Bwana Yesu asifiwe, kuanzia tarehe 1/1/2017 tutakuwa tukihamia katika website yetu iitwayo www.egospeltz.org

NEW



KAMA UTABIRI JUU YA KUZALIWA KWA YESU ULITOKEA UWE NA UHAKIKA HATA SIKU YA MWISHO INAKUJA
 Isa 9:6 inasema, "Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake, Naye ataitwa jina la ajabu, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu baba wa milele, Baba wa milele, Mfalme wa amani".
Tunaposoma hicho kifungu hapo juu tunaona utabiri wa Nabii Isaya juu ya ujio wa Yesu naye akafafanua ni kwa namna gani atakavyokuwa . Japo wako watu wa wakati huo ambao hawakuamini kwa kuwa ilichukua muda mrefu tangua Isaya na manabii wengine walipotabiri. Na kwa sababu hiyo wengi walipuuza lakini hatimaye Yesu alizaliwa. Hivyo basi hii ni kati ya utabiri mwingi ambao biblia imeeleza na kutokea. Haya pia tunaweza kuyaona katika Isa 7:14.
Japo hali ya kupuuza mambo ya msingi pia ilijitokeza kipindi cha Nuhu alipowaita wapate kujenga Safina. Pia katika ulimwengu wa sasa bado tunaona haya pia yakijirudia. Na bahati mbaya hatuna utamaduni wa kujifunza makosa ya waliopita. Biblia ambayo ilitabiri juu ya kuzaliwa kwa Yesu ndio hiyo hiyo imeeleza habari za kurudi kwake Mdo 1:11, 3:19-21, Col 3:4. Licha ya kwamba biblia imeeleza haya bado imetupa na tahadhari ya kujua kukaribia kwake kupitia mabadiliko mbalimbali yatakayo tokea  1The 5:2-6.
Biblia inapotueleza juu ya kurudi kwa Yesu ni jambo la uhakika. Kwa sababu ukiangalia tangu Ibrahimu mpaka Daudi ni vizazi 14 na tangu Daudi hata uhamisho wa Babeli ni vizazi 14 na tangu uhamisho wa Babeli hata Kristo ni vizazi 14 Mt 1:1,17. Ukijumlisha jumla ya vizazi toka Ibrahimu hata Kristo (14+14+14=42) ni vizazi 42. Tokea Yesu hata leo ni vizazi 20. Kwa hiyo toka Ibrahimu hata sasa ni vizazi 62. Kwa kuwa wastani wa kizazi kimoja huchukua miaka 100. Hivyo tukizidisha (62 x 100= 6200). Kwa hiyo toka Ibrahimu hata sasa imepita miaka 6200 kwa wastani maana viko vizazi vilikuwepo kwa zaidi ya miaka 100 na viko vilivyokuwepo chini ya miaka 100. Ndio maana nimetumia neno wastani. Ni miaka ya makadirio.
Kwa sura hii tunajua kama Mungu aliumba dunia kwa siku 7 akapumzika. Hii ina maana dunia haitazidisha siku 7 za uwepo wake. Siku moja mbinguni ni miaka 1000, hivyo basi siku 7 ni sawa na miaka 7000. Hivyo ikiwa toka Ibrahimu hata sasa imepita miaka 6200. Ni muhimu ukajua kuwa siku ile iko karibu kuliko vile unavyofikiri. Kwa kuwa dalili ambazo tunaelezwa na 1 The 5:2-6 pamoja na ufunuo ziko wazi kabisa. Hivyo ukichukua (7000-6200=800). Miaka 800 ndio muda wa makadirio wa uhai wa dunia uliobaki. Hivyo siku hiyo inaweza ikaja baada ya kipindi chochote ndani muda huu japo hakuna ajuaye.
Hii ni tafakari tu hivyo ikusaidie unapokuwa unaishi uwe unaelewa ni kitu gani kinaendelea duniani. Na inawezekana tokea sasa siku ile ikawahi kuja au ikachelewa kwa kuwa sisi sio wenye maamuzi nayo ila Mungu pekee yake. Hivyo ni vyema ukajiandaa kuanzia sasa kwa kuishi maisha ya kujihadhari. Shetani naye kwa kuwa anajua haya halali kuhakikisha anaweza kumeza watu wa kumsindikiza jehanam. Kuwa makini na kiny'ora hiki                                                                         

Na Henry Nicholaus

KUNA UHURU SAHIHI NDANI YA YESU KRISTO.
BWANA YESU asifiwe
Karibu tujifunze jinsi ya kuwa huru na kuulinda uhuru .
Mataifa karibu yote ya kiafrika yalitawaliwa na wakoloni. Ni Ethiopia na Liberia tu ndizo hazikutawaliwa baada ya mkutano mkuu wa Berlin wa mwaka 1884, Hata Misri ilitawaliwa japokuwa kwa muda mfupi. Mataifa mengine yote yalikuwa wanatawaliwa na wakoloni lakini ulifika muda wa kuwa huru baada ya utumwa na mateso ya miaka mingi. Uhuru huu ni uhuru kamili lakini baada ya uhuru huo kuna ukoloni mamboleo unafuata. ujumbe wangu leo unazungumzia uhuru au kuwa huru na uhuru huu ninaouzungumzia hauna ukoloni mamboleo bali ni uhuru kabisa. Uhuru sahihi unatolewa na MUNGU katika KRISTO YESU pekee.
Yohana 8:36 ''Basi Mwana (YESU) akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.'' 
YESU Akikuweka Huru, Unakuwa Huru Kabisa. Ndugu Yangu nina swali kwako.
Kwanini Kwenye Baadhi Ya Maeneo hujawa Huru? Kwa nini Uteswe Na Mapepo? Kwa nini Usumbuliwe Na Wachawi Na Mizimu? Kwa nini Tamaa Mbaya Ikuzonge?.
Jibu ni kwamba Kuna Kitu Unapungukiwa.
Kama Hupungukiwi Maombi Basi Unapungukiwa Neno. Kama Hupungukiwi Mafunuo Basi Unapungukiwa Nguvu za MUNGU. Kwa sababu ya matendo Yako. Kama Hupungukiwi Nguvu Za ROHO MTAKATIFU Unapungukiwa Imani. Kama Hupungukiwi Utakatifu Basi Unapungukiwa Kusoma Neno.
Lakini sasa mkiisha kuwekwa HURU, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa MUNGU, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele. Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya MUNGU ni uzima wa milele katika KRISTO YESU BWANA wetu" Warumi 6:22
Ndugu Angalia Ni Wapi Unapungukiwa Ili Utengeneza Na Uwe Huru Kwa Jina La YESU KRISTO. Na Ukiwa Huru Wachawi Wakija Watakuta Malaika Wasio Na Idadi Kwako, Kama Wakija Mapepo Watakuta Kuna Ukuta Wa Moto Ambao Hauna Mlango Wala Dirisha,Wakija Mizimu Watakutana Na Viboko Vya Moto Visivyo Na Idadi.
''Na mlipokwisha kuwekwa HURU mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki" Warumi 6:18
Hakika YESU Akikuweka Huru Unakuwa Huru Kabisa. BWANA YESU Anakupenda Sana Na Muda Huu Anakuandalia Makao Mbinguni.Ukipendwa Na YESU ni bora kuliko vyote. BWANA YESU akukumbuke na kukupa uzima wake.Ndugu unatakiwa uwe huru mbali na uonevu wa shetani. na uhuru huu MUNGU amekupa kupitia YESU KRISTO jambo la kufanya wewe ni kuitumia mamlaka ya KRISTO ambayo iko ndani yako kujiweka huru kwa maombi. Kama YESU hajaingia kwako basi mpe maisha yako leo na uhuru kamili utaupata tena uhuru wa milele.
Mwenye Nyumba Hapigi Hodi.Mwanadamu Ni Nyumba, Inaweza Kuwa Nyumba Ya MUNGU Au Nyumba Ya shetani. ukitaka kuwa huru basi shikamana na MUNGU wako katika KRISTO YESU.Kama Wewe Umemruhusu shetani Akufanye Kuwa Nyumba Yake; Nakuhakikishia Muda Wowote shetani akitaka kuingia ataingia tu maana wewe ni nyumba yake, na shetani ni Mbaya Sana Na Aliowageuza Nyumba Yake Lazima Wakabwe Na Majinamizi Usiku, Lazima Waote Wanazikwa, Lazima Waamke Asubuhi Wakiwa Wamechoka Maana Wachawi Walikua Wakilia Nyama Za Watu Juu Ya Migongo Yao Usiku Wakiwa Wamelala.
Ndugu Yangu YESU Akikuweka Huru, Utakuwa Huru Kabisa .
Kuna Dada Mmoja Zamani Tukiwa Shule ya msingi Ambaye Kwao Walikuwa Wachawi kabisa Maana Hata wao Walikuwa Wanajitangaza, Dada huyu Alituuliza Swali Kwamba " Nani Ambaye Baadhi Ya Siku Huamka Asubuhi Mdomo Wake Ukiwa Mchungu Sana?" Wengi Walinyoosha Mikono; Akasema "Ukiamka mdomo mchungu sana Ujue Usiku Wachawi Walijisaidia haja ndogo kinywani mwako " Akasema Hata Yeye Amewahi kuwawekea Mikojo Wengi, Siku Akienda Na Mama Yake Kuroga.
Ndugu yangu ona ubaya huu wa shetani kwa wale ambao hawajawekwa huru na YESU, ona ubaya huu wa shetani kwa watu ambao shetani anawamiliki, ona ubaya huu wa shetani kwa watu ambao yeye shetani ni mkoloni kwao. YESU kwa upendo wake wa ajabu akaamua kuja ulimwenguni ili tu mimi na wewe tusiteswe tena na wachawi. na wachawi ni wabaya sana maana kama wanauwezo wa kula nyama za watu watashindwaje kujisaidia kinywani mwako? wana roho ya shetani, roho ambayo haina huruma na mwanadamu yeyote. Lakini BWANA YESU akasema kwenye kikao kule mbinguni kwamba ''Mimi hii sivumilii, Lazima niende nikawaokoe wanadamu na dhambi zao, lazima nikahakikishe wote watakaonifuata watakuwa huru tena huru kwelikweli''
Ndugu Ndio Maana BWANA YESU Alikuja Ili Tusiwe Nyumba Ya shetani tena. Biblia inasema hivi katika 2 Kor 5:17 '' Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. ''
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.

JINSI YA KUFANYA ILI KUWEZA KUOMBA KWA MASAFA MAREFU.
 Nimekuwa nikipata maswali mengi kwa watu yahusuyo mambo mbalimbali lakini katika ujumuishaji wangu nikagundua katika maswali yote 70 Yananauliza ni nini chakufanya ili kuweza kuomba kwa muda mrefu. Sasa kutikana na hilo leo nimeona nikuletee mbinu hizo za kufanya ili kuweza kufaulu zoezi hili la kuomba kwa masafa marefu.
Mambo muhimu ya kufahamu kubadilisha mtazamo uliyonao kuhusu maombi. Kuna kadhia nyingi iliyojengeka mioyoni mwa wengi kuhusiana na swala la maombi ya muda mrefu, wengi wanatamani tu kuyafanya lakini wanajikuta wanashindwa kutokana na kile kilichopandwa mioyoni mwao, ipo mitazamo potofu juu ya maombi kama ifuatayo, kuna watu wanaamini kwamba kuomba kwa muda mrefu ni neema, ni karama, ni nguvu ya Roho Mtakatifu. Hii mitazamo isipofutika ndani yako kamwe hutaweza kuomba kwa muda mrefu kwa sababu ni mitazamo potofu ambayo haina ukweli ndani yake, siku zote huwa nawaambia watu kwamba KUWA MWOMBAJI SIYO NEEMA,, WALA KARAMA, MAOMBI NI JUHUDI ZA MTU BINAFSI kuwa muombaji ni maamuzi ya mtu binafsi.
Mimi nilipokuwa mchanga kiroho nilifundishwa sana habari za maombi na nilisikia watumishi wakifundisha kwamba kuomba kwa sana ni nguvu za Roho wa Mungu na neema. Mimi niliamini hivyo na nikakaa ili kuisubiri hiyo neema inishukie na hiyo nguvu inishukie lakini siku zikazidi kuyoyoma na sikupata. Siku moja nikajiuliza kwamba kwanini Mimi siwezi kuomba masafa marefu kama Mama Mchungaji wangu anayeomba masaa 7 kila siku.Hii iliniumiza sana maana nilitamani kuwa kama yeye lakini kwa kuwa niliamini ni karama basi nikaridhika maana sina hiyo karama, lakini siku moja nilikaa na yule Mama nikumuuliza siri ya mafanikio yake ya kuweza kuomba kwa muda mrefu akaniambia hivi, NIMAAMUZI NA MAZOEZI, Akaniambia hakuna neema wala nguvu itakayokushukia na kukufanya ombe bali ni JUHUDI yako mwenyewe hiyo ndiyo itakusaidia hasa pale unapofanya mara kwa mara kwa kumaanisha na hatimaye mwili unazoea hali hiyo na kuiona kuwa ni kawaida.
Nami nikajaribu kuyatafuta maandiko nikagundua kweli kuomba siyo neema wala karama bali ni juhudi na ndiyo maana Hata Paulo hakuomba kwa karama bali aliomba kwa juhudi yani kile kilichomfanya Paulo awe mwombaji ni JUHUDI zake mwenyewe 1WATHESALONIKE 3:10, na hata kanisa la kwanza wote walikuwa waombaji kwa sababu ya JUHUDI zao MATENDO YA MITUME 12:5. Baada ya mimi kupata siri hii niliamua kuanza na mazoezi Unajua kila kitu ni mazoezi na baada ya kuanza mazoezi niligundua kwamba HAKUNA KAZI RAHISI KAMA KUOMBA, nilianza kuomba. Na kila nilipotaka kuomba kabla nilidhamiria kwanza kwamba, nitakapopiga magoti hapa sinyanyuki mpaka nimalize masaa mawili.
Hivyo nikafanya hivyo kila siku nikawa napiga magoti kuomba naomba lakini kuna wakati najikuta nachooka sana na Shetani ananiambia Akilini kwamba SASA INATOSHA USIJITAABISHE MUNGU AMESHAIONA NIA YAKO, mimi nilitambua hii ni nia ya Shetani anayoileta Akilinimwangu lakini nikawa najiuliza kwamba HIVI MKULIMA ANAPOLIMA HUWA HACHOKI? Jibu napata kwamba anachoka tena sana ndiyo maana utamkuta na chupa yake ya kidumu chake cha maji pembeni kinamsubiria analima kidogo kisha anakunywa maji lakini haachi kulima kwa kisingizio cha kuchoka kwa sababu anajua faida atakayoipata baadae kwenye mavuno kulingana na taabu yake.
Sasa baada ya kujiuliza maswali hayo niliamua sasa kuendelea na maombi hata kama ndani nasikia kuchoka. Hivyo sikuacha kuomba mpaka yale masaa mawili niliyoyapanga yakatike ndipo nitahitimisha maombi hayo. Unajua mwana wa Mungu hakuna muimbaji aliyeweza kuimba pasipokuchukua mazoezi na pia kuwa na mwalimu mzuri wa kumfundisha kuimba. Vivyo hivyo na kwenye maombi haiwezekani mtu kuweza kuomba pasipo kuchukua mazoezi na kupata pia mwalimu mzuri atakayemfundisha habari za maombi.
Niliendelea na hali hiyo, nikaazimia moyoni mwangu kwamba sasa kila siku lazima nimalize masaa ma4 kwenye maombi ya mfululizo nikawa nafanya hivyo ikaenda nikapanda mapaka masaa saba. Nikapanda masaa nane, nikapanda mpaka masaa kumi hivyo nikauzoesha mwili kwa kuutesa kila siku hatua kwa hatua hata ukazoea kuomba kwa masafa marefu. Hivyo kuomba kwa masafa marefu ni sawa tu na kuimba kwa muda mrefu muimbaji haimbi kwa sababu amejawa na Roho ya kuimba, no bali anaimba kwa sababu anapenda na ameamua kuimba. Namwonaga Muimbaji jasho linamtoka sauti inakauka lakini haachi, anaendelea hii yote ni kwasabu ameamua sikwamba hachoki anachoka sana likini kwa sababu amedhamiria haachi kufanya na hivyo ndivyo ilivyo kwenye maombi.
Sasa kuna lile andiko linalotumiwa vibaya linalosema Roho hutusaidia kuomba. Hili andiko halimaanishi kwamba Roho anatuombesha hapana mimi niliamini hivyo na sikuona matokeo. Maana ya andiko hili ni kwamba Roho ndiye anayetufanya tuombe katika roho yani tuzame ndani ya Roho na kutuletea ile hali ya kuugua ndali hata kulia machozo na pia ndiye anayetupa muongozo wa kwamba ni aina gani ya maombi ya kuomba kwenye kila eneo. Lakini siyo kwamba Roho anashuka na kukufanya uwe muombaji hapana kuwa muombaji ni maamuzi ya mtu mwenyewe kwa hiari yake.
Maandiko yanazungumza habari ya Nguvu kila mtu hujiingiza kwa nguvu LUKA 16:16. bilbia haisemi kwamba kila mtu ANAINGIZWA, no soma vizuri utaona inasema HUJIINGIZA yani anazitumia nguvu zake kwa mambo ya Ufalme wa Mungu sasa hapa inategemea anazitumiaje huenda anazitumia kuhubiri, kuimba, kufanya kazi za kanisa Au kuomba hivyo ilikuweza kuomba kwa masafa marefu ni lazima kuzitumia nguvu zako katika kuomba yani kuzitoa nguvu zako zote hapo, DHAMIRA YA NDANI YA MOYO IWAZE MAOMBI TU. Kila mwanadamu anakitu moyoni mwake anachokiona kuwa ni cha thamani, ambacho anakiwaza kila wakati, moyo wake unakiona kuwa ni cha thamani ni chamuhimu sana kuwanacho hivyo kutokana na hilo anajitahidi kufanya kila liwezekanalo ili aeze kukipata, sasa kuanzia sasa hivi kifute kitu hicho moyoni na kwenye nafasi yake weka maombi.
Maombi ndiyo yachukue nafasi ya kitu hicho moyoni mwako, yani yaone maombi kuwa ni kitu cha muhimu kupita vyote niafadahali ukose muda wa kufanya kingine lakini upate muda wa kuomba. Kwa sababu maombi yamebeba kila kila kitu ndani ya maisha ya mtu. Maombi yamebeba afya, yamebeba uchumi, yamebeba kibali, yamebeba nguvu ya ushindi, yamebeba wokovu maana hakuna atakayeokoka kama hakuna muombaji anayeomba ili watu waokolewe ndiyo sababu hata Yesu hakuzaliwa pasipo maombi ya Ana, Bint, Fanuel LUKA 2:36-38. Hivyo maombi ya Ana yalituletea wokovu ndiyo maana nasema ndani mwa maombi kuna wokovu.
Hivyo ni lazima maombi yatazamwe kwa mtazamo huo maombi yanaleta vitu bali vitu havileti maombi huwezi kuwa muombaji kwa sababu una gari bali unaweza kuomba ukapata gari huo ni mfano hivyo maombi yanatangulia mbele ya vitu vyote kabla ya vitu yaanze maombi. NGUVU YA ROHO ITAKUKAMATIA NJIANI. Nguvu ya Roho haitangulii mbele ya mtu bali huja katikati ya safari, Siku ya kwanza aliposhuka Roho Mtakatifu hakuwakuta mitume barabarani wanarandaranda hovyo wala hakuwakuta Kwenye viosk wanakula mishikaki na chipsi no bali aliwakuta ghorofani wanasali kwa moyo mmoja Mdo 1:14.
Mdo 2:1-4. Hivyo Roho aliposhuka hakuwakuta wamelala usingizi no aliwakuta wanasali kwa moyo mmoja ndipo akawajaa ndani yao wakaaza kunena kwa lugha kama alivyowajaalia sasa hii inaonyesha ya kwamba Roho haanzi yani hamuanzi mtu bali mtu ndiyo anaanza kisha Roho anakuja njiani na kumtia nguvu za kuendelea na nguvu hiyo haifanyikazi nje ya matakwa ya mtu no bali inafanyakazi ndani ya matwa ya mtu kwa kadiri ile alivyojiachilia maana Roho halazimishi Yohana anabainisha kuwa upo uwezekano wa kuotoa Roho kwa kipimo YOHANA 3:34. Hii inamaanisha kwamba Roho anapenda na anataka sana watu waombe au watumikie sana kusudi la Mungu lakini wao humtoa Roho kwa kipimo yani wanafanya kwa kipimo cha matakwa yao na siyo matakwa ya Mungu.
 Mimi nimezoea maombi kwa muda wa miaka 8 nimeishi maisha ya Maombi huwa maranyingi sana inanitokea ninapokuwa kwenyemaombi kuna wakati Natakakukatisha maombi niendelee na majukumu mengine lakini kila nikitaka kufanya hivyo ndani yangu nasikia Msukumo wa kuendelea kuomba sasa Huyu ni Roho anataka niendelee kuomba lakini swala la kuendelea amakutokuenelea ni lakwangu mwenyewe naweza tu kukatisha hata kama ndani bado kunamzigo na huku ndiko kumtoa Roho kwa kipimo maana hapa unakuwa umeomba kwa kipimo kile unachokitaka wewe lakini siyo kile anachokitaka Mungu hivyo hali hiyo inaponitokeaga juwa sinyamazi na siachikuomba bali naendelea mpaka hapo Ujle mzigo utakapoisha na wakati huo wakuendelea kuchoka huwa kunanijia njiani lakini siachi kuomba pamoja na hiyi hali ya kuchoka maana najua sipotezi bali nafanya kazi yenyefaida hivyo siangalii mwili bali naliangalia liletarajio la ushindi kutokana na maombi yangu, hakika niliona miujiza ya Mungu ambayo ilinifanya nipigwe vita hata kuitwa Fremason. UDHAIFU WA MWILI NI USHINDI KWA SHETANI Usiendekeze udhaifu wa mwili Yesu alisema roho iladhi lakini Mwili ni dhaifu MATHAYO 26:41. hapa Yesu kakukurupuka tu kulisema neno hili, bali alilisema hili kwa ile picha aliyoina mbele yake kwa wanafunzi wake, Aliisoma miyo yao akagundua kwamba Imejaa visingizio tele vya kutokuomba lakini Yesu alipovisoma visingizio hivyo ndani ya mioyoyao akajua kwamba vinatokana na kutokuujua ukweli juu ya Mwili maana wao waliwaza kwamba Yesu anaomba sana kwasabu ananeema Ana Karama, Ana Roho ya Mungu wakafikiria kwamba Ukiwa na Roho wa Mungu tu basi utaweza kuwamuombaji kama Yesu mwenyewe, Baada ya Yesu kuuona Ujinga huo na giza liliwafunga mioyo ndipo akawafumbua macho kwa Kusema ROHO IRADHI LAKINI MWILI NI DAHIFU. maana yake ni kwamba Kama niyi hamtaki kuomba kwasabu ya Mwili basi mjue kamwe hataweza kuomba milele kwasabu Mwili NIDHAIFU na bado utaendelea kuwa dhaifU, Hapa Yesu hakusema Miili Yenu ni dhaifu no bali alisema Mwili nadhaifu akiwa na maana ya kwamba hata yeye mwenyewe binafsi mwili wake ni dhaifu na hii ndiyo sababu aliomba kimkombe kimuepuke maana wmili wake uligoma kwenda msalabani kitu ambacho kiliipelekea roho kuugua kiasi cha kufa maana inajua hasara itakayotokea endapo Mwili hautasulubiwa, ndiyo maana Yesu ilimbidi akautie mwili ganzi kwa maombi ya kukesha usku kucha hatimaye mwili ukafaganzi na kukubali wkenda kusulubiwa, Hivyo Yesu aliposema ROHO IRADHI LAKINI MWILI NI DHAIFU alimaanisha kwamba KUNAVITA KATI MWILI NA ROHO vinashindana hivyo ili mtu aweze kushinda ni lazima aupuuze mwili asiusikilize kwa hiyo Hapa aliwaabanishia mitume kwamb MIMI SIMBI KWASABU YA KUJAWA NA ROHO BALI NAOMBA KWASABABU NIMEUPUUZA MWILI SIUENDEKEZI, hii ndiyo siri ya Ushindi wa Yesu kwenyemaombi sasa Yesu anataka ufute hizo sababu za kuufuata mwili maana huko ni kutafuta kufa bali Mungu anataka tuishi kwa maombi hivyo kamwe usitarajie kama Mwili utakuruhu uombe no hilo halipo kuomba ni kuamua kuomba. USIACHE KUOMBA OMBI HILI NI MUHIMU SANA KWAKO Ukiisha maliza toba tu maana hakuna maombi kabla ya toba kutubu na kuomba rehema NILAZIMA kabla ya yote kisha baada ya hapo Ombi lako kubwa kwa Mungu yani ombi la pili tu baada ya toba Omba Kuwa muombaji mlilie Mungu Mwambie nata kuwa muombaji Usiombe kuwa mwana maombi no Omba kuwa Muombaji maana wapo wanamaombi wasiyoomba, mwambie Mungu nimeamua kuishi maisha ya Maombi ya Sunami nisaidie Bwana, omba sana ombi hilo usiliache litakusaidia Mungu kuugeuza moyo wako na kuanza kuyaishi maombi , litakufanya kuumbika ndani yako Kiu ya kuomba Mimi sijaacha ombi hilo mpaka leo tangu nianze kuomba na nimeona matekeo makubwa. Tena unamwambia Mungu kabisa nataka kuomba masaa kadhaa Ma4 au 6 hata 10 inawezekana.=LUKA 1:37. Ahsante kwa kunifwatilia Ahsante kwa kulike page yangu ambayo imekusudia kubadilisha maisha ya watu watoke kwenye ulokole wa Mazoea na ulegevu na kuingia kwenye UANAFUNZI halisi wa Yesu. Pia karibu kwenye Group letu jipya kabisa kwenye Whtsapp la FUNGUO ZA UFALME Group hili ni kwaajili ya watu wapya tu Kama wewe upo kwenye yale mawili ambayo yamejaa usitume Ombi maana sitokuunganisha nataka watu wapya ambao wamekosa nafasi kwenye yale magroup ya KISIMA CHA UTAKASO na MLIMA WA UAMSHO ambayo yamejaa ndiyo sababu nikatengeneza hili la tatu la FUNGUO ZA UFALME kama wewe haupo kwenye Group zile za kwanza na ungependa nikuunge kwenye Group hili jipya Nitumie Masage Kwenye Whtsapp Yangu 0767 503054 nitakuunganisha ZIDIKU BARIKIWA  Na Mtumishi Peter Lukuta.

EPUKA MAISHA YA MAIGIZO KWA KUWA HAYANA MSAADA WA KUKUFUKISHA MBINGUNI
"Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo,hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni" Mt 6:1
Mstari huu ambao Mungu ametupa kutafakari kile kilichopo ndani yake. Unapoanza unaanza na neno la tahadhari yaani 'Angalieni'. Katika neno hili tunapata kuweka makini katika kile ambacho kinaendelea kwa kuwa neno hili hutumika kuvuta umakini wa msomaji.
Yako mazoea ambayo watu wamejijengea ya kuhudhuria ibada za Jumapili lakini pindi inapotokea semina au maombi huwa watu hawana muda. Wengi hufikiri kuwa ibada ya Jumapili ni toshelevu kwa kuimarisha mahusiano yao na Mungu kumbe si kweli, bali ni siku iliopendekezwa na kuingizwa katika mfumo iwe siku ya wakristo kuabudu kama ilivyo kwa watu wa imani nyingine. Hivyo si busara kuacha kuhangaika kumtafuta Mungu wakati mwingine kwa kigezo utaenda Jumapili au ndivyo ulivyozoea.
Pia ni muhimu kwa mtu kuweka umakini na kuona uthamani pale anapopata nafasi ya kuomba au kusikiliza neno la Mungu. Unaweza kuona watu wanaomba kumbe wanaigiza ili waonekane kuwa nao wanaomba. Kadhalika na usikiaji wa neno la Mungu. Mtu ambaye ni makini situ kwamba atakwenda kanisani/katika mkutano wa injili/ kongamano na biblia bali pia na notebook. Imetupasa kuacha maigizo kwa kuwa tunakwenda kwenye ibada ili kuonekana na sio kukutana na Mungu.
Mungu alimwambia Samweli kuwa Yeye anaangalia moyo na si mwonekano wa nje wa mtu 1Sam 16:7. Hivyo kama tunapenda kutembea na Bwana ndio mfumo anaoutaka na sio vinginevyo. Katika safari ya kwenda mbinguni utayari ni jambo la msingi kwani wanaokwenda mbinguni ni lazima wadhamirie. Ukisoma 2 Nya 7:14 anasema, " Ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu.... Mungu anataka ujue kuwa mbingu si ya kila mtu bali ya wale waliotayari kuwa huko. Na kwa sababu hii anatutahadharisha sana sisi kuwa tusiwe na maisha ya maigizo bali tuwe na dhamira njema.
Mwenye dhamira njema haambiwi soma neno la Mungu kila siku au omba. Bali huwa na ratiba maalum kuhakikisha anatimiza hayo bila kuambiwa na mtu. Mtu wa aina hii ndio mwenye dhamira njema lakini pia bado haitoshi mwishowe aonganishe anachojifunza katika maisha halisia ili apate kukiishi. Sababu za kukuambia haya ni kuwa unakuta kanisani ni mwanakwaya, mzee wa kanisa, mhudumu au mtumishi lakini maisha yake hayafanani na huduma anayofanya. Jiengue mwenyewe kwenye kitanzi hiki. Na hata ukiwa umefanikiwa usijionyeshe fanya mambo yako kwa siri Mungu aliye sirini atakujazi.
Sina maana ya kukurudisha nyuma ila nina maana ya kukusaidia uwe na uhakika wa kwenda mbinguni. Kwa kuwa wapo wakristo ambao kwa staili ya maisha yao mbingu inaweza kuwa ndoto kwao. Maana wanafikiri wanafanya sawasawa lakini kumbe wanaigiza. Mpendwa jitahidi kuepuka hili nawe utaishi kwa uhakika na sio vinginevyo.
Barikiwa sana                                                                                                                                        Na Henry Nicholaus

MUNGU ANAWEZA KUBADILI MAISHA YAKO NA KUYAFANYA KUWA MAZURI
Tunaposoma Mwanzo 1:2-3 inasema, "Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.
Tunaona uwezo wa Mungu katika kubadilisha vinyonge kuvipa nguvu na vidhaifu kuvipa uthamani. Watu wengi wamekuwa wakisita sita kumpa Mungu nafasi ya kwanza katika maisha yao kwa kutazama ukubwa wa tatizo walilonalo au shida. Wakati Mungu anaumba dunia biblia inatueleza kuwa nchi ilikuwa ukiwa na tena utupu. Lakini mara baada ya kutafakari uumbaji utakuwaje. Mungu akaamuru nuru itokee.
Kwa jambo hili ni uthibitisho tosha kama Mungu aliweza kuitoa nuru katika visivyo vya thamani ina maana kuwa pale utakapompa maisha yako hutakuwa kama ulivyo kuwa pale kwanza. Na ndio maana Yer 29:11 inatuambia kuwa Mungu anatuwazia mema kutupa tumaini siku zetu za mwisho. Ina maana kile alichonacho Mungu juu yako ni uhakika lakini ridhaa ya kukichukua kutoka kwake iko kwako.
Kiwango cha maisha unayoyataka katika maisha yako kipo mikoni mwa Mungu ila kama utafanya maamuzi ya kuyataka hayo maisha hatasita kukupa. Una matatizo mpe Mungu atayabadilisha. Biblia inasema kuwa tumtwike Yesu fadhaa zetu maana yeye hushughulika navyo. Wanadamu sio suluhisho la matatizo yako hivyo usiwategemee wao bali mtegemee Mungu maana anaweza kukusaidia toka kwenye hali yeyote ile kwani yeye si mbaguzi ila ni Baba wa wote.
Usipendwe kupitwa na nafasi hii, Mungu aliotoa kwa wote wamwaminio. Tumia kila fursa ilioko kwa Mungu ikikumbuka kuwa alikufanya kuwa mwana Yn 1:11-12. Ni rai yangu kwako kuwa kwa Yesu kuna raha na faida changamkia fursa.
Barikiwa sana                                                                                                                                        Na Henry Nicholaus

NIA YA MOYO
Mungu anatazama sana nia ya moyo katika maisha ya mwanadamu kwa kuwa sababu ya kutuumba ni ili aweze kushirikisha pendo lake kwetu. Tunaposoma Yn 4:23-24 inasema, "Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambao wamuabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye watamwabudu katika roho na kweli."
Utaona wewe mwenyewe kuwa msukumo aliokuwa nao Mungu ni kuwa na shirika na watu. Mungu anataka watu waende kanisani kumwabudu yeye na sio kwa kigezo cha kutafuta uponyaji. Wengi wanahudhuria mikutano ya injili kwa sababu ya shida walizonazo na sio kwa sababu ya kutaka kusikia neno la Mungu ili waweze kuimarisha uhusiano wao na Mungu. Watu wengi wamejisahau sana. Wanawaza sana mambo ya mwilini kuliko hata mambo ya baadae. Unakuta mtu yuko tayari kukosa ibada lakini asikose kazini hii ina maana kuwa wengi wapo kimaslai zaidi kuliko kumpenda Mungu.
Tunapozungumza habari za kumpenda Mungu ni muhimu ukajua kuwa Mungu anataka udhamirie toka moyoni na sio mdomoni. Ndio maana Yesu aliwaambia watu maneno haya, "Watu hawa huniabudu kwa midomo yao lakini mioyo yao iko mbali nami." Yesu alitaka watu wajue kuwa swala la kumpenda Mungu si swala la maonyesho bali ni swala la dhamira au nia.
Anania na Safira walikuwa ni mfano mzuri wa jambo hili. Wao walikuwa na kiwanja wakadhamiria kuwa kiwe sadaka. Lakini walipokiuza wakaona walipata pesa nyingi wakaamua kupunguza baadhi ya fedha hizo wakifikiri wanamdanganya Petro kwa kuwa alikuwa mwanadamu wasijue swala la sadaka ni swala la kujiunganisha na Mungu wa mtumishi ambaye haangalii kiwango cha sadaka bali nia ya mtoaji. Mdo 5:1-11
Mungu hataki umpende kwa kuwa atakuponya bali anataka umpende kwa kuwa u rafiki yake. Mungu anachotaka kwetu ni ushirika na sio ubabaishaji. Huwezi kusema unampenda Mungu halafu hutaki kujitoa katika kanisa huo ni unafiki mkubwa na ndio kitu Mungu asichokipenda. Jifunze kujiunganisha na Mungu kama rafiki yako. Maana licha ya kutenda kwetu dhambi lakini bado alimtuma Yesu atusaidie huu ni upendo usio na sababu.
Yatupasa tujifunze kuwa na nia ya dhati toka mioyoni mwetu katika kumpenda Bwana. Kwa kuwa Mungu huangalia moyo na sio sura ya nje. Ni muhimu tukatambua haya kuliko kuigiza halafu mbingu ikawa historia kwetu. Tuzingatie haya kwa kuwa usiku umekwenda asubuhi yakaribia kupambazuka.
Barikiwa sana                                                                                                                                        Na Henry Nicholaus

JIFUNZE KUWA NA VIPAUMBELE SAHIHI KWA WAKATI NA MAJIRA HUSIKA
Neno la Bwana katika kitabu cha Hagai 1:1-5 inatueleza kuwa tunatakiwa kuwa na vipaumbele katika maisha yetu. Mungu alikuwa anawauliza watu wa wakati huo kuwa ni haki kwao kuishi katika nyumba yenye mapambo ya mbao hali nyumba yake imebaki katika hali ya kuharibika? Ni kweli watu wa kipindi kile hawakuwa na vipaumbele sahihi kwa wakati sahihi. Si mpango wa Mungu kuona watu wakiishi kwenye nyumba mbaya lakini anataka watu wake waishi kwenye nyumba nzuri hali ya kwake nayo ikiwa kwenye hali nzuri pia.
Ukiangalia kwa makini jambo analolieleza Mungu kwa watu wa wakati huo halina tofauti na wakati tulionao. Kwa kuwa unakuta watu wana nyumba nzuri lakini hawataki kuwajibika katika kukuifanya ya Bwana kuwa nzuri pia. Nilikuwa sehemu fulani waliokuwa na ujenzi wa kanisa usioisha kwa zaidi ya miaka 10, nikawauliza, hakuna mtu aliyejengewa nyumba kila mtu alijenga kwa fedha zake binafsi iweje leo ya Bwana waifanye kwa muda wa miaka mingi kiasi hicho? Hawakuwa na ya kujibu. Alichozungumza Mungu amechukua swala la ujenzi wa kanisa kama mfano.
Lakini yapo mambo mengi mno ambayo katika aisha yetu tunashindwa kuyapa kipaumbele stahiki na kuishia kutoa vipaumbele kwa vitu visivyofaa. Kwa mfano mtu anajua kuwa ni wakati wa ibada lakini unakuta mtu anakwenda katika shughuli zake kama ni mwanafunzi kusoma na kama ni mzazi kazini. Hii ni jambo baya sana kwa kuwa watu wengi hawana kipaumbele katika mambo ya Mungu isipokuwa yale yenye faida binafsi.
Kama wanadamu hatuwezi kufanya kila kitu ndio maana Mungu yupo. Ifike wakati ujue mipaka yako kama mwanadamu. Yer 17:5 inatuambia kuwa amelaaniwa mtu ategemeaye akili zake au mwanadamu. Hatuishi kwa uwezo wetu ila kwa sababu ya Mungu. Hivyo mambo tunayofanya yanatakiwa kumpa kipaumbele Mungu kwa kuwa ametuheshimu na kutupenda hivyo tusiitumie neema vibaya kwani itakuwa shubiri. Hata katika mambo ya kawaida jifunze kutoa kipaumbele katika yale yalio na maana. Acha mambo yasiyo na msingi pembeni toa nafasi kwa yale yalio na msingi.
Athari za kutozingatia vipaumbele sahihi na kwa wakati sahihi Hag 1:6-7, Kumb 28:24-25. Katika Hagai Mungu anajaribu kueleza kuwa kutokuwa na vipaumbele sahihi kunasababisha watu kupanda na kuvuna kiduchu, kupata mshahara na kuingia katika mifuko iliotoboka. Kama umewahi kuona kuna watu wakipata mshahara wanakimbilia bar, matatizo yanaongezeka au wanatafuta wake wa dharura. Ukiona mtu wa aina hiyo uwe na uhakika wa uadilifu/nidhamu yake ya kuweka vipaumbele kwa wakati stahiki.
Nataka ndugu msomaji unielewe kuwa Mungu anataka ubadili maisha yako ungali ukiwa duniani kwa kuwa mbinguni hakuna tution yeyote ya neno la Mungu isipokuwa duniani. Pia ni mpango wake kukuwezesha ufanikiwe kimaisha. Anaposema anajua anayokuazia unaweza kuyaona kwa kiuhalisia kama utaweza kujua na kuliingiza kazini hili analokueleza leo.
Barikiwa sana                                                                                                                                        Na Henry Nicholaus

ONGEZA UWEZO WAKO WA KUPOKEA ILI UPATE VINGI
Mara nyingi watu wengi wamekuwa walalamikaji kuwa wana matatizo ya uchumi huku wakiacha kutafuta muarubaini wa matatizo yao. Kuna wakati Mungu alikuwa akinifundisha kuwa mafanikio ili yaje yanahitaji mbinu. Na ndio maana hata wasioomba bado wanafanikiwa kwa kuwa wanatumia mbinu hata kama hawaamini Mungu kwa kuwa dawa ya kufanikiwa ni mbinu tu.
Sasa Mungu amekuwa akipenda kuona situ tunaingia mbinguni bali pia katika uwepo wetu hapa duniani unakuwa wenye mafanikio. Yaani tusiishi maisha ya shida na taabu. Ndio maana ameleta Somo hili. Tunaposoma Isa 54:2 unasema, "Panua mahali pa hema yako, na wayatandaze mapazia ya maskani yako; usiwakataze; ongeza urefu wa kamba zako; vikaze vigingi vya hema yako."
Kwa hiyo utaona kuwa Mungu anasema kuwa shida si Yeye bali ni sisi. Hivyo ametushauri tuongeze uwezo wetu wa kupokea kwa kuwa yupo tayari kutupatia vitu vingi. Kwa mfano mimi nina shamba la maembe halafu umekuja kuniomba maembe na mfuko mmoja mdogo wa maembe, maana yake unaniambia nipe yale tu yanayotosha mfuko huu. Lakini ungekuja na safleti ningekuwekea ya uwezo wa safleti, kwa kuwa umekuja na mfuko mdogo wa huwezi kunilaumu kuwa nimekupa maembe machache hali uwezo wako wa kupokea ni mdogo.
Hii imetokea mara nyingi huwa watu hupenda kulaumu kuwa maisha magumu hali ana duka moja tu kwa miaka kadhaa. Badala aongeze jingine kabaki kulamika. Unakuta mtu ana duka moja, kiwango cha sarafu kimeshuka na mfumuko wa bei umeongezeka. Kwa hiyo kama ni ulikuwa unapata 40,000 kwa siku mwaka jana mwaka huu utapata hiyo hiyo lakini itakuwa chini kuliko ya mwaka jana hata kama ikiongezeka kidogo.
Mpendwa usitafute maombi ya kufanikiwa acha fikra potofu. Tafuta namna ya kujua mbinu mbalimbali katika mafanikio. Hii inafanya China iwe tishio kwa Marekani kwa kuwa wao walitafuta mbinu ya kuwa na uchumi mkubwa. Ukitaka kufaulu tafuta mbinu ya kufaulu, ukitaka kufanikiwa kibiashara tafuta mbinu za kibiasha kwa kuwa apandae haba huvuna haba na apandae kwa ukarimu huvuna kwa ukarimu.
Swala la kufanikiwa ama kutokufanikiwa liko mikononi mwako na sio kwa mtu yeyeto. Usimtafute mchawi wa mafanikio yako kwa kuwa huwezi kumwona kwa kuwa ni wewe na ni vigumu mtu kujitafuta maana hatajiona hata kuingia kaburini. Ewe mwanafunzi, mfanyabiasha, mfanyakazi, mjasiriamali ongeza panua mahali pa hema yako.
Barikiwa sana
Na Henry Nicholaus

KWA NINI TUNAFANYA MAOMBI YA TOBA
Kwa haraka haraka ukimuuliza mtu kwa nini unafanya maombi ya toba atakujibu kuwa ni kwa sababu ya dhambi. Si jibu baya na yuko sawasawa lakini katika sehemu ujumbe huu Mungu anataka tujue kikamilifu kuwa, kuna nini zaidi ya hicho. Au kwa maneno rahisi ni kwamba anataka tujue kwa undani juu ya maombi ya utoba, ili mtu anapofanya asifanye kimzaa au pasipo imani.
"Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika." Mw 2:16-17
Ukitazama hiki kifungu utaona katika bustani ya Edeni kulikuwa na sheria iliokuwa inaratibu maisha ya Adamu pale bustanini na sheria hiyo inaitwa, ''sheria ya uzima wa milele" katika Kristo Yesu. Na hii sheria ndio iliokuwa ikimpa mtu kumiliki dunia na vitu vyake Mw 1:28. Lakini pale anguko kuu la mwanadamu lilipotokea aliamua kufuata sheria nyingine ilioasisiwa na shetani iitwayo "sheria ya dhambi na mauti". Na sheria hii ilimfanya mtu kurasimisha umiliki wake kwa sheria mpya ambayo aliichagua Ufu 12:7.
Na kwa sababu hiyo mtu asingeweza kukaa katika bustani ya Edeni hali anatii sheria nyingine. Ndio maana Mungu alimwondoa mwanadamu na kumwamuru aishi katika mazingira ya sheria mpya. Kama ilivyofanika kwa muasisi wake rejea Ufu 12:7.
Hivyo basi  ili mtu aweze kuishi maisha ya mbinguni akiwa duniani ni lazima aivunje sheria ya dhambi na mauti kisha aikubali sheria ya uzima wa milele katika Kristo Yesu. Na ili aweze kuikana ile sheria ya dhambi na mauti, Mungu aliweka utaratibu ambao ndio toba ila ifanyikayo katika damu ya Yesu Mt 26:28. Kwa hiyo tunafanya toba ili kujiondoa katika sheria ya dhambi na mauti na kisha kuingia katika sheria ya uzima wa milele katika Kristo Yesu.
Kumbuka kuwa kila alioikataa sheria ya uzima wa milele katika Kristo Yesu ameikataa na mbingu pia kwa kuwa mbingu huendeshwa katika staili ya sheria hiyo. Hivyo mpendwa unapofanya maombi ya toba si maombi ya mchezo bali ni maombi muhimu katika maisha yetu. Na ndio maana tunaanza nayo mwanzo mwa maombi ili hata tupate kibali cha kusikiwa na Mungu.
Barikiwa sana                                                                                                                                         Na Henry Nicholaus

KUPAMBANA HADI KUPATA USHINDI
Na Askofu Rodrick Mbwambo
Utangulizi:
Moja wapo ya maonyo yaliyotolewa na Yesu kwa wanafunzi wake wakati alipokuwa pamoja nao, ni onyo juu ya kutokukata tamaa. Yesu alisema hivyo kwa kutumia mfano wa hitaji la mwanamke maskini lililokuwa likishughulikiwa na kadhi dhalimu. Kila mara mama huyo alipolipeleka hitaji lake, kadhi huyo alionyesha kutokuwa tayari kulishughulikia. Hata hivyo pamoja na ugumu wa moyo wa kadhi huyu, bado aliendelea kumgongea yule kadhi, hadi pale alipopewa haki yake. Luka 18:2-5. Kwa kuwa kukata tamaa ni moja ya mambo yanayowazuia watoto wa Mungu kuvifikia vilele vya mapenzi ya Mungu katika maisha yao, uko umuhimu mkubwa kwa watoto wa Mungu kuelewa jinsi ya kupambana vinavyoinuka mbele zao, hadi pale ushindi unapopatikana.
Moja ya picha za watu waliopambana na hatimaye wakapata ushindi katika maisha yao, ni yule mwanamke aliyekuwa akitokwa na damu katika Israeli, kwa miaka kumi na mbili. Katika kuteseka kwake, mwanamke huyu alipambana na magumu mengi, ila kamwe hakukata tamaa. Adui alimzingira pande zote, ila alipambana hadi pale alipokutana na mapenzi ya Mungu katika maisha yake. Mambo yaliyomwezesha kupenya na kupata ushindi, yanayoweza kukusaidia hata wewe, ni pamoja na haya yafuatayo:-
KUWA NA UTAYARI WA KUPAMBANA
“Na mwanamke mwenye kutokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, alikuwepo katikati ya mkusanyiko uliomfuata Yesu.” Marko 5:25
Kila mara wakati wa kuuendea mji wa mafanikio, viko vikwazo vitakavyoinuka ili kumzuia mwamini kukutana na yale yaliyokusudiwa na Mungu kuwepo katika barabara ya maisha yake. Mwamini atakutana na ushindi katika maisha yake, pale tu atakapoamua kupambana na vikwazo hivyo na kuvishinda. Kile ninachotaka ukione hapa ni kuwa, mafanikio yoyote yatakayomjia mtu katika maisha yake, kwa sehemu yanategemea maamuzi anayoyafanya katika maisha yake ya kila siku na aina ya maamuzi hayo. Kama maamuzi yatakuwa mabaya, maisha yake yatadidimia badala ya kwenda juu.
Hivi ndivyo ilivyotokea kwa mwanamke huyu, usugu wa tatizo lake ulitengeneza vikwazo kadha wa kadha vilivyotakiwa kuvukwa kabla ya ushindi kupatikana. Ukiiangalia hali ya mwanamke huyu muda mfupi kabla ya kumwendea Yesu, unaweza kukubaliana nami kuwa, alikuwa na kila sababu ya kutoendelea na safari yake ya kutafuta uponyaji. Hata hivyo ingawa vikwazo vilionekana kuwa vikubwa kuliko uwezo wake wa kupambana navyo, yeye aliamua kupambana navyo. Kama tunahitaji kuuona ushindi katika maisha yetu ya kiroho au yale ya kimwili, ni lazima tuanze na mhimili huu wa kufanya uamuzi mzuri.
Vikwazo ambavyo mwanamke huyu aliamua kupambana navyo, ni pamoja na hivi vifuatavyo:-
KUPAMBANA NA VIKWAZO VYA KIDINI
“Na mwanamke kama akitokwa na damu yake siku nyingi, nayo ni katika majira ya kutengwa kwake, au kama anatokwa na damu kuzidi majira ya kutengwa kwake; siku hizo zote za kutokwa na damu ya unajisi wake, atakuwa kama alivyokuwa katika siku za kutengwa kwake; yeye ni najisi. Kila kitanda akilaliacho katika siku zote za kutoka damu, kitakuwa kama kitanda cha kutengwa kwake; na kila kitu atakachokilalia kitakuwa najisi, kama unajisi wa kutengwa kwake. Na mtu yeyote atakayevigusa vitu vile atakuwa najisi, naye atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni.” Lawi 15:25-27
Mara nyingi katika maisha tunaweza kugundua kuwa vikwazo vinavyoongoza katika kuwazuia watu kukutana na mapenzi ya Mungu, ni vikwazo vinavyotokana na dini. Jimmy Swagart wakati fulani katika mahubiri yake alitamka kuwa, umati mkubwa wa watu watakaoingia Jehanamu, utaenda huko kutokana na vikwazo vya kidini na kitamaduni. Hivi ndivyo ilivyotukia kwa mwanamke huyu, baada ya tatizo lake kugeuka kuwa sugu, alikutana na kikwazo cha kidini kilichohitaji kuvukwa kabla ya muujiza kutokea. Mwanamke huyu kama mwenyeji wa Mashariki ya kati na mwamini wa dini ya Kiyahudi, alijikuta katika karantini iliyotokana na andiko letu hapo juu la kutochangamana na watu kutokana na ugonjwa aliokuwa nao wa kutokwa na damu.
Mwanamke huyu angelisikia habari ya matendo makuu yaliyokuwa yakitendeka katika misafara ya Yesu ila kikwazo hiki cha kidini kilimwambia,”huruhusiwi kwenda!” Hiki ndicho kinachowatokea watu wengi katika miaka tuliyo nayo. Wanawaona wengine wakiokolewa na kupokea baraka mbalimbali za kiroho na kimwili, ila wao wanaishia kusema, “KWETU hatuokoki, hatuneni kwa lugha, hatuombei wagonjwa, na kadhalika.” Ili ukutane na mapenzi ya Mungu katika maisha yako, cha msingi ni kile kinachozungumzwa katika biblia na wala sio taratibu zinazopatikana katika tamaduni za mahali au dini. Hivi ndivyo mwanamke huyu alivyofanya, dini na utamaduni vilimwekea mipaka ila yeye akaweka juhudi za makusudi kukivuka kikwazo hiki.
KUPAMBANA NA KUTOKUWA NA NGUVU KIFEDHA
“Amegharimiwa vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya.” Marko 5:26
Kikwazo cha pili kilichomkabili mwanamke huyu katika kuuendea muujiza wake, kilikuwa ni kikwazo cha kutokuwa na nguvu kifedha. Ingawa huduma zilizokuwa zikitolewa na Yesu zilikuwa ni bure, bado kulikuwa na gharama ambazo wahitaji walipaswa kuzigharimia. Kwa mfano, kama mhitaji alikuwa mbali na eneo alipokuwa Yesu, ilimbidi yeye, ndugu au rafiki zake kugharimia zoezi la kumpeleka kule Yesu alipokuwa. Uhalisi wa ukweli huu, tunauona katika mojawapo ya huduma za Yesu, alizozifanya katika mji wa Kapernaumu. Baada ya habari za ujio wake kuenea kila mahali, kalamu ya Marko ilikuwa na haya ya kuandika. “Wakakusanyika watu wengi, isibaki nafasi hata mlangoni; akawa akisema nao neno lake. Wakaja watu wakimleta mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne.” Marko 2:1-2.
Kutokana na andiko hili, unaweza kuona kuwa, kulikuwa na gharama zilizotakiwa kulipwa ili kumfikisha mhitaji pale Masihi wa Mungu alipokuwa. Mbali na kugharimia usafiri, wakati mwingine kulikuwa kulipia gharama za chakula na malazi wakati wa kushiriki huduma zilizokuwa zikitolewa na Yesu. Marko akielezea mojawapo ya gharama hizi, aliandika yafuatayo:- “hata zilipopita saa nyingi za mchana, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa ni nyika tupu, na sasa kunakuchwa; uwaage watu hawa, ili waende zao mashambani na vijijini kando kando, wakajinunulie chakula.” Marko 6: 35-36. Kupitia mifano hii miwili, tunaweza kuona kuwa, ingawa Yesu aliwahudumia watu bure, bado kulikuwa na gharama za kibinafsi, zilizotakiwa kubewa na mhitaji. Kutokana na gharama hizi zilizotakiwa kubebwa na mhitaji, ni wazi zilitengeneza kikwazo kingine kwa mwanamke huyu aliyekuwa katika hitaji la kukutana na muujiza wake. Alitambua mahali ulipo muujiza wake, ila hali ya uchumi wake ilimwambia, huwezi kwenda huko.
Kutokuwa na nguvu za kifedha, kumewazuia watoto wengi wa Mungu kupanda ngazi za kiroho na kimwili zilizowekwa na Mungu mbele ya maisha yao. Roho Mtakatifu anaweza kuweka maono au dukuduku fulani ndani ya mtu, ila badala ya mtu huyo kuanza kuzitendea kazi dukuduku hizo, utamsikia akisema, “Sina pesa!” Waamini hawa wanashindwa kuelewa kuwa, katika mazingira ya kawaida, Mungu anapomtaka mtoto wake afanye kitu fulani kinachohitaji nguvu ya pesa, huwa haanzi kwa kumpatia mtu huyo pesa. Mungu huweka maono ndani ya mtu, na mhusika anatakiwa kuwa na utayari utakaoigeuza sifuri kuwa tarakimu iliyo na thamani. Katika hili mwamini anatakiwa akumbuke kuwa, hata ulimwengu tulio nao, ulitokana na vitu visivyoonekana.
Tukirudi katika habari inayomhusu huyu mwanamke aliyekuwa na tatizo la kutokwa na damu, tunaona kuwa alikuwa anataka kufanya mradi wa kutafuta uponyaji, ila nguvu yake ya kiuchumi ilikuwa sifuri. Ingawa hali yake ya kifedha ilikuwa mbaya kiasi hicho, bado hakukiruhusu kikwazo hicho kimzuie kufanya mradi aliokusudia kuufanya. Badala yake, aliamua kufanya yale yaliyokuwa katika uwezo wake ili kufika pale muujiza wake ulipokuwa. Ni baada ya kukishinda kikwazo hiki, ndipo alipofaulu kuwa miongoni mwa umati uliokuwa ukimfuata Yesu.
Kama unahitaji kutumiwa na Mungu na kuishi kama alivyokukusudia uishi, ni lazima uhakikishe kuwa, unakishinda kikwazo hiki kinachotokana na kutokuwa na nguvu za kifedha. Kile unachotakiwa kuanza nacho katika kupambana na kikwazo hiki, ni kujitamkia kuwa, “Pamoja na kutokuwa na nguvu za kiuchumi, hakuna kitakachonizuia kuishi maisha niliyokusudiwa na Mungu, niyaishi.”
KUPAMBANA NA MADHAIFU YA KIMWILI
“…amegharimiwa vitu vyote alivyo nayo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake, ilizidi kuwa mbaya.” Marko 5:26
Udhaifu wa kimwili ni kikwazo kingine kinachotumiwa na Shetani, kuwafanya waamini waishi maisha yanayotofautiana na vile Mungu alivyowakusudia waishi. Katika miaka tuliyo nayo, watu wengi wamemruhusu Ibilisi kutumia udhaifu wa kimwili walio nao, kuwatenganisha na mapenzi ya Mungu katika maisha yao. Kuwa na udhaifu fulani katika mwili, kamwe hakutakiwi kuwa kigezo cha kumfanya mwamini asipige hatua kwenda mbele.
Katika hili nina mfano ulio wazi wa mtu, aliyemkatalia shetani kuutumia udhaifu wa mwili wake kumtenganisha na kusudi la Mungu katika maisha yake. Mtu huyu alizaliwa bila mikono na miguu, ila bado anaweza kucheza mpira kwa kutumia kichwa, anaweza kuogelea, pamoja na amefanikiwa kupata ujuzi unaompatia riziki yake ya kila siku. Hivi ndivyo ilivyotukia kwa mwanamke huyu aliyekuwa katika harakati za kukutana na muujiza wake, ingawa ugonjwa ulimfanya kuwa nusu mfu, bado alifanikiwa kupenyeza katikati ya umati mkubwa wa watu na kugusa vazi la Yesu.
Ni kweli udhaifu wa mwili, unaweza kumzuia mtu kuwa na kasi ya mtu asiye na tatizo katika mwili wake, ila hauwezi kumzuia kwenda kwa kasi iliyoandaliwa na Mungu kwa ajili yake. Katika hili, ninaamini kuwa, ‘Mungu ameandaa vilele vya baraka kwa kila mtu na umbali wa kuvifikia vilele hivyo, unategemea vile uwezo wa mtu ulivyo.’ Kama unataka bendera ya maisha yako ya kiroho na kimwili ipepee, fanya kile kilichofanywa na mwanamke huyu. Yeye aliuangalia udhaifu aliokuwa nao kimwili na kusema, “Muda wote Yesu aishipo, bado lingaliko tumaini.”
KUPAMBANA KIKWAZO CHA UPWEKE
“Na mwanamke kama akitokwa na damu yake siku nyingi, nayo ni katika majira ya kutengwa kwake, au kama anatokwa na damu kuzidi majira ya kutengwa kwake; siku hizo zote za kutokwa na damu ya unajisi wake, atakuwa kama alivyokuwa katika siku za kutengwa kwake; yeye ni najisi. Kila kitanda akilaliacho katika siku zote za kutoka damu, kitakuwa kama kitanda cha kutengwa kwake; na kila kitu atakachokilalia kitakuwa najisi, kama unajisi wa kutengwa kwake. Na mtu yeyote atakayevigusa vitu vile atakuwa najisi, naye atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni.” Lawi 15:25-27
Mara zote tatizo la mtu linapokuwa sugu, huwa ni rahisi mno kwake kukumbwa na roho ya upweke. Kwa mfano, kulingana na sheria ya Musa, mtu aliyekuwa na ugonjwa wa kutokwa na damu muda mrefu, huyo hakuruhusiwa kuchangamana na watu wengine waliokuwa wazima. Kwa maneno mengine, ugonjwa uliomkabili mwanamke huyu, ulimweka katika kifungo kibaya mno cha upweke. Mfano mwingine unaoonyesha vile matatizo sugu yanavyotengeneza upweke kwa mtu, tunaupata katika andiko lifuatalo; “Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima? Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani..” Yohana 5:6-7.
Kutokana na upweke huu unaozaliwa pale tatizo la mtu linapokuwa sugu, waamini wengi wameshindwa kumzalia Bwana matunda. Kama hili halitoshi, waamini wengi wachanga wamerudi nyuma kiroho, kutokana na roho hii ya upweke. Hata waamini wengi wachanga wanashindwa kuendelea na maisha ya wokovu, kutokana na upweke. Wako pia kinamama waliofikia hatua ya kujinyonga baada ya kufiwa na waume zao pale waliposhindwa kupambana na roho hii ya upweke. Roho ya upweke iko kwa baadhi ya vijana waliopoteza wachumba wao, kwa ushirika uliopoteza mchungaji wake, mume aliyepoteza mke wake na kwa wanafunzi walio mbali na wazazi wao. Pamoja na kikwazo hiki cha upweke, ushindi uko katika kupambana nacho hadi kukishinda.
Hivi ndivyo alivyofanya mwanamke huyu, tunayejifunza kupitia maisha yake katika injili ya Marko. Ukiangalia mazingira yatatizo lake kama yanavyoonekana katika andiko letu hapo juu, unaweza kuona kuwa, ni mwanamke aliyekuwa katika upweke usiopimika kwa mizani wala kwa shubiri. Kama tulivyoona katika vipengele vilivyopita, utamaduni na dini yake vilikuwa havimruhusu kuchangamana na watu, pili, alimwendea Yesu Kristo bila kuwa na mtu wa kumsindikiza. Ingawa alikosa mtu wa kumshika mkono wala kumtia moyo, yeye hakukubali hali hii imkatishe tamaa. Mwanamke huyu aliitumia imani yake kama mkongojo na kusema, “kwa ‘mkongojo’ huu, nitakutana na mapenzi ya Mungu katika maisha yangu.”
Ndugu yangu, kama unakabiliwa na tatizo sugu, na tatizo hilo limekufanya uwe mpweke, napenda kukutia moyo kuwa, kwa msaada wa Mungu, unaweza kuushinda upweke unaokukabili. Jambo la kwanza ushindi utakujia kwa kutambua kuwa, upweke ni moja ya silaha zinazotumiwa na Ibilisi kuwazuia watoto wa Mungu kula mema ya nchi. Ukiujua ukweli huu, utapambana na kikwazo hiki, badala ya kukaa mkao wa kulegea kana kwamba huna la kufanya. Ukweli wa tatu unaotakiwa kuutambua ni kuwa, mara zote upweke kwa watoto wa Mungu sio kitu kilicho halisi. Kamwe haitatokea mtu aliyeokoka na kuishi sawasawa na mapenzi ya Mungu, kuwa katika hali ya upweke. Hili nalisema kutokana na sababu kubwa mbili. Sababu ya kwanza, Mungu katika neno lake, tayari ameshatamka kuwa, “Yuko pamoja nasi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.” Mathayo 28:20. Pili, sambamba na Mungu kuwa pamoja na mwamini nyakati zote, mwamini ni sehemu ya familia ya Mungu.
Familia hii iko katika makundi makubwa mawili. Kwanza, ni ile familia ya waamini wanaoishi katika eneo moja la kijiografia naye, inayojulikana kama kanisa la Mungu la mahali (local church). Kundi la pili, ni la waamini wanaoishi katika maeneo mengine ya kijiografia yaliyo mbali na mwamini, wanaojulikana kama kanisa la Kristo la kiulimwengu (universal church). Kwa vile waamini wote ni viungo vya mwili wa Kristo, ni uongo pale Shetani anapompandikizia mwamini roho ya upweke na kumtaka kuuamini uongo huo. Katika hali zote mwamini anatakiwa atambue kuwa, wako waamini wanaomjua na wasiomjua wanaomwombea kwa mzigo. Kupitia ufahamu na ukweli huu, ukatae uongo huu wa Shetani na utamke kwa ujasiri kuwa, kama mwanamke huyu ambaye hakuwa mwamini aliweza kuushinda upweke na kupokea muujiza wake, mimi kama mtoto wa Mungu, nitashinda pia kile kinachoonekana kuwa upweke katika maisha yangu.
KUPAMBANA NA VIZUIZI VINAVYOLETWA NA WATU
“Na mwanamke mwenye kutokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, alikuwepo katikati ya mkusanyiko uliomfuata Yesu.” Marko 5:25 Kikwazo kingine kilichomkabili mwanamke huyu, ni umati mkubwa uliokuwa umemzunguka Yesu, katika safari yake ya kwenda kumponya binti Yairo. Kupitia miujiza miwili iliyofanywa na Yesu ya kuwalisha watu, yawezekana kwa uchache umati uliokuwa ukimfuata Yesu, ulikuwa haupungui watu 10,000. Kutokana na umati huu, ilikuwa ni vigumu mno kwa wagonjwa waliozidiwa kumfikia Yesu na kukutana naye uso kwa uso. Wakati mwingine ilimbidi mhitaji au ndugu zake watumie nguvu za ziada, ili kuifikia mikono ya Yesu. Mfano mzuri katika hili, ni ule unaomhusu mwenye kupooza, aliyepelekwa kwa Yesu na watu wanne katika injili ya Marko. Kutokana na umati uliokuwa unamsonga Yesu, iliwabidi wale waliomchukua wavunje dari ili wapate nafasi ya kumtelemsha mgonjwa wao pale Bwana wa uponyaji alipokuwa. Marko 2:4.
Mfano wa pili, ni huu wa huyu mwanamke aliyekuwa akitokwa na damu kwa miaka 12 mfululuzo. Kutokana na udhaifu katika mwili wake, ni wazi ilikuwa vigumu mno kwake kupenya katikati ya umati wa watu, hadi kufika pale Yesu alipokuwa. Kitu cha kutia moyo ni kuwa, pamoja na ugumu huu, bado aliweza kupenya na kushika vazi la Yesu. Tunachojifunza katika mifano hii miwili ni kuwa, watu wanaweza kumsaidia mwamini kupata ushindi, na wakati mwingine wanaweza kuwa kikwazo cha kumzuia mtu kukutana muujiza wake. Kwa mfano, mwenye kupooza katika mlango wa kondoo katika injili ya Yohana, alishindwa kufunguliwa mapema, kutokana na kukosa mtu wa kumwingiza birikani. Yohana 5:2-7. Tukija kwa Bartimayo yule kipofu, mambo yalikuwa kinyume, yeye watu ndio waliojaribu kuuzuia muujiza wake!
Kwa yeyote yule anayetaka kupata upenyo na kumliza yule aliyekuwa akimliliza, anatakiwa afanye uamuzi wa kupambana na Shetani mpaka pale ushindi atakapopata majibu ya maswali yake. Hivi ndivyo huyu mwanamke alivyofanya, umati ulikuwa kikwazo kikubwa kwake, ila aliweka bidii ili kukishinda kikwazo hiki kwa lengo la kuutwaa muujiza wake.
KUWEKA BIDII YOTE KATIKA KUPAMBANA
“Na kuteswa mengi kwa mikono ya matabibu WENGI…” Marko 5:26
Jambo lingine lililochangia kumletea mwanamke huyu ushindi, ni ile bidii aliyokuwa nayo katika kupambana na tatizo alilokuwa nalo. Tatizo lilipompata, alihakikisha kuwa anawaendea madaktari wote aliokuwa anawafahamu, kwa lengo la kutafuta uponyaji. Tunapozama ndani katika kipengele hiki, ninataka utambue kuwa, katika ulimwengu tulio nao, kamwe hakuna mtu aliyeandikiwa na Mungu kuishi maisha mabaya. Mungu kama Muumbaji mwenye upendo, ametengeneza barabara nzuri za maisha kwa kila mtu, ila mtu mwenyewe, ndiye anayeweza kuamua kutembea ndani au nje ya barabara hiyo.
Kwa mfano, mtu anapoukataa wokovu, hamkatai tu Kristo, bali, anayakataa pia mapenzi ya Mungu katika maisha yake. Hali kadhalika, mtu aliyemwamini Kristo na hatimaye akalegea katika kupambana na vikwazo vinavoinuka katika maisha yake, huyo naye atakuwa mbali na mpango wa Mungu wa neema, ulikusudiwa kuwa katika maisha yake. Ulegevu tunaouongelea hapa, ni ule wa kutotumia NGUVU zote, MOYO wote na ROHO yote katika kumwishia na kumtumikia Mungu. Roho hii ya kufanya mambo nusu nusu, ndiyo iliyomfanya mfalme wa Israeli, ashindwe kuangamiza majeshi ya mfalme wa Shamu. Nabii alimwambia kupiga mshale chini, yeye akapiga mara tatu na kuacha. Alipoacha Elisha alimwambia maneno yafuatayo; “Ingelikupasa kupiga mara tano au mara sita; ndipo ungaliipiga Shamu hata kuiangamiza; bali sasa utaipiga Shamu mara tatu tu.” 2 Wafalme 13:19.
Tukiingia ndani ya kanisa la siku hizi za mwisho, tunaweza pia kuona kuwa roho hii ya kufanya mambo kwa kutumia nguvu kidogo, ndiyo inayoifanya idadi ya wafuasi wa imani ya Kikristo, kukaribia ile ya Waislamu wakati ambapo Uislamu, ulianza karine tano baada ya Ukristo kuanza. Kiongozi wa kanisa la mahali, anaweza kuhamasisha waamini kwenda kushuhudia, ila baadaye, utawakuta waamini hao wakirudi mikono mitupu bila mavuno. Kama atatokea wa kuuliza kulikoni, mara zote jibu linakuwa rahisi, “hatukupata mtu leo!” Hata hivyo ukiliangalia zoezi zima la huo ushuhudiaji, utagundua kuwa, waamini hao hawakutumia nguvu zao zote katika kulifanya zoezi hili. Udhaifu huu, uko pia katika maeneo ya ufuatiliaji, utoaji, uimbaji na kadhalika; ndio watu wanafanya, ila sio kwa kutumia nguvu zao zote.
Kwa mwanamke huyu tunayemzungumzia katika habari yetu, hakuridhishwa na madaktari wawili au watatu, wakati wa kutafuta muujiza wake. Yeye alitumia nguvu yote ya fedha aliyokuwa nayo, kutafuta tiba ya tatizo lake. Hata tunapoangalia Biblia, tunaona kuwa, watu waliotumiwa kwa namna ya kipekee na Mungu, ni wale walioweka bidii ya kutosha katika shughuli za kiroho na zile za kimwili. Mfano mzuri wa watu hawa, ni wanafunzi wa Yesu. Wao hawakumfuata Yesu nusu nusu, bali walimfuata kwa mioyo yao yote na kujitoa kwao ndiko kulikomfanya Petro atamke kuwa, “Sisi tumeacha vyote tukakufuata.” Marko 10:28.
Kama waamini wa siku za mwisho wanataka kuuona mkono wa Mungu, katika maisha yao ya kiroho na kimwili, ni lazima watumie bidii yao yote kutafuta mambo ya rohoni nay ale ya kimwili. Kwa maneno mengine, kama nguvu za wanadamu zingelikuwa sawa na mipira ya manati, wanatakiwa wajivute mpaka ifikie kikomo cha kuvutika kwake.
KUTOKUBALI KUKATA TAMAA
“Na kuteswa mengi kwa mikono ya matabibu wengi, amegharimiwa vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya; aliposikia habari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyumba, akaligusa vazi lake.” Marko 5:26
Kitu kingine kilichomsaidia mwanamke huyu kusonga mbele hadi kuufikia muujiza wake, ni ile roho aliyokuwa nayo ya kutokukata tamaa. Andiko letu hapo juu, linaonyesha vile kibinadamu, mwanamke huyu alivyokuwa na kila sababu ya kukata tamaa. Katika kupambana na tatizo alilokuwa nalo, alipitia waganga wengi, pochi yake ilikuwa tupu, ila kulingana na andiko letu hapo juu, bado aliendelea kutafuta waganga. Ni katika kutafuta huku, ndipo alipokutana na Mganga wa waganga, aliyeweza kumwondolea mzigo uliokuwa ukimlemea. Kama angelikata tamaa, angelibakia nyumbani na hapo angelikufa kile kifo Waswahili wanachokiita, ‘kifo cha kiofsa.’
Kuifungulia roho ya kukata tamaa, kumechangia mno kuzorotesha maendeleo ya kiroho na ya kimwili ya watoto wa Mungu. Mtu anaweza kumpokea Yesu leo na kesho tu anataka kuwa mhubiri kama Billy Graham au Reinhard Bonke. Hali kadhalika, kama ni mafanikio ya kimwili, nayo wanataka yaje mithili ya kumulika kwa radi. Yale wanayoyatarajia yasipokuja kwa wakati wanaoutaka, wanaamua ‘kuozea’ katika mkeka wa kukata tamaa. Wakati umefika kwa waamini kujifunza kutokata tamaa kutoka kwa watu maarufu kama vile Thomas Edson. Mskotishi huyu, alijaribu kutengeneza balbu za umeme zaidi ya mara 2,000 bila mafanikio na hapo, wakatokea watu wengi walimtembelea kwa lengo la kumkatisha tamaa. Hata hivyo, kama ilivyokuwa kwa Ayubu mbele za wataabishaji wake, mtu huyu alikataa kabisa kuifungulia mlango roho ya kukata tamaa na leo bulbu za umeme zimeenea dunia nzima.
Kama watoto wa Mungu wa kanisa la siku za mwisho wanataka kuishi maisha ya ushindi, wanatakiwa kukataa kwa gharama yoyote ile, roho hii ya kukata tamaa.
KUUONA USHINDI KABLA HAUJATOKEA
“Maana alisema, Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona.” Marko 5:28
Andiko hili linatuonyesha kiwango cha imani kilichokuwa ndani ya mwanamke huyu. Kama vile Yona alivyomtukuza Mungu akiwa ndani ya tumbo la samaki, ndivyo alivyofanya. Imani ya kupokea aliyokuwa nayo, ilimpelekea kuamini kuwa, pale tu atakapolishika vazi la Yesu, atapona msiba aliokuwa nao. Tunachokiona kwa mwanamke huyu ni kuwa, aliamini shuhuda zote alizozisikia kuhusiana na matendo makuu yaliyofanywa na Yesu na akazigeuza shuhuda hizo kuwa pumzi ya mapafu yake. Kwa maneno mengine, tunaweza kusema kuwa, ujazo wa shuhuda za matendo makuu ya Yesu, ulijaa ndani yake kiasi cha kutobakia nafasi ya mashaka ndani ya roho na ufahamu wake. Imani hii ya kupokea, ndiyo iliyomfanya auone ushindi dhidi ya tatizo alilokuwa nalo, hata kabla ya kukutana na Yesu.
Kama wewe ni mmoja wa wale wanaotaka kula mema ya nchi, itakulazimu, uruhusu aina hii ya imani kuumbika ndani yako. Mambo yote yaliyoletwa na Mungu duniani kupitia kwa Yesu Kristo, yanapatikana kwa imani. Kama vile milango mitano ya ufahamu inavyomwezesha mtu, kuwa na uhakika wa mambo yaliyopo katika ulimwengu wa kimwili, kwa imani mwamini anakuwa na uhakika wa kile kinachofanyika katika ulimwengu wa kiroho kuhusiana na maisha yake. Kupitia jicho la imani, Yusufu aliuona ukombozi wa wana wa Israeli kutoka Misri na kuwaagiza akisema, “Bila shaka Mungu atawajia ninyi, nanyi mtaipandisha huko mifupa yangu.” Mwanzo 50:25. AMENI!

NI KWA NINI WATU WENGI HAWAPENDI KUSIKA NENO LA MUNGU WAKATI LINATOLEWA BURE
Inawezekana hata wewe kwako ni swali ambalo umewahi kujiuliza, hata kama hukuwahi kujiuliza nitatamani ujiulize leo kwa kuwa lina msingi wake katika kujiuliza. Nilipokuwa katika maombi ya kifamilia usiku nyumbani wakati tulipokuwa tunaomba nikaona Mungu akinieleza ni kwa nini watu hawendi kusikia neno lake.
"Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga. Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani. Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba." Efe 2:14-16
Natamani urejee hapo juu kwenye hiki kifungu cha maneno ili tuelewane. Kama kulikuwa na kiambaza kilichobomolewa, uwe na uhakika kuwa kulikuwa na utengano. Maana kiambaza kinatenganisha na kuweka pande mbili. Au kwa maneno marahisi eneo lenye kiambaza maana yake kuna uadui. Sasa kama tumeelewa mpaka hapa.
Tambua kuwa uadui kati ya Mungu na mtu hauletwi na kitu kingine isipokuwa dhambi rejea Mw 3:23-24 utaona hili. Kilichomfanya Mungu amfukuze Adamu bustanini ni kwa sababu Adamu aliasi. Ina maana kuwa urafiki wao uliingia dosari. Na dosari hii ililetwa na dhambi. Kwa hiyo dhambi ndio inayotengeneza kiambaza kati ya Mungu na mtu.
Sasa basi ni vema ukajiuliza umegombana na rafiki yako, je unakuwa na nguvu ya kutumia vitu vyake? Kama mlikuwa mnalala chumba kimoja utaweza kuona mmoja anahama chumba. Na kama hata hama basi atatafuta mbinu ya kujiepushe nae. Sasa ndilo linalotokea kwa nini watu wengi hawapendi kusikia neno la Mungu japo si la kulipia. Unakuta semina au mkutano wa injili unatangazwa kwa juhudi lakini bado utaona mwitikio ni mdogo.
Si kwa sababu hawasikii tangazo ila ni ukweli usiopingika kuwa dhambi imetengeneza uadui kati yao na Mungu na kwa sababu hiyo hawapati ujasiri wa kushiri vya Mungu. Mtu atasema mbona Jumapili wanakuja. Nataka uelewe anaweza kuja Jumapili kwa sababu ya mfumo ulikuwepo. Mazingira yakamlazimisha kwa kuwa familia nzima inakuja kanisani, hivyo atakuja kwa sababu mazingira si rafiki kwake. Kama unataka kuelewa hili vizuri nenda na huyo mtu maeneo ambayo makanisa yapo mbali ataona vema bora asiende.
Sikiliza swala la kumpenda Mungu linaanzia moyoni na rohoni. Sio swala la shuruti ndio maana amri ya kwanza inasema mpende sana Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa akili yako yote na kwa nguvu zako zote. Kama mtu ana uadui na Mungu hata siku moja hawezi kupatana na Mungu kwa kuwa kiambaza kimejengeka. Hivyo hata neno la Mungu hawezi kusikia.
Hivi unaweza kusikiliza ushauri wa adui yako? Kama huwezi ndicho kinachotokea kwa mtu aliyetenda dhambi kukubali kuja kusikiliza neno la Mungu. Swali tunajisaidiaje kama tupo katika hali hii? Iko damu ya Yesu itumie kuondoa iko kiambaza  (Mt 26:28) na urafiki wako na Mungu utarejea na tena hutahitaji kusukumwa kuja kusikia neno la Mungu.
Barikiwa sana                                                                                                                                        Na Henry Nicholaus

MAMBO YANAYOATHIRI UTUMISHI WAKO WA KIROHO
Unapotazama kichwa hapo juu kuna maneno mawili ningependa niyaweke sawa ili tufuatane pamoja. Katika neno 'Yanayoathiri' tunapata neno athari. Na memo athari lina mitazamo miwili, linaweza kuwa na mitazamo mizuri au mibaya. Lakini neno utumishi kwa maana ya kawaida ni ile hali ya kutumika. Hivyo mtu yeyote anayetumika katika shamba la Bwana ni mtumishi iwe ni mwanakwaya, mzee wa kanisa au waumini wote ni watumishi. Nimeona nifafanue hili ili usije ukafikiri kuwa mtumishi anayezungumzwa ni muhubiri tu kumbe ni hata wewe uliookoka.
Tunaposoma Mdo 1:15-26 tunaona habari za mitume wakitafakari juu ya kifo cha Yuda na nani atakayekuwa mbadala wake. Lakini katika hiki kifungu cha maandiko tunajifunza kuwa kitendo cha Yuda kumsaliti Yesu kiliathiri utumishi wake wa kiroho kiasi cha kwenda kujiua. Lakini pia kuchaguliwa kwa Mathiya kama mtume kuliathiri pia utumishi wake wa kiroho. Kwa maana gani Mathiya aliye mtume hata kuwa kama Mathiya ambaye hakuwa mtume. Kwa maana hiyo basi viko viwango ambavyo Mathiya alipanda kwa kuwa mfumo wake wa kiroho ulibadilishwa na ngazi ya maisha alioipata. Mtu anapookoka viwango vyake vya kiroho haviwezi kuwa kama vya zamani. Na ndivyo ilivyotokea kwa Mathiya.
Yafuatayo ni mambo ya kuyatazama unapozungumzia hali yako ya kiroho
·         Uhusiano wako na Mungu
·         Nafasi yako na kiwango cha kutunza uwepo wa Mungu
·         Namna unavyoendelea na kukua ndani ya imani

Ili uweze kujua ni kwa kiasi gani hali yako ya kiroho ni muhimu ukatathimini hali yako kwa kutumia vigezo tajwa hapo juu. Unapotaka kujua kuwa uko wapi na unaelekea wapi kiroho hivi vigezo ni vya msingi sana vitakusaidia kufahamu ukweli halisi.
Baadhi ya mambo yanayoathiri hali yako ya kiroho
·         Kibali
Mara nyingi watu wanapopata kibali wanaweza kuongozeka kiroho au kudidimia. Mfano: Unakuta mtu alipokuwa hana kazi alikuwa akija kanisani. Lakini allipokuja kupata kazi na kanisa nalo likawa kituo cha polisi kwake. Ninao ushuhuda kabisa wa mtu mmoja kanisani kwetu. Hivyo utagundua kinachomfanya asije ni kibali alichonacho mahali pa kazi. Ukimuuliza mbona huonekani atakuambia mambo ni mengi. Sasa tujiulize yamekuwa mengi  kiasi hata cha kushindwa kutenga muda kwa ajili aliyekupa hicho kibali. Kumb 8:11-14, 9:1-4. Lakini pia natamani umtazame Suleimani namna Mungu alipomuuinua akajisahau akaamua kutumikia miungu migeni ambayo haikumpa kibali na Mungu alimwadhibu na adhabu yake imeisumbua Israeli hata leo 1Fal 10:1-10, 11:1-13.

·         Maono/ ndoto
Mtu yeyote asiyekuwa na maono/ ndoto hawezi kuweka bidii yeyote ile katika maisha yao maana hakuna wanachotarajia kupata au kufikia. Maana unapokuwa na maono au ndoto kuna vitu unakuwa unaviona ambavyo humfanya mtu kujiwajibisha iwe kuongeza viwango vya maombi au kuzidi kutafuta mbinu za kufika. Na mfano mzuri ni Yusufu. Hivi uliwahi kujiuliza kwa nini vijana waone na maono na wazee waote ndoto. Jibu ni jepesi ni ili kuchochea juhudi katika kile wanachokitarajia. Na moja kwa moja hali zao za kiroho zitabadilika pia.

·         Dhambi
Mtu yeyote ambaye anafanya dhambi moja kwa moja hali yake ya kiroho inadhoofika kwa kuwa inapata mashambulizi mengi ya ulimwengu wa giza. Na utumishi wa mtu yeyote hauwezi kuongezeka kwa sababu ya dhambi. Bali kushuka. Mfano uko wazi juu ya Samsoni, mara baada ya kutoa siri Mungu aliyomwonya asimwambie mtu alijimaliza mwenyewe. Dhambi ni mlango wa kushusha viwango vya kiroho vya watumishi mbalimbali. Kwa dhambi ambayo hivi sasa hutafuna watumishi wengi ni uzinzi watumishi tuamke maana Mungu anatuhitaji zaidi tumtumikie.

·         Maombi
Maombi ni eneo jingine ambalo lina mchango wa kuinua au kudumaza kiwango cha rohoni cha mtu. Mtu anapokazana na maombi hali yake ya kiroho lazima iimuke. Hivyo mtumishi asiyeomba ni rahisi sana kushambuliwa na shetani maana yeye ni simba angurumae akitafuta mtu ammeze. Hivyo kiwango cha maombi ni athari ya hali ya kiroho. Haya yalimsaidia sana Yesu, Danieli na Daudi nk

·         Neno
Rum 10:17 inasema "Imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la Mungu". Imani inakuja pale mtu anapokuwa na ufahamu wa neno la Mungu. Hivyo imani inakuwa kwa jinsi ambayo mtu anapoongeza ufahamu wa kutosha juu ya neno la Mungu. Hivyo kiwango cha kiroho kitaongezeka pindi tu mtu atapoongeza ufahamu wake juu ya neno la Mungu.

Nami namshukuru kwa ajili yako. Ni imani yangu ujumbe huu ambayo Mungu ameona aseme na wewe kama mtumishi itakusaidia katika makuzi yako ya kiroho. Hivyo ni vyema ukazingatia haya yatakusaidia kama utayatumia.
Barikiwa sana                                                                                                                                            Na Henry Nicholaus


JIFUNZE KUWA MSHINDANI NA SIO MSHIRIKI
Mungu alinitafakarisha jambo hili nami naona vyema japo kwa muda mchache tushirikiane jambo hili ili upate ufahamu toshelevu juu ya maisha tulionayo. Jambo la kwanza unalotakiwa kujua tuko mashindanoni. Haya tunayaona katika Ufu 2:10  isemayo, "Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima." Mahali ambapo pana taji kuna mashindano, huwezi kusema kuna zawadi kama hakuna mashindano. Na mashindano yeyote yana kanuni. Mfano mchezo wa mpira una kanuni 18, kadhalika na michezo mingine ili kutoa uhuru wa washindani kushinda bila upendeleo wowote. Katika maisha yetu ambayo ni sawasawa na mashindano kigezo chake kimoja wapo ni uaminifu sawasawa na Ufu 2:10
Kwa nini uwe mshindani na sio mshiriki?. Siku zote mshindani huwa na mambo yafuatayo:
·         Maono
Mtu yeyote ambaye ni mshindani huwa na maono. Maono mara nyingi humfanya kutamani kushiriki ili afike pale anapotaka kufika. Maono mara nyingi huzaa malengo. Mtu ambaye ana maono lazima atakuwa na mkakati maalum wa kumsaidia katika michezo anayoshindana. Kama nilivyosema unapokuwa mshindani na kwa kuwa tuko mashindanoni lazima utakuwa na malengo. Mfano: Uwe na maombi ya kila siku. Unapokuwa mshiriki huwezi kuwa na malengo yeyote. Kwa sababu hiyo huwezi weka jitihada.
·         Tathimini
Kwa kuwa tuko mashindanoni, tathimini ni ya msingi kwa mshiriki. Kwa maana mashindano yetu ni ya muda mrefu usiojulikana na mtu yeyote. Ni vyema mshindani akawa anafanya tathimini ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kushinda. Unapofanya tathimini unatambua wapi umekosea na nini ufanye. Wakristo wengi tumekuwa washiriki maana hatuna tabia ya kufanya tathimini ya maisha yetu. Mungu ametupa rasilimali mbali kama fedha, nafasi, muda na nyingine nyingi hivi tunajiuliza kuwa je tunavisimamia vizuri? Au tuna tumia maadam vipo? Je unajua kuna wakati wa kuvitolea hesabu. "Baada ya siku nyingi akaja bwana wa watumwa wale, akafanya hesabu nao" Mt 25:19. Kumbuka hili litakusaidia.
·          Bidii
Mshindani yeyote siku zote ni mtu mwenye dhamira ya kushinda na si kushindwa. Mshiriki yeyote kushinda au kushindwa kwake ni sawasawa kwani haimsumbui likimpa lolote lile. Wakristo wengi kukata tamaa kwao ni jambo la kawaida na hali kwao. Unakuta aliomba akakosa basi na maombi nayo yanakuwa ni kama shubiri kwake. Swala la kukata tamaa lipo kwa wengi ndio maana nasema wakristo wengi ni washiriki na sio washindani. Maana moja ya tabia ya mshindani ni mpambanaji.
Hivyo ndugu yangu Mungu anazungumza na wewe. Tunaposoma Ufunuo wa Yohana 3:21 inasema, "Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi." Tazama mstari huu Yesu anasisitiza kuwa tuko mashindanoni amka wewe usinziae maana mbingu si ya kila mtu ni ya wale washindao. Kumbuka hili litakusaidia.
Barikiwa sana                                                                                                                                        Na Henry Nicholaus

JE WAJUA KUWA INJILI UNAYOISIKIA IMEGHARIMIKIWA?
Nimeona vema niyaandike haya ili ikusaidie ewe dada, kaka, baba na mama. Kwa kuwa kwa hali iliopo sasa, bila kulisemea hili hali baadae itakuwa mbaya sana. Kitendo cha watu kuona wanaomtumikia Mungu ni washamba au wanapoteza muda wao kimeshamiri sana. Na kupelekea hata huduma kuwa ngumu. Ninapoongea haya unaweza usinielewe maana unaona makanisa yakiongezeka.Ukweli ni kwamba kuongezeka kwa makanisa ni kutimia unabii wa makristo wa uongo. Lakini ukweli ni kwamba watu wamejisahau sana tena kwa kupindukia kana kwamba maisha ya hapa duniani yana umilele.
" Au wadharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu?" Rum 2:4
Kwa kadiri wema wa Mungu unavyozidi watu wengi ndivyo wanavyopuuzia neno la Mungu. Lakini baya zaidi wasijue kuwa kuongezeka kwa neema ni kiashiria kuwa Kristo yu karibu kuja kulichukua kanisa lake. Kwa hiyo anagawa fursa nyingi sana ili wengi waweze kuwepo. Neno kanisa halimaanishi jengo kwenye biblia bali jamii ya waaminio. Nimeona nikupe ufafanuzi ili swala la wewe kuwa muumini wa kanisa fulani isiwe ajenda tena ya kukusaidia kwenda mbinguni. Kumbuka waendao mbinguni ni roho za watu. Kwa hiyo maandalizi ya kwenda mbinguni yanahitaji roho za watu.
Na kwa hivyo Mungu aliona vyema kuachilia neema yake nyingi ili watu wapate maandalizi bora ya kwenda lakini cha ajabu si wengi wanaozingatia. Watu wengi wanahangaika na kazi za mikono hata wakipewa taarifa juu ya huduma ya Mungu husema maneno yafuatayo "Niko busy siku hizi" sasa najiuliza swali moja. Je Mungu amefanya haya yote kwa ajili ya nani? Tunashindwa kujitendea haki kwa kigezo cha kutafuta kipato. Kuwa makini nalo sana. Maana neno la Mungu katika 2Tim 3:1-2 linasema, "Lakini ufahamu neno hili ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi".
Ngoja nikupe mifano michache ili uweze kuelewa kuwa Petro alichomwa moto kichwa chini miguu juu. Naye Batromayo alichunwa ngozi ili amkane Yesu lakini hakufanya hivyo. Filipo alikatwa kichwa. Kwa hiyo unaweza kuona kuwa namna gani watu wengine walivyokubali kubeba gharama ili wengine waweze kwenda mbinguni. Lakini wewe unaitwa semina, maombi au kwenye mkutano wa injili huendi. Tafakari sana.
Na ni kweli  hizi ni nyakati za hatari. Zinduka mpendwa kama wewe ni mmoja ya watu ambao wamekuwa wakipuuzia neno la Mungu. Kwa kuwa wakati uliokubalika ni sasa si kesho. Maamuzi utakayofanya sasa yana mustakabali mkubwa juu ya maisha yako ya baadae. Kesho unaweza usiwepo lakini sasa upo. Na kama umenielewe kumbuka Mungu yuko tayari kukusamehe kwa yale ulioyafanya. Fuatana nami sala hii kama unafikiri hutaweza kusema ya kwako binafsi.                                                                                                                                                                                            
Sala fupi ya toba
Ee Mungu uliye hai, naja kwako kwa njia ya damu ya Yesu Kristo. Naomba unisamehe kwa yote ambayo nimekukosea ikiwemo kupuuzia fursa ya kuujua ufalme wa mbinguni ambayo umeigarimikia mno. Kumbuka kazi yako ya msalaba ili iweze kuwa msaada kwangu katika jina la Yesu Kristo Amen!!
Barikiwa sana
Na Henry Nicholaus
 
NENO LA MUNGU LINAKUJA KWETU ILI TUPATE MAELEKEZO SAHIHI YA KUFANIKISHA MPANGO WA MUNGU KATIKA MAISHA YETU

Mungu ameliachia neno la Mungu lije kwetu ili tuweze kufanikisha mpango ambao ametuwekea katika maisha yetu. Unaposoma Yer 1:5 " Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa". Hivyo mtu haji duniani kwa mapenzi yake. Tatizo ni kwamba watu wengi wanajisahau mno wanaendekeza vitu vingine ambavyo hata Mungu hakuwaagiza wafanye.
Yn 8:32 inasema, "Tena mtaifahamu kweli, na hiyo kweli itamiweka huru" inashangaza sana kuona watu hawapendi fellowship wala kuhudhuria mihadhara ya neno la Mungu lakini wanapenda vikao vya jamii au send off na misiba. Ni jambo la kusikitisha kuona watu wanajaa kwenye misiba na kushindwa kujaa kanisani hii ni fedhea kwa Mungu kwani watu wako radhi kuhairisha shughuli zao ili nao wapate nafasi ya kuzika. Lakini hawako tayari kuacha shughuli zao waende kanisani. Halafu unashangaa mtu anasema kuwa anampenda Yesu. Unaweza jiuliza maswali mengi watu wamelogwa au wanafikiri mbinguni ni kama kanisani unaweza kuingia kirahisi tu.
Huwezi kuendesha gari bila kuwa na ujuzi wa kuliendesha, inakuaje mtu analiishia kusudi la Mungu bila kujifunza namna ya kulitunza. Hii ni vichekesho sana. Nakufikirisha wewe unayenifuatilia je rubani anapokosa mawasiliano kutoka kwa watu wa mawasiliano ardhini nini kinatokea? Jibu unalo. Watu wengi wanakufa wakiwa na deni na Mungu. Inawezekana katika kile alichoambiwa kufanya hata robo hajaweza. Kwa sababu walipokuwa duniani hawakutaka kusikiliza maelekezo ya kufuata ili waweze kuhakikisha wanafanikiwa katika kusudi waliloitiwa.
Nataka ujue jambo hili kwa msaada wako wewe binafsi. kufanikiwa kula na kulala sio mafanikio. Kwani hata mfungwa anakula na analala kwenye jela ya bure hivyo huwezi kujisifu kuwa umekula na kulala. Unachoweza kujisifu ni kutimiza mpango wa Mungu ambao uko kwako usiofanana na wa mtu mwingine. Neno la Mungu linaletwa na Mungu ili atufanyie kazi kuwa nyepesi katika kutimiza mpango wake. Kwa bahati mbaya anapoleta maelekezo anaambiwa kuwa uliokusudiwa watu kazini, vikaoni au misibani.
Umewahi kujiuliza kwa nini wewe unabaki na mwenzako amekufa na pengine ni mdogo kuliko wewe. Labda msiba ungekuwa funzo kwa wengi lakini siku hizi msiba ni fashion au sikukuu. Mungu anataka utoke kwenye mazoea na mienendo mibaya ambayo si mizuri kwa afya yako. Weka muda kwa ajili ya Bwana ili mti Mungu alioupandikiza kwako ukue hata uzae matunda maana ndipo utakapokuwa na nafasi katika ufalme wa mbinguni. Acha kuwaabudu binadamu kwa kuwapa kipaumbele hiyo nafasi mpe Mungu.
Barikiwa
Na Henry Nicholaus
PASIPO MABADILIKO HUWEZI KUONA MAPYA YAKITOKEA MAISHANI MWAKO
"...Kwa maana hamjapita njia hii bado." Yos 3:4
Wakati mwingine tunaweza tukawa tunaomba maombi mengi na hata kuunganisha nguvu zaidi ya kufunga ili kupata ufumbuzi juu ya mambo fulani na bado tusipate. Nilipojiuliza ni kwa nini haya yanaweza kutukia ijapokuwa si mara zote nilipata jibu lillilowazi kwamba tusipoendesha treni kwenye reli haliwezi kwenda.
Najua hata wewe msomaji utakuwa umejiuliza maswali wakati ukiendelea kusoma nini maana yake haya ninayoeleza. Maana inawezekana nimetumia lugha ya mafumbo kuakisi kile Roho wa Bwana alichokilenga kwako wewe unayenifuatilia. Lakini isikusumbue kwani hatukuipokea roho ya dunia ila yule atokaye kwa Bwana ili tujue na kuelewa yale tuliokirimiwa.
Mungu wakati mwingine ameshindwa kutupa majibu ya maombi yetu kwa kuwa mahali tulipo hakumruhusu Yeye kujifunua. Mfano Mw 12:1-2 tunaona Ibrahimu anaahidiwa baraka lakini akamweleza wazi kuwa hawezi kuzipata isipokuwa kama atakubali kwa dhati kuondoka nyumbani kwa baba yake. Ukichunguza kwa kina ni kipi kilimfanya Mungu amueleze hayo Ibrahimu inawezekana ni tatizo lake la mtoto, na baada ya Mungu kuona kuwa nyumbani kwa baba yake Ibrahimu kuna miungu mingine hivyo hakutaka kutoa msaada wowote kwa Ibrahimu isipokuwa amejitenga na kwa namna gani, ni kwa kuondoka kwao.
Ndugu unayeendelea kunifuatilia nataka uelewe kuwa bila mabadiliko katika maisha yako hususani ya kiroho huwezi ona ufumbuzi wa mambo yako mbalimbali. Kuna vitu ambavyo ni haki ya kila mtu aliyemwamini Kristo basi hivyo hupewa mtu mahali popote. Pia viko vingine vingi ambavyo vinahitaji hayo mabadiliko ili viweze kutokea. Nataka ulewe kuwa huwezi kutembea juu ya maji kama hujatoka kwenye boti. Kilichomfanya Petro aweze kutembea juu ya maji ni kwamba alithubutu kutoka nje ya boti halikuwa jambo jepesi kwake lakini alifanya shauri.
Hivyo mpendwa namna kanisa lilivyokuwa likienda 2005 si linavyotakiwa kwenda 2016 hivyo ni rai yangu kwako upende mabadiliko ili uweze kuona Mungu akikujibu maombi au haja za moyo wako. Swali la kujiuliza kwa nini Ibrahimu abarikiwa akiwa nyumbani kwa babaye jibu ni kwamba alikuwa anaendesha treni nje ya reli hata kufanya ugumu mwingi wa kwenda kwake. Ukisoma biblia yako utagundua alipokubali kuhamia kwenye reli alibarikiwa.
Mungu akubariki
Na Henry Nicholaus 

HAKUNA ALIYE BORA KULIKO MWINGINE
"... Kila mtu na amhesabu mwenzie kuwa bora kuliko nafsi yake." Fil 2:3
Katika maisha tulionayo kuna wakati mtu aweza kujiona yeye ni wa pekee kuliko watu wengine. Hili ni kosa kubwa kwa sababu maisha yetu yanategemea sana watu wengine. Mfano: Unaweza kununua chakula kwa mtu ukala kwa pesa zako. Lakini ukichambua kwa kina utagundua kuwa pesa zako zimetokana na kazi zako mbalimbali unazofanya. Hivyo wasingekuwepo watu wa kusaidia shughuli zako usingepata pesa. Pia asingekuwapo mkulima chakula ungepata wapi? Je ungelima mwenyewe na kuvuna na kisha kukiandaa mpaka katika mazingira ya kutumika?
Nimewahi kujiuliza kama watu ndio kisababishi cha mafanikio ya mtu mwingine jeuri za kifedha, madaraka, ukubwa, uwezo wa akili vyatoka wapi? Utagundua ni ukosefu wa maarifa tu ndio unaomfanya mtu kuwa jeuri Hos 4:4. Nataujue na kuelewa kuwa tulivyonavyo ni dhamana tu na si sababu yetu leo kujisifu. Umepata wewe mwenzio kakosa si kwamba ni mtenda dhambi kuliko wewe ila ni mfumo aliouweka Mungu mwenyewe wa maisha ya vijiti. Kama umewahi ona mbio za vijiti utagundua mmoja anakimbia mpaka mahali fulani kisha anampa mwingine. Hivyo majivuna hayana sababu kwa kuwa ukifa huzikwi navyo bali anapewa mtu mwingine unawezekana hata watoto wasipate wakati mwingine lakini ndivyo maisha yalivyo.
Kila mtu ni bora kwa kuwa Yesu amemthaminisha iweje leo tujione bora kuliko wengine. Kama kufa alitufia sote kwa nini tujione wakufaa kuliko wengine. Ni muhimu tukajishusha  sana ili tupate kuishi kwa mafanikio makubwa duniani. Kwa kuwa sisi ni wapitaji tusiwanyanyase wengine wakajihisi kuwa hawana thamani. Mpe heshima yake aliye nacho na asiye nacho maana wote ni muhimu kwa maisha yetu. Isa 43:4 Mungu anasema ameweka watu na makabila ya watu kwa ajili yetu na si wenye pesa, akili au madaraka bali kila awae yeyote
Inawezekana maneno ni makali kwako hilo lisikusumbue endelea kusoma ujumbe huu ili upate yote Mungu aliokusudia kwako. Pia natamani ujue kuwa duniani kuna watu wa kila aina ila kuvumiliana ni jambo la msingi sana katika kuishi na watu. Unakuta mtu anapigiwa simu anasema huyu kazidi kwa kuomba msaada sio vizuri kusema hivyo bora mfundishe njia ya kujitegemea lakini usimsimange. Elewana na watu nawe utafanikiwa siku zote. Kama Yesu alijishusha hali ni Mungu kwa nini sisi?
Barikiwa                                                                                                                                                              
Na Henry Nicholaus

SAFARI YA KWENDA MBINGUNI INAHITAJI MAARIFA TENA SAHIHI
Rum 10:2 inasema, " Kwa maana nawashuhudia ya kwamba wana juhudi ya Mungu lakini si katika maarifa."
Wakristo wengi katika kanisa la leo wanaishi ukristo wa mazoea ambao unawapa matatizo makubwa sana. Hii ni kwa sababu hawapendi kuwekeza katika maarifa. Unakuta mtu ni mkristo lakini ana umaskini mkubwa unabaki kujiuliza ni kweli ukristo ndio mtazamo wake? Jibu ni hapana, tena sababu iko wazi huwezi kuendesha ndege kama huna elimu ya urubani lakini tofauti kwa wakristo ni kwamba wao huendesha ndege hali hawana mafunzo ya urubani matokeo yake hugogonga kusiko julikana.
Kwa unayenifuatilia ni imani yangu kabisa hali ya maisha ya wakristo wengi haiwezi kukushtua kwani hata wewe utakuwa unanielewa vizuri sana. Na matokeo yake imesababisha jina la Yesu kuaibika kwa kuwa watu wamemvaa vibaya. Kanisani kuna wakristo wa aina mbili, moja ni washirika na mbili ni wafuasi. Jamii ya wakristo wafuasi ni kubwa sana kuliko ile ya washirika. Swali kwa nini wengine ni wafuasi na wengine ni washirika? Hii ni sababu wengi hawapendi maarifa.
Ukienda kanisani siku hizi kuna vikao vingi kuliko maombi. Unajiuliza kanisa linaenda wapi kama unapenda kuelewa hili, tazama Mdo 12:5 utaona kanisa la zamani zile liliomba baada ya Petro kukamatwa. Bali kanisa la leo kama hayo yangetokea wangekaa vikao. Hivyo utagundua kanisa la leo linaiga utaratibu ambao haukuwepo. Matokeo yake leo kanisa si msaada kwa watu. Fikiri namna kanisa lilivyoshushwa hadhi namna hii. Zamani watu wakiwa na matatizo walikuwa wakikimbilia kanisani lakini hivi leo wanakimbilia mahakamani. Sisemi ni vibaya wao kutafuta haki zao mahakamani na wala si dhambi bali napenda kukufikirisha wewe unayenifuatilia ni kwa kiasi gani kanisa limepoteza mvuto.
Wakristo wengi ni wavivu hawapendi kusoma biblia, kusikia neno la Mungu hali semina zipo na mikutano ya injili ipo. Angali neema tulionayo isije ikatupumbaza sana bali ni mtaji kwetu hususani sisi tuliokoka. Ni muhimu mpendwa tukaelezana haya ili usije siku ile ukajikuta utakapojikuta ukaanza kulalamika. Mimi nasimama katika zamu mwenye sikio na asikie.

KATIKA MAISHA TULIONAYO MUNGU AMEWEKA VYOTE UZIMA NA MAUTI
Kumb 30:15-16 inasema, "Angalia nimekuwekea leo mbele yako uzima na mema, na mauti na mabaya; kwa hivi nikuagizavyo leo kumpenda Bwana, Mungu wako, kuenenda katika njia zake, na kushikilia maagizo yake, na amri zake, na hukumu zake, upate kuwa hai na kuongezeka; Bwana, Mungu wako, apate kukubarikia katika nchi uingiayo kuimiliki".
Watu wengi wanaishi dunia wakifikiri kuna mema tu, waache kufahamu pia kuna mabaya yote yapo bali inategemea na mlango ulioingilia tu. Mlango ulioingilia unauweza wa kukufanya ukutane na kimoja wapo. Kwa sababu hiyo Mungu akiwa hapendi watu wake tukutane na matokeo ya sintofahamu katika maisha yetu. Ameamua kutuweka bayana juu ya yote.
Ndugu unayenifuatilia nataka tufikirishane kwa pamoja kabisa jambo hili. Wakati Adam alipochagua kuasi hakuwa anajua ni kura ya aina gani anakwenda kuifunua mbele yake. Nataka unielewe kidogo alivyofikiri kabla ya kula tunda ni tofauti na matokeo aliyopata baada ya kula tunda hii ni sababu kuwa kurasa aliyofunua ina mema na mabaya ndani yake. Na kwa sababu hiyo alilazimika kuanza kula kwa jasho, jambo ambalo hakuwahi kuliona. Fikra alizonazo Adam wakati huo bado zimewalevya vizazi vyake mpaka leo. Ndipo baada ya Mungu kuona jambo hili anaamua kutueleza sisi vizazi vyake uhalisia.
Ndipo kwa maelezo hayo ya Kumbukumbu ya torati Mungu aliponipa kujua kuwa matokeo ya maisha yetu sisi tuliopo duniani sasa yatategemea na baraka ama laana. Na ukisoma vizuri utagundua ametumia neno ' leo' hilo neno si urembo bali lina maana yake. Na maana yake ndio hii kuwa ni msisitizo kwa sisi tunaosoma haya sasa na sio jana. Ni muhimu ukaelewa hayo. Na ndio sababu utanielewa kwa nini duniani vipato vinatofautiana.
Nakusihi sana mpendwa ukae karibu na uwaridi nawe utanukia. Hii ina maana kuwa kama unapenda mema ni muhimu sana uhakikishe unajishikiza kwa Mungu nawe hutayatafuta. Mema au mabaya hayaombwi maana yenyewe hujidhihirisha tu pale mtu anapochagua mlango wa kuingilia lazima kimoja wapo kitokee. Ili unielewe vizuri, ukirusha shilingi hakuna namna itaonyesha na pande mbili bali ni lazima itaonyesha kichwa au mkia na ndivyo maisha yalivyo.
Barikiwa sana                                                                                                                                                                 Na Henry Nicholaus

MAZINGIRA YA KIFAMILIA AU UKOO AU KABILA YANAWEZA KUKUZUIA NDOTO YA MUNGU ISITIMIE KATIKA MAISHA YAKO
Haya tunayaona katika Amu 6:11-12 inasema, " Malaika wa Bwana akaenda akaketi chini ya mwaloni uliokuwa katika Ofra, ulikuwa mali yake Yoashi, Mwabiezeri; na mwanawe Gideoni alikuwa akipepeta ngano ndani ya shinikizo, ili kuificha machoni pa Wamidiani. Malaika wa Bwana akamtokea, akamwambia, Bwana yu pamoja nawe, Ee shujaa."
Angalia kwa makini sana maneno Gideoni anayoambiwa na malaika na kile anachofanya kama kinaendana? Gideoni anapepeta ngano kwenye shinikizo halafu malaika anamweleza kuwa yeye si mtu wa kawaida naye ni shujaa. Kwa hali ya kawaida lilikuwa neno gumu sana kwake. Kwa kuwa malaika aliona hali Gideoni aliyonayo na bado alimwambia kuwa yeye ni shujaa. Ukweli ni kwamba mbingu inamwona Gideoni kama shujaa lakini yeye haoni. Hii ni kwa sababu iko hazina ambayo Mungu aliwekeza ndani ya Gideoni lakini hakuweza kusitirika kwa kuwa familia yake ni waabudu miungu ya baali.
Utaona Gideoni akijitetea unapoendelea kusoma zaidi mistari ya sura ya 6 ya kitabu hiki cha waamuzi juu ya udogo wake na umaskinia alionao na udhaifu wa kabila lao. Tofauti na Yeremia yeye aliambiwa na Mungu tangu akiwa mdogo kuwa yeye amewekwa kuwa nabii wa mataifa. Gideoni hakulijua hilo na bado asingeweza kujua kama Mungu asingemwambia kwa kuwa eneo alilokuwepo ndio lilikuwa ni tatizo. Na eneo hilo ni kwamba waalikuwa wakiabudu miungu ya baali ambayo ilimzuia Mungu kujifunua kwao.
Wako watu wengi ni mashujaa ila wanaishi maisha dhaifu inawezekana familia, ukoo au kabila zao ni kikwazo. Inawezekana pia mila zao zimekuwa zikizuia ushujaa wao. Hujawahi kuona wanawake kwenye familia fulani wakishindwa kuolewa na kuishia kuzaa nyumbani kwao? Wanafamilia kufa kila baada wanapofikisha umri fulani? Na mengineyo yenye mfanano na hayo? Hivyo unayefuatiliana nami Mungu anakuazia mema sema kuna vizingiti vingi mbele yako.
Hali hii bila kujua imekatisha watu tamaa ya kwenda kanisani wakifikiri mchungaji au mtumishi wao hana upako kumbe si kweli hata kidogo. Nataka ubadilike uondoke huko ili uwe shujaa sasa maana ndio mpango wa Mungu juu yako.
Barikiwa sana                                                                                                                                                                 Na Henry Nicholaus

KWA NINI KANISA LA LEO HALINA IMANI?
Napenda tufikirie kwa pamoja ndugu mpendwa siku hii ya leo. Unaweza usiafikiane na mimi kwa urahisi juu ya maelezo nitakayoyatoa lakini jambo la msingi ni kwamba ni muhimu hata wewe ujiulize juu ya hili. Maana Mungu anataka kutupa uhalisia wa hili.
Yak 2:14,17 inasema, "(14) Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je! ile imani yaweza kumwokoa?....(17) Vivyo hivyo na imani,isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake".
Kanisa la leo haliishi kwa imani kwa kuwa kile watu wanachofundishwa hawakiishii. Au yale kanisa wanayosema hawayatendi. Nikupe mfano mmoja Mdo 12:5 inayosema, "Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba Mungu kwa ajili yake". Tazama kanisa la awali lilipata matatizo liliomba kwa ajili ya hayo. Na biblia imeweka wazi kiwango cha maombi yaliokuwa yanaombwa wakati huo baada ya tatizo kutokea. Soma neno la Mungu linasema kwa 'juhudi'. Kanisa la leo linafanya kitu gani? Likitokea tatizo mtumishi atasimama mbele kisha ataomba kwa dakika kadha halafu kila kitu kimesahaulika. Kuna vikao vingi badala ya kuunganisha nguvu ya Mungu ilowekezwa ndani yetu kwa njia ya maombi Efe 3:20.
Situ hayo yapo mengi na zaidi ila nataka tu nikufikirishe maana nikieleza kila jambo sitaweza kuandika. Swali kwa nini kanisa halina imani, ni kwa sababu halitendi kile neno la Mungu linavyosema, maana imani bila matendo imekufa. Kanisa limeegemea kwenye mapokeo na matokeo yake kuzaa madhehebu na sio ushirika. Kanisa la kwanza lilisimama katika ushirika (Mdo 4:34-35) ndio maana ikawa rahisi sisi leo kuipokea imani kutoka kwao. Imani inapoishiwa inakuwa hai. Sina uhakika vizazi vinavyokuja tutavirisisha nini? Leo hii kanisa limekuwa adui kwa vijana na kimbilio kwa wazee kwa kuwa wengi wakijua muda wao duniani uko ukingoni. Maisha ya vijana wa leo ilikuwa ni picha kwa kiasi gani kanisa limeshindwa kuwasaidia hadi vijana kuililia serikali. Je kanisa liko wapi?
Biblia inasema dini ilio safi ni kuwatazama yatima na wajane. Je ndivyo kanisa lifanyavyo? Yak 1:27 inatueleza yote kwa uwazi kuhusu habari hizi. Ni muhimu kila unapoishi uyatafakari haya kwa jicho jingine. Sina maana ujiengue kwenye dini au ukristo au udhehebu bali nina maana ya kukusaidia ni kwa namna gani ujipange katika safari ya kwenda mbinguni.
Sina mpango wa kunyooshea kidole kanisa lakini nakutahadharisha kuwa kama mteule ujue kama unafikiri kanisa ndio linakupeleka mbinguni hutafika na ndoto yako itayeyuka peupe. Siku hizi hata serikali inatumia kanisa kwa ajili ya siasa. Ni muhimu ukayajua haya ili ujipange na neno la Mungu ili safari yako ya kwenda mbinguni ipate kufanikiwa. Maana Mungu amenipa hiyo neema ya kusema na wewe unayenifuatilia kupitia E Gospel.
Barikiwa sana                                                                                                                                                                Na Henry Nicholaus 

UNAPOTOA SADAKA KWA MTUMISHI HAUTOI KWAKE ILA KWA MUNGU WAKE AU MIUNGU YAKE
Bwana Yesu asifiwe leo tunataka kuongeza ujuzi wetu juu ya sadaka. Ili kwa walau kama tumekuwa tukitoa kwa mazoea tuache kufanya hivyo ili sadaka unayotoa iwe na tija kwako. Kwa kuwa sadaka ni mtaji.
 Fil 4:19 inasema, "Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachohitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu".
Angalia mara baada ya Paulo kupewa vitu alisema hayo maneno hayo katika Wafilipi 4:19. Anaposema, "Na Mungu wangu atawajazeni..... Hii inatufikirisha kuwa sisi tunaosoma habari hii kuwa tunapotoa sadaka kwa mtumishi yeyote hatutoi kwake ila kwa Mungu wake au miungu yake. Na ndio maana Paulo alisema na Mungu wangu...Ni muhimu hili ukalielewa maana watu wengine wameshindwa kupokea baraka Mungu anazoziachia kupitia watumishi kwa dhana kuwa watumishi wanazila. Mungu yuko rohoni hakuna namna aweza kupokea vya mwili ila yeye hupokea vya rohoni. Hivyo sadaka tutoayo iko katika mwili hivyo hupokelewa na mawakala wa Mungu duniani na wakati huohuo Mungu huipokea katika roho kama ni ya kufaa. Kwa sababu inaweza kupokelewa na mtumishi na bado isifae kwa Mungu kumbuka hili.
Kwa sababu hiyo Mungu alimwagiza Musa kupokea sadaka watakazoleta wana wa Israeli zitokazo moyoni na sio vinginevyo Kut 35:20-22. Ukisoma huo mstari utaliona jambo hili kwa mapana yake. Niliposoma hiki kifungu ndio nikagundua kwa nini Mungu amsukume Musa asipokee sadaka kwa mtu isipokuwa imetoka moyoni. Uwe na uhakika hiyo sadaka haikuwa inakwenda kwa Musa ila kwake ndio maana alimpa hayo masharti. Mpaka hapa utaelewa kuwa sadaka unapompa mtumishi haumpi yeye ila Mungu wake au miungu yake.
 Unaposoma kifungu hiki cha Mdo 5:3-4,9 utaona Petro anamwambia Anania na Safira kuwa hawakumwambia uongo mwanadamu ila Roho Mtakatifu wakati wakileta sadaka miguuni pa Petro. Kupitia maneno hayo utagundua kuwa Petro anataka kutufahamisha kuwa utoaji wa sadaka ni muhimu ukatazamwa kwa Mungu au miungu inayopokea sadaka na sio mtumishi anayepokea. Kwa kuwa Anania na Safira walitazama kuwa watumishi ndio wanaopokea na sio Mungu au miungu yao.
Mt 6:21 inasema, "Kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo na moyo wako utakapokuwepo".Hivyo sadaka sio swala la kutazama mtumishi anayepokea ila Mungu au miungu wa mtumishi huyo.Hili ndilo la muhimu. Maana wako ambao wameshindwa kutoa sadaka wakiamini kuwa mtumishi anazila. Si mtazamo Mungu anataka uwe nao bali huu ambao amekupitisha na sio vinginevyo. Unapoona kuwa wewe una mtazamo wa kuwa sadaka zinaliwa iwe ni kweli au si kweli tambua kuwa shetani anatafuta namna ya kukutenga na baraka za Mungu zilizopo kwenye utoaji wa sadaka. Maana kazi yake ni kuwafanya watu wasifanikiwe ili waone Mungu hana cha kuwasaidia.
Barikiwa sana                                                                                                                                                                Na Henry Nicholaus

TUEPUKE UZINZI MAANA UNAHARIBU MAISHA YETU PASIPO KUJUA
Kufuatana na Mithali 6:33  "Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake"
Nafsi ni sehemu ya mtu inayomfanya mtu huyo awe hai. Uhai huu si ule unaotawala kuishi au kutoishi kwa mtu bali ule unaotawala aina ya viwango vya maisha anayoishi mtu. Mith 23:7a inasema hivi: " maana aonavyo mtu nafsini mwake, ndivyo alivyo" Hii inatupa kujua kuwa, Mungu aliumba nafsi ya mtu kwa namna ambavyo aliweka vitu ndani yake, ambavyo vinatumika kuweka aina na viwango vya uhai wa mtu katika maisha yake.
Ndani ya nafsi kuna akili, wakati katika mwili kuna ubongo. Ubongo unamsaidia mtu kufaulu masomo yake.Lakini akili inatumika ndani ya nafsi kuweka aina ya kiwango cha maisha ya mtu. Kuna mahusiano ya akili na nafsi. Sasa baada ya ufafanuzi huo nataka uelewe kuwa mtu mzinzi anaweza kutumia ubongo wake vizuri masomoni lakini hawezi akawa na viwango vizuri vya maisha kwa kuwa ameiangamiza nafsi yake mwenyewe kwa uzinzi. Hujawahi ona mhitimu wa chuo kikuu akiwa na matokeo mazuri lakini kazi hana. Sio wote husababishwa na uzinzi ila uzinzi inaweza kuwa sababu moja ya aina ya watu wa aina hiyo. Kwa kuwa akili imekuwa imepofushwa.
Biblia inasema ... Mtu aziniye ... anaiangamiza nafsi yake, ... maana yake anaiharibu isifanye kazi yake ilioumbiwa. Hali hiyo inafanya nafsi yake ipate "jeraha na kuvunjiwa heshima, wala fedheha yake haitafutika" Mith 23:7b. Ukiichunguza nafsi zaidi, utaona ya kuwa si tu imebeba nafsi ndani yake, lakini pia imebeba maeneo yanayoshughulikia hisia na maamuzi, makusudio ya mtu na dhamiri ya mtu.
Kwa mtazamo huu nafsi iliumbwa kwa jukumu la kutafsiri mawasiliano kati ya roho ya mtu na nafsi yake.Kwa tafsiri nyingine nafsi anaunganisha uhusiano wa mwili na roho. Hii ni kwa sababu roho na mwili havifanani katika haiba ya utendaji kazi. Sasa fikiri nafsi imeharibika nini kinatokea? Na ndio maana Mith 6:33 inatutazamisha haya. Kwa sababu hiyo wanafunzi wa sekondari, vyuo vikuu na vijana wamejikuta katika maisha ya sintofahamu siku za usoni.
Lakini ni muhimu kujua kuwa hatawezi kuacha uzinzi kama vyanzo vya tabia hii havijashughulikiwa. Vyanzo vipo vingi lakini vile vikuu ni utazamaji wa picha za video au sinema, nyimbo za dunia na matumizi mabaya ya internet. Hizi ndio njia kuu ambazo shetani amewekaza na kuteka fahamu za vijana wengi. Anawatajirisha wasanii duniani na kuamuru waimbe uchi au nusu uchi bila kujua hufumua hisia za mapenzi za vijana wengi. Kadhalika na picha za video na sinema za leo hugubikwa na kadhia ileile ya picha za uchi zinazohamsha hisia. Hivyo basi vyote hivi huwekwa mitandaoni pasipo matumizi mazuri mtu hujikuta akinufaika na huduma hizi.
Sina mengi ya kusema ila ni jambo la muhimu kama kijana au mtu wa rika lolote kuwa na tahadhari. Uzinzi umevunja ndoa nyingi, heshima za watu au watumishi na hata kuharibu mipango mizuri ya Mungu juu ya watu wengi. Wakijikuta wanashindwa kufikia ndoto zao mpaka kufa kwao. Sina mpango wa kumwogopesha mtu bali kutadharisha.
Barikiwa sana                                                                                                                                                                 Na Henry Nicholaus

JE BIBLIA INASEMA NINI KUHUSU UCHAWI?
Ni jambo la kusikitisha sana kuona idadi kubwa ya Wakristo ambao wanaogopa wachawi.  Imewapasa Wakristo kuchunguza maneno ya Mungu kuhusu somo hili.
"Tena mtu mume au mtu mke aliye na pepo, au aliye mchawi, hakika atauawa; watawapiga kwa mawe; damu yao itakuwa juu yao."  ( Walawi 20:27)
"Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, wala mtu alogaye kwa kupiga ma- fundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.  Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana."  (Kumbukumbu 18:10-12)
"Bwana Mungu asema hivi; Ole wao wanawake wale, washonao hirizi katika viungo vyote vya mikono, wawekao leso juu ya vichwa vya kila kimo, ili wawinde roho za watu; je! mtaziwinda roho za watu wangu, na kuzihifadhi hai roho zenu wenyewe?"  (Ezekieli 13:18)
Ewe! Mkristo mwenzangu, mbona usimtegemee Mungu tu?  Je! Mungu aliyekuumba hawezi kukulinda na uchawi na nguvu za Shetani?  Basi, unapojaribu kujisaidia kwa uchawi usisahau jinsi Yesu alivyosema "hamwezi ku- tumikia mabwana wawili."  
Tena twasoma: "Msiwaendee wenye pepo, wala wachawi; msiwatafute; ili kutiwa unajisi na wao; Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu." (Mambo ya Walawi 19:31)
"Vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashet- ani.  Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani.  Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.  Au twamtia Bwana wivu?  Je! tuna nguvu zaidi ya yeye?"  (1 Wakorintho 10:20-22)
"Nami nawaambia ninyi rafiki zangu, msiwaogope hao wauuao mwili, kisha baada ya hayo hawana wawezalo kutenda zaidi.  Lakini nitawaonya mtakayemwogopa; mwogopeni yule ambaye akiisha kumwua mtu ana uweza wa kumtupa katika Jehanum; naam, nawaambia, Mwogopeni huyo."  (Luka 12:4-5)

MADHARA YA KUFUATANA NA UCHAWI
Mfalme Sauli alitafuta msaada kwa mwanamke mmoja mwenye pepo wa utambuzi (1 Samweli 28:7-25).  Je! Mungu alifurahi naye?  La! Hasha!  Twasoma:
"Basi Sauli alikufa kwa sababu ya kosa lake alilomkosa Bwana, kwa sababu ya neno la Bwana, asilolishika; na tena kwa kutaka shauri kwa mwenye pepo wa utambuzi, aulize kwake, asiulize kwa Bwana; kwa hiyo akamwua, na ufalme akamgeuzia Daudi, mwana wa Yese."  (1 Nyakati 10:13-14)
“BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye manadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha BWANA. Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jagwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.” (Yeremia 17:5-6)
YESU ANAYO MAMLAKA YA KUSHINDA UCHAWI
Neno la Mungu linatudhihirishia ya kuwa Yesu Kristo ana mamlaka ya kushinda uchawi na nguvu zote za Shetani; Twasoma:
"Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi."  (1 Yohana 3:8)
"Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo; aka- watoa pepo kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi."  (Mathayo 8:16)
"Naye Yesu akiona ya kuwa mkutano unakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala usim- wingie tena. . . Hata alipoingia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza kwa faragha, Mbona sisi hatukuweza kumtoa?  Akawaambia, Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lo lote, isipokuwa kwa kuomba."  (Marko 9:25, 28-29)
Basi, haiwezikani kumloga Mkristo aliye mwaminifu katika kushika amri za Mungu.  

HAKUNA UCHAWI JUU YA WATU WA MUNGU
Neno la Mungu linatuthibitishia ya kuwa  hakuna uchawi juu ya watu wa Mungu. Nabii Balaamu alijaribu kutoa laana juu ya watu wa Mungu asiweze.  Ndipo alipokiri akisema:
"Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, wala hapana uganga juu ya Israeli.  Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, ni mambo gani aliyoyatenda Mungu!"  (Hesabu 23:23)
Mkristo akiambiwa amelogwa afanye nini?  Asitafute mchawi wala mganga wa kienyeji bali amtegemee Mungu. Twasoma:
"Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong'ona; je! haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao?  Je! waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai?”  (Isaya 8:19)
“Simama sasa na uganga wako, na wingi wa uchawi wako, uliojitaabisha nao tangu ujana wako; labda utaweza kupata faida, labda utaweza kushinda.  Umechoka kwa wingi wa mashauri yako; basi, na wasimame hao wajuao falaki, wa- zitazamao nyota, watabirio kila mwezi mambo ya mwezi huo, wakakuokoe na mambo yatakayokupata.  Tazama, watakuwa kama mabua makavu; moto utawateketeza; hawatajiokoa na nguvu za mwali wa moto; hautakuwa kaa la kukota moto, wala moto wa kukaa karibu nao.  Ndivyo yatakavyokuwa mambo hayo uliyojitaabisha nayo; wale waliofanya biashara nawe tangu ujana wako watatanga- tanga mbali nawe, kila mtu akienda zake; hapatakuwa na mtu wa kukuokoa."  (Isaya 47:12-15)

MUNGU HITULINDA TUNAPOMTII NA KULISHIKA NENO LAKE
Mkristo hulindwa na Mungu akifuata maneno yafuatayo:
"Basi mtiini Mungu, Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.  Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi."  (Yk. 4:7-8)
"Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.  Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha ku- yatimiza yote, kusimama.  Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.  Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; kwa sala zote na maombi mkisali kila wa- kati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote."  (Waefeso 6:12-18) 
"Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu."  (Warumi 8:38-39) 

WANA HERI WALE WANAOMTUMAINI MUNGU SIKU ZOTE
“Amebarikiwa mtu Yule amtegemeaye BWANA, ambaye BWANA ni tumaini lake. Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu hata wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda”  (Yeremia 17:7-8)
Soma pia: (Zaburi 118:7-9; 23:1-6)

UMUHIMU WA KUWA NA IMANI THABITI WAKATI WA MAJARIBU

Katika maisha tulionayo majaribu hayana budi kuja maandamu tuko duniani. Kwa kuwa yapo m]Mungu anapenda kutueleza leo namna nzuri ya kuyaendea ili maisha yetu yawe ya ushindi siku zote hapa duniani.
"Hata Daniel alipojua yakuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake; (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu), akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo." Dan 6:10
Tunaona picha yote ya hili lililotokea kama tukianza kusoma kuanzia ile aya ya 1 mpaka hapa katika aya 10. Mawaziri na maamiri walitokea kumchukia Daniel nao wakatafuta namna ya kumtia hatiani lakini wasiweze kuipata kwa kuwa Danieli alikuwa mwaminifu na mtauwa wa Bwana. Hivyo basi wakaazimia watunge sheria itakayosababisha watu wote wamwabudu mungu mmoja yaani yule watakaomtengeneza. Kila mtu itampasa kumwinamia kila panda itakapopigwa.
Lakini tunaona ujasiri wa Danieli katika mstari wa 10 wa sura ya 6. Danieli hakutaka kufanya kwa kificho ili watu wajue kuwa yeye hayuko miongoni mwao. Tendo la Danieli kuomba hali madirisha ya chumba chake yamefunguliwa katika wakati ambao kumetangazwa mbiu ya kumwabudu Mungu mmoja ni jambo la ujasiri mkubwa.
Kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho. Hivyo ni kitu gani tunajifunza katika maisha ya namna hiyo? Tunapata kujifunza kuwa wakati wa majaribu ndio wakati mzuri sana wa kuwa na misimamo juu ya maisha yetu. Haijalishi ni kwa jinsi gani jaribu lilivyo bali ndio mahali halisi pa kusimamia imani zetu. Hata kama imani ni ndogo mno bado kumbuka Yesu alituambia itauambia mlima huu ng'oka na ukajitose baharini. Hivyo kwa kiwango cha imani ulicho nacho ni vema ukatumia hicho kwa kuwa jaribu haliji zaidi ya uwezo wako.
Nini faida yake? Katika kusimamia imani ulionayo wakati wa jaribu kuna mambo mawili makubwa ambyo hutokea. Moja utaweza kushinda lile jaribu na mbili Mungu atatukuzwa katika hilo jaribu na watu watajua kuwa Mungu aliye hai ndio Mungu wa kweli. Haya tunayaona katika Dan 6:18-28. Lakini hata hivyo kama kulikuwa na watu nyuma ya hilo jaribu tunapata kujua kuwa hata wao anguko linawasubiri au huwakumba kwa haraka.
Hivyo ndugu mpendwa unayenifuatilia kwa karibu jifunze sana kuwa na imani thabiti hususani unapopatwa na majaribu maana kwa kufanya hivyo utajijengea nafasi nzuri ya kiroho na Mungu wako kuheshimiwa kwa watu wengine.
Barikiwa sana                                                                                                                                                                     Na Henry Nicholaus

JE DHANA YA KUWA MKRISTO INAELEWEKA KWA WAKRISTO?
Nimeweka katika mfumo wa swali ili mimi na wewe tujadiliane kwa pamoja. Maana nimegundua bila jambo hili kulijadili tutapata wakati mgumu sana siku ile.

LUKA 9 :23 "Akawaambia wote, mtu yeyote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe ajitwike msalaba wake kila siku anifuate.
Hebu fikiri juu ya kauli hii na tafsiri na neno 'Mkristo'. Je inatupa maana gani? Kutokana na mstari tajwa hapo juu. Naweza kusema kuwa mkristo ni mtu anayeishi kama Kristo katika maisha yake kwa hiari na dhamira yake mwenyewe bila kulazimishwa. Kwa maana hii basi kuwa mkristo huletwa na mfumo wa maisha ufananao na Kristo mwenyewe.
Kwa muda sasa watu wengi wamekuwa wakiingia makanisani kwa sababu walikulia katika ukristo. Na kwa sababu hii basi inawafanya wengi waamini kuwa hata mbinguni wataingia kwa gia hiyo hiyo. Hili ni jambo la kusikitisha sana maana jambo hili halina ukweli na ndio maana ninapokumbuka Hos 4:6 inaniumiza sana maana jamii kubwa ambayo imekuwapo kanisani kwa muda mrefu haijaelezwa njia sahihi ya namna gani unaweza kuingia mbinguni.
Mimi kusema kwamba ni rubani wakati ni mwalimu haiwezi kubadili uhalisia na kunifanya mimi ghafula kuwa rubani. Jambo hili liko kwa watu wengi wanafikiri wakikiri kuwa wao ni wakristo hali hawauishi ukristo basi watakuwa ni wakristo. Ukristo uko kwenye kipimo cha maisha na si maneno. Hebu tutazame hii mistari kadha tuone ukristo kipimo chake ni nini?
“Wakati Mwana wa binadamu atakapofika katika utukufu wake, na malaika wote pamoja naye, ndipo atakapoketi juu ya kiti chake cha ufalme chenye utukufu. Na mataifa yote yatakusanyika mbele yake, naye atawatenganisha watu, mmoja kutoka kwa mwenzake, kama vile mchungaji anavyotenganisha kondoo na mbuzi.  Naye atawaweka kondoo kwenye mkono wake wa kuume, lakini mbuzi kwenye mkono wake wa kushoto. “Ndipo mfalme atakapowaambia wale walio kwenye mkono wake wa kuume, ‘Njooni, ninyi ambao mmebarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme uliotayarishwa kwa ajili yenu tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu. Kwa maana nilikuwa mwenye njaa nanyi mkanipa chakula; nilikuwa na kiu nanyi mkanipa kinywaji. Nilikuwa mgeni nanyi mkanikaribisha; nilikuwa uchi, nanyi mkanivika. Nilishikwa na ugonjwa nanyi mkanitunza. Nilikuwa gerezani nanyi mkanijia. Mt 25:31-36
Kutokana na mistari hapo juu tunaona kwamba Yesu akituonyesha anachokiangalia si umaarufu au uhodari wa mtu kusema yeye ni mkristo au la. Bali mfumo wa maisha ya mtu je ulijaa ukristo? Na ukristo huo anaufafanua nao ni huu "Kwa maana nilikuwa mwenye njaa nanyi mkanipa chakula; nilikuwa na kiu nanyi mkanipa kinywaji. Nilikuwa mgeni nanyi mkanikaribisha; nilikuwa uchi, nanyi mkanivika. Nilishikwa na ugonjwa nanyi mkanitunza. Nilikuwa gerezani nanyi mkanijia." Mt 25:35-36
Sasa swali langu kwako Je hiki Yesu alichokisema unafanya hata kwa sehemu kama hutendi kauli yako wewe ni mkristo ni batili pasipo hata wewe kujua. Ukiwa mkristo hata ulimwengu wa roho unakujua. Swala sio kujulikana katika ulimwengu wa mwili na damu, swala ni kufahamika katika ulimwengu wa roho pia.
Wayahudi kadhaa wenye kupunga pepo wabaya, walisafiri huko na huko, wakijaribu kulitumia jina la Bwana Yesu kwa wale waliokuwa wamepagawa na pepo wabaya. Walikuwa wakisema: "Ninawaamuru kwa jina la Yesu ambaye Paulo anamhubiri." Watoto saba wa Skewa, Kuhani Mkuu wa Kiyahudi, walikuwa miongoni mwa hao waliokuwa wanafanya hivyo. Lakini pepo mbaya aliwajibu, "Ninamfahamu Yesu, ninamjua pia Paulo, lakini ninyi ni nani?" Mdo 19:13-15
Angalia jinsi watoto wa Skewa walivyojibiwa na pepo mbaya, "Ninamfahamu Yesu, ninamjua pia Paulo, lakini ninyi ni nani?" Mdo 19:15 .Nataka ujue kuwa ukiwa mkristo lazima na ulimwengu wa roho utakujua. Kuna watu wanasema wao ni wakristo angali wlimwengu wa roho hauwatambui. Pepo anawajua Yesu na Paulo si kwa sababu nyingine ila maisha yao maana walikuwa waombaji, wanasaidia watu na kuvunja kazi za ulimwengu wa giza. Na kama ulimwengu wa giza hauja kutambua wewe ni mkristo huwezi kuwa wa Yesu hata kidogo. Na kwa tafsiri hiyo wewe si wa kundi lake.
Kwa hiyo ndugu mpendwa ni imani yangu kuwa utakuwa umenielewa kwa kifupi, japo elimu hii ukizidi kukaa vizuri na Roho wa Kweli atazidi kukufundisha kwa mapana zaidi na zaidi juu ya jambo hili. Hivyo ni muhimu uelewe maana nimeona tushirikiane hili maana kuna watu wanasema wao ni wakristo tukisema tuombe hawaombi, tukisema semina hawaji, tukisema bible study hawafiki, tukisema tutoe hawatoi lakini ukiwauliza wewe ni mkristo wanasema kuwa wao ndio?
Barikiwa sana                                                                                                                                                                Na Henry Nicholaus

OMBA NA RUHUSU MUNGU AONEKANE KUPITIA NAFASI AU KITU ULICHONACHO

Tumekuja duniani kwa mpango wa Bwana na tutaondoka vilevile. Na kwa kuwa ni mashauri yake, Mungu aliaamua kuwekeza kwetu muda, vitu na nafasi tulizonazo. Hivyo ni muhimu ukajua pia kati ya hivi vyote si kila mtu ana vyote? Ni vyema ukahakikisha unatumia turufu yako vizuri. Hivyo basi katika uwekezaji alioufanya Mungu ni muhimu ukajitahidi kuhakikisha unaleta tija kwake na ndio maana tunajifunza somo hili.

Tunaposoma Mt 14:15-21 tunaona habari za Bwana Yesu akiwalisha watu zaidi ya elfu tano kwa mikate mitano na samaki wawili tu. Kabla ya yote yatupasa kutambua kwamba kuna uhusiano mkubwa kati ya Mungu na mwanadamu hasa katika utendaji kazi. Mungu humtumia mwanadamu pia kuweza kudhihirisha nguvu zake na ukuu wake lakini wakati mwingine ni lazima pia tumruhusu Mungu ili aweze kujidhihirisha kwetu na kwa wengine pia.

Mambo yafuatayo ambayo yote tunayapata katika mistari hiyo hapo juu ni muhimu kuyazingatia ili Mungu aweze kuonekana:


1. KUWA NA FARAGHA NA MUNGU (SPEND TIME WITH GOD);
Ukianza mstari wa 13 mpaka wa 14 katika Mathayo sura ile ya 14 utaona kuwa baada ya kusikia hayo(habari za kuuwawa Yohana mbatizaji) alikwenda faragha(kuongea na Mungu-kuomba). Je mimi na wewe tuna faragha na Mungu? Faragha na Mungu inatusaidia kupata maelekezo ya kuishi na matumizi ya vitu au nafasi tulizonazo. Unakuta watu wengi wanapata shida sana katika ajira na bila kupata majibu kwa kuwa hawana muda wa kuwa faragha na Mungu.


2.MAONO (VISION);
Wanafunzi walipoona muda umeenda walimfuata Yesu nakuongea kuhusu watu kula na kulala badae; waliona mbali. Je unayo maono kwa ajili ya maisha yako na Mungu pia? Mt 14:15. Ni jambo baya kuishi bila maaono. Kama huna maono huwezi kubadilika au kuongezeka. Maono ndio huweka bidii ndani ya mtu ya kusoma, kufanya kazi au kushindana. Kinachomfanya mwanariadha aongeze spidi wakati wa mashindano ni mtazamo alionao juu ya ushindi. Hebu fikiri kungekuwa na mashindano bila ushindi ni kitu gani kinatokea?


3.IMANI (FAITH);
Kumbuka wanafunzi wa Yesu walimfuata Yesu kumweleza awaruhusu watu waende kutafuta chakula. Kwa lugha nyepesi ni kwamba sisi hatuna chakula cha kuwapa. Lakini Yesu anawaambia wanafunzi wawape wao chakula kwakua aliamini inawekana kwa imani, kumbuka imani ni kuona kile usichokiona Mt 14:15-16. Yesu alitaka wajue wasitegemee uhalisia kila wakati maana kuwa sehemu nyingine hauwezi kuwa msaada kwao. Alitaka wajifunze pia matumizi hai ya imani. Na sio kwenye nyakati mbaya tu hata nzuri pia. Je unayo imani dhabiti inayomruhusu Mungu aonekane?
 
4.TUMIA ULICHONACHO (USE WHAT YOU HAVE);
Mikate mitano na samaki wawili vilionekana kidogo kwa wanafunzi lakini mbele za Mungu vilikua vingi Mt 14:17-18. Kidogo ulichonacho unaweza kukitumia na Mungu akaonekana, kumbuka hata Musa alikuwa na fimbo tu mkononi lakini Mungu alionekana katika bahari ile ya shamu. Unakuta mtu anamtaji mdogo lakini badala ya kufikiria katika kidogo hicho afanye nini? Anapanga mkakati juu ya mtaji ambao hanao. Na ndio maana wengi hawaendelei wanakuwa wakisubiri mtaji mkubwa uje. Na matokeo yake wanaungojea lakini hauji. Hii ni dhana mbaya sana.
5.SHUKRANI (THANKS GIVING);
Kumshukuru Mungu kwa kidogo ulichonacho hufungua milango ya Mungu kuonekana kwa vikubwa pia. Yesu alichukua mikate mitano na samaki wawili akaibariki na kushukuru kisha muujiza ulitendeka. Kumbuka kushukuru Mungu iwe ni katika masomo yako au kazi yako. Maana kuna mtu kakesha kusoma usiku lakini hakufaulu kuliko wewe ambaye hukukesha. Pia kuna mwingine anafanya kazi mpaka usiku lakini bado hapati kama unavyopata wewe. Usifikiri ni nguvu zako lakini unapotambua ni neema hutaacha kumshukuru Mungu. Je unamshukuru Mungu kwa ulichonacho?
6.TATHMINI (SELF EVALUATION);
Bwana Yesu aliwauliza wanafunzi wake
  watu wanasema mimi ni nani? Wakamwambia wengine husema Yohana mbatizaji,wengine nabii yule n.k. Yesu alikuwa akijifanyia tathmini. Baada ya watu kula na kushiba walihesabiwa wanaume pale wakawa elfu tano na makombo vikapu 12, hiyo ilikuwa tathmini! Je una tabia ya kufanya tathimini juu ya kazi au masomo yako. Tathimini inatusaidia kujua ni wapi tulikwama na ni wapi tumeongezeka, na kama tumekwama tufanye nini? Na kama tumekwama tufanye nini. Tathimini ndio inayofanya kile kinachofanywa kiendelee licha ya changamoto. Je unayo nafasi ya kujifanyia tathmini mbele za Mungu ili kudhihirisha nguvu zake?

Mungu atusaidie katika kumdhihirisha yeye kwa nafasi na vitu alivyotupa!

NI MUHIMU UKAWA NA TABIA YA KUSHIRIKIANA NA WATU WENGINE

Swala ushirikiano katika nchi zetu za Afrika limekuwa tatizo sana. Na limekuwa likisababisha matatizo mengi mno. Unaweza kuona mtu anafedha nyingi lakini hawezi kutafuta watu wakushirikiana naye ili awekeze pesa zake. Wengi huamini katika ubinafsi ambao umekuwa tatizo na ndio unaoongoza umaskini. Hali ilipofika jambo hili limekuwa utamaduni hata ukioa unaambiwa usimwamini kila kitu mke wako. Na baadae unakuta mtu anaishi na mkewe asijue hata akaunti za mumewe. Nimeona niseme kidogo ili uelewe kuwa jambo hili ni hatari kwa sasa maana linatishia vizazi vinavyokuja.
Kut 18:13-26 inasema " Asubuhi yake Musa akaketi ili awapishie hukumu watu; na hao watu wakasimama kumzunguka Musa tangu asubuhi hata jioni. Mkwewe Musa alipoyaona yote aliyowafanyia watu, akasema, Ni jambo gani hili uwatendealo hao watu? Kwani wewe kuketi hapo peke yako, na watu wote kusimama kwako tangu asubuhi hata jioni?Musa akamwambia mkwewe, Ni kwa sababu watu hunijilia mimi wapate kumwuliza Mungu;wakiwa na neno, hunijilia; nami naamua kati ya mtu na mwenziwe, nami nawajuvisha amri za Mungu, na sheria zake. Mkwewe Musa akamwambia, Jambo hili ufanyalo si jema. Huna budi utadhoofika wewe, na hawa watu walio pamoja nawe pia; maana jambo hili ni zito mno kwako; huwezi wewe kulitenda peke yako. Sikiza sasa neno langu, nitakupa shauri, na Mungu na awe pamoja nawe; uwe wewe kwa ajili ya watu mbele ya Mungu, nawe umletee Mungu maneno yao; nawe utawafundisha zile amri na sheria, nawe utawaonyesha njia ambayo inawapasa kuiendea, na kazi ambayo inawapasa kuifanya. Zaidi ya hayo utajipatia katika watu hawa watu walio na uwezo, wenye kumcha Mungu, watu wa kweli, wenye kuchukia mapato ya udhalimu; ukawaweka juu yao, wawe wakuu wa maelfu, na wakuu wa mia, na wakuu wa hamsini, na wakuu wa kumi; nao wawaamue watu hawa sikuzote; kisha, kila neno lililo kubwa watakuletea wewe, lakini kila neno dogo wataliamua wenyewe; basi kwako wewe mwenyewe utapata nafasi zaidi, nao watauchukua huo mzigo pamoja nawe. Kwamba utafanya jambo hili, na Mungu akikuagiza hivyo, basi utaweza kusimama wewe, na watu hawa wote nao watakwenda mahali pao kwa amani. Basi Musa akasikiza neno la mkwewe, akayafanya yote aliyokuwa amemwambia. Musa akawachagua watu wenye uwezo katika Israeli yote, akawaweka wawe vichwa juu ya watu, wakuu wa maelfu, na wakuu wa mia, na wakuu wa hamsini, na wakuu wa kumi. Nao wakawaamua watu sikuzote; mashauri magumu wakamletea Musa, lakini kila neno dogo wakaliamua wenyewe. Kisha Musa akaagana na mkwewe; naye akaenda zake, mpaka nchi yake mwenyewe."
Natamani uone kupitia hilo somo apo juu. Musa ni nabii lakini alipokea ushauri toka kwa Mkwewe Yethro ili kuimarisha huduma Mungu aliompa. Mungu katika mambo aliyofanya unayotakiwa kuelewa ni kwamba hakutukamilisha ili tutegemeane. Maana kama angetukamilisha kuna watu wangeona duniani si mahali pa kuishi. Lakini maisha yaendelee ametuweka katika mgawanyiko huo. Ndio maana si kila ni mwalimu au fundi utakuta mtu aweza kuwa na fani 2 au 3 lakini hawezi kujua zote.
Hivyo basi kama unaelewa hili ndio utajua kuna umuhimu wa kiasi gani wa kuwa na mashirikiano na watu wengine. Tuache kuwa wa binafsi maana tulivyokuja duniani hatukua na kitu hata hivyo hatuwezi kuondoka na kitu pia. Kuna watu wanapesa lakini hawana mawazo ni muhimu wakashirikiana na wenye mawazo. Bila kufanya hivyo hatuwezi kuendelea.
Ili maendeleo yaje ni muhimu watu wakapenda changamoto. Usiogope changamoto. Magari na ndege unazoziona zilikuja kwa sababu ya changamoto ya usafiri. Changamoto zinatufanya tuwe na uwezo wa kutosha wa kufikiria. Usipokuwa na changamoto huwezi kufikiri na ndio maana unaposoma kitu kuna mitihani. Mitihani inawafanya watu waongeze ufahamu wao kwa kuwafanya waje na mawazo mapya.
Nini athari yake unapokosa kupenda kushirikiana na wengine?
Kitu kimoja wapo ni uwezo wa mtu kufikiria kudumaa. Pia kama una familia ni kuisababishia matatizo. Maana wakati wa kuishi kwako mambo mengi ulikuwa unayajua wewe tu. Na kwa sababu hiyo unakuta familia nyingi za kitajiri akifa baba yao huwa nao utajiri wao unakufa kwani hawakuwa wanajua namna ya kuendeleza vilivyoachwa maana walivyokuwa navyo iwe ni miradi au kampuni ilikuwa siri ya baba yao. Na kwa kuwa ameondoka imeendelea kuwa siri. Wengi wanangoja kusema dakika za mwisho wasijue kuwa hata hizo dakika zinaweza zisiwepo kwao. Kwa sababu hii watoto wa mitaani wameongezeka na yatima. Lakini ni kweli hao watoto walikuwa na wazazi wao.
Ndugu mpendwa unaye nifuatilia Mungu anapenda kuliweka jambo hili bayana kwako ili usipatwe na matatizo baadae. Na pia kama ni mhanga ubadilike ili watu waishi kukumbuka kwa mema na si mabaya. Nimeliona na kujifunza kwa Yesu Kristo na hata watu wengine duniani kama Mwl Nyerere.
Barikiwa                                                                                                                                                             
Na Henry Nicholaus

KANUNI ZA KUWEZA KUUSHINDA ULIMWENGU
1 Yohana 5:4-5 '' Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na MUNGU huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu. Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba YESU ni Mwana wa MUNGU? '' -Utashinda ya dunia kwanza kwa wewe kuhama kutoka kwenye kutawaliwa na dunia na kuingia katika ufalme wa MUNGU kwa kumpokea YESU KRISTO. Kwa kuwa dunia imejaa mambo ya kutamanika mno. Je Tunashindaje? Hapa nimekuandalia njia 10 za kukusaidia kushinda dhambi na mambo ya dunia.
1. Tunashinda Ulimwengu Kwa Maombi Ya Imani Kupitia Jina La YESU KRISTO. Marko 14:38 '' Kesheni mwombe, msije mkaingia majaribuni, roho i radhi ila mwili ni dhaifu.'' -Maombi ni maisha na maombi ni mkono mrefu wa kupokea kutoka kwa MUNGU. ''Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.-1 Yohana 5:14-15''. -Tena maombi ni agizo kwako.Ombeni bila kukoma;- 1 Thesalonike 5:17''
2. Tunashinda Kwa Neno La MUNGU likikaa kwa wingi ndani yetu na tukilitendea kazi neno hilo. Yohana 8:31-32 ''Basi YESU akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.'' -Siku ile BWANA YESU alizungumza na wayahudi lakini leo neno lile lile anazungumza na wewe. Zaburi 119:11 ''Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi'' -Kumbe neno la MUNGU ukiliweka moyoni kwa wingi litakusaidia kutokutenda dhambi.
3. Tunashinda Kwa Kuenenda Na Kuongozwa Kwa ROHO. Warumi 8:5-9 '' Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho. Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya MUNGU, kwa maana haitii sheria ya MUNGU, wala haiwezi kuitii. Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza MUNGU. Lakini ikiwa ROHO wa MUNGU anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na ROHO wa KRISTO, huyo si wake.''
 4. Tunashinda Kwa Kujifunza Neno Na Kulitafakari Neno La MUNGU. Zaburi 119:130''Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, Na kumfahamisha mjinga. '' -Neno la MUNGU lina nuru ndani yake na ukifahamishwa neno la MUNGU itakusaidia kushinda ya dunia na kushinda dhambi. 2 Timotheo 2:15 '' Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na MUNGU, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.'' -Tumia neno la MUNGU kwa uhalali, usililazimishe neno likufuate wewe bali wewe ndio ya kulifuata neno. Usilisahihishe neno bali litii na utashinda dhambi na mambo yote ya dunia. 1 Petro 2:2''Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;'' -Neno la MUNGU ni maziwa safi ya akili yasiyochanganywa na chochote hivyo kunywa maziwa haya kila mara ndipo utasimama imara katika kusudi la MUNGU la uzima na utakaa mbali na kutumikishwa na dunia wala dhambi.
5. Tunashinda Kwa Kuishi Kama Wasafiri Tu Duniani Hivyo Wakati Wowote Tunaondoka. 1 Petro 2:11-12 '' Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho. Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze MUNGU siku ya kujiliwa.'' -Duniani hatujafika ila tuko safarini kwenda kwetu mbinguni. tunatakiwa tuwe tayari muda wote kuchukuliwa. huko ndiko kuna furaha timilifu, huko ndiko tutarukaruka kama ndama kwa furaha, huko ndiko tutafurahi na BWANA YESU aliyetuokoa. Wafilipi 3:20-21 '' Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, BWANA YESU KRISTO; atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake. ''
6. Tunashinda Kwa Kuhudhuria Ibada, semina za Neno la MUNGU au mikutano ya injili na kutii fundisho la Biblia tunalojifunza katika ibadaau mikutano hiyo ya kiroho. Waebrania 10:25 '' wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia. ''
7. Tunashinda Kwa Kujishughurisha Na Mambo Ya MUNGU. Zaburi 2:11-12 ''Mtumikieni BWANA kwa kicho, Shangilieni kwa kutetemeka. Shikeni yaliyo bora asije akafanya hasira, Nanyi mkapotea njiani,Kwa kuwa hasira yake itawaka upesi,Heri wote wanaomkimbilia ''
8. Tunashinda Kwa Kujitenga Na Dunia. 1 Yohana 2:15-17 '' Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda BABA hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na BABA, bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya MUNGU adumu hata milele. ''
9. Tunashinda Kwa Kutokukaa Barazani Pa Wenye Mizaha wala kwenda katika njia ya wakosaji. Zaburi 1:1-2 '' Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku. ''
10. Tunashinda Ulimwengu Kwa Kutokufungwa Nira Moja Na Wasio Mwamini BWANA YESU. 2 Kor 6:14-18 ''Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya KRISTO na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? Tukifungwa nira pamoja nao waweza kutuongoza hata katika miungu mingine kama ilivyokuwa kwa Sulemani.
Barikiwa sana
YATUPASA KUTAZAMA KULE MUNGU ANAKOTUPELEKA NA SIO VINAVYOTUZUIA KWENDA.
Tunaposama Mw 37:5-8 tunaona Yusufu anaoteshwa ndoto na Mungu juu ya maisha yake ya baadae. Na anagundua kuwa atakuja kuwa kiongozi mkubwa baadae.
Lakini haikuwa rahisi yeye kuona ndoto hiyo ikitimia kwani alikutana na vizuilizi mbalimbali ambavyo vilimfanya ashindwe kufikia ndoto yake kirahisi. Moja ya kivuilizi ni pale ambapo nduguze walitaka kumuua kwa sababu ya wivu Mw 37:20 na pili ni pale mke wa Potifa alipomsingizia kuwa ametaka kumbaka hatimaye kufungwa gerezani Mw 39:20.
Kwa matukio haya maawili yalitosha kumaliza kasi aliyo nayo Yusufu ya kuendea ndoto yake. Japo tunajifunza kitu cha tofauti toka kwa Yusufu kuwa mazingira ya vizuilizi si ya kutazama tunapoelekea katika ndoto zetu. Kwani twahitajikutazama kule Mungu anakotuonyesha na sio yale yanayotuzuia kufika kule. Yusufu hakuangalia nini kinamzuia bali aliangalia wapi Mungu anataka yeye afike. Bila hofu Yusufu alikaa katika tumaini akijua iko siku yatatimia.
Kuna mazoea ya watu kupenda kutazama vizuilizi kuliko maono au ndoto alizonazo. Hili ndilo anguko la wengi katika kuelekea ndoto zao. Mfano Mungu alimwambia Lutu atakapokuwa akitoka Sodoma asiangalie nyuma maana atakuwa jiwe la chumvi lakini mkewe akaangalia. Hivyo unakuta tunapenda kutazama visivyo tufaa tukaacha na vyenye kutufaa. Kazia hii ya kuona matatizo ni makubwa kuliko huko tunakoelekea ni mbaya na Yusufu anathibitisha si nzuri hata kwa kuigwa.
Ushindi wa Yusufu juu ya ndoto aliyoateshwa akiwa utotoni. Ulitokana na thana kubwa na kuangalia kule anakokwenda kuliko pale alipokuwa. Kwani aliamini kuwa matatizo au vizuilizi alivyokuwa akikutana navyo vilikuwa si vya kukaa bali ni vya muda tu. Na hii ndio siri ambayo mimi na wewe yatupasa kuitambua ili tuweze kujihakikishia ushindi kila tunapoishi katika maisha haya.
Wakati mwingine vizuilizi huja ili kukuandaa kwa ajili ya maono au ndoto Mungu alizokuonyesha. Ili uweze kufika pale Mungu alipokusudia kwa ajili yako hahitaji vigezo vya kibinadamu kama elimu au uzoefu kukuweka hapo bali anahitaji uwe umefikia vigezo vya rohoni ambavyo Roho Mtakatifu ndiye anayeviandikia ripoti. Unapofanikiwa kukabili vizuili hivyo ndipo Mungu anakupa nafasi ya kuwa mahali husika maana ndiye msemaji wa mwisho mahali popote.
Ndugu mpendwa nikutoe hofu wewe unayetamani kufika mbali. Mazingira ya kukatisha tamaa yapo lakini yasiwe kikwazo kwako bali yawe msaada kwako kwa kukufundisha mambo fulani ambayo yatakuwa msaada kwako kule Mungu anakotaka kukuweka.
Barikiwa sana                                                                                                                                        Na Henry Nicholaus
MAOMBI NI VITA
"Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho" EFE 6:12.
Ndugu yangu, Paulo anatueleza jambo zito sana katika waraka wake huu. Paulo anatufundisha kubeba silaha zote za kupigana na adui ili tuweze kusimama kwa ushindi katika hivi vita. Pamoja na silaha zote anamalizia katika mstari wa kumi na nane kwa kusema kwamba "kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo ".!
Anatuambia kwamba kupigana kwetu huku ni kwa njia ya maombi! Kimahesabu, vita vyetu hivi tunavipiga kwa kutumia maombi. Vita hivi vya kiroho tunavipiga kwa kutumia maombi. Maombi ni silaha kubwa katika vita hivi. Ukiangalia silaha zote ambazo anazitaja (1. Kweli 2. Haki (Maisha safi yenye utii) 3. Utayari ktk huduma 4. Imani 5. Wokovu (Uhakika wa mahusiano ya mtu binafsi na Mungu) 6. Upanga wa Roho ambao Neno la Mungu ) Silaha kuu yenye kubeba silaha zote hivi ni maombi! "kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho".
Ndugu, kila siku unapaswa kukaa mkao wa kivita. Paulo anamuonyesha adui kama mtaalamu wa kupanga vita hivi. Ndio maana Paulo asema katika mstari wa kumi na moja "Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani". Shetani ni mwenye hila kila wakati. Katika kazi zako ataweka hila, katika huduma yako ataweka hila. Katika kanisa lako ataweka hila. Katika uchumi wako ataweka hila. Kila kutaka kwako kumjua Mungu ataweka hila. Basi Paulo asema Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Basi acha kulala mtumishi. Simama tuvipige hivi vita.
Kuna watu wanajiona hawana huduma katika kanisa. Huduma hii ya ukamanda wa maombi nafasi hii inakusubiri. Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache. Chukua hatua. Tumia mbinu zote za kivita vya kiroho tuweze kupambana na adui. Tuungane pamoja katika kuvipiga vita hivi katika jina la Yesu na damu ya mwanakondoo.

JITAKASE ILI USIACHWE CHINI WAKATI HUU. NI HATARI, NI HATARI, NI HATARI KUBWA SANA.!

UNYAKUO sio jambo la mzaha; na dhiki kuu sio jambo la mzaha! Kanisa likinyakuliwa patatokea dhiki kubwa ambayo kamwe haijawahi kutokea tangu kuumbwa kwa ulimwengu (Mathayo 24:21).
Bwana wetu Yesu Kristo anatuambia kwamba:maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo utakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.

Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa;
wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa. Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu. Mathayo 24:37-42.

Jiweke tayari kila wakati
.

UNAHITAJI KUTAMKA MATOKEO KATIKA IMANI ILI YATIME KWAKO
1Sam 17:45-47 tunaona Daudi anasemezeshana na Goliati lakini Daudi akisema naye kwa njia ambayo Goliati asiweze kuelewa kuwa ulikuwa ni ujanja wa Daudi kujitengenezea ushindi kabla ya vita. Daudi alitamka maneno ya ushindi kabla ya kuyaona. Na hii njia ambayo ilimpa haki Daudi kupata ushindi mbele ya adui wake.
Imani ina mambo makubwa mawili.Moja inahitaji kutamkwa na pili inahitaji kuingizwa katika matendo. Ili imani ipate uhai inahitaji mambo hayo mawili yaweze kutimilizwa. Watu wengi wanaamini lakini hawataki kutamka wanachoamini pia wanaogopa kuingiza kazini wanayoamini hususani pale inapokuwa kwamba wachoamini ni kikubwa kuliko uzoefu wao.
Kanuni ya imani iko wazi unapotamka kile unachoamini ndio unatoa nafasi ya uumbaji wa kile kilichopo ndani ya moyo wako au una kitangaza katika ulimwengu wa roho kwa kuwa kile ulichonacho ni roho au unakiumba katika ulimwengu wa roho. Mungu wakati wa uumbaji wake alikuwa akitamka navyo vinatokea. Kwa nini? Ni kwa sababu kwa kutamka aliviumba kwanza kwenye ulimwengu wa roho ambayo ndio asili ya kila kitu. Hivyo usipopenda kutamka matokeo unazuia kuumbika kwa kile unachotarajia kitokee. Daudi anatamka ushindi kabla ya kuuona ndio maana ilimchukua kazi nyepesi kummaliza Goliati.
 Imani inatupa haki ya kupokea yale tunayoyataka kutokea Yn 14:12. Usiishi maisha ya bahati nasibu. Hayo si maisha ya mkristo, maisha ya mkristo ni ya uhakika na imani ndio funguo pekee ambayo yatupatia uhakika wa yale tunayohitaji yatokee kwetu. Kumbuka Mungu ni roho kama alitamka ikawa ina maana hata sisi kwakuwa tu roho pia japo tumeuvaa mwili tukiamini twaweza kutamka kitu nacho kikatokea.
Jambo la msingi ondoa shaka moyoni mwako kwa kuwa hii ndiyo silaha kubwa ya ibilisi. Angalia wana wa Israeli walikuwa na zana zote za kivita lakini walimshindwa Goliati hii ni sababu ya hofu. Angalia Daudi anakuja anakwenda na mawe hii ni imani. Hivyo kati yao tunajifunza kuwa hofu ni kizuizi kikubwa cha matarajio ya wengi kutokea.
Barikiwa sana                                                                                                                                        Na Henry Nicholaus
CHUKIA UMASIKINI, LAKINI WAPENDE MASIKINI. WAELIMISHE NA UWASAIDIE.

UMASIKINI maana yake ni hali ya kukosa maarifa pamoja na kuwa na fikra / mtazamo mbovu akilini mwako! (POVERTY simply means; Lack of knowledge and having bad attitude! The state of having negative mentality).

Umasikini sio hali ya mtu kuwa na kipato chini ya dola moja, wala sio hali ya mtu kukosa mahitaji aliyonayo. Hiyo ni tafasiri mbovu ambayo watu wengi wamefundishwa na kuiweka akilini mwao. Hayo ni matikeo ya umasikini lakini sio maana halisi ya umasikini. Narudia tena:

UMASIKINI ni hali ya kukosa maarifa pamoja na kuwa na fikra / mtazamo mbovu akilini mwako! (POVERTY simply means; Lack of knowledge and having bad attitude! The state of having negative mentality).

Watu wengi ni masikini kwa sababu wanayo BIDII KUBWA katika kuwa masikini! Wanayachukia maarifa; hawapendi kushughulisha akili zao; wanapenda kuomba omba!
Kuna wajinga wengi wanaodhani kuwekewa mikono na mchungaji ndipo watakuwa matajiri; wajinga wengine wanaambiwa panda mbegu utapata dabo dabo! Baraka za Mungu hazipo namna hiyo; bali baraka za Mungu utazipata pale unapokuwa na afya akilini mwako. Kitu cha kwanza unachopaswa kuchughulika nacho ni akili yako; uwe na fikra / mtazamo mzuri akilini mwako. Sikukatazi kutoa changizo kanisani mwako; lakini unatakiwa kuelewa kuwa Mungu leo hanashida ya kukubariki kwa sababu tayari amekwisha kukubariki; Lakini leo Mungu anahitaji uponyaji ufanyike katika akili zako ili neno Lake likae kwa wingi ndani yako na ndipo uweze kuziona, kuzifata, na kuzitumia baraka ambazo tayari amekubariki.

Ninaongea kwa maneno makali lakini ninaamini yanaleta uponyaji katika akili yako. Hakuna utajiri utakaoupata endapo kama hautapata uponyaji katika akili yako; uponyaji huo ni kupata maarifa. Soma vitabu sahihi, jifunze katika mitandao sahihi, sikiliza nyimbo sahihi, tazama vitu sahihi, na ujifunze kwa watu waliofanikiwa; Badiri fikra zako.

Penda maarifa.Watu wengi wanatamani mabadiriko lakini wao wenyewe hawataki kubadirika! Haiwezekani kukokotoa hesabu kwa kanuni iliyoshindwa! Vivyo hivyo hauwezi kupata matokeo tofauti kwa kutumia mbinu ile ile iliyoshindwa! Ukifanya hivyo utafanana na mtu mpumbavu.Mafanikio ya mtu yamo katika fikra na mtazamo wa akili alionao mtu. Mafanikio ya mtu hayapimwi kutokana na vitu aliyonavyo, wala elimu aliyonayo; bali mafanikio ya mtu yanapimwa kutokana na uwezo wake wa kufikiri akilini mwake. Watu wengi akili zao zimekufa japokuwa miili yao inaishi! Wengi wanawaza kusoma sana ili wapate vyeti vitakavyowawezesha kuajiriwa. Ndio, hayo ni mawazo mazuri, lakini sio mawazo mazuri sana. Je, usipopata ajira umejiandaa kufanya nini? Umejiandaa kulaumu serikali au umejiandaa kuwa kibaka! Au umejiandaa kuwa omba omba!

Tumia akili yako vizuri.Ni kweli wasomi ni wengi, ni kweli ajira ni adimu, ni kweli wengi hawana mitaji; lakini tumia akili yako vizuri. Kile unachoomba watu wakusaidie, ujue nao pia wamekitafuta. Jifunze kutafuta sio kuomba omba. Pesa inakuja pale unapoiwekea mtego, mtego mzuri unatokana na fikra pevu za mtegaji. Tambua kwamba: pesa sio thamani bali ni kipimo cha thamani!

Kuna mambo matatu ambayo ni muhimu kuyazingatia; kwa mtu mwenye fikra pevu hupenda kuwa na mambo yafuatayo:

1. Haki ya kuishi.

2. Haki ya kufanya maamuzi sahihi.

3. Afya bora. [Afya ni pamoja na mwili kutokushambuliwa na maradhi wala magonjwa; Akili kuwa na fikra nzuri; pamoja na uwezo wa kifedha!]

Yote hayo utayapata pale unapokuwa na maarifa. Soma vitabu vizuri, na ujifunze kwa waliofanikiwa. Hebu fikiri zaidi ya hapo awali; badili fikra zako. Usipende kuomba omba; jifunze kuwajibika kwenye maisha yako mwenyewe. Kila mtu anawajibika katika kuyabadili maisha yake yeye mwenyewe; iwe kiroho hata kimwili. Hakuna ajira itakayokufanya uwe tajiri, hakuna serikali itakayokufanya uwe tajiri; Hiyo yote ni mifumo tu! HAKUNA MFUMO ULIOTENGENEZWA ILI UKUFANYE WEWE UWE TAJIRI; kila mfumo umewekwa kumnufaisha zaidi yeye aliyeuweka! Kama wewe akili zako zote zinategemea ajira, au serikali ikuletee utajiri; basi elewa wazi umepata ziro katika mafanikio yako!
Hata kama umeajiriwa, hebu waza kuwa na mambo yako mwenyewe. Hebu nikupe siri hii itakusaidia: Dunia ya sasa imetoka katika mfumo wa kuajiriwa, bali imeingia katika mfumo wa Network Marketing! Najua hapo wengi hawajaelewa, narudia tena: Dunia ya sasa imetoka katika mfumo wa kuajiriwa, bali imeingia katika mfumo wa Network Marketing! Narudia tena kwa mara ya tatu ili uelewe vizuri: Dunia ya sasa imetoka katika mfumo wa kuajiriwa, bali imeingia katika mfumo wa Network Marketing!

Sio nia yangu hasa wakati huu kukufundisha what is Network Marketing or Direct Selling, or Personal Franchise, or Mult Level Marketing Business. Ukitaka kuyajua hayo nitafute kwa muda wako; lakini kama kweli unahitaji kufanikiwa; BADILI MTAZAMO NA FIKRA ZA AKILI YAKO.

Tunahitaji uhamsho katika kanisa; akili zilizokufa tunatakiwa tuzifufue. Hebu juilize; utakuwa omba omba mpaka lini? Nani kakwambia umasikini ni kutokana na elimu ndogo au kukosa mtaji! Ukweli ni kwamba; umasikini wa mtu umo katika fikra mbaya alizonazo.

Ongeza maarifa, acha kuomba omba, chukia umasikini lakini wapende masikini; wasaidie na uwaelimishe.Jambo la mwisho ninalopenda kukwambia, ni hili: ONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU. Pasipo Roho Mtakatifu hauwezi kumpendeza Mungu, na pasipo kumpokea Yesu hauwezi kuurithi uzima wa milele. Kila ufanyalo zingatia HAKI na KWELI.
Nimeongea mengi lakini kwa uchache sana; yatakuwa na msaada kwake yeye mwenye hekima na akili. Mungu tayari amekwisha kukubariki, tatizo limo tu kwenye akili yako!
Kumbuka kwamba:UMASIKINI maana yake ni hali ya kukosa maarifa pamoja na kuwa na fikra / mtazamo mbovu akilini mwako! (POVERTY simply means; Lack of knowledge and having bad attitude! The state of having negative mentality).

Nawatakia baraka tele katika jina la Yesu Kristo. Amen.

NAMBA NA MAANA ZAKE KIBIBLIA.
Utanguizi.
Tunapoendelea kujifunza maneno ya Mungu, Leo nimepewa fulsa ya kujadiliana kuhusu Namba ndani ya biblia na maana yake katika maisha yetu ya kimwili na Kiroho hapa Duniani.Namba ndani ya biblia zimewekwa na Mungu na tunatakiwa kuziangalia kwa umakini wake sana ili tuelewe nini Mungu amekusudia tuelewe ndani yake.Tumepewa na Mungu namba hizi tupate kulinganisha na mambo ya rohoni ili tumwelewe katika maisha yetu (1Wakoritho 2:13). Ni muhimu kujua kwa namna gani Mungu anazitumia namba.
Biblia ni kitabu sahihi kabisa hakina makosa wote tunafahamu na yamevuviwa na Mungu (pumzi ya Mungu). Mungu ameweka namba ndani ya biblia kiasi kwamba hata mtoto mdogo wa miaka 6 aweze kuelewa kwa usahihi kabisa kama anavyotaka. Ni kweli Biblia ni kama msitu unaweza potelea huko na usiweze kuelewa lakini kwa msaada wa Roho Mtakatifu tunaweza kuelewa ukweli wote wa biblia (Mk 4:11-12)
Jambo la msingi hapa ni lazima uelewe kwanza kwamba Namba ni maneno (Numbers are words) ndipo utakapo zitumia namba vizuri bila shida kama maneno.Sasa kwa nini kwa nini? Ni kwa ni nadra sana kuona somo hili likifundishwa.Namba zote ndani ya biblia zina maana fulani kwa mfano;
1.      Namba zinaweza kutumika katika kupima muda (Kutoka 12:40)
2.      Namba zinaweza kutumika kuelezea kundi fulani la watu, madhumuni mbalimbali na nk (1petro 3:20).
3.      Namba zinaweza kutumika kupima kitu fulani (Mwanzo 6:15).
4.      Namba zinaweza kutumika kutoa maana ya kawaida (Yohana 21:11) samaki 153 waliovuliwa hawa ni samaki halisi waliovuliwa.
5.      Kwa wakati mwengine namba zinaweza kuwa na maana ya kiroho au alama Fulani yenye kutambulisha kitu fulani.Kwa mfano Petro alimuuliza Yesu ni mara ngapi mtu akikukosea unaweza kumsamehe hata mara saba?(Mathayo 18:21)
Namba ndani ya biblia hazipo kwa bahati bahati tu bali zina makusudio maalumu kuwekwa hapo.Kwa kifupi na tuanze kujadili namba moja moja ina maana gani au ishara gani Kiroho.
Namba 1
Hii ni namba ya Mungu. Mungu ni mmoja ni yeye peke yake hakuna Mungu mwingine.
Namba 2
Namba 2 ni namba ya wale waeneza Neno la Mungu (Wainjilishaji) Kwa mfano Yesu aliwatuma wanafunzi wake 70 “Wawili wawili” (Luka 10:1). Ufunuo 11 tunaona wale Mashaidi 2 waliouwawa na baadaye wakafufuka kutangaza Neno la Mungu. Matendo 13, Paulo na Barnabas walipelekwa pamoja kama Wamisionari wa kwanza kutangaza neno la Mungu. Kwa hiyo namba 2 kama ina maana Kiroho au ina alama fulani basi kwa wale wasambaza neno la Mungu Wainjilisti na watu wengine waoeneza neno la Mungu kwa njia moja au nyingine.
Namba 3
Namba 3 ina maana ya nafsi za Mungu ,hujidhihirisha pale Mungu anapohusika. Mfano: Kumbuka kulikuwa na Misalaba 3 (Mk 15:27) Petro alimkana Bwana Yesu mara 3 (Mk 14:66-72) Mitume 3 walikuwa pamoja na Bwana yesu pale bustani ya gethsemani (Mk 14:33), Bwana Yesu aliomba mara 3 mle Bustanini (Mk 14:32-41), Jina “YESU WA NAZARETH MFALME WA WAYAHUDI” Liliwekwa msalabani kwa lugha 3 (Yn 19;19-20) makundi 3 Makuhani, Viongozi wa dini na waalimu na Wote walitaka Yesu asurubiwe (Mt 26:59) pakiwa na wawili watatu na Mimi Mungu nipo pamoja nao.
Namba 4
Namba 4 inamaanisha dunia nzima (Ulimwengu). Biblia inatabua kwamba kuna pande 4 za dunia Mashariki, Magharibi, Kaskazini na Kusini (zaburi 107:3). Biblia inazungumzia pepo (winds) 4 za dunia (Mathayo24:31) na inatambua kuna pande 4 za dunia (Ezk 7:2). Kwa hiyo kama namba 4 inamaanisha alama yeyote au maana yeyote Kiroho basi inatambulisha Dunia au Ulimwengu kwa ujumla.
Au
Vilevile namba 4 iamaanisha ukamilifu wa jambo linapofikia mwisho kabisa (hitimisho la jambo) kwa mfano Yesu alisubiri mpaka siku 4 Lazaro alipokufa kabla yakufufuliwa (Yohana 1:15-17) Mfalme Jehu aliruhusiwa kutawala kizazi cha 4 (2Wafalme 10:30,13:1,9-10,14:16,2915:8-18) Israeli walikaa utumwani mpaka kizazi cha 4 baada ya kutumikishwa miaka zaidi 400 (Mwanzo15:13-16).Kwa hiyo kwa maana hii Namba 4 vilevile ina maana ya utimilifu wa kitu au mwisho wa kitu ktk muda, kwa kipindi fulani. hata kumaanisha Mwisho wa dunia (2Petro 3:10).
Namba 5
Namba 5 ina maanisha Wokovu au Hukumu.Namba 5 inaweza kuonekana kama 5 50 500 5000 nk. Unaweza kufikiria wale wanawali 5 wapumbavu na 5 wenye busara (Mt 25:1-2)au ushuru wa hekalu ulikuwa shekeli 5 (kutoka 30:13) au wale watu 5000 aliowalishwa chakula Bwana Yesu (Yohana 6:10-13)  nk .kwa hiyo kama namba 5 ni alama au maana fulani ya Kiroho basi ni hiyo yaWokovu au Hukumu.
Namba 6
Kama namba 6 inamaanisha alama au maana yeyote Kiroho kama vile Mpinga Kristo Ufunuo 13:18 ambapo namba 666 imetumika. Pia huweza kumaanisha kazi. Mungu alitumia siku 6 kuumba ulimwengu (kutoka 20:11).
Namaba 7
Namba 7 inatumika sana kwenye biblia katika maana ya Ukamilifu wa Kimungu (Completed cycle) (siku7, miaka7) kama kusamehe ni 70x7times maana yake kusamehe hakuna mwisho samehe samehe samehe……Vile vile namba hii 7 inatabulika kama na namba ya Mungu. Ukiomba kitu chochote katka Mungu mara 7 hakika Mungu atakupa jibu.(Tatizo letu tunamchagulia Mungu majibu, Majibu mengine hatutaki na tunaendelea kuomba kwa hasara).Kwa mfano Ukuta wa babeli ulidondoka baada waisrael kusunguka mara 6 na mara 7 ukuta kukadondoka.Naamani aliambiwa akajichofye mara saba na baada ya hapo ukoma ukapona kabisa.
Namba 10
Namba 10 ni sawa na namba 1 inaweza kuwa 10, 100, 1000, 10000…. Nk. Namba 10 ina maanisha ukamilifu kamili. Biblia inasema kuhusu sarafu 10 (luka 15:8), Kondoo 100 (luka 15:4) miaka 1,000 (2Petro 3:8), Vizazi 1000 (Kumb.7:9) etc. Kwa hiyo kama namba 10 ni alama ya jambo fulani au ina maana fulani kiroho basi ni ukamilifu.
Namba 11
Namba 11 inatumika katika biblia inamaanisha mapungufu katika usahihihi (defective fullness). Kwa mfano kulikuwa na makabila 12 (lakini halisi ni 13) ya waisraeli, lakini Daudi alipofanya sensa Mungu alizungumzia Makabila 11 (1wafalme 11:31-32).Wakati Yuda aliyekuwa mmoja kati ya Wanafunzi wa Yesu 12 (Yohana 6:70-71) alijiua baada ya kumsaliti Yesu, Walibakia Wanafunzi 11, Baadaye alichaguliwa Mtume mwingine kuchukua nafasi yake na kuwa 12 tena (Matendao 1-13-26).
Namba 12
Kama namba 12 ni alama au ina maana yeyote kiroho basi ni utimilifu katika muonekano Kwa mfano kulikuwa na Makabila 12 na Mitume 12, Mji mtakatifu una urefu wa 12000 mara 12000 mara 12000 (Ufunuo 21-16)nk. Kwa hiyo kama namba 12 ina maanisha alama au ina maana Kiroho basi ni utimilifu katika muonekano. Namba 7,10,12 zote zinafanana kila moja kama utimilifu wa kiroho isipokuwa ikiambatanishwa na namba zingine kama 2×6,2x2x3 nk..
Namba 13
Namba 13 kama ina maanisha alama au maana fulani ya Kiroho basi ni Hakika ya Utimilifu. Biblia inazungumzia Mitume 12, Lakini hakika kabisa ni 13. Wa 13 ni Mtume Paulo aliposisitiza akiwa katika katika roho Mtakatifu kuwa amekidhi matakwa/Vigezo vyote vya kuwa Mtume kama wale 12.(1Wakoritho9:2;15:8-9; 2Wakoritho12:11-12) Biblia kwa kawaida kabisa inasungumzia Makabila 12 ya Israel lakini Uhakika na kimsingi Yalikuwa Makabila 13(Mwanzo 49:1-28;Hesabu 32:33;Joshua 16 na Joshua 17) Namba 13 ina maanisha Uhakika wa Ukamilifu.
Namba 17
Inaonekana sehemu nyingi katika biblia ikisimama kwa maana ya Mbingu/uungu (Heaven) Kwa mfano katika miaka 17 ya mwisho ya maisha yake Yakobo chini ya Yusufu ambaye ni mtoto wake kipenzi ambaye alisalitiwa kama alivyosalitiwa Yesu wakati alipotumika badala ya Mungu kuwaokoa na njaa kali (Mwanzo 47:28) Yeremia alininunua shekeli 17 kuwanunulia wana wa israel kipande cha ardhi kuonyesha kwamba Mungu amewarudisha tena kwenye nchi yao.Kipande kile kilikuwa kinamaanisha Ufalme wa Mungu umewarudia tena (Yeremia 32:9) Kwa hiyo namba 17 kama ina alama au maana ya Kiroho ni mbingu/ Uungu (heaven).
Namba 37
Inamaanisha Hukumu ya Mungu.Nuhu alikuwa kwenye Safina kwa muda wa siku 370 wakati mungu alipo hukumu dunia(Mwanzo 7:11;8:14-18).Jeshi la Sennacherib liliangamizwa na Mungu kwa usiku mmoja watu 185,000 (2Wafalme 19:35) 185,000 = 5x37x1,000. Namba 666, ambayo ni namba inamaanisha watu wasiookoka wali chini ya hukumu ya Mungu (Ufunuo 13:18) kama namba hiyo ukiivunja vunja katika namba ndogondogo ni 3x6x37.Kwa hiyo Namba 37 kama ina alama au maana yeyote Kiroho basi ni Hukumu..
Namba 40
Namba 40 inajirudiarudia katika biblia ikimaanisha Mwisho wa majaribu/Majaribu.Musa alikaa siku 40 katika Mlima Sinai (Kutoka 24:18), Huku nyuma Wana wa Islael walijaribiwa na kushindwa kuvumilia na kutengeneza miungu yao (Kutoka 32:1-4).Israel walikuwa Jangwani kwa kipindi cha miaka 40 walishindwa na hakuna aliyeokolewa wote hawakufika Kanani isipokuwa watoto wao amabao waliozaliwa baada ya kutoka Misri. (Waebrania 3:17).Yesu alijaribiwa na shetani siku 40 mchana na usiku (Mathayo 4-1-2:Luka 4:1-2) pamoja na majaribu hayo tunamshukuru Mungu kwamba Yesu hakushindwa alimshinda shetani (Mathayo 4:3-11;Luka 4-3-14) Kwa hiyo kama namba 40 inamaanisha alama au maana yeyote Kiroho basi ni Majaribu. Fikiria watu wengi wakifikia umri wa miaka 40 shida na masumbufu huwa yanakwisha na hili kila mtu anaweza kujichunguza au kuchunguza hata kama maisha ya mtu huyo ni ya kimasikini lakini amani na utulivu unakuwepo katika maisha yake( Focus on Future destenity) Utu uzima ni miaka 40. Chunguza 40 zinavyotumika katika maisha na kwa jamii kwa ujumla hizo ni maana za kiroho kumbuka!
Namba 43
Namba 43 ina maana ya Hukumu au Wokovu.Kwa mfano Israel walikaa Misri kwa miaka 430.Mwisho wa miaka hiyo 430 hHukumu ilishuka kwa Wamisri na Uhuru Wokovu kwa kwa Israel). Kwa hiyo namba 43 kama inamanisha alama au maana Kiroho basi ni Hukumu au Wokovu.
Ndugu mpendwa Mungu akubariki na tilia maanani somo hili litakusaidia na wakati mwingine kukuonyesha njia. Unaweza patwa na shida au jambo Kumbuka Mungu anazungumza kupitia Namba. Kwa nini 3 kwa nini 7,2,5,10 nk..Mungu anapozungumza na wewe anaweza kukuonyesha ishara mbalimbali za namba kati jambo fulani katika maisha yako kiroho. Vilevile kumbuka si kila namba ina maana ya kiroho.
Kuna baadhi ya dini na madhehebu huwa wana utaratibu wa kuhesabu hesabu vitu Fulani kama ushanga na nk hata kwa wachawi na waganga huwa wanahesabu hesabu kwa namna Fulani ili kupata namba na maana zake kwenye mambo yao ya kichawi. Nimekwambia hayo ili uweze kujua kwamba katika namba kuna siri kubwa kiroho kwetu sisi tulio okoka na kwa wale wasio mwamini Bwana Yesu.

JE UNA MSAADA GANI KATIKA UJENZI WA KANISA LA KRISTO
Katika ijili ya Mt 28:18-20 tunaona Yesu akiwapa agizo wanafunzi wake pamoja na wote wa waliokuwa wakimfuatilia kuwa waende ulimwenguni mwote na kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi. Nataka uelewe kuwa Yesu alipokuwa akitoa agizo hili hakunyoshea kundi fulani kidole juu ya mataifa bali juu ya kila aliyeamini katika yeye.
Hivyo kwa kipindi ambacho tumepewa duniani ni majaribu kwa kuwa tunahitajika turudishe matunda kwa mwenye shamba. Mimi na wewe tu wapangaji tu katika shamba ambalo tupo hapo kwa kitambo hivyo basi unapowadihi muda wa mavuno basi Bwana wa shamba atapenda kuona kile tulichozalisha.
Vijana wengi tunakula na kulala tukisahau kuwa tunajukumu la kuhakikisha kwamba vizazi vijavyo havikosi fursa ya kukutana na Yesu. Ikumbukwe kuwa wanafunzi wa Yesu walifanya kazi ya ziada ndio maana leo mimi na wewe tuna majina ya kikristo tena tumeokoka. Hii ni kazi iliyofanywa na wenzetu ambao hawakuwa wabinafsi bali wenye kutupenda sisi kizazi tujacho hapo baada sana kama unabisha juu ya hili Paulo peke yake ameandika nyaraka kumi na tatu. Na si tu hivyo alifanya uinjilisti mpaka Arabuni. Mimi na wewe mbona twalala.
Mbinguni tukifika hatutaulizwa tulivuna mali kiasi gani au tulisoma mpaka kiwango gani? Ila tutaulizwa katika mali tulizovuna au elimu tulioipata kwa kiasi gani ilikuwa msaada katika kuujenga mwili wa Kristo katika muda wa uhai wetu duniani. Ndio maana nimeandika leo kukumbusha wewe kama umesahau juu ya jukumu tulionalo hapa dunia. Maana tusije tukanogewa na maisha tukasahau wajibu.
Petro na Yohana walipokuwa wakienda hekaluni walikutana na mtu kiwete toka kuzaliwa. Huyu alikuwa akikaa langoni hapo akiomba sadaka na wengi yamkini walikuwa wakimpa lakini hakupata suluhisho la kudumu. Lakini Petro na Yohana walimwambia kuwa sisi hatuna cha kukupa ila tulichonacho ndio tukupacho, “Kwa Jina la Yesu wa Nazarethi simama uende” Mdo 3:1-6. Hivyo utaona Petro na Yohana walisimama kwenye zamu zao kwa ajili ya kuujenga mwili wa Kristo. Maana unaweza ukaangalia kwa jicho moja ukaona uponyaji tu ndio walichokifanya lakini walifanya vitu vingi kwa jambo moja la matumizi ya Imani kwa vitendo.
Ngoja nikuonyeshe kidogo ni uone kwa namna gani wamefanya vitu vingi hali walimponya yule kijana. Kwanza waliongeza Imani ya yule kiwete kwa kiwango kikubwa kwa kuwa alikuwa mlemavu kwa muda mrefu sana. Pia kwa wale ambao walikuwa wakimpa sadaka pale katika lango la kanisa kwa kuona matendo makuu ya Mungu kuwa, hakuna linalomshinda. Pia inawezekana kupitia uponyaji ule wako waliomjua toka udogo na hali yake ilivyo hapo awali na ambao hawakuwa wameokoka inawezekana nao walimpokea Yesu kwa sababu ya ushuda waliouona.
Hivyo ni muhimu sana ukatumia nafasi yako. Naomba nitoe angalizo kidogo. Kuna watu wanashindwa kutumika kwa ajili ya Kristo kwa kigezo kuwa Fulani yupo. Hiyo ni dhana potofu maana watenda kazi katika shamba la Bwana hawakutokea kujaa. Hivyo ni vyema ukalitambua hilo litakusaidia kusimama kwako. Vile vile kuna wengine wana karama tofauti na kufundisha wanajiona kuwa wao si sehemu ya watenda kazi wa shamba la Mungu. Kumbuka karama si kufundisha tu. Hata hivyo wako wengine wenye vipawa mbalimbali kama kuchekesha wanashindwa kutumia kuujenga mwili wa Kristo kwa kigezo kuwa hakiendani na kanisa si kweli. Natamani ufahamu kuwa vile ulivyo ndivyo atakavyo kukutumia.
Barikiwa sana
Na Henry Nicholaus
JIFUNZE KUJIZOESHA KUSOMA NENO LA MUNGU BINAFSI
Watu wengi hawana muda wa kutosha kujifunza neno la Mungu binafsi kwa kuwa wanangoja tu Jumapili na kisha hadi Jumapili nyingine. Bado hakuna mazoea ya wao binafsi kujituma katika kujifunza neno la Mungu. Duniani ni mwendelezo wa utawala wa Mungu hivyo licha ya kwamba watu wake wapo katika mwili na damu bado wanahitajika kuishi katika taratibu za mbinguni kwa kuwa ni mwendelezo wake katika mwili.
Unaposoma 1Kor 2:12 inasema "Lakini hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliokirimiwa na Mungu." Mungu ameumba dunia ili apate kutushirikisha pendo lake tukiwa dunia. Na ndio sababu alimleta Yesu Yn 3:16 na Roho Mtakatifu kwetu. Hii ni kutuonyesha kuwa japo tupo duniani bado twatakiwa kuishi kama mbinguni.
Sasa swali unaloweza kujiuliza kwa nini tujizoeshe kusoma neno la Mungu. Jibu ni jepesi ili tuweze kujua yale tuliokirimiwa. Nikufikirishe jambo. Fikiri umewekwa kuwa meneja wa kampuni lakini hujui madaraka au majukumu yako nini kitatokea? Moja unaweza kufanya kazi lakini usiletee kampuni faida, pili unaweza kushindwa kusimamia walio chini kwa kuwa hujui namna ya kuwamudu na tatu unaweza kupoteza ajira yako. Hivyo Mungu amemleta Roho wake ili atupe kujua ni kwa namna gani tunaweza kusimama katika nafasi zetu.
Mungu ametupa nafasi ya kutawala duniani Mw 1:28. Fikiri unatawala katika kampuni ya mtu lazima upate maelekezo yake ili ufanye katika yale yalio katika dhamira yake ya kuanzisha kampuni ili kampuni ifanikiwe. Bila hivyo kinachoweza kutokea ni anguko la kampuni. Kwa kuwa dunia ni mwendelezo wa utawala wa Mungu hatuwezi kutawala kwa fahamu zetu isipokuwa za Mungu kwa sababu Yeye alikuwa na mahesabu kamili juu ya dunia. Hata hivyo kutusaidia tuishi kwa mafanikio tukiwa huku duniani. Na ndio maana baada ya kuumba dunia alimpa Adamu maelekezo ya kuishi japo aliyavunja baadae.
Msukumo nilionao juu ya hili somo ni Roho Mtakatifu akupe kuelewa kuwa kila iitwapo leo kuna vitu katika maisha unapaswa kujua ili uweze kushinda dunia. Mfano Yesu alijua kuwa neno la Mungu ndio limpalo mtu kuishi ndio maana aliweza kushinda jaribu Mt 4:4 kama asingejua angeshindwa na ndio maana ni muhimu kwa mtu kufahamu neno la Mungu. Sababu jaribu alilopata Yesu halikumpa muda mrefu wa yeye kumuuliza mtu nini cha kufanya bali alihitajika kutumia muda mfupi uliopo kuvuka. Hivyo usipokuwa na hazina ya neno la Mungu ndani yako ni ngumu kustahimili hivyo vipindi.
Pia 2Fal 17:24-28 inatueleza wazi juu ya umuhimu wa mtu kujizoesha kusoma na kutafakari neno la Mungu. Maana neno la Mungu ni sheria ya Mungu. Wao watu toka makabila mbalimbali walioletwa na mfalme wa Ashuru katika Samaria hawakujua kama Israeli hawakuondoka na Mungu wao, matokeo yake wakaanza kutumikia taratibu za miungu ya kwao katika eneo ambalo Mungu wa Israeli amelikalisha jina lake. Hivyo kusababisha hasira na Mungu na kuleta simba ambaye aliwaua. Nataka nikutazamishe jambo kutokujua kwako neno la Mungu hakutazuia ghadhabu ya Mungu juu yako kama ukitembea kinyume na taratibu zake Hos 4:6.
Hivyo ni vyema ukazidi kumtafuta Mungu na kufahamu jinsi gani ya kuishi katika mpango ulio wake ili ujinusuru na jambo hili. Si kila matatizo unayoyaona katika maisha yako ni majaribu mengi ni adhabu za zitokanazo na kutojua sheria ya Bwana. Neno la Mungu linasema tafuteni ufalme wa mbinguni na haki yake na yote mtazidishiwa.
Barikiwa sana                                                                                                                                         Na Henry Nicholaus
MUNGU HAJIBU MAOMBI YETU KUTOKANA NA SHIDA TULIZONAZO BALI KUTOKANA NA IMANI ZETU
"Ndipo alipowagusa macho, akasema, kwa kadiri ya imani yenu mpate" Mt 9:29
Leo ndugu mpendwa unayenifutilia kwa karibu kipo kitu ambacho Mungu anataka kukushirikisha. Ukweli ni kwamba watu wengi wanaomba na wachache wanapokea majibu. Swali linakuja nini sababu ya haya? Tunapojifunza kile Mungu anataka tujue siku ya leo tunaelewa kuwa ukosefu wa imani wakati watu wengi waombapo imekuwa ni tatizo kubwa kwao. Ni kweli Mungu hatupi majibu kwa sababu tuna matatizo makubwa bali tumefuata utaratibu wa kujibiwa na utaratibu huo huitwa imani.
Tunapotazama mstari unaotuongoza Yesu aliwaambia hao vipofu kuwa kwa kadiri ya imani yenu mpate na sio kwa kadiri ya shida yenu. Hii inatutazamisha nini? Hii inatuonyesha wazi kuwa Mungu huitazama imani iliyobeba maombi ya mtu pale aombapo. Imani ni nni? Kwa sababu linaweza kuwa swali ambalo waweza kujiuliza. Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasiyoonekana Ebr 11:1. Hivyo imani ni uhakika ya kuwa yale unayoomba utapata. Mungu anatumia ustarabu huu kwa madhumuni kabisa kwa kuwa Yeye ni roho hivyo unavyotaka kumwendea lazima uje uhakika ya uwepo wake na tena anauwezo wa kukupa hitaji lako.
Mt 8:13 pia inaendelea kuonyesha kuwa imani ni ya msingi katika kuhakikisha unapata majibu ya maombi yako kutoka kwa Mungu. " Naye Yesu akamwambia yule akida, Nenda zako; na iwe kwako kama ulivyoamini. Mtumishi wake akapona saa ile ile". Unapotazama kwa jicho la ndani utagundua Yesu na yule akida walianza mazungumzo muda mrefu lakini mtumishi wake hakuwa amepona isipokuwa alipomwambia "Na iwe kwako kama ulivyoamini". Hii inazidi kutufikirisha kwa namna gani Mungu anatazama imani katika kuleta majibu ya maombi ya watu.
Nataka kukuulize swali kidogo je unadhani Mungu haoni watu wanakufa kwenye vyumba vya ICU na inawezekana wengine waliishi vibaya na Mungu anajua sio wake wanakwenda motoni. Je kwa nini asiwaponye warudi duniani watengeneze kwanza kisha awaruhusu waondoke. Hii utajipatia jibu la wazi kuwa bila imani hakuna kinachowezekana. Na sema na wewe unayetafuta ajira, unayetaka kuolewa/ kuoa, unayeumwa au unayepitia majaribu mengi. Msingi wa kujibiwa kwako uko kwenye imani yako. Sikatai kuwa ziko sababu nyingine zinazoweza kusababisha Mungu asikujibu lakini nimetumia neno 'msing' litazame vizuri.
Pia unaweza kunielewa vizuri ni kitu gani kilimfanya Yesu amwambie yule mnyang'anyi mmoja kuwa atakuwa pamoja naye pepo. Utagundua aliamini kuwa Yesu hakustahili kutendewa ubaya. Hivyo basi imani inaweza kukuokoa hata dakika za mwisho pasipo kujua. Hivyo ndugu mpendwa jitahidi sana kujenga imani binafsi kwa kila jambo ikiwapo wakati uombapo ili upate matokeo sahihi ya maombi yako.
Barikiwa sana                                                                                                                                        Na Henry Nicholaus
DALILI ZINAZOWEZA KUKUJULISHA KUWA UMEVAMIWA NA NGUVU ZA GIZA
Mara nyingi watu wengi wamekuwa wakiteseka na wasijue chanzo cha mateso yao. Unaweza kumwona mtu amekata tamaa kabisa kiasi asijue nini cha kufanya maana anaona mambo hayaendi. Lakini leo Mungu ametaka tuweze kujadiliana kwa pamoja tujue ni kitu gani kinasababisha haya kutokea.
Nyuma ya kila jambo lisilo baya uwe na uhakika kuna nguvu za giza zinazoshiriki. Wakati mwingine huwa ni ngumu kwa wengine kuelewa maana watu wengi hufikiri nguvu za giza ni uchawi na uganga tu. Kama ilivyo kwa nguvu za nuru, nguvu za giza ni mtandao mpana uliochini ya shetani unaoratibu mambo kinyume na mapenzi ya Mungu. Mfano: Magonjwa, ajali, hasara nk. Zifuatazo ni dalili zinazoweza kukujulisha kuwa umevamiwa na nguvu za giza.
·         Kujihisi wewe si kitu au huna thamani
Tunaposoma katika kitabu cha Isaya 43:3-4 tunaona Mungu akitueleza kuwa sisi ni watu wa thamani tena ametuheshimu. Ni vema ukatambua kuwa licha ya jinsi unavyojiona Mungu anakuona tofauti. Naye amesema wazi wewe ni wa thamani, sasa iweje leo aliyekuumba anakuona wa thamani lakini wewe unajiona hufai. Lazima uwe na uhakika kuna kitu kinakupofusha juu ya mtazamo sahihi katika maisha yako.
·         Kutojisikia kuomba
Mt 26:41 inasema, "Kesheni mwombe isiingie majaribuni, roho i radhi lakini mwili ni  dhaifu". Unapoona kuwa huwezi kuomba au hujisikii kuomba uwe na uhakika nguvu za giza zimekukamata. Hii ina maana kuwa hizo nguvu zinazuia mashambulizi unayoweza kufanya pindi unapokuwa unaaomba. Kwa sababu shetani anajua nguvu ilio ndani ya maombi ndio maana huakikisha mtu hapati muda huo. Ili kumfanya mtu wake kwa muda wote na aweze kumwongoza atakavyo yeye.
·         Hali ya kujiona mkosaji
Kuna watu hupenda sana kujiona wao ni wenye dhambi kuliko wengine. Mara nyingi inatokea pale mtu anapofanya dhambi na kugundua kuwa alichokifanya hakikuwa sahihi hata kidogo. Lakini wengine huenda mbali hata kudiriki kujiua kwa kunywa sumu, vidonge au kujinyonga. Lakini wengi wa aina hii wamesahau kama Yesu ujio wake duniani ulikuwa kwa ajili yao na sio vinginevyo. Haya tunayaona katika Isaya 53:5 unatueleza kwa bayana juu ya jambo hili.
·         Upungufu wa neno la Mungu
Pale mtu anapokuwa na kiwango cha chini cha neno la Mungu hali semina zinatangazwa, fellowship zinahamasishwa au bible study zikiandaliwa na bado mtu hafiki uwe na uhakika kuwa kuna nguvu za giza zinazomwandama. Maana shetani anajua neno ni pumzi ya Mungu ndani ya watu. Hivyo basi akiwapa watu uhuru wa kulipokea watakuwa na nguvu kubwa sana. Hivyo huweka vita juu ya jambo iwe kwa kumtwika majukumu mengi hususani wakati wa vipindi vya neno vinapowadia.
Je tufanye nini pale tunapojiridhisha kuwa tumeingia kwenye dalili hizi?
Yak 4:7 inatueleza kuwa tumpinge shetani naye atatukimbia. Hivyo kwa kuwa tumeangukia kwenye dalili tajwa basi hatuna umbali na shetani, basi ni muhimu tukampinga. Je kwa namna gani? Ni kwa kupitia silaha za ki-Mungu Efe 6:11-18 utaona zimetajwa katika hiki kifungu basi vitumie na imani yangu kuwa hizo nguvu zote zitaondoka kwa haraka. Lakini si kwa mara moja ukishaanza jambo hili liwe endelevu kwako.
Hivyo ashukuriwe Mungu atusaidiae kujua mambo haya ili tusiendelee kukaa gizani tena. Mungu anao mpango wa kuhahikisha wengi wafahamu kweli yake ili wawe huru. Kuna mambo si ya kuomba bali ni ya utekelezaji zaidi.
Barikiwa sana                                                                                                                                                                   Na Henry Nicholaus

JIFUNZE KUMPA MUNGU NAFASI YA KWANZA MAANA HUTAJUTA
Kufuatana na Isaya 45:2-3 isemayo, "Nitakwenda mbele yako na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande mahali palipo milango ya shaba, na kukata kata mapingo ya chuma; nami nitakupa hazina za giza na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni Bwana, nikuitae kwa jina lako, naam Mungu wa Israeli."
Kutokana na hichi Mungu alichokuwa akisema utagundua kuwa maisha yetu yana makorongo. Hivi ndivyo alivyokuwa akimaanisha. Kama yasingalikuwepo kwa nini kusawazisha? Hili ni swali la msingi ambalo una hitaji kulifikiri ewe unayenifuatilia. Mtu anayeendesha gari kwenye barabara iliyo na kona nyingi huwa hana uwezi wa kuona mbali. Hii ina maana kuwa kama maisha yetu yamejaa makorongo uwe na uhakika kuwa hatuwezi kuona mbele.
Unaweza uona mtu anaishi mwaka huu kama alivyoishi mwaka jana ina maana kuwa mtu wa namna hii hana mpango wa maisha. Yeye maadamu yuko hai atajitahidi tu asife njaa. Je unajua kuwa duniani hatukuja kupigania tusife njaa? Kama mtu hatambui hili ni ngumu kufanya mapenzi ya Mungu. Kwa kuwa mpango wa Mungu juu ya maisha ya mtu haufanani hivyo si rahisi swala la kujikumu chakula ikawa agenda ya maisha ya watu?
Ni vema kama wewe ni mhanga wa jambo hili, ukajitahidi kubadilika maana sivyo tunavyostahili kuenenda kama watoto wa Mungu. Maana Zab 24:1 inatueleza kuwa mali na vyote viijazavyo dunia ni mali ya Bwana. Na kama Bwana ni Baba kwako maana yake huhitaji jitihada kusumbukia mambo kama haya. Bali kufanya yale ambayo si ya mfanano.
Lakini pia katika Isa 45:3 tunaelezwa wazi kabisa kuwa, tunapomruhusu Mungu awe kipaumbele katika maisha yetu anatujaza hata yale ya mbeleni au ambayo hayako wazi katika kipindi husika. Ili kutufanya watu wa mafanikio. Watu wengi wanafanya mambo yao bila kumshirikisha Mungu na si kwamba hawafanikiwi bali kiwango chao cha kufanikiwa ni kidogo.
Hivyo ndugu mpendwa uliye mwanafunzi, mfanyabiashara, mjasiriamali, mfanyakazi nk. Ni vema kutambua kuwakumpa Mungu nafasi ya kwanza ni jambo la msingi kama unataka uinuke. Nimeona watu wengi wakifanya yao kwanza kisha Mungu baadae. Zingatia hili litakusaidia.
Barikiwa sana                                                                                                                                                                    Na Henry Nicholaus
MSINGI WA BARAKA NI UPI?
Nimeona watu wengi wakiomba baraka ikawa inanisumbua sana. Mfano mtu anasema, "Ee Mungu nakuomba unibariki katika masomo yangu". Kila ninaposoma biblia najaribu kutafakari juu ya hili lina msingi gani?
 Kumb 28:1 isemayo, "Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote  nikuagizayo leo, ndipo Bwana Mungu wako atakapokutukuza katika mataifa yote ya dunia; na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako."
Baada ya kifungu hiki nipata mwanga kuwa msingi wa baraka hauko katika uhodari wa kuiomba bali uko kwenye nafasi ya kufuta maelekezo ambayo ni neno la Mungu. Soma hicho kifungu kwanza ili wakati nikiwa naendelea nisikuache nyuma. Lakini pia kwa ufafanuzi wa kifungu hiki nimejua kuwa kadhia ya kuomba baraka imekuja wakati ambao watu wengi wakiwa wavivu wa kusoma neno la Mungu.
Unaposoma Mt 6:33 inatueleza wazi kuwa tukiutafuta ufalme wa mbinguni na haki yake basi tunacho kila tunachokihitaji. Ina maana kuwa kama mtu akifuata neno hili na kuliishi anaweza kujikuta hata asipoomba bado ataweza kuishi bila shida. Na jambo hili najifunza kwa baadhi ya watu matajiri. Unakuta wanasaidia sana na pengine hawamwamini Mungu lakini hawapungukiwi hii inanipa picha kuwa swala sio kuomba bali swala ni kuliishi neno la Mungu.
Ngoja nikupeleke Mw 12:1-2 isemayo, "Bwana akamwambia Ibrahim toka, katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako uende mpaka katika nchi nitakayokuonyesha; nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka". Ukiangalia hii mistari ya Mwanzo utaona Mungu anamweleza wazi kabisa Ibrahim kuwa kigezo cha kubarikiwa kipo kwenye kumsikiliza Yeye kama anataka kubarikiwa. Maana najaribu kufikiri kwa nini Mungu asimbariki Ibrahim pale alipo. Lakini nikagundua baraka inakuja pale unapoweza kusikia maelekezo ya Bwana na kuyafanya. Na ndivyo tunavyoona katika Mw 17:1-7.
Ninayaeleza haya ili uelewe. Ngoja ni kupe mfano kidogo. Baraka ni kama mshahara. Mshahara huja kwa mtu anayestahili yaani aliyefanya kazi kwa muda wa makubaliano. Huwezi kulipwa kama hujafanya kitu chochote na ndio inayotokea kwa wakristo wengi. Wengi ni wepesi kuomba Mungu awabariki lakini milango ya baraka hawataki kuifungua. Maana Mungu anapenda kukubariki lakini ilimradi umefungua milango ili aweze kuipitisha. Tunaona vizuri haya katika Efe 1:3 inatueleza kuwa Mungu ametubariki kwa baraka zote za rohoni.
Usipende siasa katika mambo ya kiroho. Mfano mdogo tulipokuwa sekondari tulikuwa na tabia tukiomba kukumbuka kusema, "Mungu ulisema utatufanya vichwa na wala si mkia". Siku nilijuuliza mbona hutumalizii mstari huu maana unatoka Kumb 28:13. Kipande ambacho hatukimalizii kinasema, "Kama utaisikiliza sauti ya Bwana Mungu wako nikuagizayo leo". Kwa hiyo utaona wakati mwingine tulikuwa tunapoteza muda maana huwezi ukavuna usichopanda Gal 6:7-8.
Natamani mjue kuwa baraka si zawadi bali ni kama mshahara. Haiwezi kuja isipokuwa kuna jambo umefanya ambalo linakupa haki ya kuweza kuifanya. Pale wakristo wanapoomba baraka lazima wajue si zawadi. Kama ingekuwa zawadi basi wakristo wasingekuwa masikini, maana wangekuwa nazo za kutosha maana kuna watu toka wadogo wanakuja kanisani. Hivyo kama baraka ni mshahara ni muhimu ukawajibika katika neno la Mungu hata bila kuomba Mungu atakulipa maana Yeye kiti chake cha enzi msingi wake ni haki. Ni muhimu ukalielewa hili.
Hivyo basi kama ni nia yako wewe kutaka kubarikiwa. Au kama unapenda kuona baraka za Bwana zikuendea ni vyema ukahakikisha unaishi neno la Mungu. Maana muda mwingi katika maisha yetu tunauishi. Hivyo situ kubarikiwa pia inakuweka katika nafasi nzuri ya kushida mtihani wa kwenda mbinguni.
Barikiwa sana­­­­­­                                                                                                                                                                
Na Henry Nicholaus

NJIA MUNGU SI NJIA ZA MWANADAMU

Njia za Mungu ni za tofauti kuliko zile za mwanadamu. Mungu ana taswira kubwa ya maisha yetu maana mtunzi wa zaburi anatuambia katika Zab 139:2 "Wewe wajua kuketi na kuondoka kwangu..." ina maana Mungu anatumbua mwanzo wako na mwisho wako wa kila unachofanya. Yeye anaona vitu ambavyo sisi hata hatuvioni katika maisha yetu. Katika maisha tulionayo ukijiachilia hutaweza kuwa na hofu na chochote. Chochote ambacho tunakipenda au kinatufurahisha shetani aweza kukitumia kukukosesha amani na furaha. Ukijifunza kuwa na furahi katika kila hali. Itakusaidia sana kuwa na amani hata kama mipango ulioipanga haitafanikiwa.
Tusitumie muda mwingi kuombea sana yale tunayo yatazamia bali maombi mazuri ni yale ya kuruhusu mapenzi ya Mungu yachukue nafasi katika maisha yetu. Hii ni alama inayoonyesha kuwa unamwamini Mungu kama ukifanya hivyo. Kuna wakati Mungu atakuambia ujiachie katika mambo unayopenda sana. Kama tukifanya hivyo Mungu ataleta kitu bora kuliko kile ulichokuwa ukikitazamia. Haya tunayaona Mw 22:1-2 Mungu anamwambia Abrahamu atoe mtoto wake anayempenda mno. Na baada ya yeye kukubali situ kwamba Mungu alimrejezea mtoto bali hata alimbariki Mw 22:15-18. Swali je waweza kuwa na furaha hata kama mambo yako hayatakuwa sawasawa?
Jibu ni jepesi hatuhitaji matatizo kutokuwepo ndio tuwe na furaha. Furaha yako isifungwe na matatizo. Unapoweza hili utakuwa umeonyesha kumwamini Mungu. Hapo ndipo Mungu atakupa mahitaj ya moyo wako. Hautaji kuwa na kitu ndio uwe na amani hata kama hunacho bado unahitajika kuwa na amani. Hata kama aliyoweka Mungu ndani yako huoni kama yanafanikiwa usikate tamaa. Wee endelea kumwambia Mungu apate kuyasimamia yeye mwenyewe.
Usikate tamaa juu ya maono yako hata kama mazingira yanaonyesha ugumu wa hicho kutokea. Zab 138:8 inasema "Bwana atatimiza mambo yangu..." Mungu anajua kukupeleka pale unapotakiwa kuwepo. Ukimwamini Mungu ataleta watu sahihi kwako kukusaidia na kukufungulia milango sahihi naye atabadili matatizo kuwa mafanikio. Tunaweza kupanda mbegu na kuimwagilia lakini hatuwezi kuilazimisha kuota kwani Mungu ndiye aikuzae. Hivyo acha kuwa na huzuni juu ya mambo yako ambayo hayajafanikiwa. Unaweza ukanywa dawa usipone maana Mungu ndiye aletaye uponyaji.
Hofu siku zote inafunga mikono ya Mungu juu ya maisha yako. Yoeli 2:21-27 inasema Mungu atarejesha miaka tuliopoteza wakati wa majaribu hivyo isikusumbue wewe kukaa kwa kipindi kirefu ndani ya jaribu we mpe Mungu nafasi ya kukutawala. Hili ndio jambo kubwa mno waweza kufanya kwani kwa kufanya hivyo utakuwa umeonyesha kumwamini yeye.

MUNGU AMEKUPA NAFASI YA UAMUZI JUU YA YALE ALIOWEKA WAZI MBELE ZAKO.
Mungu alimuweka mwanadamu kuwa juu ya vitu vyote. Naye amejiwekea utaratibu huo wa kumtumia mwanadamu katika kila alilolikusudia duniani. Lakini Mungu hatumii kila mtu kusimika kile anachokitaka bali hutumia wateule wake. Amo 3:7 inaeleza kwa uwazi kabisa juu ya jambo hili. Hivyo basi hakuna jambo lolote laweza kutokea mahali popote bila mtu yeyote kukosa kujua.
Unaposoma Mw 18:17-22 unaona Mungu amekusudia maangamizi Sodoma na Gomora lakini hakuweza kwenda bila kumwambia Ibrahim hii ni moja ya mfano unaodhihirisha kuwa Mungu hatekelezi jambo bila kumjulisha mwanadamu kwa yale yanayohusu ya dunia. Watu wengi wameshindwa kutumia nafasi walionayo ya uungu waliokuwa nayo matokeo yake kuishi katika malalamiko. Mw 1:26 Mungu alisema tumfanye mtu kwa mfano wetu akiwa na maana kuwa tuweze kufanya mambo mbalimbali duniani kama yeye.
Wengi wameelemea katika uanadamu wakisahahu kuwa uko uweza ulio wa tofauti unaoweza kufanya zaidi ya mipaka yetu inapokomea. Hivyo ili kuhakikisha sisi tunafanya mambo kama Mungu, Mungu ameweka jitihada kubwa za kutufikia ikiwepo kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye huyo hukaa ndani ya yule aliyetayari kumpokea. Na kwa sababu hiyo Yeye hukamilisha uungu ndani yetu Yn 1:11-12. Mungu wetu ni wa upendo na anayetupenda sisi wanadamu kuliko maelezo na ndio maana ametupa nafasi ya kufanya maamuzi ya mambo mbalimbali.
Lakini nataka ujue kuwa hatuwezi kufanya maamuzi ya kila kitu isipokuwa ya yale tu aliyotufunulia Kumb 29:29 kwa sababu yaliofunuliwa ndio ya kwetu ndio maana yakafunuliwa kwetu. Unapokuwa unahojiana na Mungu ni muhimu ukawa na hoja na sio 'interest' Yer 1:5-7. Natamani ujue kuwa Mungu anakuita uhojiane naye ila kwa hoja Isa 1:18, 43:26. Nataka ujue kuwa nafasi ya kuhojiana na Bwana ni nafasi ya kuamua mustakabali wako. Mfano wa mahojiano ni 2Nya 1:7-12 na Hes 14:11-12. Kwa mifano hii tunaona Mungu akigawa uhuru wa kutusikiliza hivyo tutumie hizi nafasi.

NI KWA NINI WAKRISTO WANAISHI MAISHA YA SHIDA HALI WANAE MUNGU ALIYEHAI
Nia ya Mungu ni yeye kuwa kwako kama baba ama rafiki na sio vinginevyo. Mara nyingi tunatofautiana naye pale tunapomtazama kama Mungu wa msaada. Mw 3:8-9 wakati Adamu na Eva wako bustanini Mungu alikuwa na utaratibu wa kuwatembelea. Huu ulikuwa ni mpango wake ili aweze kutushirikisha pendo lake.
Mungu alimfanya mtu ili aweze kushirikiana naye pendo lake Yn 3:16. Kwa sababu hatufahamu dhamira ya Mungu ni nini, hivyo inakuwa ngumu kuweza kupokea kitu kutoka kwake. Maana huwezi kupokea kitu kwa mtu ambaye hamjaelewana. Hivyo tunapomtazama Mungu kama Bwana wa msaada ina maana atahitajika tu pale tatizo linapotokea na pasipokuwa na tatizo basi haitajiki. Na huu sio mpango wa Mungu.
Kwa kipindi kifupi tulichotembea pamoja katika somo hili utaona kuna mazoea ambayo kiukweli si sahihi tena yanapaswa kuondolewa kabisa ili yasiathiri mahusiano ya mtu na Mungu. Utakuta wengi wanaohudhuria semina au mkutano wa injili si kwamba anataka akutane na Mungu bali yeye anataka uponyaji. Mtu wa jinsi hii akiponywa haonekani tena kanisani. Kwa nini? Hakwenda kumtafuta Mungu bali alikwenda kutafuta uponyaji.
Unaposoma Isa 1:17 Mungu anatuita tusemezane naye hii ameonyesha kuwa Yeye ni rafiki yetu sema sisi hatupendi urafiki naye kwa kumwendea. Nataka ujue undani wa mahusiano Mungu anayotengeneza na mtu Amo 3:7. Mt 6:33 Mungu anafanya kila jitihada ya kutengeneza urafiki na sisi lakini maamuzi yapo kwako hakulazimishi japo anakuhamasisha uwe rafiki yake. Hayo utayaona zaidi katika ufu 3:20
Tuwezaje kujenga urafiki na Mungu
  • Lazima tukubali kubadilika toka kwenye mitazamo ya kale Mw 12:1
  • Tusome neno lake ili tuelewe njia zake Zab 119:105
  • Tushike sheria zake Yn 15:10
  • Tuzungumze naye Isa 1:18
  • Kuzaliwa mara ya pili Yn 3:6-7
    Kwa nini Mungu ni rafiki yetu
  • Hutusamehe pale tunapokosa Hes 14:18
  • Hutuletea msaada wakati wa shida Zab 23:1-4
  • Hutulinda na dhiki pamoja na mabaya Zab 121:5-8
  • Hupenda kutusikiliza Yer 33:3
  • Hutueleza siri zake Amo 3:7
  • Anapenda kukaa na sisi Ufu 3:20
  • Anapenda kukaa pamoja nasi Yn 14:1-3
  • Amejitoa kwa ajili yetu Yn 3:16

    MATUMIZI BORA YA MUDA NI JAMBO LA MSINGI
    2 Kor 6:2 inasema "Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia; tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa. Hii ina maana kuwa hatuna muda mwingine wa kufanya maamuzi juu ya maisha yetu ya rohoni isipokuwa sasa. Ni muhimu ukazingatia sana muda maana ni jambo la muhimu yakupasa kulizingatia kuliko maelezo.
    Mw 1:3 tunaona Mungu anaufanya muda kama kipaumbele chake. Wakati anaanza uumbaji alianza na muda. Tafsiri yake ni nini? Ina maanisha kuwa iwe chochote kile kilicho duniani kina uhai ama hakina basi tambua kuwa kimefungwa katika wakati na hili ni jambo la msingi sana ambalo twatakiwa kulifahamu.
    Bila ya kukaa katika wakati hatutaweza kufanikiwa pia maana hata mustakabali wetu wa baadae Mungu ameufunga katika majira na wakati. Anaposema kuwa wakati uliokubalika ndio sasa ana maana kuwa kile unachotakiwa kufanya usikipe kalenda unahitaji ukifanye wakati huo huo na mwingine.
    Kuna watu na tabia ya kutoa sadaka muda anaotaka yeye. Hili ni jambo ambalo linasababisha watu wengi waingie katika kukosa baraka maana wanaona wanatoa lakini hawapokei. Ila ni kwa sababu hawajatambua kuwa hata sadaka ina nidhamu yake. Unaposoma Isa 49:8 unaona Mungu anasema wakati uliokubalika nalikujibu. Hii ina maana kuwa Mungu hamjibu tu mtu kiholela bali anajibu kwa utaratibu ulio wazi. Hivyo basi ni muhimu ukazingati nidhamu ya utoaji ili uweze kuona ukila matunda ya sadaka yako.
    CHUKUA HATUA
    Joshua 3:1-5 Joshua anawaambia wana wa Israeli kuchukuwa hatua ili kuweza kukabili safari iliyokuwa mbele yao kwa kuwa wanatakiwa wajitakase ili waweze kuanza safari.ili uweze kufanikiwa ni lazima uchukue hatua ya kutenda au kukabili jambo husika ambalo unatalaji kulifanya,hivyo tunatakiwa tuchukue hatua katika neno ili tuweze kushinda vita vinavyo tukabili ,na Mungu anatusubili sisi aone kama tunatii neno lake kwa kuchukua hatua ili aweze kushusha Baraka zake juu yetu.
    Kutoka 2:11-15 Jitahidi kuangalia hali uliyokuwa nayo kisha angalia yale unayoyafanya kama kweli yanaendana na neno la Mungu linavyotuonya na kutufundisha,na kama sivyo basi chukua hatua ya kujirekebisha ili Mungu akutendee,wakristo wengi wanajifariji kwa kuomba maombi marefu, kuhudhulia kwenye ibada kila siku,lakini wanasahau kuwa Mungu anapendezwa na wanaotii neno lake na kukubali kutubu,kwa kughaili na kuacha maovu na kutenda mema.Kutoka 3:6 acha kujifariji kwa kuigawa dhambi ukidhani kuna kubwa na ndogo,elewa kwa Mungu zote ni dhambi kwa kuwa zinampeleka mtu jehamu.Kutoka 5:1 licha kuwa utachukuwa hatua sio kwamba mambo yatakuwa mazuri hapana, inawezekana yakawa magumu sana ,kama ilivyokuwa kwa Musa na Haruni wakati Mungu anasema nao juu ya kwenda kwa Farao kuomba kibali cha wana wa Israeli kwenda kumwabudu Mungu wao.kutoka 5:1-12 tunapochukuwa hatua bwana anajidhibitisha kwetu,zipo hatua zinazotufaa sisi tuzichukue ili kuweza kupona.
    · Chukua hatua ya kuliamini neno la Mungu.Kutoka 14:13-16,wakristo walio wengi wanashidwa kwa kuwa wanakuwa mafundi wa kusikiliza na kuandika mafundisho yote yanayofundishwa,lakini ndani yao kumejaa mwalakini na kutoamini kuwa maneno yanayosemwa au ahadi zilizotolewa na Mungu kuwa ni kweli ,tunakuwa wagumu wa kuamini tunasubili mpaka tuone ndipo tuamini ,yapo mengine hatutapokea endapo hatutaruhusu kuamini ndani yetu.
    · Chukua hatua ya kutenda.yapo mafundisho ya Mungu ambayo yanatufundisha kuamini neno la Mungu ili tuweze kupokea Baraka ,lakini waliowengi ndani yetu tumekuwa na mashaka juu ya kile ambacho tunakiomba na matokeo yake watu hawapokei kwa kuwa ndani yao yamejaa mashaka mengi.Musa anaambiwa na Mungu juu ya kuwaongoza wana Israeli afanye tendo la imani la kupiga fimbo juu ya bahari na Musa alipochukua hatua bahari iligawanyika na wakapita salama,je? endapo angekuwa na mashaka wangevuka? Matendo 12:1…,Hesabu 13:1-3
    · Chukua hatua ya kuhakikisha kile unachoambiwa.katika nyakati hizi tulizo nazo ni ngumu na mbaya sana kama hatutachukuwa hatua za kumkariba Mungu ili atusaidie,kwa sasa wapo watu wanaojiita kuwa ni manabii na mitume na mafundisho wafundishayo siyo mazuri kwetu ,hivyo inatakiwa kuhakikisha kile unachojifunza kama kweli ni chema mbele za Mungu na utaweza kuhakikisha kwa kusoma neno na kumruhusu roho mtakatifu atufunulie na kutufundisha.
    · Chukua hatua ya kumng’ang’ania Mungu Kutoka 33:1-6 licha ya kuwa Musa alimg’ang’ania Mungu si kwa kutaka mahusiano mema na Mungu bali alitaka pia ushilika na yeye,hivyo na wewe usikubali kuondolewa au kujiondoa mbele za Mungu pasipo kupokea kile ambacho umeahidiwa wewe ukipate,ng’ang’ania kwa Mungu ili ashilikiane nawe katika hali zote na majira yote na yeye endapo utayatoa maisha yako kwake, atakupa yale yanayokufaa.
    Joshua23:6 inawezekana kabisa imani zetu ni kubwa sana lakini kama katika matendo hatufanyi inavotupasa basi imani zetu ni mfu,kwa kuwa neno la Mungu linasema imani pasipomatendo imekufa,Yakobo 2:14,17 unaposikia neno la Mungu epuka mizaha na kulichukulia mazoea na uchukue hatua ya kulitendea kazi ,kwa kuwa kuna mambo huwezi kupata au hayawezi kuondoka yenyewe usipochukua hatua wewe mwenyewe,na ukichukua hatua Mungu ni mwema kwetu atatutendea na atatupa Baraka. Amen
    Na Mwj PauL

    TUACHE KUISHI KWA MAZOEA AU DESTURI
    Hes 21:4-9 Tunaona wana wa israeli walikuwa wakiendelea na safari yao jangwani. Wakitokea mlima wa Hori kwa njia ya Bahari ya Shamu; ili kuizunguka nchi ya Edomu. Biblia inatueleza wazi wana wa israeli walikata tamaa kwa sababu ya njia ile. Katika maisha yetu yamkini yako matatizo ambayo kama wana wa israeli walikutana nayo kiasi cha kukata tamaa. Haikutosha wakaanza na kumnung'unikia Mungu hata wakatibua hasira yake. Manung'uniko sio suluhu ya matatizo yetu. Wana wa israeli walikuwa wakisafiri jangwani lakini bado haikutosha wao kujua kuwa jangwani hakuna maji wala chakula kiasi cha kunung'unika.
    Tunaishi kwenye dunia yenye matatizo hivyo kwa mtu kupata tatizo sio sababu ya kumlaumu Mungu. Labda nikukumbushe ndugu msomaji asili ya matatizo ilikuwa ni dhambi ambayo ilianzia Edeni, hivyo basi unapopata matatizo tambua kuwa Mungu hayuko na wewe wakati huo. Kwani Adamu alianza kuona matatizo baada ya kufukuzwa bustanini. Hii ina maana kuwa uwepo wa Mungu unapoondoka katika maisha yako ni mlango wa ibilisi kuchukua nafasi juu yako.
    Tunapoinua manung'uniko ndio kuzidi kwa matatizo yetu. Kwa sababu biblia inaeleza Mungu aliinua nyoka wa sumu kwa sababu ya manung'uniko. Kwa jicho la agano jipya nyoka wa sumu ni matatizo. Jambo la kupendeza wana wa israeli walikumbuka kutubu. Watu wengi wanapoingia matatizoni wanakurupuka kuangalia nani mchawi badala ya kuomba utakaso. Yos 3:5 Joshua anawaambia jitakaseni maana kesho Bwana atafanya matendo makubwa. Ukitaka kuona matendo makuu ya Mungu hebu anza kwa kujitakasa.
    Wana wa israeli walipoomba kusamehewa na kuondolewa nyoka, biblia haituambii kama nyoka waliondoka lakini inasema kuwa Musa aliinua nyoka wa shaba Hes 21:9. Na kila atakaye mtazama basi atakuwa salama. Sina shaka wana wa israeli walikuwa wakijua dawa ya nyoka wa sumu. Lakini walijua wale nyoka si wa kawaida kiasi cha kumwitaji Mungu ashuhulike na nyoka hao. Bado haikutosha staili ambayo Mungu aliwaletea dawa ya kuwaponya haikuwa ya kawaida kwani alimwambia Musa asimamishe nyoka wa shaba na atakaye umwa na kumtazama basi atapona. Nini nataka ujifunze hapa majibu ya Mungu hayana kanuni. Kuna watu kwa sababu tatizo alilopata anajua fulani naye aliwahi kupata naye akatumia njia fulani akafanikiwa basi naye anataka Mungu amjibu njia hiyo hiyo.
    Mungu haendeshwi na matukio yeye huweza kufanya chochote. Tuache mazoea ya  staili ya kujibiwa kama unachohitaji ni jibu la kuvuka na si kwa njia ipi uvuke. Hapa ndipo waumini wengi wanashindwana na watumishi wao kama huamini mtazame Naamani ameenda kwa Elisha kuponywa bado anataka aponywe kwa staili anayotaka yeye 2Fal 5:10-11 kwa utagundua watu wa staili wapo wengi ndio maana siku hizi uponyaji unakuwa shida makanisani. Tunahitajika tuchukue hatu juu ya kile tunachoelezwa na watumishi na sio kutaka yale tunayopenda yafanyike kwetu wakati wa matatizo.
    Ni rai yangu kwako unayenifuatilia jenga imani katika neno la Mungu lililoachiliwa bila kuangalia nani aliliachilia. Hii itakusaidia maana hata wengine wameenda mbali zaidi hata kuwabagua watumishi akisema fulani haponi ila akisema fulani basi anahisi amepona. Nataka ujue Mungu humtumia yeyote yule bila kuangalia ni nani anayemtumia na yukoje. Pasipo imani hatuwezi kumpendeza Mungu. Hivyo ni muhimu ukasimamia imani wakati wa matatizo.
    Nikukumbushe Mungu alivyomuaminisha Musa aende kwa Farao kuwatoa wana wa israeli haikuwa jambo jepesi. Ilimgharimu Musa mapigo kumi yapite mbele ya macho yake kabla ya kufikia kile Mungu alichomueleza. Hata wewe yamkini unapoanza kuamini hali ikawa ngumu kuliko pale awali isikupe shida we chochea imani maana unakokwenda ni kuzuri kuliko pale ulipo sasa.
    Barikiwa sana
    Na Henry Nicholaus
    VIZUILIZI SABA VYA UZIMA WA MILELE
    Mt 7:14 inasema " Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache. Tunapoutafakari mstari huu tunajifunza habari za vizuilizi vya uzima wa milele ambavyo ni miiba. Na ndio ambayo huwaogopesha watu kiasi cha kuamua kuchagua njia ya motoni kwani hahitaji jasho ili kuiendea. Kwa kuwa kuna miiba ni vema tukaichambua ili tunapotembea tuiruke na kukanyaga mahali pazuri. Ukweli kama neno la Mungu linavyosema safari ni ya kupandisha kwa tafsiri rahisi inahitaji jitihada ndio maana yatupasa tujifunze haya.vifuatavyo ni vizuilizi vya uzima wa milele.
    1) Kufanya dhambi kwa makusudi: Kuna wakati tunajua na kufahamu kweli halisi juu ya mambo au jambo kuwa si sahihi lakini bado tunatenda. Nini biblia inatueleza juu ya hili? Ebr 10:26 tunaweza fikiri kuwa tunasamehewa kumbe neema haiwi juu yetu.
    2)Kuipenda dunia: Duniani sio mahali petu ambapo mimi na wewe tutakaa. Bali ni mahali pa kupita. Hivyo tunapoitazama dunia ina maana kuwa hatuna mpango na makao mapya Yn 14:2-3.Tunasoma Yak 4:4 tunaelewa kuwa Mungu ana uadui mkubwa na mpenda dunia maana dunia imeshamiri uovu.
    3)Kuwa na ushirika wa ndani na watu wasiomwamini Kristo: Hatujakatazwa kuwa na urafiki na watu wasio amini bali tunatahadharishwa kuwa kuwa na urafiki nao wa ndani unaweza athiri maisha yetu 1Kor 15:33. Hivyo Zab 1:1 inatupa msisitizo juu ya hili.
    4)Magomvi na mashindano: Huwa magomvi na mashindano huleta matatizo makubwa pale tunapoyaendekeza. 1Tim 6:4-5 inaeleza wazi kuwa mashindano ni mabaya. Hivyo hatuna sababu ya kushindana na watu kwa kuwa hayana faida.
    5)Kiburi: Roho kama hii ni kuzuizi kikubwa kwa wokovu.  Tumefundishwa kujifunga unyenyekevu.  “naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema, 1 Pet. 5:5. Kiburi na uongo ni kizuizi kati ya mwanadamu na Mungu wake.  Hutangua bidii yote ya kuwa mtakatifu.  Kwa kweli Sulemani anatueleza ya kuwa Mungu anachukia wenye kiburi, “kuna vitu sita anavyovichukia Bwana , naam viko saba vilivyo chukizo kwake, macho ya kiburi, ulimi wa uongo, na mikono imwagayo damu isiyo na hata,  Mith. 6:16
    6)Moyo wa uvivu: Ni ile hali ya mtu kutokuwa na muda juu ya neno la Mungu au maombi. Kuna mambo ambayo ni muhimu kwa maisha ya mkristo ambayo ni  maombi na neno lakini wengi watoi muda kwa ajili ya hivyo. Njia ya kwenda Mbinguni ni ya kupandisha.  Yesu alisema lazima tukitendee kazi chakula kidumucho milele, Yn. 6:27.  Imani bila matendo imekufa, Yak. 2:2.  Mtu aliye mvivu katika maisha ya kawaida ataona ni vigumu kufanya kazi ya Mungu.  Yesu alikufa ili kuwakomboa watu “wale walio na juhudi katika matendo mema,” Tit 2:14.
    7)Kutosheka kiroho: Kuna watu katika jamii kwa sababu wamebatizwa au kupata kipaimara wanadhani kuwa ndio mwisho wao kusikia neno la Mungu. Hivyo unakuta hawajishughulishi katika kutafuta neno la Mungu. Wao huona kila muda ni wa kufanya kazi kuliko kuhangaika juu ya kumtafuta Bwana. Neno la Bwana linasema kupitia Yos 1:8 kitabu cha torati kisiondoke kinywani mwetu bali tuyatafakari maneno yake usiku na mchana. Kwa hiyo iko haja ya mtu kuwa na ratiba ya kusoma neno la Mungu.
    Hivyo ndugu unayenifuatilia tumekwenda kwa karibu kabisa kwa habari za vizuilizi saba vya uzima wa milele. Ni mwito wangu kwako kuona ukitendea kazi haya ambayo kwa njia ya Roho ambaye ni arabuni yetu ametupitisha.
    Barikiwa sana
    Na Henry Nicholaus
    HUWEZI FANYA MAAMUZI BAADA YA KUFA BALI WAKATI WA UHAI
    Ukifungua kitabu cha Yoeli.3:14 kinasema, “Makutano makubwa, makutano makubwa, wamo katika bonde la kukata maneno! Kwa maana siku ya Bwana i karibu”. Huyu ndugu, mtumishi wa Mungu, aliyekuwa anaitwa Yoeli, Mungu alimpa nafasi ya kuona mambo ambayo yamekuwa yanafanyika tangu kuumbwa kwa ulimwengu, mpaka hapo Yesu atakaporudi tena. Anasema, ameona makutano makubwa, makutano makubwa, katika bonde la kukata maneno. Tafsiri nyingine ya bonde la kukata maneno maana yake ni bonde la kufanyia maamuzi. Kukata maneno ni kufanya maamuzi. Sasa, bonde la kukata maneno, kwa tafsiri ya haraka ni dunia hii, wakati huu, mwanadamu anapoishi duniani. Kwa sababu kabla hujazaliwa huna uwezo wa kuamua.
    Biblia inasema Mungu alimwambia Yeremia, “Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, kabla hujatoka tumboni nalikutakasa” (Yeremia 1:5). Kabla hajawekwa tumboni mwa mama yake, Mungu alimjua Yeremia, ambayo inamaanisha Yeremia alikuweko, lakini alifananaje sijui! Lakini maandiko yananiambia ya kwamba alikuwepo na Mungu alimjua. Alipokuwa tumboni Mungu alimtakasa, maana yake alimtenga kwa ajili ya utumishi na wito wake. Lakini Yeremia hakuwa na uwezo wa kuamua. Kabla ya kuzaliwa huwezi kuamua, baada ya kufa huwezi kuamua kitu chochote. Ndio maana tunatamani kila mtu lazima aokoke, aamue anataka kuishi maisha ya namna gani baada ya kufa, maamuzi hayo unayafanya kabla hujafa. Baada ya kufa hakuna mahali pa kufanyia maamuzi hayo tena! Kwa hiyo kipindi hiki, ambacho mwanadamu anaishi ndicho kipindi cha kukata maneno. Bonde la kukata maneno ni dunia hii. Makutano makubwa; maana yake aliona watu wengi sana wamekaa katika bonde ambalo wanatakiwa kufanya maamuzi.
    Katika dunia hii, (Kama ulikuwa hujafahamu afadhali ufahamu), ya kwamba kati ya jambo muhimu sana ambalo utawajibika nalo mwenyewe ni kufanya maamuzi. Na yako maamuzi ambayo unahitaji kuwa mwangalifu sana unapotaka kuyachukua, kwa sababu yatasababisha mabadiliko ya maisha yako kabisa. Kwa mfano maamuzi ya kuokoka, kwa mfano maamuzi ya kumtumikia Mungu, yanabadilisha kabisa maisha yako, ndio maana Yesu anasema, mtu kabla hajamfuata, akae chini, ahesabu gharama; kuna gharama katika kumfuata Yesu, na kuna gharama katika kumtumikia Yesu. Maisha yako yanabadilika kabisa! Huwa saa nyingine mimi na mke wangu tunatamani kuishi maisha ya kawaida kama watu wengine, lakini haiwezekani, (watumishi wa Mungu wataelewa kitu ninacho elezea hapa), ukiishafanya maamuzi ya kusema unataka kumtumikia Mungu, maisha yako hayawezi kuwa ya kawaida tena, sio maamuzi madogo hayo.
     Kuna maamuzi ya masomo, watu wanafanya mchezo wanapotaka kufanya maamuzi ya masomo, usifanye mchezo, ni maamuzi muhimu. Kuna maamuzi ya marafiki, unataka kuwa na marafiki wakina nani. Maamuzi haya yanaweza yakakubadilishia kabisa maisha yako. Lakini pia kuna maamuzi ya unachotaka kufanya maishani mwako ni nini. Mwingine atajitetea na atasema, Mungu anajua, - sawa Mungu anajua, lakini anahitaji maamuzi yako! Wengine wanasubiri wakiishamaliza sekondari, au wakiishamaliza chuo kikuu, ndipo waamue wanataka kufanya nini. Ukiishafika chuo kikuu ndipo unataka kuamua cha kufanya maishani, utakuwa umechelewa. Kwa sababu, kama unataka kuamua kufanya kitu ambacho hukusomea, mambo yanawezayakawa magumu kwako, labda iwe ni Mungu anakupitisha hapo kwenye eneo hilo jipya.

    UMUHIMU WA KUJUA NENO LA MUNGU
    Upo umuhimu wa kujua neno la Mungu katika maisha ya Mkristo halisi.
    Biblia inatuambia Yesu Kristo ndiye Neno la Mungu. Kwa maneno mengine Yesu ndiye Neno ambalo Mkristo anapaswa kuwa nalo (Yohana 1:1).
    Kwa kusema hivyo kuna umuhimu wa kumjua Yesu na kumshika, kwa maana yeye ndiye Neno la Mungu. Katika Biblia mtume Petro anasema mbele za Yesu kwamba, twende kwa nani na wewe ndio mwenye maneno ya uzima? Petro alijua upo umuhimu wa kumjua Yesu kama Neno maana ndani ya Neno kuna uzima
    Biblia inasema neno la Kristo likae kwa wingi ndani yetu (Wakolosai 3:16).
    Kwa nini basi neno la Kristo likae kwa wingi ndani yetu? Ni kwa sababu lina mambo yafuatayo ambayo ni muhimu katika maisha yetu ya Ukristo. Mambo hayo ni…
    A) Neno la Mungu li Hai
    Uhai wa Neno la Mungu kwa mtu ndio unaoleta kushinda dhambi. Nao wakamshinda kwa neno la ushuhuda wao (Ufunuo 12:11).
    KWA NINI NENO LA MUNGU LI HAI?
    Neno la Mungu li hai kwa sababu Mungu mwenyewe analithibitisha kwamba li hai maana           a) Linafanya mabadiliko (Isaya 55:10-11).           b) Linatupa kushinda dhambi (Zaburi 119:11).           c) Neno la Mungu li hai kwa sababu linatupa mafanikio katik mwili. Petro anasema ”kwa neno lako tunatupa nyavu zetu.“ Hapa tunaona kuwa Neno la Mungu pekee yake ndilo linaloweza kuleta majibu katika maisha yetu (Luka 5:3-6).
    B) Neno la Mungu lina nguvu (Mwanzo 1:6).
    Neno la Mungu lina nguvu na ndio maana tunamshinda shetani kwa neno la Mungu.
    Yesu kama kielelezo yeye mwenyewe ni neno ndani ya neno anamshinda shetani (Luka 4:1-12). Katika mistari hiyo tunaona Yesu anamwambia shetani ”imeandikwa“ Shetani nae anageuza usemi nae anamwambia Yesu ”imeandikwa kwamba atakuagizia malaika usije ukajikwaa mguu wako.“ Kwa kuwaYesu neno la Mungu limo ndani yake hamwambii tena shetani imeandikwa ila anamwambia imenenwa. Kwa maneno mengine tukiwa na neno la Yesu ndani yetu hatuwezi kuyumbishwa. Kwanini? Kwa sababu tumeshaona jinsi ambavyo shetani anajaribu kutumia neno la Mungu kwa kusema ”imeandikwa.“ Na ni kweli imeandikwa ananukuu kutoka kitabu cha Zaburi 91 :1-12. Hata kama shetani ananukuu maandiko haina sababu yamimi kushindwa na shetani maana Yesu tayari alikwisha mshinda. Yesu kumshinda shetani ina nipelekea mimi kusoma neno la Mungu kwa bidii sana. Kwa mfano, ni kweli kabisa imeandikwa mtakula vitu vya kufisha havitawadhuru lakini je, ninywe sumu sitakufa kwa sababu imeandikwa? Hapana, ukinywa hakika utakufa. Shetani hutumia mandiko kuwafunga wasiojua neno la KristoYesu.
    C) Neno la Mungu lina ukali kuliko upanga
    Neno la Mungu lina ukali kuliko upanga. Kwa nini neno la Mungu lina ukali kuliko upanga? Upanga unaweza kukukata na usipone. Lakini neno linakata na kuponya. Kwa neno hili wafalme wanatubu. Yona alitumia neno la Mungu likawa kali watu wakatubu. (Yona 3:1-10; Matendo ya Mitume 8:18-24).
    D) Neno la Mungu linachoma hata kuzigawanya nafsi, roho viungo na mafuta yaliyomo ndani yake
    Neno la Mungu linachoma hata kuzigawa nafsi na roho na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake (Matendo 7:51-54, Yohana 4:16 -18, 27-29). Mwanamke akaambiwa mambo yake; Neno likachambua kila tabia..
    E) Neno la Mungu li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo
    Yesu kama Neno la Mungu anajua mambo ambayo watu wanawaza ndani ya mioyo yao (Luka 5:17-24, 6:6-8 ; Mathayo 16:1-4). Yapo makusudi ya moyo ambayo ni ya siri sana kwa mwanadamu lakini nataka nikuambie neno la Mungu ni jepesi kutambua makusudi ya moyo
    Mtume Petro aliyependa kujua neno la Mungu, naye pia Mungu alimjalia neema ya kuyajua makusudi ya moyo wa mwanadamu (Matendo 5:1-11). Elisha aliyajua makusudi ya moyo wa mfalme ya kuwatenda Israeli kwa siri ila Mungu alimpa neema ya kuyajua mawazo ya mfalme (2 Wafalme 6:8-12).
    Daudi aligundua au kwa maneno mengine alifahamu umuhimu wa neno la Mungu katika maisha, kama vile mtume Paulo anavyosema na Wakolosai kwa habari ya neno la Kristo kwamba likae kwa wingi ndani ya mioyo yetu. Nataka nikwambie neno la Mungu ni msaada katika maisha yetu maana hutupa majibu ya maisha yetu. Katika Luka 5:3-6 tunasoma jinsi Petro na wenzake walivyopata samaki wengi kwa kutii neno la Kristo. Kumbuka pia juu ya yule akida, alimwambia Yesu ”...sema neno tu na mtumwa wangu atapona“ (Luka 7:2-10). Yesu akisema neno lazima mabadiliko yatokee.
    Hili ni jambo la msingi katika maisha ya Mkristo yaani kulijua neno la Mungu. Neno la Mungu tukiwa nalo na likitenda kazi ndani yetu lazima tufanikiwe (Yoshua 1:8). Watu wengi tunapotea kwa kutokujua uwezo (nguvu) iliyomo katika neno la Mungu (Mathayo 22:29).Ili uwe mwanafunzi wa Yesu ni lazima ulijue neno la Mungu na kulishika.(Yohana 8:31 ; Luka 2:19). Kama neno halimo ndani yetu tunayoyafanya yanakuwa hayana Mungu, hata twaweza kusalitiana. Mtu anayelitamani neno la Yesu huling’ang’ania na kulitenda maana kwake ni nguvu. (1Wakorintho 1:18). Si kwamba Neno la Mungu ni nguvu tu: bali huleta faida (Mathayo 13:23).
    Yesu anasema, mtu anayelitenda neno la Mungu na kulishika huyo amepanda mbegu ambayo itazaa sana, maana ndani ya moyo wake imo mbegu ambayo ni neno la Mungu la uponyaji na mafanikio, msamaha, utu wema na mengi yanayofanana na hayo.Yapaswa maisha yetu yawe yenye neno (mbegu) la Mungu ili tuweze kuzaa mambo mazuri. Wokovu wetu unaimarika kwenye neno la Mungu. Hilo neno la Mungu tunalipata wapi? Isaya 34:16. Upo umuhimu wa kuyachunguza maandiko ili kujua Mungu anasema nini (Matendo 17.10-11). Je, tangu ulipowekwa msingi wa wokovu, neno limo ndani? (Hagai 2:18-19). Kila kitu kinaweza kupita lakini sio neno la Mungu (Isaya 40:8, Mathayo 24:35).

    Ili neno litende kazi katika kinywa chako unapolitamka na kuamini ni lazima iwepo nguvu ya Roho Mtakatifu. Bila hii nguvu hamna kitakacho endelea. Utasema umeamini lakini hakutakuwa na matokeo. Mungu mwenyewe alipotamka neno liliambatana na nguvu ya Roho Mtakatifu (Mwanzo1:2-3).

    Na Mwinjilisti Simon Mkanza
    Kama una swali kuhusu somo hili nitumie barua pepe (ceymera@yahoo.co.uk)
    au nipigie simu: +255 784 475622; +255 786 477021

    Mungu akubariki

    TIMIZA MAELEKEZO YA MUNGU NA YEYE ATATIMIZA AHADI ZAKE KWAKO
    Mw 12:1-5 Tunaona Mungu anampa maelekezo Abrahamu aondoke pale alipokuwa ili aweze kuwa naye kwa ukaribu. Licha ya Abrahamu kuwa na tatizo la kukosa mtoto kwa muda mrefu tangu amwoe Sara hakuona kama ni sababu ya yeye kuangalia mahitaji yake kuliko uthamani wa mahusiano atakayotengeneza kwa kukaa pamoja na Bwana. Biblia inatuonyesha Abrahamu akiondoka kwao bila kumwoji Mungu wala kumkumbusha hitaji lake la mtoto ukumbuke uzee ulikuwa umekwisha mpata.
    Hatua hii ilianzisha kurasa ya mahusiano kati ya Mungu na Abrahamu. Hivyo katika Mw 15:1-7 tunaona tena mahojiano ya Abrahamu na Mungu juu ya yeye kupata mtoto, Mungu anampa ahadi Abrahamu naye kuitimiliza baada ya muda kama alivyomueleza Ibrahimu sawasawa na Mw 21:1-7.
    Hata hivyo tunamwona Mungu tena akimwendea Ibrahimu na kumpa maelekezo mapya ya kumtoa mtoto wake ampendae Isaka kuwa sadaka ya kuteketezwa. Ibrahimu anafanya kama Mungu alivyomwambia bila kuuliza maswali kuwa atapata wapi mwingine bali aliamini kama Mungu ndiye aliyempa basi yeye ndiye ataleta Isaka wengine.
    Tunaona Mungu akifanya sawa na imani ya Ibrahimu Mw 22:15-19. Leo hii tukiwa tunajifunza namna ambayo ya kutekeleza maelekezo ya Bwana ni muhimu ukafahamu ndugu msomaji kuwa Ibrahimu hakuchagua maelekezo ya kufanya alifanya kila maelekezo ambayo Mungu alimpa. Kumbuka usifikiri kuwa Ibrahimu alipata maelekezo machache lakini yale mazito ndio yalioandika ili kutusaidia kujifunza toka kwake kwa kuwa alifaulu katika imani.
    Wakati mwingine mtu aweza kufikiri kuwa ni sauti ya shetani pale anapopata maelekezo mazito, huku akifikiri kuwa siku zote Mungu ana maelekezo marahisi. Jifunze kupokea kila aina ya maelekezo akupayo Mungu maana utakapotekeleza hautakuwa kama vile ulivyo. Kitendo cha Ibrahimu kuwa tayari kutekeleza maelekezo ya Mungu kilisababisha ahadi za Mungu alizotamkiwa na Mungu atapewa kutimia soma biblia yako inasemaje juu ya hili Mw 22:17-18.
    Unapopata maelezo ya Mungu acha kuangalia shida zako. Kama hujui kuwa uko katika ulimwengu wenye una matatizo. Hivyo hata utajirike kama Mengi bado matatizo yapo. Hivyo shida au matatizo yako yasiathiri mahusiano yako na Mungu kwa kushindwa kutekeleza maelekezo yake kwa kigezo kwa saa hiyo au wakati huo umebanwa na matatizo. Ndio maana natamani kukutazamisha hili mapema kwa kuwa imekuwa kigezo cha wengi kukwepa utekelezaji wa neno la Mungu.
    Nami naomba sana Mungu akupe kuelewa sana jambo hili kwa kina maana ndio njia pekee ambayo Mungu aweza kutupandisha utukufu bila vigezo vya kibinadamu au vya kinyakati kama ilivyo kwa Ibrahimu aliyepata mtoto alkiwa na umri wa mia ambalo si jambo la kawaida kwa mtu wa kawaida.                                                             
    Barikiwa sana                                                                                                                      
    Na Henry Nicholaus
    JE WAJUA KUWA MAFANIKIO YANA MLANGO?
    Si watu wengi ambao wanajua juu ya jambo hili, na pia wako wanaofahamu kwa sehemu lakini lisiwe shida kwa kuwa Mungu anatuweka shuleni, basi ni imani yangu baada ya somo hili utakuwa na ufahamu wa kutosha juu yake.
    Tunaposoma Mt 7:7 inasema, "Ombeni nanyi mtapewa tafuteni nanyi mtaona bisheni nanyi mtafunguliwa."
    Nilipokuwa nasoma mstari huu sikuwahi kuelewa kwa kipindi chote japo nilikuwa nimeunakiri kichwani kiasi cha kuukumbuka wakati wote. Lakini siku moja Mungu alinifunulia juu yake na ndipo nilipopata somo hili.
    Ukiangalia katika mstari tuliopewa kuna neno 'bisheni'. Neno 'bisheni' linatupa picha kuwa kinachoombwa kina mahali pa kupatikana au kina mlango wa kukipatia. Hatuwezi kubisha dirishani, tunabisha mlangoni. Kwa sababu dhima ya mstari ni kuomba kwa mwendelezo wake tunapata picha kuwa kama kuna mlango ina maana kuna mambo ambayo tunayahitaji lakini hatuko nayo karibu. Kwa tafsiri ya kawaida mahitaji yetu yapo ng'ambo hivyo ni muhimu tukapita sehemu ili tuweze kuyapata.
    Lakini kwa nini Mungu ameweka mambo haya katika staili ya namna hii. Jibu tunapata katika Mw 3:23-34. Tangu mtu alipoasi alitengana na Mungu mpaka pale tu Kristo anapoondoa hiko kiambaza. Mtu alipoasi, aliamua kuchagua sheria ya dhambi na mauti huku kwa kuasi ameikana sheria ya uzima wa milele katika Kristo Yesu. Kumbuka kuwa sheria ya uzima wa milele katika Kristo Yesu ndio iliokuwa inaongoza utaratibu wa kuishi katika Bustani ya Edeni pamoja na mbinguni. Hivyo basi kwa kuchagua sheria ya dhambi na mauti maana yake hawana nafasi tena katika sheria ya uzima wa milele katika Kristo Yesu. Hivyo wanapotaka vitu vya uzima wa milele ni lazima watumie utaratibu kuvipata kupitia mlango. Na ndio maana mafanikio yana mlango.
    Fikiri ulikuwa meneja wa kampuni fulani. Na baada ya muda uliachishwa kazi maana yake unapoteza haki zote za kuwepo katika hiyo kampuni. Kama ulipewa gari la kampuni haliwezi tena kuwa lako. Hivyo huwezi kufanya maamuzi yeyote juu ya kampuni hiyo au kupata stahili zozote juu ya kampuni hiyo. La kama unataka lazima ufanye taratibu za kuajiri mahali hapo. Sasa ndio maana mafanikio yana mlango. Hii inatupa kufikiri kuwa si mambo ambayo unaweza kupata kwa kulala na kuamka bali ni mambo ambayo hupatikana kupitia mlango. Hata hivyo mpaka uhakikishe huo mlango umeubisha.
    Nami namshukuru Mungu kwa ajili yako ndugu msomaji au unayenifuatilia kupitia somo hili. Ni imani yangu kwa sehemu fupi ya maelezo utakuwa umenielewa. Lakini kama utakuwa una swali usisite kuuliza juu ya somo hili.
    Barikiwa                                                                                                                                                                     Na Henry Nicholaus 
    HUWEZI KUWA NA UHALALI WA KUPOKEA VITU VILIVYOPO NDANI YA YESU KAMA UKIWA NJE YAKE
    Ni muhimu ukatambua nafasi ulionayo wakati unaomba kitu kwa Mungu. Je unamwomba kama mmoja wa familia yake au kama aliye jirani yake. Iko tofauti kubwa ya kibali juu ya watu wa aina hii mbili. Unaweza kunielewa kama nyumbani kwenu kuna mtoto wa ndugu unayeishi naye. Utagundua kuwa unavyoweza kuomba kwa baba yako si vile yeye awezaye kuomba na kupewa. Na hii ndio sababu inanisukuma kuandika somo hili ili liweze kukusaidia wewe katika maisha yako.
    Unaposoma kitabu cha Habakuki 1:1-4 na 2:2,4 utaona maombi ya manung'uniko ya Habakuki na majibu Mungu ambayo alimpa juu ya maombi yake. Jambo la kunishangaza ni namna Mungu alivyomjibu Habakuki katika staili ambayo mimi sikuweza kufikiri. Angalia namna alivyomjibu, "Tazama roho yake hujivuna haina unyofu ndani yake lakini mwenye haki ataishi kwa imani." Hab 2:4. Nilipokuwa nasoma kifungu hiki niligundua Mungu alitaka Habakuki pamoja na sisi tunaosoma haya tujue kuwa licha ya watu walivyokuwa wanaonewa bado mustakabali wao kimsaada toka kwa Mungu ulitegemea nafasi zao walizonazo mbele za Mungu.
    Tazama Ile sentensi katika Hab 2:4 ina pande mbili zinazozungumzia aina ya watu wawili tofauti. Sehemu ya kwanza inaeleza habari ya mtenda dhambi (asiye na haki). Sehemu ya pili inazungumzia mwenye haki. Hivyo majibu ya Mungu yalikuwa katika pande hizi mbili ilikutueleza nini kinatokea pale mtu anapoomba na kupata na pia pale mtu aombapo na kukosa kujibiwa. Na ndipo nilipopata hicho kinywa cha habari.
    Kwa wasio na haki kwa sababu ya dhambi maana yake manyanyaso kwao sio swala la kuuliza kwa nini wayapate? Kwa sababu ndio staili yao. Kwa mwenye haki Mungu akasema na afuate utaratibu yaani awe na imani. Kwa nini imani? Hii ni kwa sababu imani asili yake ni neno lake Mungu. Lakini swala la kuwa na imani sio swala la kulisema kwamba unayo bali ni swala la kuiishi. 1Yak 2:14,17 inatueleza wazi kuwa imani bila matendo imekufa. Hivyo ni vyema ukajua kuwa kama tunalisikia neno la Mungu bila kulitenda maana yake hatuna imani. Maana uhai wa imani uko katika utendaji wake. Imani iko sawasawa na gari. Gari lisipoendeshwa basi linaharibika.
    Nataka unielewe wazi kabisa kusema kwamba umeokoka si suluhisho la wewe kwenda mbinguni maana wengine husema ili wengine wajue kuwa wao ni waumini lakini zizini hayupo. Kwa hiyo hii inatupa tafsiri kwamba kuna watu huwa wanaomba lakini nafasi wanayoomba wakiwepo si ile ya familia ya Mungu. Ili maombi yako yapate upenyo mbele za Mungu ni muhimu ukawa miongoni mwa familia ya Mungu. Kwa kuwa ukweli uko wazi jinsi oambaye jirani na kupewa ni tofauti aombavyo mtoto na kupewa katika familia. Ni muhimu ukalijua hili sababu ni kwamba haki alizonazo mtoto katika familia hazifanani na alizokuwa nazo jirani katika hiyo familia. Mfano haki alizonazo mtanzania katika nchi yake ni tofauti za raia wa nchi nyingine akiwa Tanzania. Hata kwa Mungu mambo yanakwenda vivyo hivyo.
    Ndugu mpendwa ili uweze kupata haki nyingi ni muhimu ukawa miongoni mwa familia ya ki-Mungu. Hii itakusaidia.Swali tunaingiaje? Jibu kama uko nje lazima utambue kuwa nyumbani kwa Mungu kuna mlango. Hivyo tunapita kuingia kwa njia ya toba. Toba unakuwa kama ufunguo wa kufungulia huo mlango. Ni imani yangu utakuwa umenielewa, na naamini bado Mungu angali na mambo mengi ya kukuambia lakini jiweke sawasawa tu utaona mkono wake.
    Barikiwa                                                                                                                                                                     Na Henry Nicholaus
    NI VEMA TUKAACHA VISINGIZIO TUTAFUTE NAMNA YA KUSONGA MBELE
    Mara nyingi watu wengi wamekuwa na visingizio vingi pale wanaposhindwa kufanya mambo. Na hii kwa siku za karibuni imekuwa sasa kama tabia hususani kwa watu wengi kujiepusha na mambo ya msingi. Baya zaidi wasijue athari ya kutoa visingizio. Kwa kuwa athari zake ni kubwa ndio maana Mungu ametupa kibali cha kulijadili sawasawa na neno lake ili tuondoke hapo. Mfano mdogo kijana akiulizwa kwa nini huna kazi atasema serikali haijanisaidia. Si vibaya inawezekana likawa jibu lakini kama serikali haijakusaidia je utabaki hivyo hivyo.
    Mtu mmoja alifanya karamu na kualika watu. Lakini wengi wao wakatoa udhuru mbalimbali. Mwingine akisema amenunua shamba hivyo anakwenda kulitizama hataweza kufika, na mwingine vile vile akatoa sababu zake. Mwishowe Bwana mwenye karamu akatuma watumwa wake kuleta viwete, viziwe, vipofu na masikini waliopo katikati ya miji ili waudhurie karamu. Lk 14:16-24
    Kwa hiyo kutokana na huo mstari hapo juu tumeona watu wengi wakiwa na visingizio vingi pale wanapohitajika kufanya mambo. Hivi swala la kujiuliza huwezi kutazama shamba siku nyingine ukaenda kuungana na mwenzio? Utaona hakuwa na sababu ya msingi kukosa karamu hiyo ila visingizio tu ndivyo vilivyotawala. Lakini pia tunapoa soma kitabu cha Mw 3:9-12 tunazidi kujua kuwa tabia ya kutoa visingizio inawezekana ni ya kurithi. Maana ukisoma hiyo mistari utagundua kuwa hata Adamu naye alikuwa mtu wa visingizio pale bustanini. Wakati anafanya kosa Mungu alimuuliza, "Adamu umekula tunda akaanza kujibu kuwa si huyo mwanamke... Sasa angalia anavyoanza kujibu swali. Utaona kuwa analeta badala ya kujibu swali. Maana nilitegemea akiri kosa na kuomba msamaha.
    Lakini hatuwezi kulizungumzia sana maana inawezekana Adamu hakuwa na ufahamu wa kutosha wakati anatenda kosa. Lakini jambo hili hili lilitokea kwa Musa pia. Kut 3:11, 19, 4:1, 10 utaona Musa akileta visingizio vingi mara baada ya kuambiwa kuwa atahitajika kurudi Misri. Natamani uone moja ya visingizio katika Kut 4:10, Musa alikuwa akisema yeye si msemaji. Mimi binafsi sioni kama swala la kwenda kwa Farao lilikuwa linahitaji siasa ila najua labda Musa alifikiri Mungu angemwacha Musa kwa sababu ya visingizio vyake na kumtuma mwingine.
    Lakini pia haitoshi tunaona jambo hili kwa Yeremia pia kama tunavyosoma katika Yer 1:4-7. Tunaona Yeremia anaelezwa na Mungu kitu alichowekewa katika maisha yake. Naamini ilikuwa ni mpango wa Mungu kuwa Yeremia aanze kujitambua kuwa yeye ni nani na anatakiwa kuishi vipi? Lakini Yeremia akakimbilia kusema yeye ni mtoto hivyo utagundua kuwa ilikuwa ni kisingizio tu cha kukataa unabii. Kwa hiyo hili swala halikuanza jana au leo, lilianza siku nyingi mno hivyo ni vema ukatambua hilo kwanza.
    Visingizio vimekuwa na athari katika maisha yetu ya kila siku. Zifuatazo ni athari za kuishia visingizio badala ya kukubali kukabili changamoto.
  • Kudumaa kwa fikra
  • Kutoendelea/ kuongezeka iwe kimwili/ kiroho
  • Kutofanikiwa kwa mipango ya mtu
  • Ni ngumu kufundishika
    Hivyo kutokana na athari tajwa hapo juu utagundua kuwa kutofanikiwa kimaisha kwa watu wengi kumesababishwa na kutopenda kutafuta ufumbuzi wa mambo. Kwa hiyo epuke sana visingizio ili ndugu mpendwa kubali kukabili changamoto ili uweze kufanikiwa maana ukishavuka hiyo changamoto hutakaa uione tena maisha kuliko kutafuta kuiruka kwa visingizio utakutana nayo mara kwa mara.
    Barikiwa                                                                                                                                                                      Na Henry Nicholaus

    JE UNAWEZAJE KUJUA KAMA MUNGU ANAKUSEMEZESHA
    Kwa kipindi cha nyuma au zamani Mungu alikuwa akitumia watumishi ili waweze kuwaambia watu habari mbalimbali na maelekezo ya kufanya. Haya tunayona kwa Musa, Yeremia, Ibrahim, Daudi na manabii wengine. Lakini mara baada ya agano jipya kuinuliwa na Kristo Yesu viambaza vilivyopo kati ya mtu na Mungu viliondolewa na mtu akawa na uwezo wa kumsikia Mungu yeye mwenyewe moja kwa moja na si kupitia manabii kama ilivyo katika siku za nyuma?
    Sasa kwa kuwa jambo hili lipo kwa sababu agano jipya lipo likitenda kazi na nimesikia watu wengi wakilalamika ni kwa nini Mungu hawajibu. Lakini nikagundua kuwa ni sababu wengi hawawezi kujua sauti ya Mungu ni ipi na ndipo nimepata msukumo wa kushirikia na wewe jambo hili. Kwa kuwa si rahisi kufudishwa mambo ya namna hii katika makanisa.
    Moja: Ni lazima sauti unayosikia iwe na msingi wa neno la Mungu. Unaposoma Mt 4:4 inasema kuwa hatutaishi kwa mkate tu bali kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu. Ina maana kuwa hatima ya maisha yetu iko katika neno la Mungu. Hivyo basi ni vyema utambue kuwa sauti yeyote ili useme ni ya Mungu haiwezi kukinzana na neno lake. Mfano mtu anakuambia nasikia kutoka ndani nimwache mke wangu hali hajafanya zinaa hiyo si sauti ya Mungu bali ya shetani maana neno la Mungu liko wazi juu ya ndoa kuwa ni kifungo cha watu wawili yaani mwanamume na mwanamke na itavunjika kwa kifo au zinaa. Sasa inakuwaje unataka kumwacha na hajatimiza vigezo vya kuvunja ndoa? Ni muhimu tukawa makini sana ndugu wapendwa.
    Pili: Ni lazima hayo maelekezo yampe Mungu utukufu. Kama unasikia chochote ambacho hakimwinui Mungu basi uwe na uhakika hilo jambo si sauti ya Mungu bali ni sauti ya shetani hivyo ni muhimu ukawa makini. Unapotazama Isaya anasema sifa zangu sitampa mwingine kwa hiyo tambua ya kuwa maelekezo yeyote yale ni muhimu ukayachunguz kama yanampa Mungu utukufu au la. Hili ni la munhimu maana unaweza kuweka umuhimu wa kutimiza jambo kumbe si mpango wa Mungu. Mfano:
    Hivyo basi ni muhimu ukawa makini unaposikia sauti ndani yako ikikusemezesha uwe na uhakika kuwa inaweza ikawa ni ya Mungu au ni ya shetani. Maana kumbuka shetani hajahama duniani. Yuko akitafuta kumpinga Mungu kila wakati. Hivyo ni vyema ukawa makini kwa kutazama mambo mawili makubwa ndani ya hiyo sauti na kama ukijirizisha kuwa yapo basi uwe na uhakika kuwa hiyo sauti ni ya Mungu.  
    Barikiwa                                                                                                                                                                                  Na Henry Nicholaus

     

No comments:

Post a Comment