbua wakina Hajira kwa Ibrahim ili kuvunja ndoa yake Mw 12:15 - 20.Na tena ikiwa msichana amempata Ibrahimu wake na kuolewa kwa msaada wa Mungu usishangae ukiona tumbo lake likipata vita na kushindwa kuzaa.

Naamini sasa unaweza ukaelewa kwa nini Sara alipata shida ya kuzaa kwa Ibrahimu wake na kwa nini Rebeka alipata shida ya kuzaa kwa Isaka wake na kwa nini Raheli alipata shida ya kuzaa kwa Yakobo wake na kwa nini Hana alipata shida ya kuzaa kwa Elkana wake?

Ni ili wasiweze kupitisha wazaliwa wa kwanza wa haki ili Mungu apate kama lango katika kizazi kilichokuwa kinafuata baada yao.Fuatilia mwenyewe kwenye biblia uone hili.Utaona ya kuwa Sara alimzaa Isaka ,Rebeka alimzaa Yakobo, Raheli alimzaa Yusufu na Hana alimzaa Samueli.

Pia utaelewa kuwa Ibrahimu alipata mzigo mkubwa moyoni wa kuona ya kuwa mtoto wake Isaka anapata msaada wa Mungu katika kuoa kwake.Ibrahimu alimuelekeza mfanyakazi wake aliyemtuma kumtafutia Isaka mke kuwa Bwana Mungu wa mbingu aliyenitoa katika nyumba ya babaangu yeye atampelekea malaika mbele yako Mw 24:7

Unadhani Ibrahimu alijuaje hili ya kuwa Mungu wake amemtuma malaika kwa kazi maalum ya kuhakikisha kuwa Isaka aliyekuwa mzaliwa wake wa kwanza kwa haki anapata mke sahihi.Ni lazima Ibrahimu alikuwa anaomba juu ya kuoa kwa Isaka kwa mzigo sana huku ajua umuhimu wa Isaka kama lango na hivyo Mungu hawezi kuruhusu aoe mwanamke yeyote tu.

Shetani anawapiga sana vita wazaliwa wa kwanza juu ya hili kiasi kwamba anawafanya wazae watoto wao wa kwanza nje ya ndoa.Una mzigo gani moyoni mwako wa kuombea mzaliwa wa kwanza wa kiume juu ya kuoa kwake au wa kike juu ya kuolewa kwake na juu ya ndoa zao.

Ombea mzaliwa wa kwanza


Na Henry Nicholaus


SISI NI WAJUMBE WA KRISTO TUNAOTAKIWA KUISAMBAZA INJILI


Kama mkristo kamili anayemtumikia Mungu ni wajibu wetu kuendelea kumtangaza Kristo ili pale atakaporejea atukute tukifanya hivyo ili kukusanya kondoo zake.

Mt 24:44 - 51 Kabla ya Yesu Kristo kupaa mbinguni alituahidi kuwa atatuletea msaidizi kwetu naye ni Roho Mtakatifu ili aweze kutuongoza katika kumtangaza Kristo.

Kama katika mfano ulioelezwa katika Mt 24:44 - 51, Mtumwa aliachiwa kazi ya kuwapa watu chakula naye akakawia akidhani kuwa Bwana wake atachelewa kurudi.Vivyo hivyo sisi nasi wakristo ni watumwa na watoto wa Mungu tulioachiwa agizo la kuwapatia watu chakula cha roho ambalo ni neno la Mungu.

Hii ni kwa sababi kadri siku zinavyozidi kusonga na kuyoyoma ndivyo jinsi gani Yesu anavyokaribia kurudi kulichukua kanisa lake hivyo basi hatujui siku wala saa.

Kwa maana siku atakaporudi Yesu atampa kila mtu ujira wake sawasawa na kazi yake na tukimaliza kazi (sisi tulio watu wake) tutavalishwa taji ya uzima ambayo ni kutokana na juhudi katika kulitangaza neno la Mungu, tukiongeza idadi ya wamfuatao ili kwa pamoja tupate kuuona ufalme wa mbinguni ambao huanzia ndani ya mioyo  yetu na mwishowe kwenda kuurithi ule uzima wa milele


OMBEA MZALIWA WA KWANZA ILI FAMILIA YAKO IPATE KUFANIKIWA


Kut 2:23 - 24 Wana wa Israeli walikuwa katika kiwango fulani cha maisha, nao walimlilia sana Mungu, naye Mungu akawajibu kwa staili ambayo hawakutegemea.Na sisi tunajiuliza kwa nini ilimchukua Mungu utaratibu mwingine kabisa ambao hatukuufikiria.Lakini tunapojua kile anachotufundisha tunajua kuna utaratibu ambao Mungu amejiwekea yeye mwenyewe kwenye ulimwengu wa roho.Na moja  moja wa utaratibu huo ni wa mzaliwa wa kwanza.

Kut 12:13 Katika Kut 12 yote anazungumzia juu ya kila familia ichinje mwana kondoo na damu ya ke ipakwe kwenye miimo ya milango na vizingiti vya juu.Akasema hiyo damu itakuwa ni ishara kwao kwa sababu kuwa Mungu alipokuwa anawapiga pigo kwa wazaliwa wa kwanza alipoiona damu pigo halikuwapata.Na pia shetani atakapoamua kulipiza kisasi kwa ajili ya wazaliwa wa kwanza wa Israeli atakapoiona ile damu atashindwa kuingia.

Ile damu ilikuwa ishara kwa wana wa Israeli.Hivyo Mungu alitaka wajifunze ile ishara wapate kuelewa kilichopo ndani ya ile ishara.Maana katika ishara kuna ujumbe, kuelekeza.Maana ishara haiji yenyewe bali ilikuja ili wana wa Israeli  waiangalie na kuifuta inapokuwaelekeza.Kama kibao kinaelekeza Moshi usiangalie Morogoro.Kibao kilicho juu ya mlango kilicho na damu kinawaelekeza wapi?Kwa mzaliwa wa kwanza.

Ili waweze kujua kuwa Mungu hashughulikii milango kama milango bali huwashughulikia wazaliwa wa kwanza kama lango au kipitishio.Na ndio maana mzaliwa wa kwnza ni lango.Mungu anapomtazama mzaliwa wa kwanza hamtazami kama tunavyo mtazama sisi, anamtazama kama lango linaloitwa mzaliwa wa kwanza na linapewa majina ambalo linaweza kupitisha vitu ama la

Nawe kama mwiisraeli kama biblia inavyotueleza una mpango gani juu ya jambo hili.Muhimu kulizingatia maana linachukua nafasi kubwa katika maisha yako na si tu maisha yako hata ya familia yako.Hivyo fanya maamuzi sasa sawasawa na neno lilivyotufundisha.

Barikiwa sana


Na Henry Nicholaus


NGUVU KAMA MATOKEO YA KUHIFADHI NENO LA MUNGU


Unapokuwa na neno nguvu ni zao lake.Nguvu ni udhihirisho wa neno la Mungu ndani yetu.Au ni matokeo ya kuhifadhi neno la Mungu ndani yetu.Imani chanzo chake ni kusikia,unaposikia unapata udhihirisho wa neno ambao ni nguvu na hiyo hupelekea kujenga imani.

Mdo 1:6-8 Udhihirisho wa nguvu huja kwa Roho Mtakatifu tofauti na vitu vingine neno huhifadhiwa katika moyo na si akili.Fil 4:13 Paulo anasema mengi anayoyafanya yasingekuwa katika uweza wake kama nguvu haipo ndani yake.Neno huanza kisha nguvu hufuata.

Mith 24:5 Ili uwe na nguvu ni lazima uwe na hekima yaani neno la Mungu.Kusoma neno la Mungu sio tija lakini uwepo wa neno ndani ya moyo wako ndio tija.2Pet 3:5 Mbingu na nchi zilifanya kwa neno la Mungu.Lile neno lilileta nguvu ya uumbaji.1Kor 1:24 Kristo ni neno hivyo neno huanza na kisha nguvu hufuata

Gal 3:22 Imetupasa kulijua neno la Mungu ili tuweze kupata nguvu.Neno lilmefunga kila kitu ndani yake.Watu wengi wanataka fedha lakini hawataki chanzo cha fedha ambacho ni neno la Mungu.Kol 1:29 Ukiwa na nguvu ndogo hata udhihirisho wa Mungu kwako huwa mdogo.Mungu anataka tulisimamie neno lake.Neno ni chanzo cha ushindi 1Kor 15:55-57.Hivyo ilitushinde majaribu ni lazima tuwe na neno la Mungu.Na hilo neno ni lazima likubalike ndani yetu.

Gal 5:24 Neno haliwezi kukaa ndani yako kama hujalikubali na ndio maana wamataifa hawana ufalme wa mbingunin kwa sababu hawakulikubali neno la Mungu.Nguvu za Mungu zinapotenda kazi ndani yako kunakuwa na udhihirisho wa nguvu ya Mungu.Ebr 4:12 Neno lina uweza wa kutuwezesha kushinda dhambi.Tunatenda dhambi kwa sababu hatuna neno la Mungu.Ili uweze kuuteka ufalme wa mbinguni ni lazima uwe na nguvu Mt 11:12

Tuaache kutafuta makanisa,watumishi na ibada bali tulitafute neno la Mungu ili tupate nguvu za kutawala vitu vyote.Maana kila kitu kimefungwa katika neno la Mungu.Hivyo Yesu alisema utafuteni ufalme wa mbinguni na haki yake na vyote mtazidishiwa.

Ili uwe hai siku zote ni lazima ushinde majaribu na hii hutokea pale tu neno la Mungu linapokuwa limetawala ndani ya mioyo yetu.Hii ndio sababu kubwa iliyomfanya Yesu amshinde shetani kila wakati na kila hali jisomee mwenyewe Mathayo sura ya nne yote utayaona haya

Ubarikiwe

Na Joseph Luoga


 NI KWA NINI WATU HAWASIKII NENO LA MUNGU


Yn 8:47
"Yeye aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu, hivyo ninyi hamsikii kwa sababu ninyi si wa Mungu".

Binadamu wengi wa leo wamekuwa wakisikia neno likihubiriwa kila pande za dunia, je mbona hatuoni watu wakibadilika. Wakristo wengi wa leo maisha yao yapo mikononi mwa shetani.Kwa kuwa shetani ndio usukani wao katika maisha yao, ni vigumu wao kuabadilika na kuingiza neno la Mungu kwenye nafsi zao kwa sababu ya utumwa ndani ya shetani.

Watu wa leo hawana hofu ya Mungu ndani yao ila wanahisi kuwa wana hofu ya Mungu.Au hofu ya Mungu katika midomo yao na sio nafsi yao. Hii ni kwa sababu shetani ametawala maisha yao kiasi kwamba wamesahau ukuu wa Mungu. Kwani akili zao zipo gizani na shetani anazidi kuziweka mbali na nuru ya Mungu kwa kuwapeleka gizani zaidi. Katika maisha, asili ya binadamu siku zote ni kuwa na kinachomwongoza,hakuna binadamu ambaye anaishi tu.

 Na siku zote binadamu akiongozwa na Mungu atafwata ya Mungu na akiongozwa na shetani atafuata ya shetani. Kwa kuwa binadamu wamekuwa wakimfuata ibilisi wamejikuta wakivutiwa na tamaa za ibilisi na kwa kuwa wamefumbwa macho hawaoni tatizo hivyo hata wakihubiriwa watasikia lakini havita ingia katika nafsi zao. Kwani akili ikisikiliza yale mahubiri wakati ikiwa chini ya shetani mtu huya puuzia na kuyaacha. Ukisoma Yn 8:42-47 Utaona jinsi Yesu alivyokuwa akijaribu kuwaelewesha watu jinsi akili zao zilivyokuwa zimefumbwa ndio maana walikuwa huwasikii walichokuwa wakihubiriwa.

Je mwanadamu afanye nini ili aweze kusikia neno kama Mungu anavyotaka. Siku zote ukiwa ndani ya mfumo fulani au ukiwa mwanachama ni vigumu sana kuona au kujua makosa yako mpaka utakapokaa nje nakuangalia ule mfumo utajua makosa yake. Basi ili uweze kusikia maneno ya Mungu itakubidi ufute mfumo wote wa shetani ndani ya akili yako hapo ndipo utakapokuwa unatawala akili yako na ndipo utakapobidi kumwalika Mungu akamate upeo wako na aandae maisha yako na hapo ndipo utakapoona jinsi gani shetani alipokuwa ametawala akili yako na alivyokufanya ufanye vitu vya ajabu lakini kwa kuwa uliikuwa ndani ya mfumo wake ilikuwa ni vigumu kwa wewe kuona na kujua.

Mungu akusaidie, akutie moyo wa kutamani kufanya mapinduzi katika maisha yako na kuongozwa na mfumo wa Mungu

Ubarikiwe

Na Frederick Apina

HAIJALISHI NI NAMNA GANI ULIVYOFANYA MTIHANI WAKO BALI MAOMBI YAKO YANA NAFASI KUBWA KATIKA KATIKA KUAMUA MATOKEO YAKO


"Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni na lolote utakalofunga duniani litakuwa limefungwa mbinguni na lolote utakalolifungua duniani litakuwa mbinguni na lolote utakalolifungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni" Mt  16:19

Yesu anapoeleza habari za ufunguo anatumia siri ya mamlaka ya maamuzi ndani yetu. Si watu wengi wanajua kuwa Mungu huachilia watu wake kufanya maamuzi pamoja naye katika dawati lake. Ni kweli yamkini ulivyofanya mtihani wako, kwa mtazamo wako huwezi kufikia malengo yako. Lakini Mungu anapokutazamisha kwa habari za mamlaka ya maamuzi uwe na uhakika kwa mamlaka haya kila kitu chaweza kubadilika.  

Yer 32:27 inatuambia hakuna jambo lisilowezekana.Na ndio maana aliweza kubadili Bahari ya Shamu kuwa nchi kavu.Haikuwa rahisi kwa wana wa israeli kumuelewa Mungu.Kumbuka Mungu aliwatoa utumwani akiwaambia atawapatia nchi yenye maziwa na asali lakini Mungu alipokuwa akiwapeleka katika nchi ya ahadi, Farao aliwafuatilia kwa nyuma akiwataka kuwarudisha hali wakijua hataweza kuwashika wakajikuta njia wanayoishika imefungwa kwa mbele na bahari huku pembeni ikifungwa na miamba.Basi katika hali ya kukata tamaa Mungu anageuza majonzi yao kuwa furaha mara baada ya kutenga maji na kuwaamuru wapite.

Hata wewe yamkini ikawa ngumu kwako kumuelewa Mungu.Kwa sababu kama kuomba, uliomba na kama kutoa sadaka ulitoa.Ngoja nikuambie Mungu anataka kujitukuza katika maisha yako yamkini hukuwa kumwona Mungu kwa macho katika maisha yako sasa amekuja kujidhihirisha kwako usihofu bali fuata kile nichokueleza wakati huu.

Ninachotaka ni wewe kuamini  jambo hili.Je unadhani kama Mungu tunayemuabudu aliumba dunia na vyote viujazavyo hivi hivyo vya kwako kweli vitamshida?Imani ni kuwa na uhakika ya mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasiyoonekana Ebr 11:1.Jijengee uhakika wa jambo hili ili kile ulichokitazamia kiwe chako.

Ngoja nikueleze maombi utakayoyasimamia yatabadili huzuni yako kwani yana nafasi ya kubadili maksi,kusahihisha makosa na kutoa upendeleo kwa karatasi lako.

Ndugu yangu unayesoma waraka huu natamani uamini neno hili kwani ni amini na kweli. Hata mimi nilipokuwa nafanya mtihani wangu wa taifa niliingiza neno hili katika uhalisia hatimaye Mungu alijiinua kwa viwango vya juu mno.

Nakutakia kila heri

Na Henry Nicholaus



MWENYE KUVUMILIA HATA MWISHO NDIYE ATAKAYEOKOKA

Lk 12:35-40 Uvumilivu ni jambo la muhimu sana kuzingatia wakati huu wa siku za mwisho.Uvumilivu ni hali ya kuwa na subira katika jambo fulani.Subira lazima iambatane na matayarisho ili iweze kukaa.Matayarisho haya hufanyika kwa neno la Mungu.Kazi ya hilo neno ni kukutia katika subira ulionayo.Maana si rahisi kuwa na uvumilivu katika mengi ya dunia kama huna nguvu ya Mungu inayokuwezesha kufanya hivyo.

Daudi alipakwa mafuta akiwa na umri wa miaka 17, 1Sam 16:-12.Lakini ilimchukua miaka 13 hadi alipokuwa mfalme wa Israeli 2Sam 5:4.Lakini utagundua kilichomfanya afanikiwe ni uvumilivu uliokuwa ndani yake.Hata hivyo uvumilivu huo ulikuja kwa njia ya Mungu mwenyewe maana haikuwa rahisi kwa Daudi kumuelewa Mungu ni kwa nini kama alimtaka awe mfalme ampitishe kwenye shida nyingi ikiwepo kukimbizwa na Sauli ikiwa moja wapo.

Hata ukimtazama Ayubu unaweza ukajiuliza ni kitu gani kilimuwezesha akastahimili majaribu (Ayu 1:13-20) haya yote kwa kipindi kirefu.Cha kushangaza mara baada ya kupotelewa na kila kitu aliishia kusema Bwana ametoa na yeye ametwaa jina lake lihimidiwe Ayu 1:21-22.Kwa hali ya kibinadamu usingeweza kumuelewa bado.Wakati tunazidi kujiuliza maswali mengi kwa nini aliweza tunapata jibu kuwa ni kwa sababu neno la Mungu lilikuwa limemtawala ndani yake Ayu 1:9-10.

Wana wa Israeli walipokuwa jangwani walipofika eneo ambalo walikosa maji waliingia katika manung'uniko na lawama.Jambo hili lilimkwaza Mungu kwa sababu walikosa uvumilivu Hes 14:11-21.Lakini baada ya ukosefu wa uvumilivu Mungu aliazimu wasifike katika nchi ya Kanani Hes 14:22-24.

Nami sina hakika kama Mungu amebadili uamuzi wake kwa watu wakosao uvumilivu katika maisha haya.Basi tujiweke tayari maana hatujui ni wakati gani Mwana wa  Adamu atakaporudi Mt 25:1-12


TUNASHINDWA KUFANIKIWA KWA SABABU HATUMWAMINI MUNGU


Mt 20:29-34 Biblia inatueleza habari ya vipofu wawili waliomlia Bwana Yesu awaponye mara tu baada ya kusikia kuwa anapita. Hili lilikuwa jambo la imani kwao. Maana kwa kusikia tu walipata kuamini Yesu anao uwezo wa kuwaponya Rum 10:17. Ndipo hata alipowauliza awafanyie nini walijibu wanataka kupona. Nao walipokea kama walivyosema.

Utagundua kilichowafanya waponywe ni imani ilikuwa ndani yao. Imani yao yaweza kuonekana dhahiri pale hata waliponyamazishwa wao walipaza sauti zao wakisema "Mwana wa Daudi uturehemu".

 Watu wengi wanapoomba msaada kutoka kwa Mungu ambao waweza kuwa uponyaji, ufaulu, kupandishwa kazi na mafanikio mengine wanaposhindwa kupokea kwa mda waliotarajia wengi hukata tamaa na kuachana na maombi na kuamua kufanya wanavyoona ya kuwa inafaa kwao. Hii hupelekea anguko pasipo kujua kwao. Na kwa sababu hii hukutana na magumu sana hata wasiweze kupata kabisa wanachokitazamia.

Natamani ukumbuke kuwa wakati wale vipofu walipomwita Yesu awaponye walinyamazishwa hii ina maana katika kuomba kwetu msaada wa kimungu kuna wakati msaada huo unacheleweshwa. Tunapokata tamaa maana yake tunavunja makubaliano ya awali tuliowekeana na Mungu. Hata kufanya ule msaada uliocheleweshwa kutofika kabisa.

Imani hukupa uhalali wa kupokea kile unachokiomba. Lakini wengi wameshindwa kuamini hata kuwafanya kukosa uhalali. Maana imani ni kitambulisho katika serikali ya Mungu impayo mtu ruksa ya kuamua katika dawati la Mungu. Biblia inasema ijapokuwa alifanya ishara nyingi lakini hawakumwamini Yn 12:37-43. Hivyo uwepo wa imani ya mtu hausababishi na yeye kuitwa mkristo bali husababishwa na kusikia kwake Rum 10:17.

Wakristo wengi ni wahudhuriaji wa kanisani lakini sio waamini. Hii hutokana na wao kufungwa na mapokeo na sio neno la Mungu. Watu wengi hujishughulisha na mambo ambayo Mungu hakuyaagiza ili wapate sifa na baraka ya watu. Hivyo kuwakosesha uhalali wa umiliki kwa vile waviombavyo.

Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu bali jawabu la ulimi hutoka kwa Bwana ndivyo anavyotueleza Mithali. Ina maana kama huna connection ya mbinguni katika vile uombavyo haitakuwa rahisi kwako kuweza kupokea.

Ngoja nikueleze ndugu yangu unayenifuatilia. Akuwaziayo Mungu siku zote ni yalio mema Yer 29:11. Tatizo linabaki kwako maana hayo akuwaziayo umeyakataa hivyo hana la kufanya maana umeshindwa kuamini. Mwamini leo Yesu ili akupe ruhusa ya kuamua na kupanga.

Ubarikiwe

Na Henry Nicholaus

 JE UNAFAHAMU UZURI WA MBINGUNI?


Mpendwa msomaji, kwanza pole sana na shughuli nyingi za kila siku. Ninajua kwamba muda wako ni mchache sana, kutokana na shughuli zako nyingi. Hata hivyo ninakuomba muda wako mfupi tu, ili tuzungumze juu ya jambo muhimu ambalo nimeona kwanba ni vema nikushirikishe. Je umekubali ombi langu? Natumaini umelikubali. Asante sana. Basi ninakusihi tufuatane pamoja katika mazungumzo haya.


Huenda utakuwa umewasikia watu wengi waliofiwa na ndugu, jamaa au marafiki zao wapendwa, wakisema, ”Mungu waweke mahali pema peponi“. Jambo hili linadhihirisha jinsi kila mmoja wetu anavyoamini kwamba kuna mahali pema peponi yaani mbinguni. Na tena inaonyesha jinsi sisi sote na jamaa zetu tunavyopenda kwenda huko. Je,wewe una shauku ya kwenda mahali pema peponi au mbinguni, baada ya kuiaga dunia hii? Najua wewe pia una shauku ya kwenda mbinguni siku moja. Hata hivyo, shauku yako itaongezeka zaidi utakapokuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu uzuri wa mbinguni. Peponi au mbinguni, ni wapi na kukoje? Peponi au mbinguni, kuna uzuri usioweza kufananishwa. Tukifahamu jinsi mbinguni kulivyo kuzuri, kila mmoja wetu atazidi kuwa na shauku ya kufika huko siku moja. Tufuatane basi ili upate ufahamu wa kutosha kuhusu mbinguni au peponi.


Peponi au mbinguni ni wapi na kukoje? Mbinguni au peponi, ni juu sana, mbingu ya tatu. Biblia inasema katika 2 WAKORINTHO 12:2-4, ”Namjua mtu mmoja katika Kristo,…Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu. Nami namjua mtu huyo,…ya kuwa alinyakuliwa mpaka Peponi…“ Mbingu ya tatu ni wapi? Mbingu ya kwanza, ni hii iliyo na mawingu yanayoleta mvua, na mawingu mengine. Ni anga hili lililo juu ambalo sehemu yake huonekana kwa macho ya kawaida. Ndege au eropleni zote zinazobeba abiria, huruka katika mbingu hii ya kwanza. Mbingu ya pili, ni mbingu iliyo mbali zaidi yenye sayari na nyota zote, Sayari zilizoko katika mbingu ya pili, ni pamoja na Zebaki, Zuhura, Mars, Mshtarii, Zaharii, Uranus, Neptune, na Pluto. Sayari nyingine ziko mbali sana. Kwa mfano, umbali wa dunia yetu kutoka kwenye jua ni maili 93 milioni (kilometa 148,800,000). Lakini umbali wa sayari ya pluto kutoka kwenye jua ni maili 3,666 milioni (karibu kilometa 5,900 milioni). Nyota ziko nyingi sana, zinakisiwa kufikia bilioni 400. Nyota ziko mbali sana na dunia yetu. Nyota iliyo karibu zaidi na dunia, iko karibu maili 26,000 bilioni (karibu kilometa 42,000 bilioni). Sasa basi, baada ya sayari zote hizi na nyota hizi, ndiyo tunafika mbingu ya tatu. Mbingu ya tatu, au Peponi, kwa msingi huu ni kilometa mabilioni kutoka hapa duniani. Yesu Kristo alipopokelewa na wingu, na kupaa kwenda juu mbinguni ( MATENDO 1:9-11) alikwenda mbali sana kiasi hiki. Huko ndiko waliko watakatifu waliotutangulia.


Tupige hatua tena na kuangalia mambo mengine. Sasa je, mtu anapokufa, anasafirije kwenda mbinguni, mbali kiasi hiki? Hatupaswi kuogopa kifo, ikiwa tunaishi maisha yaliyo mbali na dhambi. Biblia inasema katika ZABURI 116:15, ”Ina thamani machoni pa Bwana, mauti ya wacha Mungu wako“. Kufa kwa watakatifu ni faida (WAFILIPI 1:21). Ni heri wafu wafao katika Bwana (UFUNUO WA YOHANA 14:13). Kufa kwa mtu anayeishi maisha yaliyo mbali na dhambi, ni mwanzo tu wa utukufu. Mtu anayeishi maisha yaliyo mbali na dhambi, anapokufa, roho yake humiminwa katika mwili mwingine wa roho unaoitwa mwili wa mbinguni, kama mafuta yaliyo katika chombo kibovu kinachovuja, yanavyoweza kumiminwa katika chombo kingine kilicho kizuri. Kufa, ni kumiminwa! Mtume Paulo aliyepata neema ya kuchukuliwa na kupelekwa mpaka mbingu ya tatu wakati wa uhai wake ( 2 WAKORITHO 12:2-4) ulipofika wakati wa kufariki kwake, alijua ni wakati mzuri wa kumiminwa. Kwa maneno yake, katika 2 TIMOTHEO 4:6, alisema, ”Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika“.


Kuhusu miili ya mbinguni, Biblia inasema katika 1WAKORINTHO 15:40-41,44, ”Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani, lakini fahari yake ile ya mbinguni ni mbali, na fahari yake ile ya duniani ni mbali. Kuna fahari moja ya jua, na fahari nyingine ya mwezi, na fahari nyingine ya nyota; maana iko tofauti ya fahari hata kati ya nyota na nyota…Ikiwa uko mwili wa asili, na wa roho pia uko“. Miili hii tuliyonayo ni mibaya sana. Ni kama vyombo vibovu. Fahari yake, yaani uzuri wa ile miili ya mbinguni ni zaidi sana kuliko miili tuliyo nayo. Miili ya mbinguni inang’aa mno na kupendeza sana. Mtakatifu anapokata roho, roho yake mara moja humiminwa katika mwili mzuri wa jinsi hii. Mtu akiwa katika mwili wa mbinguni, atapenda kujitazama wakati wote. Mwili huu hauna makovu wala ulema wala makunyanzi ya uzee! Baada ya mtu kuwa na mwili mzuri wa jinsi hii, huvikwa mavazi mazuri meupe sana yanayometameta sana. Weupe wa mavazi haya, ni weupe usio na mfano duniani (UFUNUO WA YOHANA 3:4-5;7:9; MARKO 9:2-3). Baada ya kuvikwa mavazi haya, mtu hufunguliwa mlango wa gari na malaika, na kuingizwa katika gari zuri sana lisilokuwa na mfano duniani. Yako mabilioni ya magari ya Mungu, yanayowasubiri watakatifu. Biblia inasema katika ZABURI 68:17, ”Magari ya Mungu ni ishirini elfu, maelfu maelfu“. Mtu huchukuliwa na malaika katika magari haya yanayoitwa magari ya moto, yanayoambatana na farasi wa moto na kuchukuliwa kwenda mbinguni kwa upepo wa kisulisuli (LUKA 16:22; 2 WAFALME 2:11).


Magari yanayoitwa magari ya kifahari yanayowabeba Marais na Wafalme duniani kama Mercedes Benz, BMW n.k.si kitu yanapolinganishwa na magari haya. Magari ya Mungu  hayatumii dizeli au petroli, bali huendeshwa na upepo wa kisulisuli, na huenda kasi sana. Kwa muda mfupi sana, mtu hufika mbinguni na kulakiwa na malaika wanaoimba nyimbo za shangwe. Hakuna mapokezi yoyote ya Rais au mfalme yeyote duniani, yanayolingana na mapokezi ya mtu anayeingia mbinguni, yanayofanywa na malaika.


Sasa tupige hatua nyingine. Mbinguni kwenyewe kukoje? Mbinguni ni nchi iliyo bora kuliko nchi yoyote duniani (WAEBRANIA 11:16). Waza juu ya nchi yoyote duniani inayowavutia watalii wengi kutokana na uzuri wake. Nchi hii siyo kitu ikilinganishwa na Peponi. Mbinguni ni kuzuri mno! Hakuna usiku wala mchana. Hakuna joto wala baridi. Jua au mwezi havitumiki kutoa mwangaza. Utukufu wa Mungu ndiyo nuru ya mbinguni (UFUNUO WA YOHANA 21:23-25). Neno ”Peponi“, linatokana na neno la Kiyunani, ”Paradeisos“, linalotafsiriwa pia, ”Paradiso“, na kwa tafsiri fasaha, lina maana ya ”bustani nzuri kubwa iliyojaa matunda mazuri“ na tena linamaanisha mahali palipojaa furaha na raha kuu isiyo na kifani (UFUNUO WA YOHANA 2:7; WAEBRANIA 4:1-11). Matunda ya miti iliyomo katika bustani hii isiyokuwa na mfano, ni pamoja na mti  wa uzima uzaao matunda aina kumi na mbili. Maisha mbinguni, ni pamoja na kula matunda haya katika bustani ya Mungu, na kupunga upepo wa raha kuu isiyo kifani, Paradiso (UFUNUO WA YOHANA 2:7; ).


Kipi cha ziada tena kuhusiana na mbinguni? Mbinguni, ni mji uliobuniwa na kujengwa na Mungu (WAEBRANIA 11:10-16). Miji yote ya dunia hii imebuniwa na kujengwa na wanadamu wenye upungufu wa ubunifu wa michoro, fedha, vifaa n.k. Mbinguni, ni mji uliobuniwa na Mbunifu Mkuu, Mungu mwenyewe mwenye uwezo wote. Hakuna mji kama huu duniani. Barabara zake siyo za lami, bali ni za dhahabu iliyo kama kioo kiangavu ambayo hakuna mfano wake duniani. Mtu anapotembea barabarani, hujiona kama katika kioo (UFUNUO WA YOHANA 21:21). Katika YOHANA 14:2, Yesu anasema, katika mji huu kuna ”makao“ mengi. Neno la kiyunani linalotafsiriwa hapa ni ”mone“, linalotafsiriwa katika kiingereza ”Mansion“, katika Biblia ya tafsiri ya King James Version. ”Mansion“, ni jumba kubwa la kifahari. Jumba la Meya wa Jiji la London, Uingereza (”Lord Mayor of London), linaitwa ”Mansion House“. Vivyo hivyo mbinguni, kuna makao mengi, au majumba mengi  ya kifahari. Kila mtu atakayeingia mbinguni, atapewa ”kao“, au ”jumba mojawapo la kifahari“, la kuishi. Kao lako linakusubiri! Majumba haya, hayakujengwa kwa tofali za sementi au udongo, bali kuta zake zimejengwa kwa madini ya aina nyingi. Biblia inasema katika UFUNUO WA YOHANA 21:18-20,  ”Na majenzi ya ule ukuta wake yalikuwa yaspi, na mji ule ulikuwa wa dhahabu safi mfano wa kioo safi. Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa yaspi wa pili yakuti samawi; wa tatu kalkedoni; wa nne zumaridi; wa tano sardoniki; wa sita akiki; wa saba krisolith; wa nane zabarajadi; wa kenda (tisa) yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso, wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto“.


Vito hivi au madini haya, yanafanya majumba ya mbinguni, yapendeze mno. Yaspi, ni madini yanayong’ara sana yenye rangi ya kijani iliyochanganyika na bluu. Yakuti samawi, ni mawe ya bluu, mazuri sana yenye ugumu unaofuatia madini ya almasi. Kalkedoni, ni aina ya madini mazuri sana yenye rangi aina nne  balimbali-nyekundu iliyochanganyika na njano, hudhurungi (brown) iliyochanganyika na nyeusi, bluu iliyochanganyika na nyeupe, na rangi ya maziwa. Zumaridi, ni madini yenye rangi ya damu. Krisolitho, ni madini yaliyo kama dhahabu, ila yana rangi aina ya kijani iliyochanganyika na njano, Zabarajadi, ni madini maangavu (yanayoona ndani), yenye  rangi ya bluu iliyochanganyika na kijani. Yakuti manjano, ni madini  mazuri yenye rangi ya njano na mchanganyiko wa kijani.Krisopraso, ni madini yenye rangi  tatu pamoja; njano, kijani, na bluu. Hiakintho, ni madini yenye rangi iliyochanganyika na njano. Amethisto, ni madini yenye rangi ya zambarau, yenye bluu na wekundu ndani yake.


Nini zaidi? Mwangaza wa mbinguni siyo kama wa duniani usio na rangi. Mwangaza wa mbinguni ni wa rangi ya yaspi yaani kijani iliyochanganyika na bluu (UFUNUO 21:11). Mavazi meupe ya wale walioko mbinguni, hubadilika  rangi mara kwa mara kutokana na rangi ya mwangaza na ya majengo hivyo kufanya watu wapendeze mno. Ndani ya makao ya mbinguni kuna fenicha za kifahari. Fenicha alizoagizwa Musa kuzitengeneza na kuziweka katika maskani, zilikuwa mfano tu wa fenicha za mbinguni(WAEBRANIA 8:5; KUTOKA 25:9-40). Chemchemi za maji na mito ya maji ya uzima inazunguka mji. Mbinguni kuna  kula na kunywa, hakuna mauti wala maumivu au taabu (LUKA 22:14-16, 29-30; UFUNUO 2:17; 21:4-5; 14:13). Kuna kuimba nyimbo za sifa, na vinanda (UFUNUO 14:2-3; 15:2-4). Ufahamu wetu utaongezeka (1WAKORINTHO 13:12). Kuna mengi zaidi yasiyotamkika katika lugha hii ya duniani (WAKORINTHO 12:4). Ni heri twende wenyewe kujionea. Tusikubali mume au mke kutuzuia kuingia mbinguni maana mbinguni hakuna kuoa au kuolewa (LUKA 20:34-36; MATHAYO 22:30).   


Ni sifa ipi ya kukuwezesha kuingia mbinguni? Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14). Ndani yake hakitaingia chochote kilicho kinyonge (UFUNUO 21:27). Kinyonge ni kipi? Ni yule anayetenda dhambi. Huyu ni mtu asiyefaa, Ni mnyonge! Je, wewe ni mtakatifu? Jibu ni la! Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini, hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13; YOHANA 14;6). Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii? Najua uko tayari. Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni,



”Mungu Baba, asante kwa ujumbe huu. Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi. Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha. Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo.Bwana yesu, niwezeshe. Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu. Amen.“



Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni. Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu. MUNGU AKUBARIKI!!!


 UPO UMUHIMU WA KUJUA NENO LA MUNGU


Biblia  inatuambia Yesu Kristo ndiye Neno la Mungu. Kwa maneno mengine Yesu ndiye Neno ambalo Mkristo anapaswa kuwa nalo (Yohana 1:1).

Kwa kusema hivyo kuna  umuhimu wa kumjua Yesu na kumshika, kwa maana yeye ndiye Neno la Mungu. Katika Biblia mtume Petro anasema mbele za Yesu kwamba, twende kwa nani na wewe ndio mwenye maneno ya uzima? Petro alijua upo umuhimu wa kumjua Yesu kama Neno maana ndani ya Neno kuna uzima

Biblia inasema neno la Kristo likae kwa wingi ndani yetu (Wakolosai 3:16).Kwa nini basi neno la Kristo likae kwa wingi ndani yetu? Ni kwa sababu lina mambo yafuatayo ambayo ni muhimu katika maisha yetu ya Ukristo. Mambo hayo ni…

A) Neno la Mungu li Hai
B) Neno la Mungu lina nguvu (Mwanzo 1:6).
C) Neno la Mungu lina ukali kuliko upanga
D) Neno la Mungu linachoma hata kuzigawanya nafsi, roho viungo na mafuta yaliyomo ndani yake
E) Neno la Mungu li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo


KWA NINI NENO LA MUNGU LI HAI?
Neno la Mungu li hai kwa sababu  Mungu mwenyewe analithibitisha kwamba li hai maana

a) Linafanya mabadiliko (Isaya 55:10-11).
b) Linatupa kushinda dhambi (Zaburi 119:11).
c) Neno la Mungu  li hai kwa sababu linatupa mafanikio katik mwili. Petro anasema ”kwa neno lako tunatupa nyavu zetu.“  Hapa tunaona kuwa Neno la Mungu  pekee yake ndilo linaloweza kuleta majibu katika maisha yetu (Luka 5:3-6).


Uhai wa Neno la Mungu kwa mtu ndio unaoleta kushinda dhambi. Nao wakamshinda kwa neno la ushuhuda wao (Ufunuo 12:11).Daudi aligundua au kwa maneno mengine alifahamu umuhimu wa neno la Mungu katika maisha, kama vile mtume Paulo anavyosema na Wakolosai kwa habari ya neno la Kristo kwamba likae kwa wingi ndani ya mioyo yetu
Neno la Mungu lina nguvu na ndio maana  tunamshinda  shetani kwa neno la Mungu.Yesu kama kielelezo yeye mwenyewe ni neno ndani ya neno anamshinda shetani (Luka 4:1-12).

Katika mistari hiyo tunaona Yesu anamwambia  shetani  ”imeandikwa“   Shetani nae anageuza usemi nae anamwambia Yesu ”imeandikwa kwamba atakuagizia malaika usije ukajikwaa mguu wako.“ Kwa kuwaYesu neno la Mungu limo ndani yake hamwambii tena shetani imeandikwa ila anamwambia imenenwa. Kwa maneno mengine tukiwa na neno la Yesu ndani yetu hatuwezi kuyumbishwa. Kwanini? Kwa sababu tumeshaona jinsi ambavyo shetani  anajaribu kutumia neno la Mungu   kwa kusema ”imeandikwa.“  Na ni kweli imeandikwa ananukuu kutoka kitabu cha Zaburi 91 :1-12. Hata kama shetani ananukuu maandiko haina sababu  yamimi kushindwa na shetani  maana Yesu tayari alikwisha mshinda. Yesu kumshinda shetani ina nipelekea mimi kusoma neno la Mungu kwa bidii sana. Kwa mfano, ni kweli kabisa imeandikwa mtakula vitu vya kufisha havitawadhuru lakini je, ninywe sumu sitakufa kwa sababu imeandikwa? Hapana, ukinywa hakika utakufa. Shetani hutumia mandiko kuwafunga wasiojua neno la Kristo Yesu.

Katika Biblia tunasoma pia kwamba ”imeandikwa“ Wanandoa MKE na MUME wasinyimane. Kwa kutojua neno vijana wa kiume na wa kike wamedanganywa. Si hao tu hata walioko kwenye ndoa wametegwa kwa andiko hilo. Neno linasema katika Mithali 6:32 ”Aziniye na mwanamke hana akili kabisa“ na Mwanamke vivyo hivyo akizini na mwanaume hana akili kabisa. Watu wamepata hasara ya mambo mengi kwa kutojua neno la Mungu. Ili tuweze kumshinda shetani  ni lazima  neno la Yesu liwe ndani  yetu ndiposa tutamshinda shetani. Ayubu kwa neno la Mungu alishinda. (Ayubu 19:25-27, Waefeso 6:17).

Nataka nikwambie neno la Mungu ni msaada katika maisha yetu maana hutupa  majibu ya maisha yetu. Katika Luka 5:3-6 tunasoma jinsi Petro na wenzake walivyopata samaki wengi kwa kutii neno la Kristo. Kumbuka pia juu ya yule akida, alimwambia Yesu ”...sema neno tu na mtumwa wangu atapona“ (Luka 7:2-10). Yesu akisema neno lazima mabadiliko yatokee. Neno la Mungu lina ukali kuliko upanga. Kwa nini neno la Mungu  lina ukali kuliko upanga? Upanga unaweza kukukata na usipone. Lakini neno linakata na kuponya. Kwa neno hili wafalme wanatubu. Yona alitumia neno la Mungu likawa kali watu wakatubu. (Yona 3:1-10; Matendo ya Mitume 8:18-24).

Neno la Mungu linachoma hata kuzigawa nafsi na roho na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake (Matendo 7:51-54, Yohana 4:16 -18, 27-29). Mwanamke akaambiwa mambo yake; Neno likachambua kila tabia. Neno la Mungu li jepesi kutambua mawazo na makusudi ya moyo.Yesu kama Neno la Mungu anajua mambo ambayo watu wanawaza ndani ya mioyo yao (Luka 5:17-24, 6:6-8 ; Mathayo 16:1-4). Yapo makusudi ya moyo ambayo ni ya siri sana kwa mwanadamu lakini nataka nikuambie neno la  Mungu ni jepesi kutambua makusudi ya moyo.

Mtume Petro aliyependa kujua neno la Mungu, naye pia Mungu alimjalia neema ya kuyajua makusudi ya moyo wa mwanadamu (Matendo 5:1-11). Elisha aliyajua makusudi ya moyo wa mfalme ya kuwatenda Israeli kwa siri ila Mungu alimpa neema ya kuyajua mawazo ya mfalme (2 Wafalme 6:8-12). Hili ni jambo la msingi katika maisha ya Mkristo yaani kulijua neno la Mungu. Neno la Mungu  tukiwa nalo na likitenda kazi ndani yetu lazima tufanikiwe (Yoshua 1:8) .

Je unahitaji kuwa na imani katika neno la Mungu? Basi, ni neno la Mungu peke yake ambalo laweza kuumba imani, maana pasipo neno la Mungu hakuna imani (Waebrania 11:3 ; Warumi10:17). Ili uwe mwanafunzi wa Yesu ni lazima ulijue neno la Mungu na kulishika.(Yohana 8:31 ; Luka 2:19). Kama neno halimo ndani yetu tunayoyafanya yanakuwa hayana Mungu, hata twaweza kusalitiana. Mtu anayelitamani neno la Yesu  huling’ang’ania na kulitenda maana kwake ni nguvu. (1Wakorintho 1:18). Si kwamba Neno la Mungu ni nguvu tu: bali huleta faida (Mathayo 13:23).

Watu wengi tunapotea kwa kutokujua uwezo (nguvu) iliyomo katika neno la Mungu (Mathayo 22:29).Yesu anasema, mtu anayelitenda neno la Mungu na kulishika huyo amepanda mbegu ambayo itazaa sana, maana ndani ya moyo wake imo mbegu ambayo ni neno la Mungu la uponyaji na mafanikio, msamaha, utu wema na mengi yanayofanana na hayo.
Yapaswa maisha yetu yawe yenye neno (mbegu) la  Mungu ili tuweze kuzaa mambo mazuri. Wokovu wetu unaimarika kwenye neno la Mungu. Hilo neno la Mungu tunalipata wapi? Isaya 34:16. Upo umuhimu wa kuyachunguza maandiko ili kujua Mungu anasema nini (Matendo 17.10-11).  Je, tangu ulipowekwa msingi wa wokovu, neno limo ndani? (Hagai 2:18-19). Kila kitu kinaweza kupita lakini sio neno la Mungu (Isaya 40:8, Mathayo 24:35).

 Ili neno litende kazi katika kinywa chako unapolitamka na kuamini ni lazima iwepo nguvu ya Roho Mtakatifu. Bila hii nguvu hamna kitakacho endelea. Utasema umeamini lakini hakutakuwa na matokeo. Mungu mwenyewe alipotamka neno liliambatana na nguvu ya Roho Mtakatifu (Mwanzo1:2-3).

MAISHA TULIONAYO LEO YANA NAFASI YA KUBARIKI AMA KULAANI VIZAZI VIJAVYO


2Fal 4:1-7 Inatueleza juu ya mwanamke mmoja ambaye alikuwa amefiwa na mumewe ambaye alikuwa mwana wa nabii.Mumewe alikuwa anadaiwa na hata alipofariki hakuwa amelipa hilo deni.Hivyo kumfanya yule aliokuwa anamdai kutaka kuwachukua watoto wa yule mama na kuwafanya kuwa watumwa  kama malipo ya hilo deni.Jambo hili halikumpendeza yule mama na kuamua kumwomba Elisha amsaidie tu kwa sababu mumewe alikuwa mcha Mungu.

Hivyo utaona yule mama aliomba msaada kwa Elisha kwa sababu kuwa mumewe alikuwa mcha Bwana na Elisha aliamua kumsaidia.Hivyo kigezo cha Mungu kumsaidia yule mama kupitia Elisha ni kwa sababu mume alikuwa ni mcha Mungu.Maana yake Mungu ana utaratibu wa kuachilia msaada kwa watu kwa sababu ya wazazi wao au ndugu zao au waume au wake zao walikuwa wanamtukuza.

Hili utaliona kwa Ibrahimu ambaye Mungu alibariki vizazi vyake kwa sababu tu ya maisha ya kupendeza aliokuwa nayo mbele zake katika maisha yake Mw 17:4-7.Ukiona familia au ukoo fulani umebarikiwa uwe na uhakika kuwa ni kazi nzuri iliofanywa na baadhi ya watu waliopita katika familia hiyo au ukoo uo ambao ulimpendeza Bwana.Na kwa sababu hiyo akaamua kuwa bariki kupitia maisha ya hao.

Hata hivyo maisha mabaya ya mtu huweza kusababisha shida kwa vizazi vyake kama isemavyo Hes 14:18 Mungu huwapatiliza wana wa uovu wa baba zao katika kizazi cha tatu na cha nne.Hivyo basi mkao mbaya tuliokuwa nao leo huweza kusababisha maisha mabovu na ya shida kwa vizazi vingine.Maana siamini kama Mungu amebadili utaratibu huu hata leo.Mungu ana taratibu mbalimbali ambazo amejiwekea katika ulimwengu wa roho kama ulivyo utaratibu wa mzaliwa wa kwanza.Na utaratibu mmoja wapo ni huu wa kubariki watu sawa na mikao mizuri wa mababa zao na kulaani pia sawa na mikao mibaya ya mababa zao.

Najua uliwahi kusikia mtu akisema kuwa anasumbuliwa na magonjwa ya kurithi kama pumu.Uliwahi kujiuliza kwa nini iwe magonjwa ya kurithi?Hii ni kwa sababu yamkini yuko mmoja ambaye hakukaa vizuri hata kuweza kusababisha laana ya magonjwa kutafuna ukoo wao.Kama nilivyokueleza uko utaratibu ambao alijiwekea Mungu hivyo Mungu huangalia huo katika kuamua vitu mbalimbali.

Hivyo kaka yangu,dada yangu,baba yangu na mama yangu kumbuka Mungu hukuazia mema siku zote Yer 29:11.Hivyo chagua mkao mzuri ili ujenge msingi mzuri wa kizazi chako kijacho.Kumbuka itakuwa jambo la furaha kama vizazi vyako vikifanikiwa kwa sababu yako.

Ubarikiwe

Na Henry Nicholaus


THE HOLY SPIRIT WORKS


Before Jesus Christ descends to heaven, he said that we his people shall be sent a helper who will assist us in everything after he has left. The helper or our assistant is the holy spirit. The holy spirit was sent to us in so many things in our daily life of today. The holy spirit make sure that we are able to make the right decision that is to please God. God wants everyone to obey his commandments because if one  lives in them, he/she will never commit a sin.

Satan does not like it when a person pleases God because he does not want to be the only one who will end up in the everlasting fire, so he tries to make everyone go against what God wants so as the person to be punished by God to the everlasting fire with him.

The Work of the Holy Spirit

When Satan keeps temptations on a God's child, the holy spirit is the one who prevents and help the child to overcome the temptation and trials from Satan. The holy spirit is the one who gives ways to an individual so as to live a life that will always please God.

Remember when you had feeling when you were alone at your dining table that you should take your fellow's bread  early in the morning then there is this part of you inside was telling you that, "Just take it and eat, you are very hungry now and by the way the owner of the bread will take break some few minutes and hours from now". But there is also this part in you which was telling you that, "What you are about to do is very wrong, because the owner of that bread is also hungry and also what is yours is that what you have been kept for only. If you take it, you will hurt the owner". The one telling you this is the holy spirit but the first sound was Satan.

Satan will always want to make you do the wrong things but the Holy Spirit will always lead you to the right path and that part is God's. The Holy Spirit will not lead you to hurt somebody or being disobedient to God. In your life you will always hear these two sounds. That is the bad one and the good one. Be able to differentiate them because the bad one is Satan's and you will always hear it telling you to do something against God's will. Always choose to listen to the good one because that is the Holy Spirit talking to you. The Holy Spirit will always tell you to do God's will.

Where the Holy Spirit Dwells

Everyone has got the Holy Spirit in him or her but it depends on how each one allows the Holy Spirit to operate. The holy Spirit does not dwell in an unpleasant soul in front of God. This tells us that we should always please God and make our souls clean because a clean soul is the temple of the Holy Spirit 1Cor 3:16

Question : How do we please God?
Answer   : We please God by doing all that he wants us to do that is to obey and follow his commandments. For all those                      who go against God's commandments in which does not please God, the Holy Spirit does not dwell in them. Always pray for the Holy Spirit to dwell in your and most of all prepare a good environment for him to live in that is a good temple.

This temple is nothing else but your body. Treasure your body, keep it free and clean from all Satan's dirt. Respect your body and keep it the way God wants you to keep it as a Christian. If you do all this your body will always be the temple of the Holy Spirit and he will dwell in you.

How to Make the Holy Spirit Work/Operate in you

Always pray :Prayers are very powerful, if you did not know this you should know it by now. Prayers connect you with                        God. The more you pray, the more the Holy Spirit gets the chance to operate in you. This tells us that by our prayers is when the holy spirit works in us.

Read the word of God: The word of God is the food of our souls. When we feed our souls with God's word, the Holy Spirit dwells in us and operates and we even get the chance to know him well and how to use him in our daily life.

Do not commit sins :When one commits a sin, he or she chases away the Holy Spirit because the Holy Spirit never operates in a dirty soul. Ask the Holy spirit to give you the strength and ability to overcome all Satan's and trials and he will do so.

Respect your body :Your body is the temple of the Holy Spirit. If you impurify it ,example wearing improper clothes, sex out of wedlock or before marriage then you are going to chase the Holy Spirit away.

When one faces hardship in life or in a dilemma such that he or she does not know what to do, he or she should ask the Holy Spirit to show him the way out of it or to know on which path he or she should take. No matter how hard the problem is or how much complicated it is one should just call for the Holy Spirit's help and he or she will get a way out (solution). There is nothing which is impossible to God therefore one should know that there is a solution to everything.

A Christian's life is not always straight. There are always temptations and trials that he or she will face. They are always there so as God can know how much faith that one has and also they are a part of Satan so as to get followers. In order to overcome them, one should ask the Holy Spirit to always lead or direct him or her in the paths that will make him or her out/through it and will make him or her meet up with God in the end.

If one's faith is very strong, the Holy Spirit may lead him or her speak in tongues. Speaking in tongues is led by the Holy Spirit and it is the language spoken in the world of faith. This language works and Satan cannot interfere with it. In order one to have such a capability, he or she should pray hard for the Holy Spirit to help him or her to have it. One does not get it easily because it can also not be forged. The Holy Spirit controls everything in this.

If you feel the Holy Spirit wants to talk to you or to work in you in anyhow, do not stop him. The word of God says that if one tries to do so then he or she is committing a sin. Everyone must have the Holy Spirit in him or her because in the absence of the Holy Spirit one will always commit sins and he or she will end up in the everlasting fire.

At this time, Satan is hunting really hard for souls that will go with him to hell, therefore we should pray very hard for the Holy Spirit to dwell in us and give him our lives so as he can control and operate them and in the end, we go up in heaven and have an everlasting happy life with Christ the Lord.

Be blessed

By Margret Ng'ondia    


 NI VIGEZO GANI TUVITUMIE WAKATI WA KUOMBA?


"Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukomba kitu sawa na mapenzi yake, atusikia". 1Yoh 4:14

Maombi ni mawasiliano kati ya Mungu aliye hai na mwanadamu. Utaratibu huu haukuwepo awali bali ulikuja mara baada ya dhambi kuingia duniani ikumbukwe kuwa wakati wa mwanzo wa misingi ya dunia Mungu alikuwa akimtembelea Adamu na kuongea naye hivyo maombi hayakufanya kazi maana Mungu alikuwa karibu mno na mwanadamu Mw 3:8-10 utaona ndio utaratibu kuwa tembelea Adamu na Hawa.

Hivyo basi mara baada ya dhambi kuingia ilimsogeza mwanadamu mbali na uso wa Mungu hivyo kupelekea uwepo wa mawasiliano mapya yanayohitaji imani ili yafanikiwe maana pale mwanzo imani haikuwa na nafasi maana Adamu alimwona Mungu. Hivi sasa uko umuhimu wa imani maana Mungu haonekani kwa jinsi ya mwili. Imani ni kuwa na uhakika ya mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasiyoonekana kama isemavyo Ebr 11:1. Katika maombi imani hukupa uhalali wa kuweza kupokea kile tukiombacho.

Imani hiyo humwakishishia Mungu huyu ndiye sahihi mpe maana astahili, lakini licha ya uhakikisho huo sio kigezo pekee kitufanyacho yale tumwombayo Bwana basi tuweze kupokea. Kigezo kingine ni kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu. Sawa imani inakupa nafasi ya kuweza kupiga simu mbinguni hio ni hatua moja lakini kupokewa ni hatua nyingine na kujibiwa ni jambo jingine pia. Natamani tutazame maombi kwa mtazamo wa hili Roho Mtakatifu analokufundisha wakati huu. Naomba usichoke kukaa naye maana kuna vizuri anavyotamani akufundishe kwa ajili ya afya yako wewe na wengine pia.

Paulo mtume alisema mna omba lakini hampokei kwa sababu hamwombi sawasawa na mapenzi ya Mungu. Kuomba huko ni kwa namna gani? Huku ni kuomba kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Unajua yamkini yako mambo mengi ya kuombea ila namna yakupeleka mbele za inaweza ikawa kikwazo hivyo unapomshirikisha Roho Mtakatifu yeye hukupa usemi sahihi na maeneo gani tusimame.

Ngoja nikueleze kuomba kwa Roho Mtakatifu ni kwa ajabu sana maana licha ya wewe kuta kuombea vitu vyako lakini anakupa msukumo wa kuombea vitu vingine ili Mungu apate kuingilia mahitaji yako. Hata hivyo unaweza ukany'any'ania kuombea mambo yako na kumbe kuna 'barrier' inayokuzuia kujikonecti na madhabahu ya Mungu hivyo kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu ni kuomba kwa utaratibu kwa msaada wa Roho Mtakatifu.

Unaposoma Yn 16:24 inasema Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapewa; furaha yenu iwe timilifu. Unaweza kuwa na furaha kila wakati maana ndio biblia ituambiavyo Fil 4:4 Hivyo basi utaona kuwa furaha tunayo lakini sio timilifu. Utimilifu wake huja pale tupokeapo vile tuviambapo. Hivyo yatatimia hayo kama ukiweza kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu. Mungu akutie nguvu katika hili ewe mpendwa ulie ichagua huduma hii.

Barikiwa sana

Na Henry Nicholaus

KUNA MAENEO AMBAYO TUMEFUNGWA NA NDIO MAANA HATUFANIKIWI


"Na sasa, tazama,nakufungulia leo minyororo hii iliyo mikononi mwako…" Yer 40:4

Watu wengi huweka mikakati mingi wapo anza mwaka mfano kama tulivyo anza 2013. Lakini mara nyingi anapomaliza mwaka anagundua kuwa katika mikakati mingi aliojiwekea baadhi yake tu ndio iliyofanikiwa. Hii husababishwa na minyororo ambayo imewafunga watu katika maisha yao. Ndio maana Mungu anatueleza habari za kuwekwa huru katika mstari unaotuongoza hapo juu.

Efe 1: 3 Biblia inatueleza kuwa tumebarikiwa na Mungu baraka zote za rohoni. Ina maana gani? Mungu amekupa kibali katika kila lengo lililojema katika maisha yako. Lakini minyororo ndio imekuwa kikwazo katika kufanikiwa ndio maana hatuoni udhihirisho wa baraka hizo.

Dhambi kama moja ya mnyororo ambao umewafunga wengi ndio umekuwa mnyororo unaotesa wengi. Kwa sababu wengi waipenda dunia na biblia inasema ukiipenda dunia kumpenda Mungu hakupo ndani yako. Tunapotazama 1Kor 3:16 tunaona kuwa miili yetu ni hekalu la Mungu. Kwa maana hiyo tunapotenda dhambi tunamzuia Roho Mtakatifu kukaa ndani yetu hivyo tutakayo yaamua na kuyapanga yatakuwa yamekosa kibali cha Mungu. Hivyo kupelekea kutofanikiwa kwa mambo yetu Mith 16:1. Hata ukisoma Rum 3:23 biblia inasema kwa kufanya dhambi tumepungikiwa na utukufu wa Mungu. Ukosefu wa utukufu wa Mungu wakati wa kufanya maamuzi huathiri matokeo ya baadae.

Hata hivyo imani nayo ni mnyororo mwingine ambao umekuwa kikwazo katika mafanikio. Wengi hawana Imani katika wanayotazamia kufanya au wayaombayo. Hivyo kusababisha anguko lao. Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo Ebr 11:1 hivyo basi unapokosa uhakika kwa kile ulichoazimia ulipoanza mwaka hauwezi kufanikiwa. Imani hukupa uhalali wa kupokea kile ambacho kwa hali ya mwili hakipo kwa wakati huu. Pasipo kuwa na imani hatuwezi kuomba maana ni sawa na kazi bure.

Sadaka pia husababisha watu kutofanikiwa kama isipotolewa kwa uaminifu Mal 3:10 Biblia inasema tupeleke chakula ghalani mwa Bwana naye atatufungulia madirisha ya mbinguni. Tunapopokea hukumbuki kutoa tukisahau kama sisi nasi pia tumepokea kutoka kwa Mungu. Wengi huona wamepata kwa nguvu zao kisa waliangaika na kupata fedha. Lakini Mungu ndie aliefanikisha mchakato wote. Sadaka ni moja ya eneo linalomgusa sana Mungu. Ukisoma hata Elia alitumia kigezo hiki kuweza kumdhirisha Mungu wa kweli kati manabii wa baali.

Hivyo ni vyema unapoanza mwaka 2014 usitamani kufanya makosa tena. Tazama hiyo minyororo kisha amua kubadilika ngoja nikueleze huna hasara kama utaamua kubadika. Kumbuka mabadiliko haya yatakufanya utofautiane na wengine katika mtazamo na mwenendo hilo lisikuogopeshe bali tamani mafanikio tu achana na wanadamu kwa maana hao siku zote wapo. Hata hivyo biblia inatuonya tukiipenda dunia kumpenda Mungu hakumo ndani yetu.



THE WORD OF GOD


The word of God is power and the power is transferred to one place by the means of prayer through faith in the name of Jesus Christ. We pray for people to transfer the power of God's word that brings healing, deliverance and blessing. A servant has a word of God from God. The word God brings changes by its power that is working by prayers from faith. It is from that one can receive the power of God's word to change salvation.

The word of God must be spoken to anything, the word of God is spirit which gives life to anything hearing the word of God. That why if we speak to dry bones will set life spirit of darkness will flee away and presence of God to reign from Holy Spirit. By God's word we can speak to anything even that which has no life to have life because God speak to the lifeless and change them to abundant life the void face of the that has no form.

We need to pray so that Holy Spirit can make us to speak the word of God and so that we may speak by his authority of the Holy Spirit. Changes required by the word of in life of people. This is why God gives us his word. It is important to receive the word of God because it changes everything as we learn to speak by the authority of the Holy Ghost. We seek this in prayers to ask the Holy Spirit to make us bold to speak the word of God.

Speak from the Holy Spirit
When we speak the word of God the power in the word of God is released and brings effects and to speak by the help of Holy Spirit in this. Without the power of the Holy Spirit we are not strong enough to speak the word of God as it is needed. Many time in our lives are still the same because we have not understand to make the word of God real. It must be spoken by the tension and be heard. We need to understand how Holy Spirit will use our mouth to speak the word of God.

Holy Spirit speaks through us. He makes the will of God to us by speaking the word of God. We say healing but don't see healing, we say blessing no blessing, we say A no A , we say prosperity, we rebuke, we destiny works of the evil are still see nothing. Let the one inside you speak through you. This is the problem to many. Many people don't let the Holy Spirit speak through them by this don't give a room to Holy Spirit to speak the word through them.

God has promised whatever we need in his word in John 14:16. If you love me you will obey my command and  I will ask my father to give you a counselor who will be with you forever. Also in John 7:31 whosoever believes in me as the scripture has said streams of the living water will flow within him and by this he meant the spirit.

Holy Spirit (help us to speak the word through us. Believe in the name of Jesus. This is the command of God. And those who believe the following signs they will speak in tongue put hands in the sick and get health. Speaking in tongues is very important in this. John 6:6 The words which Holy Spirit speak to you are spirit. If you are in Christ you possess promise victory. You don't need to ask for it . When you in Christ the bible says you are not condemned but your are righteousness you have all the promise of God to you as his child he says you are the heir according to the promise of God. Don't think God is going to bring them no you have right in them. You have power anointing victory and all that he promised as the child of God to have, you just need to believe to have them. God has given us in the spirit and receive them in the spirit as use them by the spirit for the good of God. You have all first chance between for what you have with rejoice heart. I have it through faith in Christ Jesus.

When you are in Christ, victory is yours because God has promised victory to his children not other else and if you are a child of God the promise is fulfilled in you. I just need to say I have it Satan cannot take it from me because I have been made righteous by the blood of Jesus. What Satan tries always because he is not able to take what belongs to you by fear. Fear makes you lose your right as a child of God . When fear comes just tell Satan and am a child of God it is over. He understands and leaves. Because the word says you did not receive the spirit of fear but of son ship. Then if and am a son of God am the heir of his promise. If am a child of God the spirit of fear cannot dwell in me. Then fear goes away from my life because it is the same word that chased him, I will say again and again. Amen and Amen to my Soul.

Be blessed

By James Nyimbo.
             

UPATANISHO TENA


Unaweza kuanza kuwaza kwa nini neno upatanisho tena na sio upatanisho hilo lisikupe shida bali andamana nami wakati huu ili uweze kuelewa nini makusudi ya Mungun katika hili.

"Watu wale waliokwenda katika giza wameona nuru; Wale waliokaa kwenye uvuli wa mauti nuru imewaangaza, Umeliongeza taifa, umezidisha furaha yao; Wanafurahi mbele zako,Kama furaha ya wakati wa mavuno, Kama watu wafurahiyavyo wagawanyapo nyara. Isa 9:2-3

Kwa muda mrefu tulitembea katika shida kubwa kwa kutangatanga na katika giza totoro. Lakini Mungu akiona hili aliamua kumwachilia mwanae mpendwa Yesu Kristo ili arudishe furaha tena. Hivyo Yesu alikuja kwetu kama kipatanisho kati ya mwanadamu na Mungu aliye hai.

Kwa nini kutupatanisha tena? Ukumbuke kuwa toka mwanzo mwanadamu alikuwa rafiki wa Mungu. Mara ya dhambi kuingia katika bustani ya Edeni jambo hili lilisababisha mawasiliano ya Mungu na mwanadamu kuwa magumu. Kwa sababu Mungu hakai karibu na dhambi hivyo ile hali ya Adamu kutolewa katika bustani ilikuwa na maana yake yaani kuvunjika kwa mawasiliano ya karibu na Mungu.

Mara baada ya kuvunjika mawasiliano hayo maisha ya mwanadamu yakawa ya miangaiko mingi hivyo atakaye jitaabisha ndiye atakaye kula asiyefanya hivyo atakaa na njaa. Yesu anakuja kuleta neema kwa njia ya Mungu ili tuwe na Mungu tangu ile zamani Yn 3:16.

Unajua dhambi ni kitu kibaya sana ilisababisha mwanadamu apoteze nafasi aliokuwa nayo ya kumiliki na kutawala ipotee. Na nafasi hiyo kuchukuliwa na shetani basi ujio wa Yesu ulikuwa wa thamani sana kurudisha nafasi ya mwanadamu mbinguni na duniani. Unaposoma Mt 16:17-19 Yesu anamweleza Petro kuwa amempa funguo za ufalme wa mbinguni atakalolifunga duniani na mbinguni litafunguliwa atakalolifungua duniani na mbinguni litafunguliwa. Kwa utaona kwa ujio wa Yesu nafasi yetu ya utawala na kumiliki imerudishwa. Ndio maana kusema nimekupa funguo za ufalme wa mbinguni.

Upatanisho huu haupo kwa mtu ambaye hamwamini na kumkubali Yesu kama asemavyo Yn 1:11-12 "Alikuja kwake,wala walio wake hawakumpokea. Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake". Maana wako wengine wanamchukulia Yesu kama wa kawaida kumbe sivyo hawa wote na wengine wakataao kuwa yeye si Mungu hili jambo haliko kwao.

Hivyo kwa upatanisho wa pili ndugu mpendwa tumebariiwa kwa baraka za rohoni kama asemavyo Efe 1: 2 .Si tu hilo tumechaguliwa na yeye na kuwekwa muhuri na Roho Mtakatifu hili ni jambo la thamani kwetu hususani ukitazama kuwa yeye Roho wa kweli  hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa Rum 8:26 hili ni la thamani sana.

Kuzaliwa kwa Bwana Yesu ni neema na baraka kwa wengi hususani wale waeleao maana yake. Kwa sababu amekuja lakini sio wote wanaona sababu ya kumkabidhi maisha yao. Wewe ambaye umefahamu hili kwa msaada wa Roho wa kweli nenda ukafanyie kazi jambo hili maana hutajuta hata siku moja kwa busura unayochukua leo. Nakushukuru sana maana umemsikia Mungu. Basi sema sala hii

Baba wa Mbinguni uliye umba vyote nakushukuru kwa pendo lako lisilo na kipimo kwetu. Asante maana umekubali nirejee kwako tena. Nakusihi usitazama zamani zangu mbaya bali unirehemu kama neno lako lilivyonifundisha kwa habari ya upatanisho. Asante kwa kuwa unanisikia, sifa na heshima ni vyako. Amen.

Na Henry Nicholaus

Barikiwa sana.


 KUNA MAHUSIANO MAKUBWA KATI YA KUTOA SADAKA NA MAJIBU YA MAOMBI YAKO


Utoaji wa sadaka unafananishwa na upandaji wa mbegu. Kanuni ya kutoa sadaka inafanana na kanuni ya kupanda mbegu shambani. Mkulima timamu lazima atajiuliza kuwa nitaandaa shamba halafu nitapanda mbegu kwa kiasi kipi? Na mbolea gani atatumia na kwa kiasi gani? Na atavuna nini kwa kiasi gani na kwa ajili ya nini? Wengine kusomesha watoto, kununua gari, nyumba, kupata mtaji mwingine.

1Fal 18:21-29 Mungu hujidhihirisha kwa sadaka.  Elia alikuwa na mabishano ya kidini na manabii wa mabaali, hivyo akawaambia wanunue ng'ombe wawili na kisha watoe sadaka Mungu atakayejibu kwa moto huyo ndiye mungu wa kweli. Biblia inatuambia Elia aliwaambia waanze wao, waliangaika hadi kujichanja miili yao lakini hakuna kilichotokea hivyo ikawa zamu ya Elia naye akawaambia wamwage maji juu yake lakini Elia alipoomba moto ulishuka kutoka mbinguni na kuchukua sadaka.

Swali : Unadhani ni kwa nini mungu wa baali alishindwa kushuka?
Jibu : Hii ni kwa sababu Mungu wetu anapowekewa sadaka hataki ushirika na mtu hivyo basi. Miungu mingine lazima ikae pembeni wakati ambao Mungu anashuka maana hakuna kinachoweza kustahimili nguvu yake. Ndio maana miungu mingine ilikaa kimya.

Mungu anapotamani kusema na wewe usikatae. Maana kuna neema ambayo inataka kushuka ndani yako. Inawezekana hukumwona Mungu kwa macho ya damu na nyama. Lakini ndio staili ya Mungu kushuka katika sadaka. Kila sadaka inatakiwa kuwa na ujumbe nyuma yake 2Nya 1:1-10. Wakina dada msikubali ofa za ovyo maana hata ofa nazo zinaujumbe nyuma yake uliofichika. Suleimani baada ya kutoa sadaka ya kuteketeza ya maelfu. Mungu akashuka akamwambia na ujumbe sasa ni nini?

Unapoitazama sadaka itazame kama mkulima maana yeye huwaza mavuno kwa lengo kuwa atavuna kiasi gani na kwa ukubwa gani? Ebr 11:4 Habili alitoa sadaka kwa imani. Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo. Habili wakati  anatoa sadaka yake alikusudia kupata kitu. Atoe kwa imani atapokea mabadiliko maana sadaka yake ilipata kibali. Tatizo sio kutoa sadaka bali kufuata utaratibu na imani. Tusitoe kwa sababu ya utaratibu wa ibada. Tunatoa kwa sababu tumepata msukumo utokao ndani wa kutoa na si kwa sababu umeambiwa utoe.

Sikiliza hata madhabahu ya shetani inataka sadaka ili ipate kujibu ndio maana wengine hutoa watoto, ndugu, wazazi na hata viungo vya binadamu. Shetani ameiga mfumo huu ili apofushe watu waone ni sawa na Mungu lakini sio kweli. Zab 20 inatueleza kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya sadaka na majibu ya moyo wako.

2Fal 4:8-17 Elisha alikwenda Shunemu, mama mmoja tajiri alimshurutisha ale chakula kwake. Lakini yule mama alimwona Elisha kuwa ni mtumishi wa Mungu hivyo aliazimia na kumwambia mumewe wajenge chumba ili wapate kumwifadhi Elisha akipita katika mji huo. Sadaka ya kwanza ya yule mama hakumgusa Mungu bali ilimpa upako au maono ya sadaka ambayo hiyo ndio itakayoachilia majibu ya matatizo aliokuwa nayo. Na hiyo ndio sadaka ya chumba cha kulala alichokiandaa.

Ebr 11:4 Biblia inatuambia tofauti ya sadaka ya Habili na Kaini haikuwa kwa vitu bali Habili alitoa kwa imani lakini Kaini hakutoa kwa imani. Macho ya habili yaliona matokeo.Hatimaye sadaka yake ikapata kibali. Wako watu mazoea shida yuko tayari kupambana na matatizo kuliko kumwachia Yesu apate kushughulika nayo. Hivyo wanataka sana dini kuliko Yesu. Ndio maana hata Yesu aliuliwa kwa sababu ya dini.

Unapotoa sadaka shughulikia utu wako wa ndani maana utu wako wa nje ni mavumbi. Pesa hazitoki usipotoa pesa maana zina masikio ya kusikia, macho ya kuona ijapokuwa hazina uhai zinajua zielekee wapi. Hivyo pesa ni roho ziendee rohoni ili ziwe zako. Toa pesa ili upate pesa.

Barikiwa kwa kunisikiliza

Na  Henry Nicholaus


TUSIPOKUBALI KUACHA NCHI TULIOPO NA KWENDA ILE ALIOTUAGIZA MUNGU HATUTAFANIKIWA


Mw 12: 1-4 Kuna mahali ambapo Mungu amekuandalia ndio hiyo nchi. Usipofika hiyo nchi huwezi kuona baraka. Ibrahim hakuweza kubarikiwa mpaka alipoamua kuondoka katika nchi Bwana aliowaonyesha.Kabla Mungu kumwambia Ibrahim aondoke katika nchi alioishi ilikuwa ya baba zake. Baba yake alikuwa muuza vinyago, hata Ibrahim naye alifanya biashara hiyo. Hivyo hiyo nchi ilikuwa imefungwa na miungu ya baba zake pamoja na laana za mizimu na mambo ya kimila. Hivyo Mungu asingeweza kulikalisha jina lake eneo kama hilo. Ndio sababu ya kumwambia Ibrahimu aondoke.

Ukitazama utaelewa wakati Ibrahim anaondoka alikuwa na umri wa miaka 75 lakini ilimchukua miaka 24 kupata mzaliwa wake wa kwanza wa halali tena wa haki yaani Isaka. Sababu hii ilitokana nchi aliokuwepo awali Ibrahimu isingeweza kumlea vyema mzaliwa wa kwanza Ibrahim. Mw 12:2 Mungu anamwambia Ibrahimu kuwa atamfanya kuwa taifa kubwa na kumbariki. Natamani uchunguze wewe mwenyewe hivi Mungu alishindwa nini kumfanya taifa kubwa akiwa kwenye nchi aliokuwepo. Utagundua miungu ilokuwa inamiliki nchi ya baba yake ndio ilikuwa kikwazo.

Yamkini mpaka leo upo kwenye nchi za baba zako usipotoka huko Mungu hana msaada wa kukupa. Nchi yako yaweza kuwa desturi ya maisha, mazoea fulani au mapokeo ulioyapata toka kwa mababa zako. Haya yote ni nchi hivyo ni lazima ubadilike ili Yesu akumilikishe ufalme kisha aingilie kati mambo yako.Kwa mfano tabia za kufanya arubaini, ulevi, matambiko ya kimila, desturi ya kuishi nk. Hizi ni lazima uziache sikiliza Mungu ni mwenye wivu hawezi kushare ufalme miungu mingine.

Lk 5:2-7 Yesu anamwendea Petro alisameme kwenye mashua yake awezekuhubiri Petro anakubali. Ndipo baada ya kumaliza kazi hiyo Yesu anamwambia Petro shusha nyavu kilindini. Ukumbuke ni asubuhi, na jana yake waliangaika usiku kucha wasipate samaki lakini Yesu alipomwambia licha sio kawaida ya wavuvi kuvua asubuhi biblia inasema nyavu zilianza kukatika.Ina maanisha nini Petro hapo awali alikuwa anavua katika miungu ya baba yake kwa sababu babaye alikuwa mvuvi naye alirithi taaluma hiyo. Hiyo miungu ina viwango vya kufanya kazi haiwezi kila kitu. Hivyo Yesu alipokuja alipomwambia Petro shusha nyavu zako ali ni asubuhi naye akakubali ilionyesha Petro alikubali kutoka katika nchi aliokuwepo na kwenda katika nchi aliomwonyesha Yesu.

Ndio maana Lk 5:8 Petro anamwambia Yesu ondoka kwangu mimi ni mwenye dhambi.Petro aligundua nchi aliokuwepo si nzuri lakini ile Yesu aliokuwa anampeleka ni nchi ya kweli. Ewe mama, baba, dada,kaka na kijana mwenzangu unayesoma waraka huu ni wakati muafaka ambao Mungu ametaka wewe uhame katika nchi ya mazoea. Efe 1:3 inatuambia umebarikiwa kwa baraka za rohoni kama umepewa kila kitu mbona unaishi maisha ya shida hii ni kwa sababu hujaweza kujua utaratibu wa kuwa na hizo baraka.

Namshukuru Mungu maana sasa umeelewa kutoka katika nchi uliopo. Jaribu kubadili mfumo wa maisha uliokuwa nao kama kutokana na Roho Mtakatifu alivyokufundisha siku hii ya leo. Maana Mungu anataka kukubariki katika masomo, kazi upandishwe cheo maradufu, uajiri usiajiriwe, umiliki viwanda, magari, na pesa nyingi.

Chukua hatua
Barikiwa

Na Henry Nicholaus



No comments:

Post a Comment